Dreamliner Economics-Gharama za uendeshaji wa dreamliner

ubongokid

JF-Expert Member
Apr 30, 2017
2,018
3,874
Kwa kawaida kila aina ya ndege ina gharama za uendeshaji ambao ndio kigezo kinachotumika katika kufanya maauzi ya kununua aina fulani ya ndege.
Kwa mujibu wa takwimu mbalimbali gharama za kuendesha dreamline kwa lisaa limoja ni kama dola 8000 hivi sawa na Milioni 18 kwa lisaa.Iwapo itabeba wastani wa watu 330 basi gharama ya kila mtu kwa lisaa limoja ni Shiling 54000 hapo ni bila kuweka kodi za serikali,mishahara ya wafanyakazi na ndege ijae kabisa,

Kila atakapopungua mtu mmoja basi gharama itaongezeka kwa wastani wa shilingi 165 kwa kila abiria aliesalia mpaka ifike mara mbile yake kwa idadi ya abiria 165 na mara tatu yake kwa idadi ya abiria 100.Kwa maana nyingine ili dreamline iruke na watu 100 kwa lisaa limoja gharama kwa kila mtu ni shilingi 180,000 bila kulipa kodi yoyte ile na bile kuweka faida na kulipa wafanyakazi mishahara.

Gharama ya kupata abiria mmoja wa anga kwa wastani ni Shiling 8000 hadi 15000 kwa sababu ya mifumo ya kuuzia,matangazo commision.n.k.Ukiongoze hii katika 180,000 pamoja na kodi unapata kama shilingi 225000 kwa watu mia.Ukiweka na bima na gharama nyingine unaweza fikia TZS 275000 kwa abiria 100 tu ambapo utaweza kuirusha tu ndugu na kulipa kodi bila kulipa mishahara na kutengeneza faida.

Ukioneza gharama za mishahara na faida kiduchu basi unaweza kuhitajika kuuza tiketi kwa gharama ya TZS 325000 na 375000 kwa mtu mmoja na hapo unakuwa katika kitu tunaita tight margins.

Iwapo ndege itaruka na chini ya abiria 100 na hawa wakilipa chini ya 375000 basi inaanza kuingiza hasara.Sio kwamba watu wakilipa 375000 ndo wanapata faida hapana ili dreamliner itengeneze faida basi anagalu tulip laki 4 na kuendelea

Kwa hi basi ushauri wangu ni huu.Watanzania tuwe wazalendo tupande ndege zetu na tujitahidi kulipa premium fare ili angalau shirika letu liweze kujiendesha Lisje kututia hasara.
 
Chadema mnajifanya kila kitu mnajua ila sijui kwa nini mmeshidwaje kujenga hata choo cha ofisi ya makao makuu ya chadema licha ya kupata ruzuku ya bilioni tatu kwa mwaka?
 
Chadema mnajifanya kila mnajua ila sijui kwa nini mmeshidwaje kujenga hata choo cha ofisi ya makao makuu ya chadema licha ya kupata ruzuku ya bilioni tatu kwa mwaka?
Mkuu tunataka tununue dreamliner ya chama kwanza
 
Nauli ya dala dala tu na mabasi kwa watanzania ni shida, alafu unaongelea nauli za malaki kujaza dreamliner?
 
Unajua sisi waTanzania ni watu waelewa sana na tuko radhi kulipa hio premium price kwa sharti kwamba mahesabu ya ATCL yawekwe wazi na CAG ayakague.Siwezi kuweka pesa yangu wakati sina uhakika inatumbukia chooni au inakwendamahali salama.
 
Kwa kawaida kila aina ya ndege ina gharama za uendeshaji ambao ndio kigezo kinachotumika katika kufanya maauzi ya kununua aina fulani ya ndege.
Kwa mujibu wa takwimu mbalimbali gharama za kuendesha dreamline kwa lisaa limoja ni kama dola 8000 hivi sawa na Milioni 18 kwa lisaa.Iwapo itabeba wastani wa watu 330 basi gharama ya kila mtu kwa lisaa limoja ni Shiling 54000 hapo ni bila kuweka kodi za serikali,mishahara ya wafanyakazi na ndege ijae kabisa,

Kila atakapopungua mtu mmoja basi gharama itaongezeka kwa wastani wa shilingi 165 kwa kila abiria aliesalia mpaka ifike mara mbile yake kwa idadi ya abiria 165 na mara tatu yake kwa idadi ya abiria 100.Kwa maana nyingine ili dreamline iruke na watu 100 kwa lisaa limoja gharama kwa kila mtu ni shilingi 180,000 bila kulipa kodi yoyte ile na bile kuweka faida na kulipa wafanyakazi mishahara.

Gharama ya kupata abiria mmoja wa anga kwa wastani ni Shiling 8000 hadi 15000 kwa sababu ya mifumo ya kuuzia,matangazo commision.n.k.Ukiongoze hii katika 180,000 pamoja na kodi unapata kama shilingi 225000 kwa watu mia.Ukiweka na bima na gharama nyingine unaweza fikia TZS 275000 kwa abiria 100 tu ambapo utaweza kuirusha tu ndugu na kulipa kodi bila kulipa mishahara na kutengeneza faida.

Ukioneza gharama za mishahara na faida kiduchu basi unaweza kuhitajika kuuza tiketi kwa gharama ya TZS 325000 na 375000 kwa mtu mmoja na hapo unakuwa katika kitu tunaita tight margins.

Iwapo ndege itaruka na chini ya abiria 100 na hawa wakilipa chini ya 375000 basi inaanza kuingiza hasara.Sio kwamba watu wakilipa 375000 ndo wanapata faida hapana ili dreamliner itengeneze faida basi anagalu tulip laki 4 na kuendelea

Kwa hi basi ushauri wangu ni huu.Watanzania tuwe wazalendo tupande ndege zetu na tujitahidi kulipa premium fare ili angalau shirika letu liweze kujiendesha Lisje kututia hasara.

ubongokid
Mkuu tutafutie gharama za kuendesha SGR ya umeme.
 
Back
Top Bottom