Dkt. Wilbert Kleruu - Utata wa kifo chake, historia na maisha yake

IMG-20201227-WA0004.jpg
IMG-20201227-WA0005.jpg
IMG-20201227-WA0002.jpg
 
SITASHANGAA UTAWALA HUU KUTOA MATUKIO KAMA HAYA MAANA TUNAPOELEKEA KWA UBABE NA KUWAPIGA RAIA KUNA WENGINE HAWATAKUBALI

Mfano mzuri wale wakuu wa wilaya na mikoa wanaochapa watu
 
Umeona eennhh???!!!,Wanasaikolojia wanasema Kuna mwisho wa Binadamu kuvumilia,akishavuka viwango hivyo binadamu anaweza kufanya chochote bila kuogopa chochote,hiyo wanaita'The point of no return", Hapo unasikia harufu ya damu ya binadamu tu.
 
Mwamwindi alionewa na Mahakama kwa kuhukumiwa kifo kwa mauaji ya 'kukukusudia'

Mtu kakufuata Shamba, anatoa maneno ya kashfa na kejeli

Umeamua kumkwepa unaondoka na kurudi Nyumbani bado anakufuata kwa nyuma anatoa maneno ya kejeli, mfano anapokejeli Makaburi ya Wazee wako uliowazika na kuwaita 'mirija' wenzio… hii ni provaction ya wazi kabisa sema ndo hivyo tena 'Mlalamilaji,ndio Mwendesha mashtaka, ndie Jaji, ndio mtoa hukumu na ndie anaesaini hati ya kifo'

Ujasiri wa Mwamwindi ulileta nidhamu sana kwa Ma RC na DC Nchi nzima

Said Mwamindi alikuwa mchapakazi sana aliekuwa anapambana na jamii ya watu wavivu

'Kwanini mje mpore mashamba yetu na kugeuza ya kijiji wakati kuna Mapori mengi tu…'

Miaka 20 baada tu ya kadhia hiyo Ujamaa unapelekwa Mortuary na tunaanza tena kudalalia Ubepari

Kwangu Mzee Said ndio Shujaa wa muda wote, wangekuwepo akina Mwamindi zama hizi ufala fala wa kufokeana na kudhalilishana hadharan ungeshapatiwa 'Alkasuus'
 
Mnara wa Kreluu kwa nyuma nyumbani kwetu Mkungugu.. home sweet home.
20141019_140805.jpg
 
Hakika hata mimi namkubali Sana huyu baharia, Siku hizi unakuta kimjamaa kimepata kacheo basi full dharau.
 
JF imekuwa ni mahali pa kupashana habari na kuweza pia kuzungumzia mambo ya historia yetu na mwelekeo wa nchi.

Kuna Huyu bwana anajulikana kama marehemu Dr Kleruu, mie nimekuwa nikimsikia katika wimbo wa Mbaraka Mwinshehe kuwa alikuwa mwanamapinduzi.

Je, kuna yeyote anaweza kutupatia taarifa kumhususu huyu Dr Kleruu alikuwa nani hasa na uana mapainduzi wake ulikuwa vipi katika historia na siasa za Tanzania?

Mnara wa kumbukumbu kifo cha Dr. Kleruu kijijini Isimani

Mtoto wa Said Mwamwindi

=== Historia ya Dr. Kleruu kwa ufupi ===

HISTORIA: MKULIMA ALIYEMUUA MKUU WA MKOA SIKU YA KRISMASI-

ILIKUWA siku ya Sikuku ya Noeli almaarufu Christmas mnamo mwaka 1971. Mkuu mpya wa Mkoa wa Iringa aliyehamishiwa hapo akitokea Mtwara, Dkt. Wilbert Kleruu, msomi wa Shahada ya Uzamivu (PhD) wa Uchumi wa kijamaa katika Kilimo aliuawa na Mkulima aitwaye Said Mwamwindi.

Kipindi hicho kulikuwa na kampeni ya kutaifisha mashamba ya wakulima wakubwa na kuyafanya mashamba ya kijiji. Na Dkt. Kleruu alipelekwa Iringa ili akatekeleze kazi hiyo kwani kipindi hicho Iringa ilikuwa na wafanyabiashara wakubwa waliomiliki mashamba makubwa ya Kilimo hasa maeneo ya Isimani.

