EMT
Platinum Member
- Jan 13, 2010
- 14,483
- 15,308
Chama cha Soka cha Uturuki kimewaita wachezaii wawili wa Ivory Coast, Didier Drogba and Emmanuel Eboue ili kuwaadhibu kutokana na kutenda kosa la kuvaa na kuonyesha uwanjani nguo zinazomkumbuka na kumshukuru Mandela. Wachezaji hao walionyesha nguo zao za ndani zenye maandiko ya kumkumbuka na kumshukuru Mandela kwenye mechi kati ya Galatasaray na B Elagizspor kumalizima.
Chama cha soka cha Uturuki hakiruhusu wachezaji kuvaa nguo zinazoonyesha maandiko yenye ujumbe wa kisiasa, kidini, kibiashara au maandiko binafsi. Hii ni kwa mujibu wa sheria ya FIFA inayokataza wachezaji to "reveal undershirts which contain slogans or advertising". Kwa mujibu wa sheria hiyo, "basic equipment must not contain any political, religious, or personal statements".
Sheria hiyo inaendelea kusema kuwa mchezaji ambaye atakiuka sheria hii ataadhibiwa na waandaji na wa shindano husika. Pia timu anayochezea mchezaji husika nayo itaadhibiwa na FIFA au waandaji wa shindano husika. Aidha sheria inamtaka refa aweke kosa hilo kwenye taarifa yake baada ya mechi.
[video=youtube_share;4pM0MjRznHg]http://youtu.be/4pM0MjRznHg[/video]