Dr. William: Madhara ya vinywaji vya kuongeza nguvu(Energy drink)

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,107
18,323
Usingoje kusimuliwa bidha yangu ya Energy Drink , ukinywa hii hata Kama ulikuwa huna nguvu utahisi kupa mawinguni Kama malaika wa mbinguni.

Usihofu Caffeine niliyokuwekea humo , ni kiwango kingi sana ndio maana sitaki mjamzito atumie maana inaweza kutoa mimba au kuharibu ila kama huna mimba bugia kwa Sana, maana najua caffeine ukifika kwenye ubongo wako itakufanya kuchangamka ila figo zako ndio zitaumia zaidi ila ukikosa usingizi usijari kesho kunywa tena utapata tatizo la usagaji chakula na tatizo la moyo sio mpaka nikwambie.

Guarana siwezi kuacha kuiweka, itakupa msisimko ikifika kwenye figo zako, zitashindwa kuchujwa hivyo figo zitakuwa dhaifu katika kuchuja damu yako, kama figo zako zikiwa mbovu kweli utaweza shika mimba ?

Sukari niliyokuwekea kwenye Energy Drink, ni nyingi sana sawa na kunywa vijiko 26 vya sukari ila kwani hilo ni mhimu sana ? Basi tulipoteze maana bila sukari kuwa nyingi huwezi vutiwa na Energy Drink yangu.

Mimi mjanja Sana nimekuweka vitamins B najua huwezi ni hoji madhara yake maana nataka kuipandisha presha kwenye damu yako, na kuharibu ini zako , ukose hamu ya kula Ila sio Sana kidogo Sana, itakupa mawazo kidogo pia na gesi kiasi ila kibofu chako cha mkojo kitapata tabu Sana baada ya kunywa Energy Drink yangu maana ukianza kuitumia hutatamani kuiyaacha hata kidogo.

Mwenye akili ndio ata -share-na wengine bidha yangu.

Dr William ( USA).
 
Sijawahi kunywa hayo madude ila watu wanayabugia siyo mchezo ndiyo maana viharusi, presha, na magonjwa yameongezeka sana siyo kwa watu wazima wala watoto, masikini wala matajiri shida kubwa ni vile tulavyo na kunywa

Kwanini mtu asinunue kimfuko cha buku cha Rozella ukachemsha na sukari robo tu ukapata juice yako fresh karibia lita 2 ukanywa ukaachana na vinywaji hivyo vya hovyo na vyenye madhara
 
Elimu hii huwa tunafundishwa sana kanisani kwetu kwenye somo la afya
Na hata coke ina some of the ingridients hatari sana bila kusahau sukari . na kwa kutuzuga wametengeneza ambazo hazina sukari wamesahau zile ambazo hazina caffein
 
Inasemekana asilimia 80 ya vifo vyetu sababu kubwa ni hivi vitu tunavyovila na kuvinywa,so sad,magonjwa ya figo yamezidi kukua leo hadi kesho.
 
Nakumbuka kipindi nasoma huko Arusha,kuna jamaa alikunywa energy kabla ya kulala.
Usiku wa manane alijikuta anavuja jasho mwili mzima,halafu anatetemeka na kuyumbayumba, akajaribu kukojoa ikashindikana kabisa hadi baada ya masaa kadhaa mwili ulirudi kwenye hali ya kawaida.
Hizi ENERGY hata ukimpa shetani anakataa.
 
kumbe umemaliza shule juzi tu enzi za energy drink
 
Hizi hazifai. Kuna siku nilikunywa energy 2, nilikesha usiku 'nazima moto' wa UE, kesho yake kwenye chumba cha mtihani nashindwa hata kushika pen mikono inatetemeka, na mtihani haukuwa wa kwanza kusema nilikuwa na exam fever.
 
Babu yangu anavuta sigara tangu akiwa na meno hadi saivi ni kibogoyo ana piga nyota pakti mbili mpk 3

Bibi yangu anakunywa common tangu akiwa binti hadi leo ana run 80 something

Mimi kunywa ka energy tu mnanitisha ivyo,niacheni ebu

Wapi dragoniiiiiiii yangu mimi

500mlred.jpg
 
wasipokunywa na wakapata hayo madhara, nani wayapate.?
waache watu wafanye biashara na wengine waendelee kunywa.
 