Katika eneo hilo la Isimani kulikuwa na mkulima mmoja aliyekuwa anamiliki takribani hekari 400 za mashamba na mfanyabiashara aliyekuwa anamiliki majumba Iringa mjini - Said Mwamwindi-
Kwa wakati ule ilishauriwa angalau kila mtu awe na shamba lisilo zidi hekari 4. Jambo ambalo lilileta mvutano mkubwa kati ya wakulima wakubwa na Serikali.

Sasa siku hiyo ya Christmas, Dkt. Kleruu alikwenda Isimani akiwa katika utekelezaji wa sera ya kutaifisha mashamba. Moja kwa moja alikwenda hadi shambani kwa Mwamwindi, na kumkuta analima.

Mkuu huyo wa Mkoa akamuuliza mbona unalima shamba lako mwenyewe na si la kijiji? Mwamwindi akajibu, sioni tatizo hakuna mtu shambani, leo ni Jumapli tena ni sikukuu.

Maneno yale yalimuudhi Dkt. Kleruu, ambaye alikuwa akisifika kwa ukali, kutekeleza sera za serikali na maneno makali au kutukana watu hadharani pale wanapo fanya makosa.

Dkt. Kleruu baada ya kuudhika alimtukana Mwamwindi tusi lililomlenga mama yake ambaye tayari alikuwa marehemu. Mwamwindi alihoji inakuwaje anamtukania mama yake, huku akimuonyesha kaburi alimozikwa?

Mkuu wa Mkoa, aliendelea kuja juu, huku akisema kaburi ndio nini? Huku akilipiga mateke kaburi la Mama yake Mwamwindi. Kwa kabila la wahehe makaburi yana heshima yake, kwani ndipo nyakati nyingine hutumika katika sala, matambiko na mila kadha.

Kitendo kile kilimghadhabisha Mwamwind, na kuanza kukimbia kuelekea nyumbani. Mkuu wa Mkoa akadhani Mwamwindi anamkimbia, akaamua kumfuata.

Alipofika nyumbani, tayari Mwamwindi alisha ingia ndani na kuchukua bunduki yake, Dkt. Kleruu baada ya kuona hali ile mara moja alianza kumuomba msamaha, lakini hasira zilimuwaka Mwamwindi kama moto wa nyika; hakuwa na msamaha, alimfyetulia risasi kichwani Dkt. Kleruu na kumuua.

Baada ya kumuua, Mwamwindi aliuchukua mwili ya Mkuu wa Mkoa na kuuweka ndani ya gari (inadaiwa kwenye boneti) alilokuja nalo Mkuu huyo wa Mkoa.

Kisha alichukua kofia ya Dkt. Kleruu na kuivaa, akaingia ndani ya gari na kuanza safari ya kuelekea Iringa mjini tena akipita njia isiyo ruhusiwa kwani barabara ilikuwa 'one way'.

Alipo karibia mjini, askari walishangaa ni nani anaye pita njia isiyo ruhusiwa, ila mara waligundua ilikuwa gari ya RC wa Iringa, hivyo walidhani amepata dharura.

Gari lilipowasili kituoni, Polisi walijiandaa kupiga salute, mara alishuka Mwamwindi akiwa na bunduki yake na kuelekea ndani (counter). Askari walipigwa na butwaa.

Alipofika aliwaambia "Nendeni mkachukue Nguruwe wenu ndani ya gari," na Kisha akakabidhi bunduki yake.

Lilikuwa tukio la kustaajabisha, na kushangaza na lililofanyika kwa haraka sana.

Baada ya taarifa kuenea, msako wa polisi ulianza mara moja. Ila katika msako huo, Polisi waliwakamata baadhi ya watu walio kuwa wakinywa bia kwa furaha, shangwe na nderemo baada ya kusikia Dkt. Kleruu ameuawa. Kwani wanadai alikuwa na dharau.

Kesi ya Mwamwindi alipelekwa haraka sana na ndani ya miezi kadhaa, Juni 1972, Mwamwindi alihukumiwa kunyongwa hadi kufa, ikiwa ni moja ya hukumu chache za kunyongwa zilizo wahi kuidhinishwa.

