DST: Kwanini Waziri Mwigulu aliipongeza JamiiForums na Mkurugenzi wake?

Maxence Melo

JF Founder
Feb 10, 2006
4,230
13,415
Wakuu,

Kwa heshima kubwa nachukua nafasi hii kuwashukuru wengi waliotupongeza kwa mchango wetu kutambuliwa na Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango mnamo jana, Juni 14, 2022 wakati Bajeti ikisomwa Bungeni. Asanteni sana.

Nini hasa ulikuwa mchango wa JF?
JamiiForums ilipata taarifa mapema mwaka jana juu ya uwezekano wa kuwepo kwa Digital Services Tax na ikawa na taarifa ambazo zilikuwa zinakinzana. Wadau walijadili maeneo mengi (online na offline) na ilionekana wazi kuna sintofahamu kubwa.

Mnamo mwezi Januari 2022, JF na uongozi wake uliamua kuwasiliana na mamlaka husika kujiridhisha juu ya uvumi na kutaka kujua ni kwa namna gani inaweza changia kuhakikisha watumiaji wa mitandao si waathirika wa kodi hii. Wizara ilikuwa tayari kusikiliza na hoja ziliwasilishwa. Kimsingi tukakubaliana tuwatafute hao wadau wetu wa kimataifa ili kujiridhisha kuwa wana utayari wa kulipa kodi. Hapa ni vema nikiri kuwa utayari wa serikali kusikiliza ni jambo jema sana na wanastahili pongezi.

Februari 2022, JF iliweza kuandaa kikao (physical) kati ya wadau na Wizara kilichofanyika jijini Dodoma. Kikao hicho kilipelekea kuhitajika kikao kikubwa zaidi (chenye wadau wengi) ambacho kilifanyika virtually kati ya Mamlaka husika za Serikali (Wakiwemo TRA na Wizara ya Fedha na Mipango) na wadau wa kimataifa.

Mnamo Mei 13, 2022 JF iliratibu kikao maalumu cha wadau na Serikali na wadau wa kimataifa walioshiriki kikao hiki ni pamoja na Zoom, Meta, Uber, Google, na waliwawakilisha kundi zima la 'Business at OECD' ikiwa ni pamoja na Microsoft, Netflix, Booking.com na wengine. Kimsingi, kikao kilienda vema na mamlaka za serikali zilitoa ushirikiano (toka bara na Zanzibar) na hoja ziliwekwa mezani.

Matokeo yake nini?
Utaratibu ambao huenda ndio ungetumika awali uliweza kufanyiwa marekebisho na kilichowasilishwa bungeni kupatikana. Kuna kodi kuu mbili ambazo ni tofauti; marekebisho ya VAT (kwa bidhaa za kidijitali); na kodi ya asilimia 2 ya mapato (turnover) maarufu kwa jina DST.

Kwa upande mmoja, tunaipongeza serikali kwa kufanya marekebisho katika sheria ya VAT kuwezesha makampuni ya nje ya kidijitali kuweza kulipa kodi kama ambavyo ilivyo kwa makampuni yaliyojisajili hapa nchini. Kinachohitajika sasa ni ushirikishwaji katika kufanikisha hili kama ilivyofanywa katika nchi nyingine kama Ghana, Cameroon, na Uganda. Kwa upande wa pili, kutoza kodi ya 2% ya malipo ya watoa huduma za kidijitali wa kigeni ina changamoto zake na suala hili linahitaji kuatizamwa zaidi.

JF inashauri nini hasa?
Bado JF inaamini kunatakiwa kufanyika maboresho zaidi kwa hiyo kodi ya 2% hasa kwa kuzingatia kuwa nchi zote duniani zilizokuwa na kodi kama hiyo zimeiondoa isipokuwa kwa Kenya. Pia kodi hiyo ni rahisi kugeuka kuwa kandamizi maana makampuni kama Google, Amazon na Apple wamekwishatangaza kuwa kodi kama hiyo (2% DST) zinalipwa na watumiaji wa mwisho (mtumiaji wa kawaida).

