Dr Wlbroad Slaa na Freeman Mbowe ongezeni juhudi karibu kunakucha. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr Wlbroad Slaa na Freeman Mbowe ongezeni juhudi karibu kunakucha.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Molemo, Sep 5, 2012.

 1. M

  Molemo JF-Expert Member

  #1
  Sep 5, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  WanaJF

  Ni ukweli ulio wazi kwamba watawala wanapata hofu kuu kwa sasa kila wakisikia neno CHADEMA.Hakika wanaweweseka.Kiwango cha umma kuunga mkono chama pinzani katika historia ya Taifa hili kwa sasa tunashuhudia CHADEMA ikivuka mipaka ya kupendwa! Fantastic!

  Wachambuzi wa mambo tunajiuliza kuna nini? Hata hivyo bila shaka yoyote CHADEMA kwa sasa kimejipambanua kama wakili na mtetezi mkuu wa wananchi wa Taifa hili.Watanzania wa leo si wajinga wanaona.Ukitazama bunge huhitaji kuwa msomi kujua ni chama kipi kinatetea wanyonge wa Taifa hili.Ni CHADEMA.

  Nimefanya utafiti wangu binafsi katika mikoa mitano.Shinyanyanga,Rukwa,Lindi,Mwanza na Singida.Kila mkoa tumehoji watu 50 na jula ya mikoa 5 tumehoji watu 250.Pamoja na mambo mengine kulikuwa na swali tuliwauliza watu.."NI CHAMA KIPI UNACHOKIONA NI MTETEZI WA KWELI WA MATATIZO YA WANANCHI NA UNACHOONA KINAFAA KUONGOZA TAIFA TUKAPATA MAFANIKIO?" Majibu ya swali hili yaliniacha mdomo wazi kama ifuatavyo: Shinyanga waliosema CHADEMA ni 41,Rukwa CHADEMA ni 36,Lindi CHADEMA ni 31,Mwanza CHADEMA ni 46 na Singida CHADEMA ni 38.Vyama vingine vyote ikiwemo CCM waligawana kura zilizobaki katika watu 50 waliohojiwa katika kila mkoa.Watu watashangaa nilikuwa nafanya utafiti wa nini-Hakika nilikuwa nafanya Research kwa ajili ya Masters degree yangu ninayokamilisha ya mambo ya siasa.Huo ndiyo mtizamo halisi wa umma.

  Kwa upande mwingine nguvu ya CHADEMA inazidi kupaa kutokana na watawala kuihofia mno kupita kiasi.Vitendo wanavyofanya kulitumia jeshi la polisi kuzuia harakati za kisiasa huku wakiwaua kwa risasi wafuasi wa CHADEMA ni sawa na kuchochea moto wa kuzidi kupendwa na kuonewa huruma na jamii.

  Tunafahamu majemadari wawili wa chama hicho Dr Wilbroad Slaa na Freeman Mbowe wanapita katika kipindi kigumu sana kwa sasa.Wanajua watanzania wanawatizama kama tumaini pekee la kuipeleka nchi katika neema.Pia wanafahamu wanatakiwa kuchukua nchi kwa amani na salama bila umwagaji damu.Viongozi hawa wakitizama vitisho na mauji ya polisi dhidi yao huku wakiona kundi la watanzania milioni 40 likiwa nyuma wanaona mambo mawili makubwa.Kwanza wanapata moyo na Ari lakini hata hivyo kwa vile wao ni wanadamu kama wengine akili ya kukata tamaa pia inawajia.Hii ni kwa sababu kamba hukatikia pembamba.Hata hivyo sisi wananchi tunawatia moyo mashujaa hawa kwamba wasikate tamaa,waongeze juhudi kwa sababu kumeshapambazuka sasa na siku si nyingi watalihutubia Taifa wakitokea magogoni baada ya uchaguzi!.

  WanaJF nawakilisha.
   
 2. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #2
  Sep 5, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Nimemshangaa nchimbi anaposema chadema wanaweza wakachukua nchi baada miaka 20,au 15 nilimwona tahaira kweli na kile nikathibitisha kweli anatumia kufuga nywele,isotoshe analahumu kwanini akukamatwa slaa,hapa ndipo naona shida sio sensa shida ni chadema na viongozi wake ambao wana windwa ikiwezekana hata kuuwawa,na serekali hii ya hawa dhaifu,natoa rai sasa wawe makini na waangalifu kila wanapo kwenda,kama ccm wameingiza silaha hapa mashambulio hayo yataelekezwa kwa chadema na yatakua ni mauaji kama ni kweli alaaniwe mwenyekiti ccm kikwete hatuachie nchi kwa amani sio damu na mateso kwa raia wa nchi hii.
   