Inadaiwa Mwalimu. Nyerere alihuzunishwa sana na kifo hicho, na hata kesi ya Said Mwamwindi ilipoisha na kupewa hukumu ya kifo, Inasemekana Nyerere hakusita kusaini, na ni mojawapo ya hukumu tatu tu za kifo zilizotekelezwa wakati wa utawala wa Nyerere

MICHANGO YA WADAU:

-----------------------------

Habari nyingine inayohusiana na habari hii fuatilia - Binti wa Dkt. Wilbert Kleruu atoa ya moyoni
Samahani chief kwa elimu tu, hukumu zingine 2 zilizosainiwa na Nyerere ni zipi?

Sent from my SM-J730F using JamiiForums mobile app
 
Alikuwa daktari wa nini huyu Kleruu? Alikuwa kabila gani?
Inasemekana alikuwa na shahada ya uzamivu akiwa na umri mdogo tu wa miaka 29 aliyoipata kule Marekani. Aliporudi nchini alikataa kazi ya kufundisha pale UDSM akachagua kufanya kazi pale Lumumba kama Afisa wa TANU. Alikuwa ni mtu aliyeamini sana siasa za ujamaa. Ndipo Mwalimu alipompa kazi ya ukuu wa mkoa. Jamaa alikuwa ni mtu mmoja katili, jeuri, mwenye dharau na nyodo za hali ya juu. Alikuwa hapendwi hata na maofisa wenzie wa serikali kutokana na tabia zake mbaya.
 
JF imekuwa ni mahali pa kupashana habari na kuweza pia kuzungumzia mambo ya historia yetu na mwelekeo wa nchi.

Kuna Huyu bwana anajulikana kama marehemu Dr Kleruu, mie nimekuwa nikimsikia katika wimbo wa Mbaraka Mwinshehe kuwa alikuwa mwanamapinduzi.

Je, kuna yeyote anaweza kutupatia taarifa kumhususu huyu Dr Kleruu alikuwa nani hasa na uana mapainduzi wake ulikuwa vipi katika historia na siasa za Tanzania?

Mnara wa kumbukumbu kifo cha Dr. Kleruu kijijini Isimani

Mtoto wa Said Mwamwindi

=== Historia ya Dr. Kleruu kwa ufupi ===

HISTORIA: MKULIMA ALIYEMUUA MKUU WA MKOA SIKU YA KRISMASI-

ILIKUWA siku ya Sikuku ya Noeli almaarufu Christmas mnamo mwaka 1971. Mkuu mpya wa Mkoa wa Iringa aliyehamishiwa hapo akitokea Mtwara, Dkt. Wilbert Kleruu, msomi wa Shahada ya Uzamivu (PhD) wa Uchumi wa kijamaa katika Kilimo aliuawa na Mkulima aitwaye Said Mwamwindi.

Kipindi hicho kulikuwa na kampeni ya kutaifisha mashamba ya wakulima wakubwa na kuyafanya mashamba ya kijiji. Na Dkt. Kleruu alipelekwa Iringa ili akatekeleze kazi hiyo kwani kipindi hicho Iringa ilikuwa na wafanyabiashara wakubwa waliomiliki mashamba makubwa ya Kilimo hasa maeneo ya Isimani.

Katika eneo hilo la Isimani kulikuwa na mkulima mmoja aliyekuwa anamiliki takribani hekari 400 za mashamba na mfanyabiashara aliyekuwa anamiliki majumba Iringa mjini - Said Mwamwindi-
Kwa wakati ule ilishauriwa angalau kila mtu awe na shamba lisilo zidi hekari 4. Jambo ambalo lilileta mvutano mkubwa kati ya wakulima wakubwa na Serikali.

Sasa siku hiyo ya Christmas, Dkt. Kleruu alikwenda Isimani akiwa katika utekelezaji wa sera ya kutaifisha mashamba. Moja kwa moja alikwenda hadi shambani kwa Mwamwindi, na kumkuta analima.

Mkuu huyo wa Mkoa akamuuliza mbona unalima shamba lako mwenyewe na si la kijiji? Mwamwindi akajibu, sioni tatizo hakuna mtu shambani, leo ni Jumapli tena ni sikukuu.

Maneno yale yalimuudhi Dkt. Kleruu, ambaye alikuwa akisifika kwa ukali, kutekeleza sera za serikali na maneno makali au kutukana watu hadharani pale wanapo fanya makosa.

Dkt. Kleruu baada ya kuudhika alimtukana Mwamwindi tusi lililomlenga mama yake ambaye tayari alikuwa marehemu. Mwamwindi alihoji inakuwaje anamtukania mama yake, huku akimuonyesha kaburi alimozikwa?

