Dream Team: Sitta, Magufuli, Mwakyembe na Urais wa 2015

Hakuna mtu yeyote ndani ya ccm anayefaa kuwa Rais wa nchi hii. Hii ni kwa sababu tatizo la CCM siyo kikwete wala nani, Tatizo ni sera. Ufisadi kwa mfano ndani ya CCM ni sera. Huyo magufuli unayemsema hawezi kwenda kinyume na sera za chama chake. Muulizeni Nape kilichompata akafyata mkia kuzungumzia ufisadi ndani ya chama. Aliitwa na bw mkubwa akapewa karipio kali sana kwa nini anaenda kinyume na sera ya chama. Tangu hapo Nape Kimyaaaaaaaaaaaa mafisadi wanapeta.
 
Sipati picha kama Magufuli akiwa Rais itakuwa balaa huyu jamaa naweza kusema wote saa kumi na mbili jioni tuwe tumelala na ikawa hivyo!
 
Lowassa sasa hivi ana nguvu kweli kweli

Ndo atapita kwa ccm

Leo niseme openly, Lowassa anafaa saaaaana, nampenda saaana, ni kiongozi, period, kataeni, mkubali, anafaaa kuwa rais, ila maskini Richmond sijui ndio imemchafua/ kabebeshwa mzigo, nilipatwa na huruma kuuuuuu kumwona akiachia uPM, kwani ni mtendaji kazi kweli, ee Mungu huyu Lowassa zaidi ya Richmond kwani mbona miaka yote sikusikia ana tuhuma zozote, ila kama akipitishwa na CCM Lowassa anayo kura yangu, my standing here is very clear, ni mchapa kazi, hacheki na hapendi ujinga, Mungu msaidie Lowassa au Magufuli 2015.
 
Soma tena post yangu kabla haujakurupuka kujibu, nimeuliza waziri sijauliza Rais.

We wa wapi, umekosea swali! Mimi nimekupa jibu sahihi, hivyo wewe badili swali lako kama una kiriba cha roho mbaya kwa Pombe uwe muwazi. Mbona alipo agiza mabango ya RA yatotelewe kwenye reserve ya barabara uliona makombola yalitokea wapi?

Pombe alikwisha sema yeye ni sawa na houseboy, akiambiwa na boss wake fagia atafagia, akiambiwa acha leo pumzika, tatekeleza! Mlaumu Boss wake siyo yeye kwenye issue za collective agreement!
 
Labda wewe mwenzangu unaejuwa zaidi unisaidie tu, kama waziri hakubaliani na yale anayotaka Rais, anatakiwa achukuwe uwamuzi gani?
 
Umesahau sifa yake moja katika utendaji wake wa kazi, kwamba alisimamia kwa uwezo wake wote uuzwaji wa nyumba za serikali kwa watu wake na marafiki zake. Kweli anafaa sana kuwa rais wakati ujao. Itafaa sana kama ataiuza hata Ikulu yenyewe atakapo utwaa urais.
 
CCM hata wamsimamishe mtoto wa mwl nyerere hapiti! Watu wamechoshwa na huu mchama. Muulizeni Nape huko Sumbawanga kawahutubia kina nani, au tafuteni mwanachi ya leo.
 
Wana CCm wana tabia ya kuwaogopa viongozi wao hivyo mgombea anayeungwa mkono na rais aliyeko madarakani ndiye atakayepita na la ikishindikana mtandao wenye hela ndio utakaotoa mgombea na ikishindikana Chama kitagawanyika na hivyo kuwa na CCM A na CCM B. ikumbukwe hakuna Nyerere wa kumkemea yeyote. tusubili tuone. Angalia pia ukanda wa Pwani ulivyojimilikisha utawala:
1985 - 1995 A.H. Mwinyi - Pwani (Zanzibar)
1995 - 2005 W.B. Mkapa - Pwani (Mtwala)
2005 - 2015 J.M. Kikwete - Pwani (Pwani)
2015 - H.A.H. mwinyi - Pwani (Zanzibar) - kumbuka UVCCM Pwani waliishasema mgombea urais kupitia CCM 2015 anamjua kikwete pia refer wajumbe wa CC baada ya kujivua gamba.

Ili ndoto za mtu kama Mwandosya, Lowasa, Maghufuli n.k zitimie si kuptia CCM ya sasa, labda CCM nyingine.

Source: Self political analyizer.
 
Magufuli ni kati mafisadi ambao wanadtahili hata kupelekwa mahakamani au mmesahau ya kwamba ndie aliyekuwa kinara wa kupora nyumba za serikali

Tena moja ya kwake mwenyewe. Mambo yote lowasa. Magufuli ataiponza ccm hajui kugawa kanga, fulana, kofia na vibaasha, ataamrisha watu wampigie kula.:smow:
 
nazani umetumwa na samweli sitta mwanzilishi wa ccj aliyeifisadi cda dodoma mpaka ikafirisika

Mkuu
Kwa mawazo yangu tatizo la CDA tutamwonea tukilitupia kwa Samweli sita. CDA ilishindikana wakati wa neema Sir George Kahama akiwa ndo kizito pale, sasa hawa kina sita na kimario tutawaonea "always kamba hukatikia pabovu".
 
Mlishaambiwa JK ana mtu wake Asha Rose Migiro au Hussein Mwinyi hamtaki kuelewa tu!!!!! Yeye mwenyewe wala Chama chake, si nape hata Ridhiwani hawajakanusha. Sasa ninyi mnatutajia Makafili waongoze hii nchi, thubutu.... tunamwachia nchi mtu wetu.

Anyway mimi nawasilisha tu katika kunogesha mjadala. Sio muumini wa dini na siasa at a go. Naamini katika uongozi imara wa nchi na watu wake bila kubagua.
 
Anko Sam said:
We wa wapi, umekosea swali! Mimi nimekupa jibu sahihi, hivyo wewe badili swali lako kama una kiriba cha roho mbaya kwa Pombe uwe muwazi. Mbona alipo agiza mabango ya RA yatotelewe kwenye reserve ya barabara uliona makombola yalitokea wapi?

Pombe alikwisha sema yeye ni sawa na houseboy, akiambiwa na boss wake fagia atafagia, akiambiwa acha leo pumzika, tatekeleza! Mlaumu Boss wake siyo yeye kwenye issue za collective agreement!

Anko Sam,

..hoja kwamba Magufuli alikuwa anatekeleza uamuzi wa Mkapa au Cabinet ktk kuuza nyumba za serikali kwa bei poa haina uzito.

..tukiendelea namna hiyo mafisadi watakuwa wanatuhujumu halafu wanasingizia kwamba wametumwa na Raisi, au ni maamuzi ya Cabinet.

..uamuzi ule ulikuwa hauna maslahi kwa taifa letu na kama Magufuli alikuwa hakubaliani nao alipaswa kuupinga na kujiuzulu nafasi yake.

..tatizo la Magufuli siyo kutekeleza uamuzi ule mbaya, bali kwenda kinyume na maelekezo ya baraza la mawaziri kwa kuwauzia nyumba hata wale ambao "hawakustahili" mfano vimada na ndugu zake wa karibu.

..Mkapa is no longer in power, kama Magufuli anadai alilazimishwa na Raisi[Mkapa] kuuza nyumba za serikali, basi anaweza kutubu mbele ya wa-Tanzania wenzake kwa kurudisha nyumba aliyojiuzia yeye binafsi na zile alizouzia vimada na ndugu zake.

NB:

..Magufuli pia anatuhuma za kujipendelea[ukabila] kwa kupora mradi wa barabara toka eneo moja mkoani Kagera na kuuhamishia jimboni kwake.

..pia amesababishia serikali hasara ya bilioni 14 pale alipodharau ushauri wa wataalamu na kuvunja kituo cha mafuta kule Mwanza. suala hili lilipelekwa mahakamani na ikabainika kwamba Magufuli alikaidi ushauri wa wataalamu.
 
Mlishaambiwa JK ana mtu wake Asha Rose Migiro au Hussein Mwinyi hamtaki kuelewa tu!!!!! Yeye mwenyewe wala Chama chake, si nape hata Ridhiwani hawajakanusha. Sasa ninyi mnatutajia Makafili waongoze hii nchi, thubutu.... tunamwachia nchi mtu wetu.

Anyway mimi nawasilisha tu katika kunogesha mjadala. Sio muumini wa dini na siasa at a go. Naamini katika uongozi imara wa nchi na watu wake bila kubagua.

Hakuna bwana sisi tumeshashitukia mipango yao na Lowasa. Sasa mbona Mukama amefuta siku tisini?:pound:
 
Wana CCm wana tabia ya kuwaogopa viongozi wao hivyo mgombea anayeungwa mkono na rais aliyeko madarakani ndiye atakayepita na la ikishindikana mtandao wenye hela ndio utakaotoa mgombea na ikishindikana Chama kitagawanyika na hivyo kuwa na CCM A na CCM B. ikumbukwe hakuna Nyerere wa kumkemea yeyote. tusubili tuone. Angalia pia ukanda wa Pwani ulivyojimilikisha utawala:
1985 - 1995 A.H. Mwinyi - Pwani (Zanzibar)
1995 - 2005 W.B. Mkapa - Pwani (Mtwala)
2005 - 2015 J.M. Kikwete - Pwani (Pwani)
2015 - H.A.H. mwinyi - Pwani (Zanzibar) - kumbuka UVCCM Pwani waliishasema mgombea urais kupitia CCM 2015 anamjua kikwete pia refer wajumbe wa CC baada ya kujivua gamba.

