Elections 2010 Dr. Willibrod Slaa umefanya kazi kubwa sana bado tunakuitaji

rennychiwa

Member
Oct 14, 2010
13
45
Sina budi kumpongeza Rais wa CHADEMA Dr. Willbroad Slaa kwa kazi kubwa aliyoifanya pamoja na team yake yote kukiunua chama.

Amefanya kazi kubwa sana kuhakikisha chama kinaongeza idadi ya viti vya ubunge kutoka 4 hadi kufikia 22 huku majimbo mawili ya mpanda ambayo ni ngome ya CHADEMA yakiwa bado hayajapigiwa kura. Ongezeko la vijana waliojitekeza kupiga kura na kukiunga mkono chama ni kubwa sana ingawa wengi wao majina yao yalichakachuliwa ili kupunguza idadi ya wapiga kura. Tutegemee maajabu 2015 na kwenye chaguzi zijazo kama CHADEMA hakitabweteka.

Ni imani yangu kwamba Dr.Slaa ataendeleza pale alipoachia, kuzisaidia baadhi ya halmashauri ambazo chama kimechukua ili ziwe za mfano. Kuimarisha mshikamano wa wabunge na madiwani waliochaguliwa ili kukijenga chama kizidi kuwa na mtandao kote nchini. Kuzidi kuwahamasisha vijana wengi wasomi ambao hawana vyama kujiunga na CHADEMA. Kutoa elimu ya uraia vijijini ili watu wengi waweze kujitambua kabla ya uchaguzi. Kuwaandaa vijana kugombea nafasi mbalimbali za uongozi vijijini ili kuleta changamoto kwa wale wanaopita bila kupingwa. Kufanya tafiti mbalimbali za kutosha ili kujua mustakabali wa chama ktk mapungufu na kuyatatua kwa haraka.

Naamin CHADEMA ndio chama mbadala, kina watu makini sana na watu wengi wanaimani nacho hakuna budi kuwatendea haki wapiga kura wenu. Kuna kila haja ya kulelekeza mapambano yetu na kudai haki zetu katika misingi ya upendo, na katika uwanja wa AMANI.

A time like this demands strong minds, great hearts, true faith and ready hands. Martin Luther King Jr.

If u cant be a pine on the top of the hill, be a scrub in the valley but be the best little scrub by the side of the hill. Be a bush if u cant be a tree
 

CHAUPEPO

New Member
Nov 5, 2010
4
0
Ahadi ya Dr. Silla ni kwamba hata kama hawatafanikiwa kuingia Ikulu this time ccm wakati wanaapishwa kuingia Ikulu wao watendelea na kampeni za kujenga chama nchi nzima.........hakuna kulala mpaka kieleweke................
 

Kituko

JF-Expert Member
Jan 12, 2009
9,557
2,000
Nadhani hapo sio kazi ya Slaa peke yake ni kwa watu wote wenye mapenzi mema na ukombozi wa nchi hii, kampeni ya 2015 inatakiwa kuanza na kuwa zoezi endelevu, kama Operation Sangara ilivyoiteka Tanzania basi ndani ya miaka Mitano inatakiwa kuwa na Operation kama hizo si chin ya kumi ili chamakiimarike
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom