Dsm na mipango ya hasara: Bomoa barabara mpya ubungo-kimara, jenga upya mabasi yaende kasi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dsm na mipango ya hasara: Bomoa barabara mpya ubungo-kimara, jenga upya mabasi yaende kasi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Midas Touch, Aug 4, 2012.

 1. M

  Midas Touch Member

  #1
  Aug 4, 2012
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 74
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 15
  DSM NA MIPANGO YA HASARA: BOMOA BARABARA MPYA UBUNGO-KIMARA, JENGA UPYA MABASI YAENDE KASI YA RISASI
  Kwa maoni yangu, barabara ya Morogoro kipande cha Ubungo-Kimara Mwisho Jijini Dar es salaam siyo ya siku nyingi, sidhani kama ina miaka 10 tangu ijengwe na kukamilika kabisa. Pia sidhani kama tulikopa pesa za kuijenga tumeshalipa (Sina data, aliyenazo atuwekee hapa jamvini). Hii barabara ilijengwa kwa umakini na usahihi wa hali ya juu na lifespan yake ni zaidi ya miaka 20, ceteris peribus.In short, ni barabara ya kisasa Jijini kwani ilichukua tahadhari nyingi za kimazingira na hali ya hewa kama mvua na mafuriko.
  To my surprise, naona heavy construction equipment (Matrekta Makubwa na malori) yakiisambaratisha barabara ile nzuri na mpya! Nikauliza kulikoni! Nikaambiwa eti Magufuli anajenga barabara mpya kwa ajili ya MABASI YAENDAYO KASI YA RISASI! Kimoyomoyo nikajisemea, kama hayo mabasi yanakwenda KASI YA RISASI kiasi cha Magufuli kubomoa barabara yetu mpya na nzuri si yapae juu tuyakute kule Posta Mpya!
  Hali hii ikanikumbusha enzi zile za kubadilisha lori kuwa basi la abiria and vice versa. Mchezo huu wa basi kuwa lori na lori kuwa basi huwa una gharama kubwa sana. Ni afadhali uliache basi kuwa basi na lori kuwa lori ili ujazie pesa ulizo nazo ununue basi au lori lingine.
  Likewise, Magufuli wetu angeacha bara bara hiyo kama ilivyokuwa na a-plan jinsi ya ku-accommodate hayo mabasi yaendayo kasi katika barabara hiyo hiyo. Angeweza kupanua pande zote mbili na akawafidia watu wachache lakini siyo kutumia “A lot for cash” katika kuvunjavunja barabara ile mpya na nzuri ili mabasi yaende kasi ya risasi!
  My take: Mimi siyo Civil Engineer wa TANROAD na wala siyo Economist wa Wizara lakini sikuridhika na huo ubomoaji wa barabara mpya ili ujenge mpya nyingine. Kulikuwa na alternative nyingi kabla ya kuibomoa barabara ile mpya na nzuri. Nadhani gharama za kuibomoa ni kubwa sana kiasi kwamba hiyo barabara mpya ya mabasi yaendayo KASI YA RISASI itakuwa ghali sana na TUMEKOPA HIZO PESA kwa asilimia kubwa, pia kwa riba kubwa. HII NDIYO MIPANGO YA HASARA ninayoisemea mimi.
   
 2. omujubi

  omujubi JF-Expert Member

  #2
  Aug 4, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 4,144
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  jamii inayoendeshwa na matukio (event oriented) utaijua mkuu.

  Kabla hata ya kuongelea huo upande wa Ubungo- Kimara, hebu angalia uzuri uliokuwa kwenye kipande cha Ubungo- Magomeni kilichojengwa na KONOIKE kama miaka 15 tu iliyopita, ile miti yote ambayo ni muhimu wameifagilia mbali.