Ili ndoto za mtu kama Mwandosya, Lowasa, Maghufuli n.k zitimie si kuptia CCM ya sasa, labda CCM nyingine.

Source: Self political analyizer.

Mkuu
Mimi nafikiri kigezo cha mtu ni uwezo alio nao wa kiutendaji, kama tukienda kwa kanda au majimbo, nina wasiwasi tuna jenga fikra za kikabila, tukitoka huko itabidi kuchunguza na kuchagua mtu kidini.
Tuchague kiongozi wa nchi kutokana na uwezo wake na wala siyo antoka wapi na dini gani.
Labda tatizo ambalo limetufikisha hapa ni uzoefu tulioupata wananchi kutokana na baadhi ya viongozi wetu. Ni hakika kabisa na wala sitafuni mdomo naposema kwamba hali ya kushamili udini ilianza tu mara Mzee Mwinyi alipoingia madarakani. Sasa hilo linatujengea wasiwasi ya kutoaminiana, kwa mtazamo wangu ninaimani kama Salim Ahmed angekuwa rais wa nchi asinge weza kuyumbishwa na hali ya udini.
Hivyo basi kigezo cha viongozi wetu sasa iwe ni uwezo wa mtu na si kabila wala dini yake. Ina ikibidi tunahitaji watu wajulikane mapema siyo dhambi kufanya hivyo ili itupe muda wa kuwachunguza na kuwajua. Tumeumizwa sana na watu tunaoletewa dakika za mwisho mwisho, ndo kwa maana watu wanakurupuka na kusema wameletewa "chaguo la Mungu baada ya siku mbili wananza kurushia mawe chaguo lao la Mungu".
 
Naunga mkono hoja.Kwa nchi yenye uvundo kama Tanzania you need an iron hand kama ya Magufuli.Tatizo la Magufuli hata hivyo ni kwamba, kwa jinsi alivyo, inaelekea sio Freemason.Kama hujui, ni kwamba huwezi kuwa kiongozi wa nchi yeyote duniani leo kama wewe sio Freemason.Wanataka mtu ambaye atawatii.So kama Magufuli sio Freemason asahau kuwa Raisi wa Tanzania.Freemasons ndio wanaoitawala dunia.
Kila mtu anamfahamu vilivyo kwa utendaji kazi, si ndugu yangu, si jirani, wala hanijui, ila nchi hii CCM wakitaka washinde uchaguzi bila wasiwasi let them select Magufuli to be a Presidential candidate 2015, najua wengi mtanisuta hapa, but truth itabaki pale pale, Magufuli ni mchapa kazi, ana maamuzi, target, na kutoa adhabu kwa wazembe wote, ni mfanyakazi wa namna ya Magufuli ndiye anayatakiwa kwa sasa kuongoza nchi, ni miaka michache kipindi cha uongozi wa Mkapa alitoa amri, wafanyakazi wote waliochukua magari ya serikali na kujimilikisha na
kubadili plate namba immediately warudishe, tuliona, magari maelfu kwa maelfu yakirudishwa, leo hii barabara zote give it 3 yrs mtaniambia, utaona zimejengwa, haletewi report ofisini, ni mfuatiliaji na mtendaji, ni kiongozi, as we know most candidate before election they pretend to be Servant but soon after winning election they turn to be Masters, that is not for Magufuli, kila wizara aliyopewa aliinyoosha, he will be a right presidential candidate for 2015, CCM chukueni huu ushauri wangu, otherwise itakula kwenu, kwani Lowassa kashachafuka kila kona though ni mtendaji kweli Magufuli type, Magufuli wish u bright days to come ahead.
 
Mkuu
Kwa mawazo yangu tatizo la CDA tutamwonea tukilitupia kwa Samweli sita. CDA ilishindikana wakati wa neema Sir George Kahama akiwa ndo kizito pale, sasa hawa kina sita na kimario tutawaonea "always kamba hukatikia pabovu".

Mh...Sitta alichangia zaidi kuiua CDA aiseee!
 
Back
Top Bottom