Dkt. Wilbert Kleruu - Utata wa kifo chake, historia na maisha yake

Nimejaribu kufuatilia hiki kifo cha dr. Kleruu nikapata muunganiko wa tukio lililompata kamanda Barlow kwanda baadhi wachaga wana mambo ya kujikweza wanapokuja kwenye jamii ya watu.
Wanakuja na ule usemi wa "unajua mimi ni nani??"
rest in peace BARLOW, MWAMINDI na mwenzio KLERUU.
 
Mazingira yote yanaonesha kulikuwa na uonevu dhidi ya raia. Yeye Mwamwindi hakuwa mpumbavu kumpiga risasi mkuu wa mkoa lazima jamaa laimu harass sana akaona enough is enough akaamua liwalo na liwe. Nasikia Mwamwindi alihukumiwa kunyongwa na Nyerere dikteta akasaini fasta jamaa akanyongwa.

Mkuu alifanyanini hasa? hadi kuchapwa risasi, hii ilikuwa mbaya kiana?
 
Mkuu alifanyanini hasa? hadi kuchapwa risasi, hii ilikuwa mbaya kiana?

Mambo ya siasa za ujamaa na kujitegemea hizo bro, wakina mwamwindi walikuwa wanaji establish kiujasiriamali na wakati huo ilikuwa inaonekana kama wewe kupe au bwanyenye!
 
Bila kuona haya nadhani katika hii issue Mwamwindi ndiye shujaa. Hakukubali ushenzi na uonevu usiokuwa na maana, hivyo alikuwa tayari kufa kuliko kuona uchafu huo.

Tanzania ya sasa inahitaji watu kama Mwamwindi ambao watasimama na kupigania haki zao na nchi yao. Tungekuwa na akina Mwamwindi wengi hapa Tanzania basi hata pesa za EPA zingerudi.
Kibanga ampiga mkoloni?
 
Alikuwa daktari wa nini huyu Kleruu? Alikuwa kabila gani?

Nitakujibu kimoja Kleruu alikuwa mchagga na mzinzi mzoefu alimfauta Mwamwindi shambani kwake siku ya xmas kwa dharau kubwa eti kwakuwa alikuwa akimchukulia mke wake akadhani hata Mwamwindi atamuogopa JAMBO AMBALO MNYALUKOLO HAKUKUBALIANA NALO, KWA KUJIAMINI KABISA AKAMTWANGA RISASI NA BILA WOGA AKABEBA MAITI YAKE MPAKA POLISI NA KUWAKABIDHI, SHUJAA MWAMWINDI ALINYONGWA KWA SABABU ZA KISIASA NA SI KISHERIA KWANI UKIREJEA KESI HIYO MAHAKAMANI ALISHINDA LAKINI NYERERE ALIMNYONGA KWA HOFU YA KUSHINDWA UJAMAA ALIOUANZISHA. BINAFSI SIONI SABABU YA KUITWA MWANAMAPINDUZI KWA SABABU ALIKUFA KIFO CHA AIBU (UZINZI) NA SI CHA KISHUJAA KUITWA MWANAMAPINDUZI NI KUPOTOSHA UKWELI KWA KUPAMBA UBAYA KUWA UZURI
 
Mambo ya siasa za ujamaa na kujitegemea hizo bro, wakina mwamwindi walikuwa wanaji establish kiujasiriamali na wakati huo ilikuwa inaonekana kama wewe kupe au bwanyenye!

Hapa unampotosha mwenzako Shujaa Mwamwindi alimuuwa RC Kreluu kwa kuwa alikuwa anamfanyia ubabe kwa kutembea na mke wa Mwamwindi na mbaya zaidi siku ya kuuawa kwa dharau alimfuta Mwamwindi shambani kwake bila ulinzi wowote na alikuwa akiendesha gari yeye mwenyewe Mkuu wa mkoa na siku hiyo ilkuwa ya XMAS Shujaa Mwamwindi akaona this is too much kutokana na maneno ya dharau aliyoambiwa na Kreluu uzalendo ulimshinda akamtwanga risasi na kwa kujiamini kwa kile alichokifanya akapeleka maiti yake mpka polisi na kuwataarifi polisi kuwa chukueni mbwa wenu polisi wakadhani ni mbwa kweli kuangali nyuma ya gari lahaula ni MKUU WA MKOA DR. KRELUU APIGWA RISASI NA KUFA.
 
