Drone, Nyambizi za Iran zapiga picha manowari ya US

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,809
34,193
4bk13a8922bf1a33bg_620C350.jpg

Ndege isiyo na robani (drone) ya kipelelezi ya Jeshi la Wanamaji la Iran imeruka juu ya manowari yenye mitambo ya hali ya juu ya Marekani katika Ghuba ya Uajemi na kuchukua picha wakati wa luteka inayoendelea katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Fars, drone hiyo iliweza kuchukua picha za video wakati wa oparesheni ya kuipeleleza meli hiyo ya kisasa ya kivita ya Marekani.

Wakati huo huo, nyambizi ya wanamaji wa Iran ijulikanayo kama Ghadir nayo pia imefika karibu na manowari hiyo ya Marekani kwa lengo la kuipeleleza na pia kuchukua picha chini ya maji.

Imearifiwa kuwa nyambizi hiyo ya Iran imefanikiwa kuchukua picha safi pasina wanajeshi walioko kwenye meli hiyo ya kivita ya Marekani kutambua kuwa manowari hiyo ilikuwa inapelelezwa.

Siku ya Jumatano Jeshi la Majini la Iran lilianza mazoezi ya siku kadhaa katika eneo pana Ghuba ya Uajemi, Lango Bahari la Hormuz na Bahari ya Hindi, kusini mwa Iran.

Kamanda wa Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Admeli Habibullah Sayyari amesema lengo la mazoezi hayo ya jeshi la majini la Iran yaliyopewa jina la ‘Velayat 94’ ni kudhihirisha uwezo wa kujilinda na chokochoko za maadui sambamba na kutuma ujumbe wa amani na urafiki kwa nchi za eneo hili kuwa vikosi hivyo vina uwezo wa kukabiliana na uvamizi wa maadui.

subutu yake hata gadafi alisema hayahaya.irani ni sawa na simimizi kwa u.s.a mwarabu hana technologia yoyote
 
Tuache utani jamani, Iran walipigana na Saddam miaka kibao vita ikaisha bila pande zote mbili kushinda. Jiulize US walichukua siku ngapi kumtoa Saddam? Halafu leo hii Iran inajitutumua! Shauri yao, kwa jinsi navyowajua wa marekani wanaweza wakawa wanatafuta sababu za kuwachapa.
 
Iran ilipigana peke yake kwa miaka minane na Iraq ikisaidiwa na dunia nzima ikiwemo Marekani,mosi.
Pili,kushinda vita si kuua watu na kuharibu miundombinu,kushinda vita ni kutimiza malengo ya vita kwa upande mmoja au kuzuia malengo ya vita kwa upande wa pili,ss je Iran ilishinda vita,ndiyo kwa sbb lengo la Iraq lilikua ni kuipundua serikali ya kimapinduzi iliyompindua Mfalme Shah ambayo ilikua haijatimiza hata mwaka,lkn Iran iliweza kuzuia lengo hilo la adui aliekua na silaha za kisasa kutoka Marekani na hadi Leo ndiyo serikali inayotawala Iran,hivyo Iran ilishinda vita ile
 
Tuache utani jamani, Iran walipigana na Saddam miaka kibao vita ikaisha bila pande zote mbili kushinda. Jiulize US walichukua siku ngapi kumtoa Saddam? Halafu leo hii Iran inajitutumua! Shauri yao, kwa jinsi navyowajua wa marekani wanaweza wakawa wanatafuta sababu za kuwachapa.

Katika vita ya miaka 8 kati ya Saddam Husein(R.I.P-Iraq) na Iran ambavyo viliisha bila mshindi, Iraq alikua supplied na silaha za maangamizi kama zile za Chemikali kutoka US, hata hivyo bado Iran aliwadhibiti. Na ndiyo maana US walipokuwa wanampiga Saddam walikomaa kuwa ana silaha za maangamizi kwa kuwa walijua walimpa za kutosha ili kumuangamiza Iran. Hivyo kusema kirahisi tu kuwa Iran ni sisimiz ni kweli lakini siyo kiuwepesi hivyo.
 
Iran inanunua drone....marekani anatengeneza mwenyewe , lkn hata iraq walikua na maneno kama haya lkn marekani akatumia siku kadhaa tu.

Siyo kweli kuwa alichukua siku kaDhaa, huo ni uongo. Kama una kumbukumbu Gulf War I ilipiganwa miaka ya 90 kati ya Iraq(Saddam) na US na Allies wake(Bush Sr). Ni vita kali kabisa kwa wakati ule US ilibidi atafute namna isitishwe kwanza, ndipo Iraq aliwekewa ban/vikwazo ya kununua silaha au kitu chochote, hivyo alipodhoofika na Sanctions ikawa ni rahisi kwa Bush Mtoto kumaliza mchezo. Hivyo ni uongo mkubwa kusema ilikua rahisi kwa US kumaliza mchezo. Ni fitina pekee ilitumika kuishinda Iraq kwani kama kawaida US huwaambia Washirka wake wasiruhusu kufanya biashara yoyote na Iraq, na ndiyo maana tunasea US ikikuwekea vikwazo ujue washirika wake wote wataunga mkono(maana kuna uzi humu JF unaozungumzia uwezekano wa Sanctions kwa Tanzania hasa juu ya issue ya Zanzibar)!

Hivyo Iran huwez kuibeza, na drones za Iran zinatengenezwa na wanasayansi wake wenyewe walioiba ujuz maeneo tofauti funiani.

Issue hii kama ilivyoabdikwa humu JF nimeisikia saa1 asubuhi kwenye taarifa ya habari Radio One Stereo, hivyo ni habari genuine kabisa!
 
IRAN ina tengeneza Drone zake mwenyewe...haijawai nunua drone ata moja zaidi inatengeneza aina zaidi ya 10 ya hizi ndege zisizo rubani...Ata hiyo submarine au nyambizi Ghadir ni IRAN made na inaogopeka sana kwani haitoi kelele hivyo kua balaa japo sio kubwa lakini ina 120 ton ambapo inabeba silaha zijulikanazo km torpedo au underwater missile ambapo ni rahisi sana kuzamisha meli vita au tanker..rejea Northkorea ilivyozamisha meliVita ya southkorea na kuua wanajeshi wake....so hizi nyambiz ndogo ni balaa
 
Iran bado anahitaji muda kufikia level ya kushindana na US, kama Israel pekee ahafanya missions ndani ya Iran na kuua watu bila kupata upinzani wowote toka kwa Iran, ubora wake uko wapi??
 
Tuache utani jamani, Iran walipigana na Saddam miaka kibao vita ikaisha bila pande zote mbili kushinda. Jiulize US walichukua siku ngapi kumtoa Saddam? Halafu leo hii Iran inajitutumua! Shauri yao, kwa jinsi navyowajua wa marekani wanaweza wakawa wanatafuta sababu za kuwachapa.
Unajidanganya
Hujui lolote kuhusu vita ile
Kulikuwa na washirika kibao wa marekani
 
Back
Top Bottom