DSTV king'amuzi bora kuliko vyote vinavyopatikana Tanzania

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
116,416
215,176
Kupata habari ni haki ya kikatiba , ni makosa kuwakosesha habari watu waliolipia , ni wizi wa mchana na haukubaliki .

Kupokea malipo ya wananchi ili kuwapa huduma ya kuwaonyesha channel kadhaa ni mkataba na ni lazima utekelezwe , inyeshe mvua au liwake jua .

Ndani ya ofisi yangu iliyoko Mbozi road karibu na chuo cha VETA tumeweka ving'amuzi kadhaa , vikiwemo StarTimes , Azam na Dstv , lakini cha kushangaza kwa zaidi ya masaa 7 ni DSTV pekee iliyo hewani , zingine zote zimezima kwa sababu ya mvua , ni nani atanifidia masaa haya yaliyopotea bure ? je mvua ikiendelea kwa siku kadhaa itakuwaje ?

Nakala kwa TCRA
 
DSTV na mvua? Wewe utakuwa unaongea kinyume!
 
Dstv ni majanga sana kwenye mvua sijawahi kuona..

NB sina kingamuzi cha Dstv na zuku
 
DSTV haina mpinzani hapa Tanzania!
Kama dishi la dstv likifungwa vizuri yaani wakati wa initial installation Sginal strength ikiwa 94 au zaidi na Signal quality hivyo hivyo hakuna picha kupotea!
Nipo mkoa wa Kilimanjaro na ni mteja wa DStv kwa zaidi ya miaka kumi sijawahi kuexperience tatizo lolote iwe mvua au jua!
Itachukua miaka mia na ushee hapa Tanzania kuwa na mshindani wa dstv kwa wenye hela zetu!
 
Naipenda Dstv kwa kweli! yaani mpaka naumwa!
Dstv quality sana, najiulizaga kwanini wasitoe huduma ya kuuza channel moja moja kwa bei nafuu ili watu wajikune wanapofika. Mfano mi Ninunue za wanyama kama discovery channel, entertainment kama sony max, na za mziki kama trace mziki, soundcity pamoja na moja ya cartoon kwa ajili ya watoto tu hata kwa 10k hizo zingine zote wapige makufuli waache za local free.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom