Drama za wanasiasa zimeanza kuhusu ajira 800,000

NGOGO CHINAVACH

JF-Expert Member
Apr 8, 2011
943
368
SERIKALI inatarajia kutoa ajira 800,000
kwa vijana kuanzia mwakani
kuliwezesha kundi hilo kuondokana na
utegemezi katika jamii na kuchangia
uchumi wa nchi.
Akizungumza Dar es Salaam jana
wakati wa kongamano la taifa la ajira,
Makamu wa Rais, Dk. Gharib Mohamed
Bilal alisema programu hiyo
itatekelezwa kwa awamu na awamu ya
kwanza ya miaka mitatu itaanza
kutekelezwa katika mwaka wa fedha
wa 2014/2015.
Licha ya uchumi kukua kwa kiwango
cha kuridhisha cha asilimia 6.5 kwa
mwaka, bado kasi hiyo haijaweza
kuzalisha ajira ya kutosha
ikilinganishwa na idadi ya wanaoingia
katika soko la ajira, alisema.
Alisema soko la ajira nchini lina uwezo
wa kuzalisha ajira 300,000 kwa mwaka
katika sekta rasmi ikilinganishwa na
wastani wa wahitimu 600,000 hadi
800,000 wanaoingia katika soko la
ajira nchini.
“Vijana wasiofanya kazi wanaongeza
utegemezi katika jamii na familia na
kuathiri uchumi na wengine
wanajiunga na makundi ya uchochezi
na uvunjifu wa amani.
“Wengine wanaweza kujiingiza kwenye
vitendo vya wizi, kutumia madawa ya
kulevya na biashara ya ngono hivyo ni
muhimu kwa serikali na jamii kwa
ujumla kuchukua hatua
zitakazowezesha kuongeza fursa za
ajira kwa vijana kujiajiri au
kuajiriwa,”alisema Dk. Bilal.
Hata hivyo, alisema kati ya mwaka
2010 hadi 2013 ajira 610,285
zimepatikana na kwamba kati ya hizo
ajira 185,929 zilizalishwa kupitia
miradi ya uwekezaji 1,845 iliyosajiliwa
Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).
Alisema tatizo jingine linaloikabili sekta
ya ajira nchini ni vijana kutoweza
kubaini fursa zilizopo na kuzitumia
katika kujiajiri katika sekta mbalimbali
nchini na kuondokana na dhana ya
kuwa ajira ni kuajiriwa.
Naye Waziri wa Kazi na Ajira,
Gaudensia Kabaka alisema
umeanzishwa a mtandao utakaosaidia
vijana kujifunza ni taaluma ipi
inahitajika kwenye soko la ajira.
-MTANZANIA
 
Back
Top Bottom