Mwisho, kimataifa mfumo wa OECD unaokubalika kimataifa na rahisi kuweza kukusanya kwa kufuata mfumo wake badala ya DST ambayo hata kwa majirani zetu Kenya unaonekana kugonga mwamba. Ni bahati mbaya kuwa hakuna nchi ya Afrika Mashariki imekuwa mwanachama wa (angalia orodha ya nchi 134 wanachama wa mfumo huu https://www.oecd.org/tax/beps/oecd-...ges-arising-from-digitalisation-july-2021.pdf )

Tunaamini muda bado unaruhusu, kabla ya kuwa wanachama mfumo wa VAT unaweza kuendelea kama ilivyo nia ya Serikali lakini pia inatoa uwanja mzuri kwa Taifa letu kufuata mifumo ya kimataifa na kuweka mazingira rafiki ya kikodi yanayoeleweka na yasiyomuumiza mwananchi.

Kuhusu JamiiForums (Taasisi)
Sisi ni Asasi ya Kiraia (NGO) inayojihusisha masuala ya uchechemuzi katika Haki za Kiraia na Kidigitali, Haki za Kijamii, Demokrasia, Utawala Bora na Uwajibikaji. Taasisi hii huratibu mtandao wa JamiiForums.com ikiwa ni pamoja na kurasa zake za mitandao ya kijamii.
 
Asante kwa andiko hili. Wengi tulikuwa hatuelewi hiyo Digital Services Tax (DST) lakini angalau kupiyia JF tumepata mwanga.

Nawapongezeni kwa uzalendo huu, msikate tamaa katika kupambania maslai ya umma.
 
Sio kwamba serikali haijui kwamba DST italipwa na mtumiaji wa mwisho(in this case raia wa Tanzania), simply ni kwamba they don't care who pays it.

Bila internet data, hakuna Digital Services na tayari serikali inakusanya kodi kwenye data bundles. Sasa hii DST ya 2% ambayo serikali inataka kutoza ipo vipi?

Mfano, Mimi natumia Google kwa ajili ya search engine, kutazama YouTube.com pamoja na Google Services nyingine nyingi(zote huduma za bure), je, hiyo 2% ya DST kwa upande wangu inapatikana vipi?
 
Tuelimishane..!
Je, mtumiaji wa kawaida wa meta (Facebook, whatsapp and instagram) hiyo 2% ya DST inapatikana kwa valuation gani?
Yaani analipa 2% of what value? Na je, hiyo value inapatikana vipi?
 
Wakuu,

Kwa heshima kubwa nachukua nafasi hii kuwashukuru wengi waliotupongeza kwa mchango wetu kutambuliwa na Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango mnamo jana, Juni 14, 2022 wakati Bajeti ikisomwa Bungeni. Asanteni sana.

Nini hasa ulikuwa mchango wa JF?
JamiiForums ilipata taarifa mapema mwaka jana juu ya uwezekano wa kuwepo kwa Digital Services Tax na ikawa na taarifa ambazo zilikuwa zinakinzana. Wadau walijadili maeneo mengi (online na offline) na ilionekana wazi kuna sintofahamu kubwa.

Mnamo mwezi Januari 2022, JF na uongozi wake uliamua kuwasiliana na mamlaka husika kujiridhisha juu ya uvumi na kutaka kujua ni kwa namna gani inaweza changia kuhakikisha watumiaji wa mitandao si waathirika wa kodi hii. Wizara ilikuwa tayari kusikiliza na hoja ziliwasilishwa. Kimsingi tukakubaliana tuwatafute hao wadau wetu wa kimataifa ili kujiridhisha kuwa wana utayari wa kulipa kodi. Hapa ni vema nikiri kuwa utayari wa serikali kusikiliza ni jambo jema sana na wanastahili pongezi.

Februari 2022, JF iliweza kuandaa kikao (physical) kati ya wadau na Wizara kilichofanyika jijini Dodoma. Kikao hicho kilipelekea kuhitajika kikao kikubwa zaidi (chenye wadau wengi) ambacho kilifanyika virtually kati ya Mamlaka husika za Serikali (Wakiwemo TRA na Wizara ya Fedha na Mipango) na wadau wa kimataifa.

Mnamo Mei 13, 2022 JF iliratibu kikao maalumu cha wadau na Serikali na wadau wa kimataifa walioshiriki kikao hiki ni pamoja na Zoom, Meta, Uber, Google, na waliwawakilisha kundi zima la 'Business at OECD' ikiwa ni pamoja na Microsoft, Netflix, Booking.com na wengine. Kimsingi, kikao kilienda vema na mamlaka za serikali zilitoa ushirikiano (toka bara na Zanzibar) na hoja ziliwekwa mezani.

Matokeo yake nini?
Utaratibu ambao huenda ndio ungetumika awali uliweza kufanyiwa marekebisho na kilichowasilishwa bungeni kupatikana. Kuna kodi kuu mbili ambazo ni tofauti; marekebisho ya VAT (kwa bidhaa za kidijitali); na kodi ya asilimia 2 ya mapato (turnover) maarufu kwa jina DST.

Kwa upande mmoja, tunaipongeza serikali kwa kufanya marekebisho katika sheria ya VAT kuwezesha makampuni ya nje ya kidijitali kuweza kulipa kodi kama ambavyo ilivyo kwa makampuni yaliyojisajili hapa nchini. Kinachohitajika sasa ni ushirikishwaji katika kufanikisha hili kama ilivyofanywa katika nchi nyingine kama Ghana, Cameroon, na Uganda. Kwa upande wa pili, kutoza kodi ya 2% ya malipo ya watoa huduma za kidijitali wa kigeni ina changamoto zake na suala hili linahitaji kuatizamwa zaidi.

JF inashauri nini hasa?
Bado JF inaamini kunatakiwa kufanyika maboresho zaidi kwa hiyo kodi ya 2% hasa kwa kuzingatia kuwa nchi zote duniani zilizokuwa na kodi kama hiyo zimeiondoa isipokuwa kwa Kenya. Pia kodi hiyo ni rahisi kugeuka kuwa kandamizi maana makampuni kama Google, Amazon na Apple wamekwishatangaza kuwa kodi kama hiyo (2% DST) zinalipwa na watumiaji wa mwisho (mtumiaji wa kawaida).

Mwisho, kimataifa mfumo wa OECD unaokubalika kimataifa na rahisi kuweza kukusanya kwa kufuata mfumo wake badala ya DST ambayo hata kwa majirani zetu Kenya unaonekana kugonga mwamba. Ni bahati mbaya kuwa hakuna nchi ya Afrika Mashariki imekuwa mwanachama wa (angalia orodha ya nchi 134 wanachama wa mfumo huu https://www.oecd.org/tax/beps/oecd-...ges-arising-from-digitalisation-july-2021.pdf )

Tunaamini muda bado unaruhusu, kabla ya kuwa wanachama mfumo wa VAT unaweza kuendelea kama ilivyo nia ya Serikali lakini pia inatoa uwanja mzuri kwa Taifa letu kufuata mifumo ya kimataifa na kuweka mazingira rafiki ya kikodi yanayoeleweka na yasiyomuumiza mwananchi.

Kuhusu JamiiForums (Taasisi)
Sisi ni Asasi ya Kiraia (NGO) inayojihusisha masuala ya uchechemuzi katika Haki za Kiraia na Kidigitali, Haki za Kijamii, Demokrasia, Utawala Bora na Uwajibikaji. Taasisi hii huratibu mtandao wa JamiiForums.com ikiwa ni pamoja na kurasa zake za mitandao ya kijamii.
Tunaamini muda bado unaruhusu, kabla ya kuwa wanachama mfumo wa VAT unaweza kuendelea kama ilivyo nia ya Serikali lakini pia inatoa uwanja mzuri kwa Taifa letu kufuata mifumo ya kimataifa na kuweka mazingira rafiki ya kikodi yanayoeleweka na yasiyomuumiza mwananchi.
 