Hizi hazifai. Kuna siku nilikunywa energy 2, nilikesha usiku 'nazima moto' wa UE, kesho yake kwenye chumba cha mtihani nashindwa hata kushika pen mikono inatetemeka, na mtihani haukuwa wa kwanza kusema nilikuwa na exam fever.
Wengi wamepoteza maisha..

Bila kujua mtu anabugia 3 kisha ana fanya yale 6x6..

Unataka damu izunguke mwilini mwako kwa speed ya engine ya jet?

Tatizo kubwa ni kwamba more than 80% ya watumiaji ni vijana.

Pita mitaani, chupa za energy drink zimetapakaa kila sehemu tena kuliko hata zile za milinda au cocacola.
 
Hiyo dragon nasikia ndio shida.. unaweza kaa siku 3 bila usingizi..
Babu yangu anavuta sigara tangu akiwa na meno hadi saivi ni kibogoyo ana piga nyota pakti mbili mpk 3

Bibi yangu anakunywa common tangu akiwa binti hadi leo ana run 80 something

Mimi kunywa ka energy tu mnanitisha ivyo,niacheni ebu

Wapi dragoniiiiiiii yangu mimi

View attachment 1216534
 
Usingoje kusimuliwa bidha yangu ya Energy Drink , ukinywa hii hata Kama ulikuwa huna nguvu utahisi kupa mawinguni Kama malaika wa mbinguni.

Usihofu Caffeine niliyokuwekea humo , ni kiwango kingi sana ndio maana sitaki mjamzito atumie maana inaweza kutoa mimba au kuharibu ila kama huna mimba bugia kwa Sana, maana najua caffeine ukifika kwenye ubongo wako itakufanya kuchangamka ila figo zako ndio zitaumia zaidi ila ukikosa usingizi usijari kesho kunywa tena utapata tatizo la usagaji chakula na tatizo la moyo sio mpaka nikwambie.

Guarana siwezi kuacha kuiweka, itakupa msisimko ikifika kwenye figo zako, zitashindwa kuchujwa hivyo figo zitakuwa dhaifu katika kuchuja damu yako, kama figo zako zikiwa mbovu kweli utaweza shika mimba ?

Sukari niliyokuwekea kwenye Energy Drink, ni nyingi sana sawa na kunywa vijiko 26 vya sukari ila kwani hilo ni mhimu sana ? Basi tulipoteze maana bila sukari kuwa nyingi huwezi vutiwa na Energy Drink yangu.

Mimi mjanja Sana nimekuweka vitamins B najua huwezi ni hoji madhara yake maana nataka kuipandisha presha kwenye damu yako, na kuharibu ini zako , ukose hamu ya kula Ila sio Sana kidogo Sana, itakupa mawazo kidogo pia na gesi kiasi ila kibofu chako cha mkojo kitapata tabu Sana baada ya kunywa Energy Drink yangu maana ukianza kuitumia hutatamani kuiyaacha hata kidogo.

Mwenye akili ndio ata -share-na wengine bidha yangu.

Dr William ( USA).
Ukimchunguza sana bata huwezi kumla naona mwalimu wetu madhala yapo kwenye energy tu sijakuona ukizungumzia unga wa sembe soda peps ,Coca-Cola mafuta ya chakula tunayopikia majumbani karibia watu 95% tunatumia mafuta yakutoka nnje mfano mo au korie tunambiwa tusile nyama nyekundu nafikiri mnaijuwa sasa nyinyi wachambuzi wa mambo haya mnaweza kukabiliana nahaya yote au mnataka kuharibu biashara za watu umenichekesha uliposema energy kwenye kikopo cha gram 300 wanatuwekea vijiko26 vya sukari , sasa hiyo sukari wenzetu watengenezaji was vinywaji hivi wanapewa bure kama wanavopewa bure maji na mungu wetu mkuu lakini sishangai hawa ndowasomi wetu wakibongo au hiyo sukari ni mchanga wanaubadilisha kuwa sukari
 
Benefits of energy drinks

• Improve brain function
• Reduce risk of developing Alzheimer’s disease
• May help boost long-term memory
• Weight loss
• Increasing alertness
• Improve sporting performance
• May help prepare the colon for an endoscopy/colonoscopy
• May help decrease the risk of cirrhosis
• Slow down the rate of disease progression in hepatitis C infection
• May help protect people from blepharospasm
• May help protect the lens of the eye
• Lower the risk of developing kidney stones
• Lowers the risk of cancer (prostate, endometrial, breast)
• Lowers the risk of stroke
 
Leo tutaona mengi
 
Back
Top Bottom