 3. only83

  only83 JF-Expert Member

  #3
  Sep 5, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Mkuu malizia hiyo dissertation yako utupe full report hapa JF...I think it will be very mwaaa!!
   
 4. M

  Molemo JF-Expert Member

  #4
  Sep 5, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Hata wakati wa uchaguzi wa Arumeru walisema CDM italichukua jimbo baada ya miaka 20.Kila mtu anajua matokeo yake.
   
 5. M

  Molemo JF-Expert Member

  #5
  Sep 5, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Usijali mkuu itawekwa nikishamalizia...!
   
 6. Domy

  Domy JF-Expert Member

  #6
  Sep 5, 2012
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 4,702
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kama ingekuwa ni usiku wa kawaida basi muda huu ni sawa na saa 12.45 alfajili.
  Tunakaribia nchi ya ahadi ya asali na maziwa waliyoahidiwa wana wa israel (Watanzania).MUNGU ibariki Tanzania,MUNGU wabariki viongozi wa Chadema wasife moyo.
   
 7. M

  Molemo JF-Expert Member

  #7
  Sep 5, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Amina..!
   
 8. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #8
  Sep 5, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,847
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  nAKUBALIANA na ushauri wako, hii ni sawa na kuuguza mgonjwa ambaye hali yake ni mbaya sana, kuna wakati wauguzaji wanakata tamaa, lakini siku zote daktari hakatishi tamaa wauguzaji.Wakati nauguza marehemu mama yangu daktari aliendelea kunipa hope kwamba kwa dawa hizi alizokunywa leo zitaleta mabadiliko, lakini kimoyo moyo nilijikatisha tamaa na ndicho kilichotokea.

  Kwa upande wa ccm daktari wao ni TISS, polisi na jeshi hawa madaktari wanaendelea kuvuta mikwanja kwa watawala na huku wakiwapa matumaini kwamba watahakikisha chadema hawatingi magogoni.lakini kwa kuwa wao ndiyo madaktari wanaelewa jinsi CCM ilivyotaabani, lakini sababu ya mkwanja wataendela hivyo hadi kura zitapigwa na baada ya matokeo mkuu wa majeshi polisi na TISS watapiga saruti kwa SLAA kuashiria mkuu mpya wa nchi.CCM ni mgonjwa anayemtumainia daktari
   
 9. M

  Molemo JF-Expert Member

  #9
  Sep 5, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Asante sana Kamanda.Imetulia mno.
   
 10. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #10
  Sep 5, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,700
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 11. M

  Mshind Member

  #11
  Sep 5, 2012
  Joined: Jul 10, 2012
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Amina!
   
 12. W

  Wimana JF-Expert Member

  #12
  Sep 5, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 2,453
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 145
  Usimshangae Dk Nchimbi, si wajua dbe tupu halikosi kuvuma? Lakini pia anayo maana yake;
  CCM hawako tayari kuona Chadema wanachukua nchi kirahisi, hivyo si ajabu kuanza kuona damu za Watanzania zinamwagwa na Serikali pasipo sababu ya maana.
   
 13. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #13
  Sep 5, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  pamoja sana kamanda
   
 14. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #14
  Sep 5, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Yeyote asiyeamili hili basi; ukweli wa mambo ni kwamba katika uongozi wa kisiasa MAMBO KARIBU SANA YANAJIPA kwa hisani ya nguvu ya umma.

  Na kwa dokezo tu, wala mtu asishangae kusikia Tanzania tumepewa adhabu ya kunyimwa msaada na hata hatua nyinginezo zaidi.

  Hayo yote yatakua ni matokeo ya aina ya rekodi ya haki za binadamu tunayoendelea kuweka kama taifa na kule kufinya demokrasia. Hilo ndilo neno la leo kwa kifupi chake.
   
 15. Gedeli

  Gedeli JF Gold Member

  #15
  Sep 5, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 452
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  fmpiganaji asante kwa utafiti wako lakini nina maswali ya kukuuliza hapa 1 kwanini umehoji watu wachache hivyo. 2 huo utafiti wako umefanya mjini au vijijini. huu utafiti tunauhitaji sana ila wako uko narrow sana uongeze nyama tafadhali.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...