Dream League Soccer 2020 special thread

Frustration

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
3,095
4,059
Hapa ni mahala salama kwa mpenzi wa Dream League Soccer(DLS). Game hili limetengenezwa na Kampuni ya FIRST TOUCH SOCCER(FTS). Game la DLS ni game bora zaidi kwa sasa duniani kwa upande wa soccer.

SIFA PEKEE YA DLS
1. Linachukua nafasi ndogo kwenye simu. Pamoja na ubora wake wa graphics bado game hii ina 500MB na ni tofauti na magame mengine yanaanza na 2GB mfano PES.

2. Uhalisia wa wachezani wa timu wanazochezea
Kitu pekee kinachotofautisha game hii na magame mengine ni uwezo wa ku update wachezaji kadri timu mpya zilivyo. Mfano Mess kwenye game hii anachezea PSG na magame mengine bado Mess anachezea Barcelona. Mfano FIFA hadi leo Xavi,Iniesta bado wanakipiga soka. Huko kwingine hata ukimtaka Gaucho au Drogba au Maradona au Arteta au Guardiola utawapata na bado wanacheza mpira. Ili kujua sajiri za ulaya na kwingineko karibu DLS utawajua wachezaji wote current.

3. Wepesi wa kucheza

Game hii haihitaji rocket science ili uweze kucheza kwani vya kuchezea viko 3 tu 1. B kwa ajili ya pass fupi 2. C kwa ajiri ya kuchop,kubadili wa kumchezesha na pass ya juu. 3. A kwa ajili ya shuti na pass ndefu. Vitufe vyote hivi unakadilia kwa kubovya tu ni simple sana kama kuvaa nguo tu.

4. Wachezaji hawatabiriki uwanjani
DLS huwezi kucheza kwa namna moja mfano, uje angle au sehemu fulani ukishuti ni goli au chenga fulani tu. Hili game sio la kukariri kama Real football lenyewe mchezaji akivuka tu mstari wa kati, apige hatua tatu alafu jaza shuti basi ni goli. Hili game ni real kweli yaani kunakipindi hadi unaacha kula.

5. Uwezo wa kucheza kwa kupanda daraja kwa kikosi chako
Huko kwingine unaambiwa chagua timu, na kisha uichezeshe. Huku mambo ni tofauti Kwanza utapewa squad yako na itabidi uipandishe daraja toka Academy, daraja la 4, 3, 2, 1, daraja la Junior kisha ligi kuu (Legendary). Kuna kupanda na kushuka katika ligi hili kwa hiyo sio ni burudani bulibuli. Pia kuna ligi zingine hapo kati yaani mfano tu wa shirikisho na uefa.

NB: Kikosi bora ndicho kinachoshinda. Game ni ya online(kwa ligi zote) na offline kwa friendly match.

Screenshot_20220129-132354_DLS22.jpg
Screenshot_20220129-132515_DLS22.jpg
Screenshot_20220129-133906_DLS22.jpg
Screenshot_20220129-124019_DLS22.jpg
Screenshot_20220129-122917_DLS22.jpg


KARIBU KWA KUPEANA MAUJANJA NA STORI ZA GAME HILI

Best player kwa game hili ni Ngoro Kante na Mousa Sisoko. Hawa ni wachezaji wenye uwezo mkubwa sana katikati kwa maana wanakaba na kushambulia vizuri.

VITU VYA KUZINGATIA WAKATI WA KUNUNUA MCHEZAJI

1. Acceleration

Kabla ya kumsajili mchezaji yeyote kwanza angalia acce yake ili awe na maamuzi ya haraka. Wengi sana wanaangalia speed tu ya mchezaji bila kuona acc yake. Hata ukimchukua mchezaji mwenye speed 100 ila kama acceleration yake ni 27 ni kazi bure kwani atachelewa kuanza kukimbia na ataporwa mpira mda wote.

2. Stamina

Baada ya kuona acceleration basi angalia stamina yake. Hapa panamwezesha mchezaji kukaba kwa nguvu lakini pia hanyang'anywi mpira kirahisi. Viungo na back wawe na stamina kubwa sana isiwe chini ya 75.

3. Speed
Kitu cha tatu ni pendwa kwa wachezaji wengi wa magame yani kukuimbia kwa kasi hasa kwa fowadi na back za pembeni. DLS wanashambulia sana winga hivyo hakikisha back zako namba 2 na 3 wanakuwa na speed kubwa na acceleration kubwa.

NB: Usimruhusu adui apige kross ni hatari sana, kabla adui hajapiga kross press A ila uwe kwa pembeni yake na umsogee sana ili apige takoling. Takoling ya mbele ni kwa mbali kiasi ili mpira uwahi kuugusa ili kuepusha umeme.

4. Head
Kwa beki za kati head nzuri sana kwani mipira ya kona na kross itasaidia sana kuokoa. Uwezo wa kupiga kichwa ni kwa beki na viungo.

5. Shoot na pass
Kwa fowadi pia lazima uangalie uwezo wao wa kushuti ili hata nje ya 18 uwe unashuti na unafunga. Poor shoot inapelekea kupaisha au shuti kuwa chakula kwa golikipa.

NB. Formation au mfumo mzuri ni 4 4 2 na weka defensive kama unajifunza, moderate kama mchezaji wa kawaida na Attacking kama mzoefu kama mm.

Pia ukifungwa au kufunga unaweza kubadili ili kuendana na mchezo.
 
PESS 2021 SIO GAME HALISI
1. Timu unayocheza nayo wanaweza wakavaa jezi za kufanana na za timu yako.
2. Hadi leo Mess yupo baka, wachezaji wa zamani wote bado wanacheza mfano mkubwa eti Michael Owen bado wanakipiga Man United
Screenshot_20220129-171411_Google Play Store.jpg
Screenshot_20220129-171338_Google Play Store.jpg


Screenshot_20220129-171343_Google Play Store.jpg
 
Ndugu huwa nalitumia sana hili game lakini tangu nilivyo update to 2022 halitaki kabisa kuplay na kama nikibahatika kuplay nacheza kwa tabu maana ina stuck sana na muda mwingine kutoweka ghafla.....shida inaweza kuwa nini wataalamu....??


Hili game ndio ugonjwa wangu pindi nipatapo muda wa kutulia.....
 
Kwa wale ambao kwao game ni mzito cha kufanya.
1. Nenda setting ya game
2. Advanced
3. Kabofye kitufe cha kwanza cha kushoto chenye umbo kama spana.
4 . Hakikisha Quality ipo low. Ile low(auto) sio nzuri kwa mwonekano wa graphics
NB: 60 FRP ni bora zaidi kuliko frp 30.
Ukiweka 30FRP na Quality Low(auto) wachezaji wako wanakuwa wepesi kama pamba na hawana stamina. Hii na kwa wenye android version 5-, version hata uki update kufikia nougat bado original yake ni lolpop hivyo weka 60FRP na Quality low
 
MI naomba mnielekeze kulipata gem linaitwa FTS SOCCER
FTS ni DLS ya zamani, wamebadili jina la game lao na FTS wanatumia wahuni tu wa ku mode game. Kiufupi FTS utakayoikuta sasa sio original game bali wamelichezea na unacheza unlimited coin,offline n.k. Nenda google katafute tu FTS 2022 moded game au unlimited coin utapata
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom