Droni zawapa changamoto kubwa waongoza ndege

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875
KUWEPO kwa ndege nyuki (droni) imetajwa ni miongoni mwa changamoto wanazokabiliana nazo waongoza ndege nchini kutokana na teknolojia ya mawasiliano ya vifaa hivyo kutoonekana wakati vinaporushwa angani.

Hayo yalisemwa jana na Rais wa Chama cha Waongoza Ndege Tanzania (TACC), Shukuru Nziku wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya waongoza ndege duniani.

Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo Dar es Salaam jana, Nziku alisema pamoja na kuwepo kwa changamoto nyingi katika utendaji kazi wao, uwepo wa droni umeonekana kuwa na changamoto kubwa, hivyo kuhatarisha usalama wa ndege angani.

Alisema kifaa hicho kinachotumika kurahisisha kazi kama ujenzi wa miundombinu na upigaji picha za kawaida katika maeneo mbalimbali nchini, wanashindwa kukifuatilia kutokana na kutoonekana kikiwa angani.

“Hii ni changamoto kubwa kwa hizi ndege ambazo hazina rubani ndani, kwakuwa waongoza ndege hawazioni katika satellite, japokuwa sheria ya mwaka 2018 inazuia kifaa hicho kurushwa angani na endapo zitaruka basi kuwepo na mawasiliano ya redio na waongoza ndege, hii ni ngumu kwakuwa hiki kifaa hakina rubani, kinaongozwa na mtu aliyepo chini,” alisema Nziku.

Alisema hivi sasa droni ni nyingi na zinatumiwa kwa shughuli mbalimbali, lakini ni hatari zinapokuwa angani kutokana na kuweza kugongana na ndege kwa kuwa nyingine zinatakiwa kuruka juu zaidi ili kuona eneo kubwa.

Nziku alisema nchi kama Australia kifaa hicho kimesababisha majanga kwa ndege, hivyo wanafanya jitihada ya kutafuta namna ya kuzifanya zitumike pasipokuleta madhara kwa ndege zinapokuwa angani.

“Japokuwa ni nzuri na zinarahisisha kazi katika uchukuaji wa picha, pia zinapunguza gharama ambazo zingeweza kutumika kwa kutumia ndege ndogo kupiga picha angani, tatizo hazina teknolojia ya kuziongoza, ni vyema watengenezaji wa hiki kifaa waje na mfumo wa mawasiliano na wa kuwezesha kuonekana kwenye mifumo ya kuonekana (Trucking system) kama ilivyo kwa nchi nyingine,” alisema Nziku.

Meneja wa TACC wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Mwanajumaa Kombo, alisema mamlaka inakabiliwa na changamoto ya ufinyu wa bajeti ambapo kwa sasa mabadiliko ya teknolojia yanawataka waongoza ndege kupata mafunzo mara kwa mara ili kuendana na teknolojia.

“Inatakiwa hawa waongoza ndege wapate mafunzo mara kwa mara, lakini tunashindwa kutokana na bajeti kuwa ndogo, haitoshelezi japokuwa tunajitahidi kuwapa mafunzo kwa uchache,” alisema Mwanajumaa.

Katika kuadhimisha siku hiyo, chama hicho kimetoa msaada wa cherehani tano kwa wafungwa wa gereza la Ukonga zenye thamani ya Sh milioni 1.7 ili kuwasaidia katika shughuli za ushonaji.
 
Kapicha mkuu
Ndo haka kadude
101821536-d801d9db-f919-4300-95ba-0b3bd54ee521.jpg
 
Hao Traffic Controllers ina maana hawajui hata TCAA mamlaka ya Anga nchini ambayo ndio Mamlaka inayowasimamia ilishatoa amri kwa barua na matangazo nchi nzima kuwa mtu yeyote anayetaka kutumia drone anatakiwa kuomba kibali na kusajiliwa na Mamlaka ya Anga, yaani TCAA.. sasa hawajui kitu gani wakati mamlaka inalishughulikia.. Alafu hapa kwetu, drones hazipo nyingi wala sio changamoto kubwa hata kidogo..
 
Kujijweza na kutafuta sababu na visingizio tu. Nani mwenye drone yenye uwezo was kupaa mpaka ndege zinakipita huko juu. Hata hivyo hapa hatuna air traffic kubwa sana mpaka drone zionekane tishio. Pia hatuna done nyingi za kuleta madhara
 
Sio drone hizo za Coco Beach jamani , Ni drone ambazo zinaweza kubeba na silaha ningepata kapicha ningeweka.
 
Hao Traffic Controllers ina maana hawajui hata TCAA mamlaka ya Anga nchini ambayo ndio Mamlaka inayowasimamia ilishatoa amri kwa barua na matangazo nchi nzima kuwa mtu yeyote anayetaka kutumia drone anatakiwa kuomba kibali na kusajiliwa na Mamlaka ya Anga, yaani TCAA.. sasa hawajui kitu gani wakati mamlaka inalishughulikia.. Alafu hapa kwetu, drones hazipo nyingi wala sio changamoto kubwa hata kidogo..
Subiri uchaguzi uishe wewe utaziona tu.
 
