DRC: Kambi ya wanajeshi wa Tanzania na Malawi yavamiwa na kuchomwa moto, raia wanne wauawa

MSAGA SUMU

JF-Expert Member
May 25, 2015
6,482
20,426


Habari zaidi hivi punde
MAELEZO ZAIDI WAKUU.
Imetokea Congo ,ni kambi ya umoja wa mataifa ilio na askari wa Tanzania na Malawi imevamiwa na waasi wa ADF,askari mmoja wa Malawi kauawa na raia wanne.

---
Kambi ya Wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania na Malawi imeshambuliwa na watu wanaodhaniwa kuwa ni Waasi wa kikundi cha ADF

Watu wanne wanaoishi katika kijiji hicho wamefariki huku Mwanajeshi mmoja wa Malawi akijeruhiwa. Hakuna Mwanajeshi wa Tanzania aliyejeruhiwa wala kufariki

Kambi hiyo ipo maeneo ya uwanja wa Ndege wa Mavivi mjini Beni ambapo Ndege za Umoja wa Mataifa hutua

Kambi hiyo ilishambuliwa kwa kutumia makombora ya RPG ambapo hema mbili za Askari kutoka Tanzania zilichomwa moto
 
Kambi ya askari wa umoja wa mataifa wa kulinda amani kutokea Tanzania na Malawi huko DRC, imevamiwa na mahema mawili kuchomwa moto na watu wanaodhaniwa kuwa ni waasi wa ADF katika uwanja wa ndege wa Mavivi usiku wa kuamkia leo katika mji wa Benni

Raia wanne na mwanajeshi wameuawa na askari mmoja wa Malawi amejeruhiwa, waasi hao wamekimbia na wanasakwa



Chanzo ni Radio One
 
Back
Top Bottom