Mkuu wa Mkoa, aliendelea kuja juu, huku akisema kaburi ndio nini? Huku akilipiga mateke kaburi la Mama yake Mwamwindi. Kwa kabila la wahehe makaburi yana heshima yake, kwani ndipo nyakati nyingine hutumika katika sala, matambiko na mila kadha.

Kitendo kile kilimghadhabisha Mwamwind, na kuanza kukimbia kuelekea nyumbani. Mkuu wa Mkoa akadhani Mwamwindi anamkimbia, akaamua kumfuata.

Alipofika nyumbani, tayari Mwamwindi alisha ingia ndani na kuchukua bunduki yake, Dkt. Kleruu baada ya kuona hali ile mara moja alianza kumuomba msamaha, lakini hasira zilimuwaka Mwamwindi kama moto wa nyika; hakuwa na msamaha, alimfyetulia risasi kichwani Dkt. Kleruu na kumuua.

Baada ya kumuua, Mwamwindi aliuchukua mwili ya Mkuu wa Mkoa na kuuweka ndani ya gari (inadaiwa kwenye boneti) alilokuja nalo Mkuu huyo wa Mkoa.

Kisha alichukua kofia ya Dkt. Kleruu na kuivaa, akaingia ndani ya gari na kuanza safari ya kuelekea Iringa mjini tena akipita njia isiyo ruhusiwa kwani barabara ilikuwa 'one way'.

Alipo karibia mjini, askari walishangaa ni nani anaye pita njia isiyo ruhusiwa, ila mara waligundua ilikuwa gari ya RC wa Iringa, hivyo walidhani amepata dharura.

Gari lilipowasili kituoni, Polisi walijiandaa kupiga salute, mara alishuka Mwamwindi akiwa na bunduki yake na kuelekea ndani (counter). Askari walipigwa na butwaa.

Alipofika aliwaambia "Nendeni mkachukue Nguruwe wenu ndani ya gari," na Kisha akakabidhi bunduki yake.

Lilikuwa tukio la kustaajabisha, na kushangaza na lililofanyika kwa haraka sana.

Baada ya taarifa kuenea, msako wa polisi ulianza mara moja. Ila katika msako huo, Polisi waliwakamata baadhi ya watu walio kuwa wakinywa bia kwa furaha, shangwe na nderemo baada ya kusikia Dkt. Kleruu ameuawa. Kwani wanadai alikuwa na dharau.

Kesi ya Mwamwindi alipelekwa haraka sana na ndani ya miezi kadhaa, Juni 1972, Mwamwindi alihukumiwa kunyongwa hadi kufa, ikiwa ni moja ya hukumu chache za kunyongwa zilizo wahi kuidhinishwa.

Inadaiwa Mwalimu. Nyerere alihuzunishwa sana na kifo hicho, na hata kesi ya Said Mwamwindi ilipoisha na kupewa hukumu ya kifo, Inasemekana Nyerere hakusita kusaini, na ni mojawapo ya hukumu tatu tu za kifo zilizotekelezwa wakati wa utawala wa Nyerere

MICHANGO YA WADAU:

-----------------------------

Habari nyingine inayohusiana na habari hii fuatilia - Binti wa Dkt. Wilbert Kleruu atoa ya moyoni
Wewe ni mtizamo na msimamo wako kuhusu yafuatayo:
1.Hukumu iliyotolewa kuhusu Mwamwindi kumuua Kleruu,je ni sahihi?
2.Je,Mwamwindi kumuua Kleruu,ilikuwa kosa au sahihi?
3.Ingekuwa wewe ndiye Mwamwindi,je,ungefanya nini?
 
Hii ya ugonjwa wa psychosis kwenye familia ya Nyerere ni kweli nimeisikia muda mrefu sana kuwa hata mwalimu mwenyewe alikuwa na daktari wake aliyekuwa anamtibia hayo mambo, huyo daktari alikuwa anajitahidi sana mzee asije akalipuka uchizi waziwazi, na kweli alimdhibiti vizuri hali hii haikutokea. Watoto wake pia wana matatizo hayo kwa viwango mbalimbali, lakini kuna mmoja wa kiume ambaye ni tatizo kabisa (si adabu kusema "kichaa" maana huo ni unyanyapaa, lakini ama matatizo makubwa kwa kweli, hajaweza kabisa kujimudu). Lakini magonjwa ya akili n magonjwa kama mengine, yakidhibitiwa bado mtu anaweza ku-function vizuri sana katika jamii.