Sisi ni Asasi ya Kiraia (NGO) inayojihusisha masuala ya uchechemuzi katika Haki za Kiraia na Kidigitali, Haki za Kijamii, Demokrasia, Utawala Bora na Uwajibikaji. Taasisi hii huratibu mtandao wa JamiiForums.com ikiwa ni pamoja na kurasa zake za mitandao ya kijamii.
Ahsante kwa maelezo mazuri mkuu 'Maxence, ambayo umeyatoa kwa ufasaha kabisa na lugha iliyonyooka vizuri.

Kuna watu bado wana mashaka na lugha hii adhimu kabisa, ambayo kiuhakika ipo tayari kutumika katika eneo lolote la kitaalam.

Ahsante kwa msamiati mpya, "uchechemuzi", ambao bila shaka nitapata msaada juu yake.

Mwisho, ni dhahiri umeonyesha umejiwekea kiwango katika thamani 'value' ya unayoyawasilisha'yawe na kiwango cha kusomeka na kueleweka na wasomaji wako. Bila shaka kiwango hiki kinaweza kuwa ni chachu ya kuwafanya wachangiaji wengine katika kumbi mbalimbali humu JF kuiga mfano huo.

Wachangiaji katika majukwaa haya ni kiasi kidogo tu cha umma wa waTanzania, lakini nani ajuae, pakiwepo na mifano ya 'standard', pengine huo ndio unaweza kuwa mwanzo wa kunyoosha sehemu nyingi zilizopinda katika utendaji wetu wa mambo mbalimbali.

Tanzania tumekuwa na tabia mbaya sana ya kutofuata na kutimiza mahitaji ya viwango katika jambo lolote.
 
Wakuu,

Kwa heshima kubwa nachukua nafasi hii kuwashukuru wengi waliotupongeza kwa mchango wetu kutambuliwa na Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango mnamo jana, Juni 14, 2022 wakati Bajeti ikisomwa Bungeni. Asanteni sana.

Nini hasa ulikuwa mchango wa JF?
JamiiForums ilipata taarifa mapema mwaka jana juu ya uwezekano wa kuwepo kwa Digital Services Tax na ikawa na taarifa ambazo zilikuwa zinakinzana. Wadau walijadili maeneo mengi (online na offline) na ilionekana wazi kuna sintofahamu kubwa.

Mnamo mwezi Januari 2022, JF na uongozi wake uliamua kuwasiliana na mamlaka husika kujiridhisha juu ya uvumi na kutaka kujua ni kwa namna gani inaweza changia kuhakikisha watumiaji wa mitandao si waathirika wa kodi hii. Wizara ilikuwa tayari kusikiliza na hoja ziliwasilishwa. Kimsingi tukakubaliana tuwatafute hao wadau wetu wa kimataifa ili kujiridhisha kuwa wana utayari wa kulipa kodi. Hapa ni vema nikiri kuwa utayari wa serikali kusikiliza ni jambo jema sana na wanastahili pongezi.

Februari 2022, JF iliweza kuandaa kikao (physical) kati ya wadau na Wizara kilichofanyika jijini Dodoma. Kikao hicho kilipelekea kuhitajika kikao kikubwa zaidi (chenye wadau wengi) ambacho kilifanyika virtually kati ya Mamlaka husika za Serikali (Wakiwemo TRA na Wizara ya Fedha na Mipango) na wadau wa kimataifa.

