DRs na Wana-Jf: USHAURI WENU TAFADHALI KUHUSU HUU UTARATIBU WA KULA NA MAISHA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

DRs na Wana-Jf: USHAURI WENU TAFADHALI KUHUSU HUU UTARATIBU WA KULA NA MAISHA

Discussion in 'JF Doctor' started by JATELO1, Jun 12, 2012.

 1. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #1
  Jun 12, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Drs. na Wanajf,

  Naomba kufahamishwa kwa utaratibu wangu huu wa maisha nakosea sehemu au niko sawa?

  Mara nyingi huwa naamka saa 12 asubuhi. Asubuhi nikiamka kila siku nakunywa maji ya uvugu uvugu lita 1 kabla sijapiga mswaki na hata kula chochote. Na baada ya kunywa maji, napiga mswaki na maandalizi mengine na ikifika dk.45 hivi baada ya kunywa maji ndipo nakunywa chai kikombe 1 yenye asali na green tea na slesi tatu za mkate (Volkonbrot) kila siku. Baada ya hapo naelekea ofisini na ikifika masaa 2 baada ya kunywa breakfast huwa nakunywa maji tena ya kawaida (siyo ya moto) lita 1. Baada ya muda kama dk.45 hivi nakula ndizi 1+apple 1+ Karote 1. Baada ya hapo nitaendelea na kazi zangu na ikipita kama dk. 45 hivi baada ya kula matunda nakunywa tena maji lita 1. Ikifika saa 10 jioni naondoka ofisini na kurejea nyumbani na nikifika ndipo huandaa chakula. Mara nyingi nakula chakula kabla ya saa 12 jioni kila siku, na baada ya hapo naendelea na kazi zangu mpaka saa 4 au 5 usiku ninakula kijiko 1 cha Asali, ndipo naingia kitandani kulala.

  Vyakula vyangu kwa mwezi mara nyingi ni ugali, wali tambi na kwa upande wa mboga ni mboga za majani hasa Kabeji, Kuku 1, Mayai 6, maziwa lita 1, karanga 250 gram, maharage na samaki (sato) kilo 1. Hapa ni kwamba, maharage ndiyo chakula changu kikuu kwa mwezi, kwani hivyo vyakula vingine navitumia tu mara moja kama nilivyoonyesha hapo juu.

  Pia kwasababu sina uhakika wa kufanya mazoezi kila siku, hivyo najitahidi kila siku ninapokwenda ofisini natumia ngazi badala ya Lifti kwenda na kurudi. Na ofisi yangu iko ghorofa ya 7. Lkn pia ninapofanya muda huwa natembea kwa umbali kama wa km 2 kwa siku na kufanya Indoor mazoezi ya mwili kama kuruka kichura, kurukaruka na Yoga.

  Hivyo, wadau naombeni ushauri kama kuna kitu nakosea, kwasababu sasa yapata miezi 3 na huu ndiyo umekuwa kawaida yangu na binafsi sijaona tatizo.
  TELO.
   
 2. Rogie

  Rogie JF-Expert Member

  #2
  Jun 13, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 6,277
  Likes Received: 3,008
  Trophy Points: 280
  Hueleweki unataka nn. Umetoa mlolongo mreefu halafu huoni tatzo. Kwa utaratibu huo we wataka kuona tatizo gani? au una maanisha mabadiliko kutokana na huo mpangilio wa chakula??
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Jun 13, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Ni Vizuri kabisa huo Utaratibu wako ila hapo kidogo umekosea unapokunywa maji ya uvuguvugu changanya na kijiko kimoja cha Asali hapo tu nakurekebisha kwengine kuko bravo unajitahidi na inshallah maradhi yatakuwa mbali na wewe Akipenda Mwenyeezi Mungu utakuwa na afya nzuri Tendo la kunywa Asali wakati unapo lala Asali itakusaidia kusafisha ini na figo ukidumu hivyo kunywa asali asubuhi na usiku kwa wakati wakulala. ....TELO
   
 4. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #4
  Jun 13, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Mkuu ametowa Menu yake yaani Utaratibu wake wa kila siku anavyoishi kwakula chakula chake anataka mawazo ya Watu je anakosea au hakosei? Wewe hujamuelewa lengo lake mkuu.. Rogi
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. Evarm

  Evarm JF-Expert Member

  #5
  Jun 13, 2012
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,499
  Likes Received: 186
  Trophy Points: 160
  Hongera sana mkuu kama umeweza kumaintain hivyo kwa muda huo, endelea tu ni utaratibu mzuri sana
   
 6. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #6
  Jun 13, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Ahsante sana MziziMkavu na ubarikiwe.
   
 7. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #7
  Jun 13, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Ahsante sana na Ubarikiwe ndugu yangu.
   
 8. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #8
  Jun 13, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Ahsante Dr., kwa kunielewa.
   
Loading...