Hata mimi katika kufanya kwangu kazi nilishawahi kuwa na bosi mwenye ugonjwa wa akili, lakini mwenyewe alikuwa anajitahidi sana kuudhibiti kwa kuzingatia dawa na kuhudhuria kliniki, katika miaka 4 niliyofanya naye kazi "alilipuka" mara moja tu tukiwa safarini (alikuwa amesahau kuchukua dawa zake, na kabla hajalipuka alianza kuongea kama utani tukiwa kikaoni "mnanikebehi, leo nisipojeruhi mtu, bahati sana". Sisi tulichukulia maskhara tukacheka, kumbe ndio tulikuwa tunamtibua! Wakati huo tulikuwa hatijajua tatizo lake, alitunza sana siri yake!) Aliendelea na kazi na kuna wakati alipewa cheo cha ukurugenzi akahamishiwa wizara ya elimu makao makuu, nadhani sasa amestaafu. Kwa hiyo ugonjwa wa akili ukidhibitiwa vizuri bado mtu anaweza kuitumia 'potential' yake, kuchangia maendeleo ya jamii na taifa na kutimiza malengo yake ya maisha. Vichaa wengi tunaoona wakirandaranda mtaani nadhani mojawapo ya kinachochangia hali hiyo ni kukisa tiba sahihi, na wale wanaobahatika kupata tiba bado kuna tatizo la uzingatiaji (adherence) na family support.
Yanaweza yakawa siyo matatizo ya akili as such bali uzalendo wao kwa nchi ndiyo uliosababisha wakawa kama wana matatizo ya akili, kwa sababu kwenye vita ya mwaka 1978, inasemekana baadhi yao (watoto wa mwalimu) walikuwa kwenye kikosi cha mizinga. Kwa teknolijia ya kipindi hicho, askari waliokuwa wnafanya kazi kwenye kikosi hicho baadhi walikuwa wanaonyesha dalili kama zimefyatuka kidogo
 
Samahani chief kwa elimu tu, hukumu zingine 2 zilizosainiwa na Nyerere ni zipi?

Sent from my SM-J730F using JamiiForums mobile app
Sina uhakika sana ila kuna mtu mwingine aliwahi kumuua mtu nadhani mke wake kwa kumchoma akiwa ndani ya gari pale mlima wa Kironga na hatimaye kulisukuma gari hilo likaporomoka chini kwenye korongo refu nia ikiwa alipwe hlea ya BIMA. Huyu yeye alitengeneza ajali ya makusudi kwa kuchoma mtu ndani ya gari ili aweze kulipwa hela za bima. Niliwahi kusoma humu na pengine details nilizotoa hapa zinaweza zikawa haziko sahihi sana, nilishapoteza kumbukumbu
 
Makaburi yana maana kubwa hata ki-Biblia.
Waisrael walipokuwa wanatoka utumwani Misri kwenda kwenye nchi ya ahadi Kaanani, walihama wakiwa na mifupa ya Yusufu kwa maana kuwa walihama na kaburri la Yusufu kwa sababu alikuwa ameagiza hivyo
 
Sina uhakika sana ila kuna mtu mwingine aliwahi kumuua mtu nadhani mke wake kwa kumchoma akiwa ndani ya gari pale mlima wa Kironga na hatimaye kulisukuma gari hilo likaporomoka chini kwenye korongo refu nia ikiwa alipwe hlea ya BIMA. Huyu yeye alitengeneza ajali ya makusudi kwa kuchoma mtu ndani ya gari ili aweze kulipwa hela za bima. Niliwahi kusoma humu na pengine details nilizotoa hapa zinaweza zikawa haziko sahihi sana, nilishapoteza kumbukumbu
Huyo mtu alikuwa muasia ambaye alimsukumiza mkewe aliyekuwa na Bima kubwa ya maisha kwa kampuni moja ya huko UK.
Na ni milima ya Lukumburu kuelekea Songea sio kitonga. Milima hiyo kabla ya barabara kuwa ya lami ilikuwa ya hatari sana.
Upelelezi wa hapa ndani uliona ile ilikuwa ajali hadi ndugu wa mwanamke marehemu walipo hire wa pelelezi binafsi toka Scotland yard ndio waligundua kila kitu.
Jamaa alinyongwa, signed by mchonga.
 
Back
Top Bottom