Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 55,881
- 29,246
Drogba: Ninataka kuichezea AC
LONDON, England
MSHAMBULIAJI wa Chelsea, Didier Drogba ameweka wazi kwamba Chelsea walimzubaisha: Ndoto yangu ni kuitumikia AC Milan.
Mshambuliaji huyo amekiri wiki moja kabla ya Chelsea 'Blues' kucheza na Manchester United katika mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Lakini, Moscow inawezekana ikawa ni mara ya mwisho kwa Drogba kuichezea Chelsea baada ya kuelekeza kwamba alikutana na mchezaji mkongwe wa Milan, Paolo Maldini na maofisa wa klabu hiyo mwanzoni mwa msimu uliopita kabla ya jaribio la kutaka kumnunua.
Drogba alisema: Wachezaji wengi ndoto zao ni kusaini AC Milan. Nilimweleza Paolo Maldini kwamba Milan ni klabu ambayo ninapenda kujiunga nayo.
Katika maelezo yake, Drogba aliweka wazi kwamba alisafiri mpaka Milan kwa kutumia ndege ya kukodi.
Baada ya kuwasili, alikutana na Milans vice-president Adriano Galliani, ambaye alimuuliza Lini utahitaji kuichezea Milan?
Drogba alijibu: Wakati wowote utakaotaka, yote ni juu yako, ukiwa na pesa tayari nenda kawaone Chelsea.
Siku iliyofuata, Galliani aliwasiliana na Blues tkwa nnia ya simu kujua ofa yao.