Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,495
- 9,275
Rais Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amesema anavunja ushirikiano wa kisiasa baina ya muungano wa vyama vinavyomuunga mkono-CACH, na vile vilivyo upande wa mtangulizi wake, rais mstaafu Joseph Kabila-FCC.
Ushirikiano huo umekuwa ukiongoza serikali ya Kongo kwa miaka miwili iliyopita, Kabila akilidhibiti bunge, huku Tshisekedi akiwa na mamlaka ya rais. Uamuzi huo Tshisekedi ameutoa katika hotuba kwa taifa jana Jumapili.
Hotuba yake rais Tshisekedi ilikuwa ikisubiriwa kwa shauku, baada ya mazungumzo ya mashauriano aliyoyafanya mwezi novemba, kwa kile kilichoelezewa kuwa lengo la kuunda muungano wa taifa.
Katika hotuba hiyo, Tshisekedi ameyagusia masuali mengi ambayo amesema yalijitokeza katika mazungumzo hayo, la muhimu zaidi likiwa ni hatua za kuhitimisha ushirikiano baina ya muungano wa vyama vinavyomuunga mkono yeye, maarufu CACH, na ule wa vyama vilivyo upande wake rais mstaafu Joseph Kabila yaani FCC.