Mnamo Mei 13, 2022 JF iliratibu kikao maalumu cha wadau na Serikali na wadau wa kimataifa walioshiriki kikao hiki ni pamoja na Zoom, Meta, Uber, Google, na waliwawakilisha kundi zima la 'Business at OECD' ikiwa ni pamoja na Microsoft, Netflix, Booking.com na wengine. Kimsingi, kikao kilienda vema na mamlaka za serikali zilitoa ushirikiano (toka bara na Zanzibar) na hoja ziliwekwa mezani.

Matokeo yake nini?
Utaratibu ambao huenda ndio ungetumika awali uliweza kufanyiwa marekebisho na kilichowasilishwa bungeni kupatikana. Kuna kodi kuu mbili ambazo ni tofauti; marekebisho ya VAT (kwa bidhaa za kidijitali); na kodi ya asilimia 2 ya mapato (turnover) maarufu kwa jina DST.

Kwa upande mmoja, tunaipongeza serikali kwa kufanya marekebisho katika sheria ya VAT kuwezesha makampuni ya nje ya kidijitali kuweza kulipa kodi kama ambavyo ilivyo kwa makampuni yaliyojisajili hapa nchini. Kinachohitajika sasa ni ushirikishwaji katika kufanikisha hili kama ilivyofanywa katika nchi nyingine kama Ghana, Cameroon, na Uganda. Kwa upande wa pili, kutoza kodi ya 2% ya malipo ya watoa huduma za kidijitali wa kigeni ina changamoto zake na suala hili linahitaji kuatizamwa zaidi.

JF inashauri nini hasa?
Bado JF inaamini kunatakiwa kufanyika maboresho zaidi kwa hiyo kodi ya 2% hasa kwa kuzingatia kuwa nchi zote duniani zilizokuwa na kodi kama hiyo zimeiondoa isipokuwa kwa Kenya. Pia kodi hiyo ni rahisi kugeuka kuwa kandamizi maana makampuni kama Google, Amazon na Apple wamekwishatangaza kuwa kodi kama hiyo (2% DST) zinalipwa na watumiaji wa mwisho (mtumiaji wa kawaida).

Mwisho, kimataifa mfumo wa OECD unaokubalika kimataifa na rahisi kuweza kukusanya kwa kufuata mfumo wake badala ya DST ambayo hata kwa majirani zetu Kenya unaonekana kugonga mwamba. Ni bahati mbaya kuwa hakuna nchi ya Afrika Mashariki imekuwa mwanachama wa (angalia orodha ya nchi 134 wanachama wa mfumo huu https://www.oecd.org/tax/beps/oecd-...ges-arising-from-digitalisation-july-2021.pdf )

Tunaamini muda bado unaruhusu, kabla ya kuwa wanachama mfumo wa VAT unaweza kuendelea kama ilivyo nia ya Serikali lakini pia inatoa uwanja mzuri kwa Taifa letu kufuata mifumo ya kimataifa na kuweka mazingira rafiki ya kikodi yanayoeleweka na yasiyomuumiza mwananchi.

Kuhusu JamiiForums (Taasisi)
Sisi ni Asasi ya Kiraia (NGO) inayojihusisha masuala ya uchechemuzi katika Haki za Kiraia na Kidigitali, Haki za Kijamii, Demokrasia, Utawala Bora na Uwajibikaji. Taasisi hii huratibu mtandao wa JamiiForums.com ikiwa ni pamoja na kurasa zake za mitandao ya kijamii.
Sasa bwana yule angewafunga sijui pongezi hizo mngezipata kupitia wapi! Bwana yule aliamini kila jambo alifanye yeye na polisi wamalizie.
 
Kwa maneno machache ni kwamba "MWISHO WA SIKU HII 2% ITAMRUDIA MWANANCHI WA KAWAIDA KWANI HAYO MAKAMPUNI YA NJE HAWATAILIPA HIYO OECD"....
Kodi siku zote inamuangukia mtumiaji wa mwisho. Mtoa huduma anacheza na profit tu. Zaidi zaidi itamuangukia mtoa huduma kama super profit asipoiwakilisha kwenye mamlaka kama inavyotakiwa.
 
Back
Top Bottom