Ukweli wake ni uongo kwako na
uongo wako ni uongo kwa kila mtanzania mwenye akili timamu

Acha ubishi shujaa Mwamwindi alimpiga risasi kreluu kwa sababu alikuwa anamchukulia mke wake na mbaya zaidi alimfuata mpaka shambani kwake akiendesha gari yeye mwenyewe RC bila walinzi na zaidi ya yote ilikuwa siku ya sikuu ya X-Mass na kwa dharau alianza kum-harass Field Marshal Mwamwindi, baada ya kuona dharau imezidi akaamua kumpumzisha kwa amani kwa kutumia mtambo maalum wa kudhibiti wazinzi na wababe-Bunduki. Haikutosha kwa kujiamini bwana yule alibeba maiti ya mbaya wake mpaka kituo cha polisi Iringa mjini na kuwakabidhi polisi maiti wao kwa maneno "KACHUKUENI MAITI YA MBWA WENU" Ukifanya rejea ya ile kesi FIELD MARSHAL MWAMWINDI alishinda lakini alinyongwa kwa sababu za kisiasa kulinda ujamaa. Nimemwita Field marshal kwa kuwa ni MTANZANIA WA KWANZA kufa kishujaa akitetea haki yake na heshima yake. Ni nani leo hii anaweza kupambana na Mkuu wa Mkoa akimchukulia mke wake? zaidi ya kulalamika kwenye magazeti ya udaku tu? Mwamwindi hilo alilikataa na mpaka leo tunamkumbuka.
 
Bado Aman Mwamwindi anaweza akawa si source nzuri....yeye ni diwani wa Mlandege na Meya kuna mambo hayasemi sbb tu yanagusa serikali...ngoja ntakuja baadae
 
Dah! unazidi kunipa Utata na kuwaza Zaidi

Mkuu hii ni thread ya mwaka 2008.Soma Thread yote nafikiri Utata wako utaondoka.Pitia majarida ya TLA pia utaona case hii inajitokeza sehemu nyingi.Kuna wengi pamoja na Mimi tunaoamini mpaka leo kwamba Kifo cha Mwamwindi kilitokea (kwa Rais wa wakati huo kutia saini) kwa sababu tu alimuua mtetea siasa za Kuhamia ktk vijiji vya Ujamaa za Rais na Waziri Mkuu wa wakati huo.Marehemu Alhaj Mwamwindi hakuyataka hayo alionekana kama Kikwazo!
 
Jambo wanajf! Siku moja tulikuwa safarini na kati ya watu waliokuwa kwenye gari wakawa wanatia story kuhusu Dr Kieruu alivyouawa. Kwa kufupisha, walichoongea pale ni kwamba Dr Kleruu alipigwa risasi na mtu aliyeitwa Mamwindi alipokuwa shamba , na huyo Mamwindi akapeleka maiti ya Dr Kleruu polisi na kuwaambia 'chukueni mzoga wenu huo'. Kisa cha kupigwa risasi eti ni kutembea na mke wa huyo Mamwindi. Ninachoshindwa kuelewa ni kwa nini Dr Kleruu anasifika sana Tz mpaka kuna wimbo wa zamani kuna kisehemu unaimba '... Dr Kleruu, alazwe pema kiongozi wetu shujaa, mwanamapinduzi.....' Kama kuna mwenye uelewa tofauti naomba aweke mambo hadharani!
 
Dr kleruu alikuwa muumini wa ujamaa na kujitegemea tarafa ya isimani kulikuwa na mashamba makubwa sana ya mahindi ya matajiri na watu wadogo dr alianzisha mashamba ya ujamaa.kila kijiji zilifungwa kengele asubuhi inagongwa wanaenda kwenye shamba la ujamaa na yeye anapita kukagua wenye mashamba makubwa ikawa wanalima wakati wa week end siku ya tukio ilikuwa xmas mwamwindi alikuwa analima kwake akafuata akamwambia kalime shamba la ujamaa na kumtolea maneno makali mwamwindi akaingia nyumbani kwake na kuchukua silaha na kumuua dr
 
Ninaomba Kwa anayeijua kesi ya kihistoria ya kumuua aliyekuwa RC Iringa Hayati Dr.Wilbert Klerruu mauaji yaliyofanywa Na mkulima Abdallah Mwamwindi.Tafadhali atujuze.
 
Back
Top Bottom