Kujijweza na kutafuta sababu na visingizio tu. Nani mwenye drone yenye uwezo was kupaa mpaka ndege zinakipita huko juu. Hata hivyo hapa hatuna air traffic kubwa sana mpaka drone zionekane tishio. Pia hatuna done nyingi za kuleta madhara
Ndege inapita kwenye usawa wowote inategemea na stage iliyopo. Kuna wakat inapata na wakat wa kutua pia. Pia Luna ndege zinaruka urefu mfupi kama zile zinazotumika kwenye kilimo etc.
 
Kujijweza na kutafuta sababu na visingizio tu. Nani mwenye drone yenye uwezo was kupaa mpaka ndege zinakipita huko juu. Hata hivyo hapa hatuna air traffic kubwa sana mpaka drone zionekane tishio. Pia hatuna done nyingi za kuleta madhara
Hapa kwetu tuna vindege vya kuhesabu na hata hizo drones wanaozijua na watumiaji wake pia bado ni wachache. Hivi huko kwa wenzetu (wenzetu kweli?) ambako kuna heavy air traffic na drones zisizo na idadi wao watasemaje?
 
KUWEPO kwa ndege nyuki (droni) imetajwa ni miongoni mwa changamoto wanazokabiliana nazo waongoza ndege nchini kutokana na teknolojia ya mawasiliano ya vifaa hivyo kutoonekana wakati vinaporushwa angani.

Hayo yalisemwa jana na Rais wa Chama cha Waongoza Ndege Tanzania (TACC), Shukuru Nziku wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya waongoza ndege duniani.

Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo Dar es Salaam jana, Nziku alisema pamoja na kuwepo kwa changamoto nyingi katika utendaji kazi wao, uwepo wa droni umeonekana kuwa na changamoto kubwa, hivyo kuhatarisha usalama wa ndege angani.

Alisema kifaa hicho kinachotumika kurahisisha kazi kama ujenzi wa miundombinu na upigaji picha za kawaida katika maeneo mbalimbali nchini, wanashindwa kukifuatilia kutokana na kutoonekana kikiwa angani.

“Hii ni changamoto kubwa kwa hizi ndege ambazo hazina rubani ndani, kwakuwa waongoza ndege hawazioni katika satellite, japokuwa sheria ya mwaka 2018 inazuia kifaa hicho kurushwa angani na endapo zitaruka basi kuwepo na mawasiliano ya redio na waongoza ndege, hii ni ngumu kwakuwa hiki kifaa hakina rubani, kinaongozwa na mtu aliyepo chini,” alisema Nziku.

Alisema hivi sasa droni ni nyingi na zinatumiwa kwa shughuli mbalimbali, lakini ni hatari zinapokuwa angani kutokana na kuweza kugongana na ndege kwa kuwa nyingine zinatakiwa kuruka juu zaidi ili kuona eneo kubwa.

Nziku alisema nchi kama Australia kifaa hicho kimesababisha majanga kwa ndege, hivyo wanafanya jitihada ya kutafuta namna ya kuzifanya zitumike pasipokuleta madhara kwa ndege zinapokuwa angani.

“Japokuwa ni nzuri na zinarahisisha kazi katika uchukuaji wa picha, pia zinapunguza gharama ambazo zingeweza kutumika kwa kutumia ndege ndogo kupiga picha angani, tatizo hazina teknolojia ya kuziongoza, ni vyema watengenezaji wa hiki kifaa waje na mfumo wa mawasiliano na wa kuwezesha kuonekana kwenye mifumo ya kuonekana (Trucking system) kama ilivyo kwa nchi nyingine,” alisema Nziku.

Meneja wa TACC wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Mwanajumaa Kombo, alisema mamlaka inakabiliwa na changamoto ya ufinyu wa bajeti ambapo kwa sasa mabadiliko ya teknolojia yanawataka waongoza ndege kupata mafunzo mara kwa mara ili kuendana na teknolojia.

“Inatakiwa hawa waongoza ndege wapate mafunzo mara kwa mara, lakini tunashindwa kutokana na bajeti kuwa ndogo, haitoshelezi japokuwa tunajitahidi kuwapa mafunzo kwa uchache,” alisema Mwanajumaa.

Katika kuadhimisha siku hiyo, chama hicho kimetoa msaada wa cherehani tano kwa wafungwa wa gereza la Ukonga zenye thamani ya Sh milioni 1.7 ili kuwasaidia katika shughuli za ushonaji.
hawaijui drone mkuu
 
Changamoto kubwa ni kutokuendana na teknoloji. Vifaa vyao vimepitwa na wakati.
 
Back
Top Bottom