  Kwa maana hiyo ina maana miaka 15 iliyopita katika utawala huu huu (maana hatujabadilisha) hawakujua na wala hawakuwa na takwimu za nini kitatokea leo! Hivyo hivyo na leo kwenye watawala hawa hawa hakuna anayejua hii nchi itakuwaje miaka 15 ijayo. Lakini eti nasi ni nchi na tuna kiti UN, bendera nk. Si ni bora hata mipango ingelikuwa valid kwa agalau miaka 50+ ambao ni umri wa mtu!? ...ili imaanishe kuwa japo tulishindwa kupanga juu ya wanetu lakini angalau tulijipangia hata sisi. Watu 60,000,000 soto bureee kweli!!!!!!!!!!!!!????
   
 3. k

  kasimba123 JF-Expert Member

  #3
  Aug 4, 2012
  Joined: Apr 18, 2010
  Messages: 1,318
  Likes Received: 188
  Trophy Points: 160
  nakumbuka mji fulani katika pitia zangu wanajenga subway na design yao ni ya miaka 50 kama nikuipanua au kuongeza ni baada ya miaka 50
   
 4. M

  Mjenda Chilo JF-Expert Member

  #4
  Aug 4, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 1,425
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Kama ulikuwa kichwani mwangu. Juzi nilicomment the same. Tatizo la politics zetu hakuna continuity. Inawezekana kabisa plan hiyo ipo ila kuwalipa watu ili wavunje nyumba wameona mtihani. Wanawaza output ipatikane ndani ya muda wa uongozi say 5 years hata kama haiwezekani. Na ndo maana utasikia kauli kama jambo hili halikutokea katika awamu hii nk. Ni statement ya ajabu sana coz najua serikali haina term ni faces tu ndo zinabadilika.
   
 5. m

  mambomengi JF-Expert Member

  #5
  Aug 4, 2012
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 829
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Hiyo yote ni poor planning ndugu yangu. Kwa taarifa barabara zote kuu zitafumuliwa...Sam Nujoma, Mandela, Kilwa, Kawawa, na hii Bagamoyo inayojengwa sass hivi. Huu mradi uko toka miaka ya 1990. Utashangaa barabara mpya kama Sam Nujoma,Kilwa, Bagamoyo hawakkuongeza hio provision ya bus lanes.....someone has to be accountable. Ni ujinga mkubwa sana kufumua barabara mpya....they should have construct it in phases, lakini walihifanya wabishi waliposhauriwa. Dar Road Improvement Project, DRIP iliosanifiwa na JICA/JEC ilitahadharisha hilo na ikashauri sehemu ya kati, median, isanifiwe kuwa njia za mabasi, wasioona mbali wakaona huo ushauri ni ujinga, matokeo yake ndio hayo, unashangaaa Barbara iliojengwa miaka 10 inabomolewa....subiri utakapoona Kilwa Road, Sam N na B'moyo zinabomolewa kupisha huo mradi....
   
 6. m

  mambomengi JF-Expert Member

  #6
  Aug 4, 2012
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 829
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Kuna vitu vya kijinga na kipuuzi vinaendelea bongo, hapa wanajigamba kuwa wanajenga flyovers....hawawaelimishi wananchi manufaaa ya hizo flyovers kwa sababu hawajui zinafanya kazi vipi. Wanakimilia kufumua Barabara ya Morogoro.....sasa unajiuliza kama wanazitaka hizo flyovers si wazijenge sass hivi......vinginevyo Midas Touch atarudi na same thread kushangaaa poor planning. Naamini kuwawatendaji serikalini wamerogwa.....hawa wa TANROARS nashauri wapelekwe internship Kenya kwa KURA kwa walau miezi 12 wakajifunze kifanya kazi kwa manufaa ya jamii. Pathetic.......
   
 7. Kibajajitz

  Kibajajitz JF-Expert Member

  #7
  Aug 22, 2017
  Joined: Apr 20, 2013
  Messages: 3,634
  Likes Received: 1,642
  Trophy Points: 280
Loading...