Drogba: Nataka Kuichezea Ac Milan

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,720
21,779
Drogba: Ninataka kuichezea AC

LONDON, England

MSHAMBULIAJI wa Chelsea, Didier Drogba ameweka wazi kwamba Chelsea walimzubaisha: Ndoto yangu ni kuitumikia AC Milan.

Mshambuliaji huyo amekiri wiki moja kabla ya Chelsea 'Blues' kucheza na Manchester United katika mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Lakini, Moscow inawezekana ikawa ni mara ya mwisho kwa Drogba kuichezea Chelsea baada ya kuelekeza kwamba alikutana na mchezaji mkongwe wa Milan, Paolo Maldini na maofisa wa klabu hiyo mwanzoni mwa msimu uliopita kabla ya jaribio la kutaka kumnunua.

Drogba alisema: “Wachezaji wengi ndoto zao ni kusaini AC Milan. Nilimweleza Paolo Maldini kwamba Milan ni klabu ambayo ninapenda kujiunga nayo.”

Katika maelezo yake, Drogba aliweka wazi kwamba alisafiri mpaka Milan kwa kutumia ndege ya kukodi.

Baada ya kuwasili, alikutana na Milan’s vice-president Adriano Galliani, ambaye alimuuliza ‘Lini utahitaji kuichezea Milan?’

Drogba alijibu: “Wakati wowote utakaotaka, yote ni juu yako, ukiwa na pesa tayari nenda kawaone Chelsea.”

Siku iliyofuata, Galliani aliwasiliana na Blues tkwa nnia ya simu kujua ofa yao.
 
Biashara hiyo let him go.. Blue they can do it without him

inaonekana jamaa kashachoka na klabu and its only fair to cut him loose otherwise he might not deliver.Mbali na yote hayo, the gentleman has done the blues a lot of proud na heshima yake anastahili!
 
He is a man and he has to determine his destine.
All the best kijana uko uendako ila upunguze misifa
 
Naamini Drogba anasubiria Mourinho akabidhiwe Timu ili amfuate. Ac Milan ni kama njia tuuu ya kutoa taarifa kwamba hawezi kuendelea kukaa Chelski.
 
Aende Tuu Ac Hakuna Kumzuiaa Ingawa Ndio Mpika Mabao Mkuu Wa The Blues..hakuna Kumzuiaa..muda Wake Umeshakwisha......nenda Drogba Nenda Baba,ila angalia sana viatu huko Italy..ukiwa majeruhii na mpira wenyewe wa mazoezii huoo..........utajikuta unaishiaa kustaafu ukiwa majeruhii................
 
Tumowmbee Mungu Yasije Mkuta Yakina Owen ,,,thienry Na Wengineo Wakasaaaulika Kabisa Ulimwengu Wa Soka Kazi Ipo..mungu Akubariki Uendako Kaka.....
 
Jamaa anatikisa kiberiti anataka aongezewe mshahara
 
Tusisahau kwamba Drogba ana miaka 30 sasa na ni lazima ameanza kufikiria kupumzika sasa lakini kwa kuongeza sifa kwenye CV yake.
 
I have always thought Drogba was in his mid twenties, Anyways I think angeendelea kubaki Chelsea maana mpira wa Italy nao unataka moyo asijekuwa majeruhi kila baada ya miezi mitatu.awaulize akina Ronaldo, Marco Van Basten.
 
Drogba: Ninataka kuichezea AC

LONDON, England

MSHAMBULIAJI wa Chelsea, Didier Drogba ameweka wazi kwamba Chelsea walimzubaisha: Ndoto yangu ni kuitumikia AC Milan.

Mshambuliaji huyo amekiri wiki moja kabla ya Chelsea 'Blues' kucheza na Manchester United katika mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Lakini, Moscow inawezekana ikawa ni mara ya mwisho kwa Drogba kuichezea Chelsea baada ya kuelekeza kwamba alikutana na mchezaji mkongwe wa Milan, Paolo Maldini na maofisa wa klabu hiyo mwanzoni mwa msimu uliopita kabla ya jaribio la kutaka kumnunua.

Drogba alisema: “Wachezaji wengi ndoto zao ni kusaini AC Milan. Nilimweleza Paolo Maldini kwamba Milan ni klabu ambayo ninapenda kujiunga nayo.”

Katika maelezo yake, Drogba aliweka wazi kwamba alisafiri mpaka Milan kwa kutumia ndege ya kukodi.

Baada ya kuwasili, alikutana na Milan’s vice-president Adriano Galliani, ambaye alimuuliza ‘Lini utahitaji kuichezea Milan?’

Drogba alijibu: “Wakati wowote utakaotaka, yote ni juu yako, ukiwa na pesa tayari nenda kawaone Chelsea.”

Siku iliyofuata, Galliani aliwasiliana na Blues tkwa nnia ya simu kujua ofa yao.

"When people think of Italy, after the mafia and pizza, they think of AC Milan"
 
Drogba umri haudanganyi baba! Nia haizeeki lakini mwili unazeeka! Mwili ukizeeka hauwezi tena kutekeleza matakwa ya nia! Hapo MTU anabaki anauma kidole tu!
Nia unayo lakini haitekelezeki! Pumzika baba Drogba! Labda ukocha!
 
Umesoma hii ni post ya lini?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom