DSTV kwa hili mnaionea Tanzania,halikubaliki

AKILI TATU

JF-Expert Member
Feb 10, 2016
2,658
2,803
Niende moja kwa moja kwenye mada,DSTV kwa miaka mingi imekuwa ikichuma pesa kedekede za watanzania kwa kufanya kazi zao hapa TZ,pamoja na ukweli kuwa wanalipa na kodi na mambo kama hayo lakini ukweli utabaki kuwa kwa TZ DSTV toka zamani wamekuwa wananguvu sana katika solo la TZ.

Shida yangu kubwa ni hii tabia yao ya kuwadharau watanzania ambao nadiriki kusema bila takwimu kamili kuwa ukiacha Nigeria,Afrika kusini,Tanzania inafuata kwa kuwa na RAIA wengi wanaotumia Dstv.

Hivi karibuni,hasa pale time zetu za Tanzania zinapowakilisha nchi,dstv wamekuwa hawaonyeshi kutujali sisi mashabiki zao wa Tanzania kutuonyesha mechi hizo mubashara.

Kuanzia kipindi Yanga wanacheza hatua ya makundi kombe la shirikisho hats wakti huu Simba wanacheza hawa Dstv hawatuonyeshi mechi za away .

Hali ni tofauti na kwa timj za Kenya,Nigeria au afrika kusini,kwani timu zao zimekuwa zikionyeshwa live kwa mwchk zao za home and away.

Ikumbukwe hawa no wadhamini was Caf kwa michuano hii kwa upande wa matangazo ya runinga.

Mfano Leo ,hawataonyesha mechi ya Simba na al ahly ya misri ambapo simba wako ugenini,lakini ajabu simba wakiwa home watajitokeza kutaka kuuonyesha.

Dstv mtachosha na mnazingua.Badilikeni
 
Mbona hii SS4 kma itarusha game live
1549109202698.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye Dunia ya leo anayekubagua kaa naye mbali.
Zama za kuonewa na kubaguliwa zimepita.
Tanzania ni nchi kubwa yenye watu wengi kuliko Kenya wanayoipapatikia, sasa kama unadhani jamaa wanaleta ubaguzi au uonevu nyakati hizi za ushindani wa kibiashara hamia King'amuzi kingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom