DRC yapata makubaliano ya kisiasa

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,497
36829520_303.jpg

Wanasiasa katika Jamhuri ya Kidemokarsia ya Kongo wamefikia makubaliano ya kuumaliza mkwamo wa kisiasa uliotishia kuiingiza tena nchi hiyo kwenye machafuko, baada ya muda wa Rais Joseph Kabila kumalizika kikatiba.

Kwa mujibu wa rasimu ya makubaliano hayo, ambayo shirika la habari la Reuters limepata nakala yake, sasa Rais Kabila ataondoka madarakani mwishoni mwa mwaka 2017, hatua ambayo haikutarajiwa, hasa baada ya watu zaidi ya 20 kuuawa kwenye maandamano dhidi ya Kabila wiki hii.

Wanasiasa wa upinzani waliozungumza na Reuters wanasema makubaliano hayo "yanamzuia pia Kabila kufanya mabadiliko ya katiba ambayo yangelimruhusu kuwania muhula wa tatu".

Vile vile, pataundwa serikali ya mpito ambayo itasimamiwa na waziri mkuu kutoka kundi la wapinzani lenye nguvu, huku kiongozi mkuu wa upinzani, Etienne Tshisekedi, akipewa jukumu la kusimamia utekelezaji wa makubaliano hayo.

Msemaji wa serikali amekataa kutungumzia chochote kuhusiana na makubaliano hayo, yaliyofikiwa leo chini ya usimamizi wa Kanisa Katoliki nchini Kongo.

Chanzo: DW
 
Tatizo la wakongo ni kusalitiana. Pia wahamiaji DRC ni wengi mno unakuta hawana mapenzi mema na nchi bali wanawaza kwenda kuishi ufaransa wakizifuma
 
  • Thanks
Reactions: MTK
Tatizo la wakongo ni kusalitiana. Pia wahamiaji DRC ni wengi mno unakuta hawana mapenzi mema na nchi bali wanawaza kwenda kuishi ufaransa wakizifuma

Wahamiaji watupu kuanzia Kabila mwenyewe mnyarwanda!
 
Tatizo la wakongo ni kusalitiana. Pia wahamiaji DRC ni wengi mno unakuta hawana mapenzi mema na nchi bali wanawaza kwenda kuishi ufaransa wakizifuma
mbona Obama mwenyewe wa kuja, Trump nae wale wale lkn wanapiga kazi, shida ni u Africa ndo unatusumbua
 
View attachment 449982
Wanasiasa katika Jamhuri ya Kidemokarsia ya Kongo wamefikia makubaliano ya kuumaliza mkwamo wa kisiasa uliotishia kuiingiza tena nchi hiyo kwenye machafuko, baada ya muda wa Rais Joseph Kabila kumalizika kikatiba.

Kwa mujibu wa rasimu ya makubaliano hayo, ambayo shirika la habari la Reuters limepata nakala yake, sasa Rais Kabila ataondoka madarakani mwishoni mwa mwaka 2017, hatua ambayo haikutarajiwa, hasa baada ya watu zaidi ya 20 kuuawa kwenye maandamano dhidi ya Kabila wiki hii.

Wanasiasa wa upinzani waliozungumza na Reuters wanasema makubaliano hayo "yanamzuia pia Kabila kufanya mabadiliko ya katiba ambayo yangelimruhusu kuwania muhula wa tatu".

Vile vile, pataundwa serikali ya mpito ambayo itasimamiwa na waziri mkuu kutoka kundi la wapinzani lenye nguvu, huku kiongozi mkuu wa upinzani, Etienne Tshisekedi, akipewa jukumu la kusimamia utekelezaji wa makubaliano hayo.

Msemaji wa serikali amekataa kutungumzia chochote kuhusiana na makubaliano hayo, yaliyofikiwa leo chini ya usimamizi wa Kanisa Katoliki nchini Kongo.

Chanzo: DW
Inapendeza sana
 
Back
Top Bottom