Droo ya Kombe la Shirikisho Africa ni leo mchana Cairo, Yanga na Waarabu tena?

Wonderful

JF-Expert Member
Apr 8, 2015
7,347
5,984
ZILIZOFUZU NANE BORA LIGI YA MABINGWA;
Enyimba (Nigeria), Al Ahly (Misri), AS Vita (DRC), Asec Mimosas (Ivory Coast), Wydad Casablanca (Morocco), ES Setif (Algeria), Zamalek (Misri) na
Zesco United (Zambia).

ZILIZOANGUKIA KOMBE LA SHIRIKISHO;
ES Sahel (Tunisia), Yanga SC (Tanzania), Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini), Ahly Tripoli (Libya), TP Mazembe (DRC), El Merreikh (Sudan), MO Bejaia (Algeria) na Stade Malien (Mali).

ZILIZOFUZU KOMBE LA SHIRIKISHO;
Kawkab Marrakech (Morocco), Mounana (Gabon), Misr Makkassa (Morocco), Medeama (Ghana), FAR Rabat (Morocco), Esperance (Tunisia), Sagrada Esperanca (Angola) na Stade Gabesien (Tunisia).

ANGA SC inaweza kurudishwa Kaskazini mwa Afrika kwa ajili ya mchezo wa kuwania kuingia kwenye makundi ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika.
Yanga jana ilitolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kufungwa mabao 2-1 na Al Ahly Uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria katika mchezo wa marudiano hatua ya 16 Bora.
Al Ahly imesonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-2 baada ya awali kulazimisha sare ya 1-1 Uwanja wa Dar es Salaam wiki mbili zilizopita.
Abdallah Said aliifungia Ahly bao la ushindi dakika ya sita ya muda wa nyongeza baada ya kukamilika kwa dakika 90 za kawaida za mchezo akimalizia krosi ya Walid Soliman kutoka upande wa kushoto.
Al Ahly walitangulia kupata bao katika mchezo wa leo kupitia kwa kiungo Hossam Ghaly aliyeunganisha kwa kichwa kona ya Ahmed Fathi dakika ya 52.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Zimbabwe, Donald Dombo Ngoma akaisawazishia Yanga dakika ya 57 kwa kichwa akimalizia krosi nzuri ya beki wa kulia Juma Abdul.
Kwa matokeo hayo, Yanga itamenyana na moja ya timu zilizofuzu Kombe la Shirikisho kuwania nafasi ya kupangwa kwenye makundi.
Na kati ya timu hizo nane, tano zinatoka Kaskazini mwa Afrika, ambazo ni Kawkab Marrakech, Misr Makkassa, FAR Rabat zote za Morocco, Esperance na Stade Gabesien za Tunisia.
Timu nyingine zilizofuzu hatua hiyo ni CF Mounana ya Gabon, Medeama ya Ghana na Sagrada Esperanca ya Angola.
Mbali na Yanga, timu nyingine zilizoangukia kwenye kapu la kuwania hatua ya makundi Kombe la Shirikisho ni pamoja na waliokuwa mabingwa wa Afrika, TP Mazembe ya DRC, Etoile du Sahel ya Tunisia, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Al Ahly Tripoli ya Libya, El Merreikh ya Sudan, MO Bejaia ya Algeria na Stade Malien ya Mali.
Kwa Yanga, hii ni mara ya pili kufikia hatua hiyo baada ya mwaka 2007. Mwaka huo Yanga ilifungwa 3-0 na Esperance ya Tunisia katika hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika kabla ya kutoa sare 0-0 Mwanza.
Katika kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho na ilitolewa na El Merreikh ya Sudan, ikitoa sare ya 0-0 Mwanza na kufungwa 2-0 Khartoum.
Droo ya mchujo wa mechi za kuwania hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho inatarajiwa kupangwa mchana wa leo mjini Cairo, Misri. Je, safari hii Yanga itapangwa na nani?
 
wapigwe tu hawana adabu...

Mimi sio mpenzi wa Yanga lakini kwenye hili sikuungi wa sikubaliani na wewe hata kidogo, tuwe wazalendo kidogo walau. Binafsi nawapongeza Yanga kwa jinsi walivyocheza mechi ya jana hata kama walitolewa. Ushauri wangu kwao next time wacheze vizuri zaidi hasa wakiwa nyumbani Tanzania, maana ukweli nikinganisha walivyocheza mechi ya nyumbani Dsm na ile ya jana kwangu mimi naona hakika jana walicheza vizuri zaidi

Niwatakie kila la heri sana katika kombe la shirikisho, ila wajitahidi kucheza vizuri na zaidi sana nyumbani mbele ya washabiki wao.
 
Duuuuuuih! hizi timu za Waarabu zipo nyingi jamani!!!!!!? Any way yeyote atakaekuja mbele yetu tutamshughulikia. Ni kujipanga tu
 
Mkuu fuatilia kwa makini yanga anakuwa kwenye wakat mgumu anapocheza dar kutokana na kupata upinzan wa kishabiki uwanjani lkn ni tofauti anapokuwa away tazama mechi zote alizocheza nje ya nchi yanga imecheza vzuri kuliko za hapa ndani.
 
Mimi sio mpenzi wa Yanga lakini kwenye hili sikuungi wa sikubaliani na wewe hata kidogo, tuwe wazalendo kidogo walau. Binafsi nawapongeza Yanga kwa jinsi walivyocheza mechi ya jana hata kama walitolewa. Ushauri wangu kwao next time wacheze vizuri zaidi hasa wakiwa nyumbani Tanzania, maana ukweli nikinganisha walivyocheza mechi ya nyumbani Dsm na ile ya jana kwangu mimi naona hakika jana walicheza vizuri zaidi

Niwatakie kila la heri sana katika kombe la shirikisho, ila wajitahidi kucheza vizuri na zaidi sana nyumbani mbele ya washabiki wao.
uzalendo kwa yanga!? shindwa...
 
Mbona inaonekana kuna baadhi ya nchi zilikuwa zina mwakilishi zaidi ya mmoja ktk shindano moja mfano al ahly na zamalek toka misri na timu za morocco,afadhali drc najua imetoa na bingwa mtetezi lakini hizo nyingine kimetumika kigezo gani?
ndiyo ilivyo mkiwa na club zenye mafanikio mnaongezewa nafasi ni kama ulaya tu..
 
Kwenye mashindano ya shirikisho (CAF) kwa nini morocco wameingiza timu 3? wakati huku kwetu timu moja inashiriki club bingwa na moja CAF
 
Back
Top Bottom