Dream Team: Sitta, Magufuli, Mwakyembe na Urais wa 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dream Team: Sitta, Magufuli, Mwakyembe na Urais wa 2015

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Fareed, May 18, 2011.

 1. F

  Fareed JF-Expert Member

  #1
  May 18, 2011
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Nilikaa nikawaza tu,

  Mwaka 2010 niliamka asubuhi na mapema na kumpigia kura Dk. Willibrod Slaa wa CHADEMA kuwa Rais wa Tanzania. Yaliyotokea kwenye uchaguzi huo wote tunajua na tulishuhudia jinsi kura zetu zilivyoibiwa na Jakaya Kikwete wa CCM akatangazwa Rais kwa kura za wizi.

  Uchaguzi wa 2015 bado uko mbali. Sijui kama Dk. Slaa atagombea tena au la. Pia ni dhahiri kuwa kuna uwezekano mkubwa tu kuwa mgombea wa CCM mwaka 2015 akatangazwa tena kuwa Rais by any means necessary. Maandamano ya kudai katiba mpya haraka yako wapi? Tume ya kupitia katiba mpya mpaka leo haijaundwa, bado kuna referendum inatakiwa ifanyike nk. Sitashangaa uchaguzi wa 2015 ukifanyika chini ya katiba hii hii na mambo yakawa yale yale.

  Viongozi wa upinzani wako "bize" kutumika (knowingly and unknowingly) kwenye kampeni ya kuwasaidia mapacha watatu (Edward Lowassa, Rostam Aziz na Andrew Chenge) wasifukuzwe kutoka CCM.

  Kutokana na hayo yote, imenibidi niangalie uwezekano wa CCM kuutwaa Urais tena 2015.

  Wangeteuliwa (ingawa najua haiwezi kutokea) viongozi hawa hapa wa CCM kwenye nafasi hizi nyeti, kwa kweli ningepata wakati mgumu wa kufanya maamuzi kama niipigie tena kura CHADEMA au nihamie CCM safari hii:

  (The CCM Dream Team)

  Rais wa Tanzania -- Samuel Sitta

  Makamu wa Rais -- Omar Yusuf Mzee

  Waziri Mkuu -- John Magufuli

  Waziri wa Nishati na Madini -- Dr. Harison Mwakyembe

  Waziri wa Maliasili na Utalii -- Prof. Anna Tibaijuka

  Waziri wa Kilimo -- Dk. Enos Bukuku

  Waziri wa Fedha -- Dr. Asha-Rose Migiro

  Waziri wa Mambo ya Nje -- Bernard Membe/Juma Mwapachu

  Waziri wa Viwanda na Biashara -- Ali Mufuruki

  Watanzania wangepewa chaguo la Rais wao kuwa Dk. SLAA au SITTA, mpenda maendeleo yoyote angeweza kusema yoyote atakayeshinda Urais ni sawa tu.

  Ila Tanzania si taifa lenye bahati. Limekuwa na nuksi ya kutawaliwa na watawala wabovu na iliwahi kupata viongozi watatu tu wa kujivunia -- Mwalimu Juliua Nyerere, Edward Sokoine na Abeid Karume.

  Ingekuwa timu ya mpira, Tanzania ningeifananisha na ARSENAL FC ya Uingereza. So much potential, so much promise lakini si rizki. Ni ugonjwa wa moyo tu... Wacha niendelee kuota!
   
 2. l

  luhwege Member

  #2
  May 18, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 90
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Kweli unaota mchana
   
 3. annamaria

  annamaria Senior Member

  #3
  May 18, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 135
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wana ubavu wa kupenya primaries za chama?
   
 4. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #4
  May 18, 2011
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Nakubaliana na wewe FAREED kwa asilimia mia moja.

  Ni ukweli usiopingika kwamba mgombea urais wa CCM ndiye atakayetangazwa mshindi hata kama atakuwa amebwagwa na wa upinzani. Sababu ni wazi:

  Tume ya uchaguzi sio huru na hata 2015 haitakuwa huru. Itapewa maelekezo ya kumtangaza mgombea wa CCM kuwa rais. Sasa nini kifanyike? Watanzania lazima tuamke sasa kuhakikisha kwamba tunajenga mazingira ya kumpata rais bora na sio bora rais. Wote tumeona jinsi nchi yetu ilivyoyumba kwa kuchagua bora rais. Tusirudie makosa haya 2015. Hakika tutajuta!

  Nimeona wengi wanaojichomoza kutaka urais 2015 hawana tofauti kubwa na msanii huyu aliyepo Ikulu hivi sasa. Tunataka rais anayeguswa na umaskini wa Watanzania na ambaye atakuwa tayari kujitoa mhanga kulinusuru taifa letu.

  Mimi nina imani na SITTA na MAGUFULI. Hakika mmoja wao, au wote kwa pamoja wakishika hatamu ya uongozi wa juu wa nchi tutaona mabadiliko makubwa.
   
 5. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #5
  May 18, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Samuel Sitta si rahisi labda pawepo na Memorandum of Understanding katika yake na watuhumiwa wa ufisadi wanaotajwa sasa na ambao hawatajwi kwa sababu moja au nyingine kwamba hatafufua ya kale dhidi yao. Vinginevyo mimi namwona kama atafuata mkondo wa yule Raisi Marehemu wa Zambia dhidi ya watangulizi wake

   
 6. F

  Fareed JF-Expert Member

  #6
  May 18, 2011
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  SLAA vs SITTA would be a most fascinating contest kwa Urais wa 2015. Pamoja na kuichoka CCM kwa kushindwa kuleta maendeleo baada ya miaka 50 ya uhuru, ninaamini kwa moyo wangu wote kuwa yoyote atakayeshinda kati ya hao wawili kuwa Rais basi Tanzania itakuwa kheri zaidi kuliko ilivyokuwa katika miaka 10 hii ya kusikitisha chini ya utawala wa Kikwete.

  Wote SLAA na SITTA wana akili, ni wazalendo, waadilifu, wanachukia rushwa na wanakerwa na umasikini wa nchi licha ya utajiri wake mkubwa wa rasilimali. Hebu imagine kuwe na midahalo mitatu itakayotangazwa na TV na redio zote nchini huku SLAA vs SITTA wakipambana kuhusu sera na mwelekeo sahihi wa kuipeleka Tanzania kutoka kwenye utumwa wa umasikini fukara kwenda kwenye maendeleo.

  Magufuli/Tundu Lissu akiwa Waziri Mkuu na apewe madaraka yote ya nafasi yake Wallahi nchi hii ingenyooka.

  Ingekuwa ndoto zinaweza kutokea kweli. We acha tu!
   
 7. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #7
  May 18, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 738
  Trophy Points: 280
  hebu nenda dom mkuu...ukirudi usome ulichokiandika.
   
 8. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #8
  May 18, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  hawatapata nafasi ya kuunda serikali 2015 - kwa hiyo tusipoteze muda kujadili vitu ambacho havipo.

  kama ni kuota basi umeota ukitembea.
   
 9. Kitumbo

  Kitumbo JF-Expert Member

  #9
  May 18, 2011
  Joined: Jun 16, 2010
  Messages: 547
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Nakupa 15/100. In future jaribu kupangilia essey yako iwe na mtiririko mzuri wa habari, unapoelezea ubora wa kitu husisha na muono wako ni kwa nini unasema hiki au kile ni bora nk.
   
 10. s

  sativa saligogo Senior Member

  #10
  May 18, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 126
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waaah! :smow:Nakupongeza sana kwa vision yako, ww ni mnajimu!!! Huo ndio mwelekeo wa vua gamba!!! Lkn je Dr William Shija vp! Binafsi naamini ikitokea hivyo watz kwa mara yakwanza watashuhudia serkali ya kitaifa kama ilivyokuwa kwa Mandela !!! yaani DOUBLE-SS (Sitta-Slaa) kwa sababu wote wako serious !!! ukizingatia ni Standard and Speed (SS) hapo ndipo tunaweza kusema tanzania yenye neema tele inawezkana!! Hoja hazijengwi kwa maandamano ya cdm wala mipasho ya ccm!!!! CUF wameonyesha njia dialogue/nagotiation is best way of maintaining tranquility. WE NEED TO LEAVE IN TANZANIA IN PEACE NOT IN PIECES!!!!!

  LETS AVOID THE SOLIDARITY TO THE GRAVE!!! :mod:
   
 11. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #11
  May 18, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  unfortunately siamini katika SITTA....it is very unfortunate jamani!

  mix with yours
   
 12. s

  sativa saligogo Senior Member

  #12
  May 18, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 126
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  :tonguez:Kwa mara ya kwanza dunia itashuhudia mdahalo hot wa SITTA vs SLAA kama itakuwa kweli na mtangazaji atakuwa Shacka Sally!!! wATZ wa leo si wa jana!

  FABRICANDOR FIT FABER!!!
   
 13. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #13
  May 18, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  SITTA ni flip flopper mtu wa kususa chama kilimbwaga akataka aende CCJ sasa Kikwete angetaka kuhamia CUF/NCCR 1995 unafikiri angepewa urais??

  DR Asha Rose Migiro ni mtu mkubwa sana labda umuweke yeye Rais au PM otherwise haiwezekani!!!

  Magufuli ana ujuzi sana wa kukremu lakini utendaji I am not very sure
   
 14. m

  matunge JF-Expert Member

  #14
  May 18, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 346
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 60
  Nimeipenda. Ila Migiro,,,,,ungelimpa wizara nyingine
   
 15. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #15
  May 18, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Hadi kesho najiuliza, kwa Sitta jipya hasa ni nini?
  Waziri toka enzi za mzee Nyerere so what? amefanya nini katika maeneo aliyopita?
  Eti alikuwa speaker machachari, upuuuuzi.... hebu tuache kuliangalia hili taifa kwa jicho la unyonge as if tumeandikiwa kuwa masikini milele.
  Kwenye mjadala wa Tanzania kama taifa la WATU tunaotaka kuelekea kuwa taifa kubwa la viwanda na wafanyakazi pamoja na wafanyabiashara wakubwa, hamna cha Sitta, Mwakyembe wala Magufuli wote hawa ndio walewale tu watafanya mambo kimazoea na kulindana.​
   
 16. Nyami2010

  Nyami2010 JF-Expert Member

  #16
  May 18, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mh. Fareed, tuko pamoja 99%. Niongezee kwa kile utakachoota siku zinavyozidi kuelekea 2015: Tutakuwa na Serikali ya Shirikisho

  Rais wa Tanzania: Mh. Sitta/Mh. Pombe Magufuli
  Waziri Mkuu: Dr. Peter W. Slaa
  Waziri wa Fedha: Prof. Ibrahim P. Lipumba; Naibu wake: Zitto Z. Kabwe
  Mambo ya Nje: Anna K. Tibaijuka, Naibu wake: Prof. Safari
  Sheria na Katiba: H. Mwakyembe; Naibu wake: T. Lissu
  Ujenzi na Miundombinu: Dr. Pombe Magufuli (Endapo hatakuwa Rais); Naibu wake: F. Mbowe

  List inaendelea......
   
 17. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #17
  May 18, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  great piti great piti SITTA to bekamu our PRESIDENT....natamani hii iishie kuwa ndoto.........

  mix with yours
   
 18. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #18
  May 18, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0

  [​IMG]
   
 19. N

  Ngao One Member

  #19
  May 18, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 33
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Kwa kweli mpambano wa Urais kati ya SLAA na SITTA ungeleta tija kubwa sana katika kupata ufumbuzi wa vita ya ujinga, maradhi, umasikini na ufisadi ambavyo vinaendelea kulitafuna taifa letu.
   
 20. T

  Taifa_Kwanza JF-Expert Member

  #20
  May 18, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 443
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mmekata tamaa sana watanzania, mnatia huruma kweli kweli.

  Nachojua mimi Mtanzania yeyote anayefikiria kuchagua Rais kutoka CCM, Hata kama angekuwa
  nyerere kwa hali ya sasa, atakuwa ni ndondocha tu lazima.

  Woote hao ni maji ga nyanja woote
   
Loading...