Dr.WHO na ujumbe wake: Je, Mangapi Aliyosema Yana Ukweli?

Status
Not open for further replies.

Steve Dii

JF-Expert Member
Jun 25, 2007
6,414
2,000

samahani naenda nje ya topic lakini pia ni vema kumjua MWANAKIJIJI AMBAYE AMEKUWA CELEBRITY WA BONGO-USA


drwho Says: December 14, 2007 at 9:26 am

THE TRUE COLOURS OF MWANAKIJIJI (MKJJ)

MKJJ Kwa nini mada ya waitwao ‘waliofanya mzaha’ ndo iwe na umuhimu katika masahili baina yako naye? Wewe Mwanakijiji na Mwakyembe mlijuaje kuwa maafisa wa Serikali ndio wamefanya mzaha au wameongopa na isiwe wengineo waliowasilisha taarifa mapema?
HATIMAYE UZALENDO UMEKUSHINDA UMEANZA KUONYESHA RANGI ZAKO KAMILI KWA KUWAPIGA MKWARA WATUMISHI WA UMMA.

Leo nakuondolea uvivu ewe ujiitaye MKJJ maana suala la KUJITAHIDI KUWACHANGANYA NA KUDANGANYA UMMA KUWA WEWE NI MWANAHARAKATI WA HAKI NA MAENDELEO KUTOKA KAMBI YA UPINZANI WAKATI SIYO NI UNAFIKI WA HALI YA JUU. Unatakiwa kufanya kazi ambayo kwayo umeajiriwa kwa kufuata maadili ya kazi yako kama walivyo wenzako wengi na si vinginevyo.

Ndg.zangu Watanzania, mwanadamu ajiitaye Mwanakijiji Mtanzania aliyezaliwa 1953 huko Iringa (sitasema jina lake kamili) ni kiumbe mwenye majukumu, mitizamo na nia tofauti kabisa na yale anayoyaandika na kuyatangaza.
Hakuna cha mgongano wa fikra wala cha kusoma alama za nyakati yeye ndiye damu ya chaka mpikaji wa mazingaombwe kupitia taaluma yake anayoitumia kwa utaalamu unaoonekana kuwa wa hali ya juu lakini sasa anaumbuka baada ya kukutana na ama wanaolingana naye au wanaomzidi.


1.MKJJ yuko katika payroll (isiyo rasmi) ya Serikali yetu katika kazi ya usalama wa Taifa. Sio rasmi kwani ajira yake na majukumu yake hayafuati muundo wa kawaida(organogram) uliopo kitu ambacho kina utata hasa inapokuja katika uajibikaji wake na pia ulipwaji wa maslahi yake.

2. MKJJ ni mhitimu wa shahada ya kwanza (BA in Political Science)- Tanzania na pia Shahada ya uzamili (MA in Mass Communication & Media Arts)- USA. Baadaye alifaulu vizuri sana mafunzo ya upelelezi (Intensive course in Nationalism & Espionage) – Cuba chini ya Mwalimu wake gwiji aliyempenda sana kwa jina Mosses Powel . Hii inaeleza sababu ya MKJJ kupewa nafasi ya kuwa muhudumu (Usher) mmojawapo katika mazishi ya Powell 22.01.2005. Alipelekwa pia Trinidad & Tobago kwa ajili ya mafunzo ya ukakamavu na ulinzi wa kujikinga chini ya kitivo cha Powell ambaye ndiye mwanzilishi wa mashambulizi ya Sanuces Ryu Jujutsu lakini bahati mbaya MKJJ hakuwa mzuri sana katika somo hili.


MKJJ baada ya kushauriwa , alichagua kuendelea zaidi kubobea katika mbinu za kipepelezi za steganografia (steganography), Saitografia (Cytography) na Utafiti (Research) siraha zilizompa nafasi kupata mazoezi kwa njia ya vitendo katika Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Ministry of Defence).

3. Kwa sasa MNKJJ anafanya kazi ya kunusa na kuwachanganya Watanzania kwa kuandika na kuongea kwa style ya kukandia Serikali kwa sana kupitia majamvi na majukwaa mbalimbali kama vile Jamboforums.com, (http://jamboforums.com/); Gumzo la Kijiji (www.phpbbcity.com/forum/baraza.html); KLH news (http://mwanakijiji.podomatic.com); habari Tanzania (http://www.habaritanzania.com); Blog.co.tz (http://www.blog.co.tz/profiles/Mwanakijiji/); Bongo5 (http://www.bongo5.com); Podomatic (http://www.podomatic.com/people/index/mwanakijiji); Bongo radio (http://www.bongoradio.com); Dar Young African (http://www.youngafrican.com) na magazeti mbalimbali yaliyo katika mtandao.

Hutumia majina bandia kibao kama hilo la Mwanakijiji, Mkimbizi wa Kiuchumi, Madele wa Madilu, Lydia Ngosha n.k na idadi kubwa ya hayo majamvi anamoandika ya mtandaoni ni yeye anayeyamiliki ambayo mengi yake ni ya bure tu nay eye huonekana kuwa senior member mwenye nyota lukuki !

