DRC yakabiliwa na wimbi la tatu la maambukizi ya Virusi vya Corona

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,001
9,866
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inakabiliwa na wimbi la tatu la maambukizo ya corona, na huku kitovu kikiwa katika mji mkuu, Kinshasa, ikiwa ni moja ya miji yenye idadi kubwa ya watu barani Afrika, Waziri wa Afya Jean-Jacques Mbungani alisema Alhamisi.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, kama nchi nyingine nyingi za Kiafrika, Congo imeripoti visa na vifo vichache, lakini maafisa wa afya wana wasiwasi juu ya kuongezeka kwa hivi karibuni kwa maambukizo ambayo yalisababisha visa vipya 243 vilivyorekodiwa Jumatano, idadi kubwa zaidi ya kila siku tangu mwezi Machi.

“Natangaza rasmi kuanza kwa wimbi la tatu la janga la COVID-19 katika nchi yetu, Kinshasa ikiwa kitovu chake”, Mbungani aliwaambia waandishi wa habari.

Kiwango cha chini cha chanjo na kutozingatia kanuni za usafi zilizopendekezwa zilikuwa ni sababu za kuongezeka kwa kiwango cha maambukizo, alisema.

VOA Swahili
 
Hiyo DRC ni ya huko Buzza au wapi? Mpaka sasa niko Kisangani nikitokea Lubumbashi,hiyo Korona wala hawana habari nayo. Kinachofanyika ni Serikali kuanza mikakati ya Kula Hela za Wazungu za COVAX kwa kuleta data za Uongo kama anavyofanya Museveni kwa kutaja taja takwimu ukwara za Korona baada ya Kusikia Mfuko wa COVAX umekusanya misaada yenye thamani ya USD 9.6B (Tsh 24 Trillioni) kwa ajili ya Mataifa masikini yanayorekodi visa vingi vya CORONA.Wakongo hawataki Lockdown kabisa.
 
Back
Top Bottom