Awapo mtatandaoni huungwa mkono mara kwa mara na wanachama wasiomtambua (kama vile akina Steve D ) na wale wanaomtambua kama vile akina Theleza Nesaa, Da- chemi na motto wa Mkulima au pia ajiitaye Katibu Tarafa na wengine wengi.

4. Kwa kutumia utaalamu wake wa sanaa na fani ya uandishi na utangazaji, MKJJ anajificha ndani ya mbinu ya kijasusi ijulikanayo kama ‘The Italian Strategy of Tension with False Flag’. Ingawa ni mwanachama CCM lakini anapokuwa mtandaoni huvaa ngozi ya mbwa mwitu na kujiita Mkuu wa Taasisi ya Kitanzania ya Demokrasia, Maendeleo na Amani (TAKIDEMA). Kazi zake ni kama ifuatavyo:-

a. Kuanzisha mada chokozi (provocative topics) zenye kuleta hisia kali akisukuma makombora kwenye Serikali ikiwa ni namna ya kuwachokoza wananchi ili mnapoanza kusema au kuandika basi yeye anachukuwa notisi zake na kuwakabidhi waliomtuma kwa ajili ya kurekebisha panapotakiwa haraka iwezekanavyo. Hadhira yake kusudiwa ni hasa Watanzania walioko nje na hususani wasomi ambao wanaweza kuleta upinzani. Wachache walimshtukia alipopinga kinamna kuruhu suala la Uraia wan chi mbili !! sababu iko wazi nayo ni “you are either with us or against us!’

Nawahurumia wale wote ambao wamekuwa wakitoa maoni yao kwake kizembe na kwa uwazi bila kinga na au kupiga simu na pengine kutoa michango eti kwa ajili ya kuimalisha Podomatic yake ambayo aliahidi siku kibao kuwa itakuwa ni live radio live na itaunganishwa na Jump Tv k.m StarTV n.k. Mbinu atumiayo hapo ni ya kukufuatilia mienendo yako ulipo popote (surveillance) na kunasa maongezi au IP yako kupitia headers kama uko kwenye mailing list au unaandikiana naye emails n.k . Hapa hutumia kitu tukiitacho ‘wire tapping’. Katika KLH news hakuna cha eti ana msaidizi aitwaye Ngosha wala fundi mitambo ni yeye mwenyewe tu na vifaa kama one way voice link vitumiavyo FM radio broadcast na komputa yenye vikolombwezo vyake .

Aidha yeyote aliyepiga simu kwake alishanaswa isipokuwa kama nawe uko protected! Kumbuka huyu ni mmoja wa wataalamu wachache ambao wanaweza kusoma maandishi yako na au kusikiliza sauti yako na wakakunyambulisha kisawasawa. Najua atajaribu sana kunitafuta lakini hata na mimi nimejiandaa sana kabla ya kupasua hili jipu.

b. Pamoja na wenzake wanachunguza na kutoa mapendekezo yao juu
ya utendaji wa watumishi mbalimbali wa ngazi za juu Serikalini, Mahakama na Jeshi, katika Bunge na pia ndani ya CCM. Kazi hii huifanya kwa kushirikiana na vijana wengine watano ambao wako nje na ndani ya nchi na wote ni makada damu wa CCM. Wawili ni waandishi wa habari hapa jijini Dar. Wengine wote hawana noma maana wanawajibika kama walivyotumwa kwa nia nzuri ya kuimalisha nidhamu kazini na huduma kwa wateja. MKJJ anaonekana yeye sasa kuwa kama ndiye mwamuzi na akiwa hakupendi hata kwa sababu zake binafsi atakusukia ajali. Mbaya zaidi amejisahau na kuanza kujadili pasipo aibu namna ya kujaza kila nafasi wazi za juu majukumu ambayo hakupewa.

Alizizungumza sana juu ya Gavana BOT, IGP, Mkuu wa JW&JKT, Balozi Washington DC, Jaji Mkuu, Katibu Mkuu CCM, etc mpaka alipoitwa na kupewa warning ndio kesho yake akaandika katika Jambo forums eti amenyanyua mikono na amekubali sasa kujiunga na CCM. Maana yake ilikuwa anatoa mkwara kuwa hakika sasa anataka kujiunga na upinzani! Kumbuka anaishi chini ya ‘false flag’. Sasa ameanza tena juu ya Costech! Kosa jingine analolifanya ni kuwa eti yeye ni expert wa kila kitu kuanzia uchumi, siasa, sanaa, historia , elimu, utamaduni na hata fisikia ya kinyuklia? .k Ni mtu gani asiyekubali kutojua kitu Fulani au kusahihishwa hata siku moja???

c. Amekuwa anawaita pia watu mbalimbali zaidi na kuwahoji kupitia KLH News. Kwa wastani mwanzoni aliifanya kazi yake kama alivyotumwa lakini sasa amelewa umaarufu na kuanza kupitiliza! Na mfano mzuri utaona kuwa siku hizi anajisahau sana. Anakula posho yake nzuri na kustarehe na anapogundua kuwa hajaposti chochote cha maana anakurupuka na mahojiano kama haya yaliyo chini ya kiwango chake na cha taaluma yake na tena kwa viashiria vya majibu anayotegemea!! MKJJ maelezo ya watumishi yanapogongana na taarifa walizo nazo tume si tiketi ya kusema kuwa hao Watumishi wa Serikali na Mashirika ya umma walisema uongo chini ya kiapo au eti wanafanya mzaa.

Kwa nini pia msifikiri kuwa waliowapa taarifa mlizonazo mwanzoni ndio waongo ? Msianze kupiga watu mikwara baada ya kugundua kuwa wamelipua bomu! Mada yake ya awali iliyomgusa Seif haikuwa imeenda shule akaitwa na kuonywa kuwa watu watamshutukia ndio maana sasa tunaona anawaita akiwa Mrema , Zito n.k . Wapinzani wa kweli walio smart wameshamnasa . Kazi ya kuongea na wapinzani ni ya kutumia akili sana maana mbinu ni kuteka agenda zao na au kuwachanganya ili washughulike na ambayo hapo baadaye watagundua kuwa hayana uzito.Source: BongoCelebrity.com


Je, 'jipu' hili litamuuma na kumkosesha usingizi Mkjj au litasinyaa na kutoweka bila hata kovu kubakia?

SteveD.
 

YournameisMINE

JF-Expert Member
Aug 29, 2007
2,250
1,225
Duh......kaaaaazi kweli kweli!!. Labda yote, sidhani kama kuna haja ya kum-doubt unless bwana mshutumiwa aseme vinginevyo kama anaona kuna haja ya kufanya hivyo.
Kama kweli huyu bwana kazaliwa mwaka 1953, basi anaweza kuwa mzazi wa baadhi yetu humu jamvini. Well, sie wengine yetu macho.
 

Steve Dii

JF-Expert Member
Jun 25, 2007
6,414
2,000
Ha ha ha ha ha ha! check hapa chini:

MKJJ ni mhitimu wa shahada ya kwanza (BA in Political Science)- Tanzania na pia Shahada ya uzamili (MA in Mass Communication & Media Arts)- USA. Baadaye alifaulu vizuri sana mafunzo ya upelelezi (Intensive course in Nationalism & Espionage) – Cuba chini ya Mwalimu wake gwiji aliyempenda sana kwa jina Mosses Powel . Hii inaeleza sababu ya MKJJ kupewa nafasi ya kuwa muhudumu (Usher) mmojawapo katika mazishi ya Powell 22.01.2005. Alipelekwa pia Trinidad & Tobago kwa ajili ya mafunzo ya ukakamavu na ulinzi wa kujikinga chini ya kitivo cha Powell ambaye ndiye mwanzilishi wa mashambulizi ya Sanuces Ryu Jujutsu lakini bahati mbaya MKJJ hakuwa mzuri sana katika somo hili.


MKJJ baada ya kushauriwa , alichagua kuendelea zaidi kubobea katika mbinu za kipepelezi za steganografia (steganography), Saitografia (Cytography) na Utafiti (Research) siraha zilizompa nafasi kupata mazoezi kwa njia ya vitendo katika Wizara ya Ulinzi ya Marekani
Sina mbavu...
Tanzania inavipaji bwana..


SteveD.
 

Quemu

JF-Expert Member
Jun 27, 2007
986
1,250
Shabashi!!!...Aisee haiwezekani kabisa...mimi naamini huyu jamaa ni mzee wa kijijini kwetu kabisa.

Kama Dr.Who yuko sawa, basi kweli naamini Richimundi ni ya Richadi. Bigi braza Afrika ni changa la macho tu, na kwamba ile dola laki moja ni malipo ya mwisho ya serikali kwa kijana wetu anayevaa suruali zisizo na zipu.

Gademu!!!!
 

Pundit

JF-Expert Member
Feb 4, 2007
3,740
1,225
This n**ga makes Mwanakijiji sound like some espionage expert of some sort wakati kuanzisha hiyo redio alihitaji msaada wa watu wa ICT.

I find it hard to believe the accusations, especially given the passionate commitment on the part of Mwanakijiji to exposing the nepotism and inefficiency of the Tanzanian so called leadership.

If there is anybody who is trying to play political games, it is the author of the above piece.
 

Mtoto wa Mkulima

JF-Expert Member
Apr 12, 2007
685
0
Hahah sina mbavu wazee hiyo CV kiboko ila kwa yote jamaa kama ni kweli basi. Nachuweza kusema mwanakijiji ni mwandishi tuu anayejificha nyuma ya komputer yake na kuandia ila hizi sifa nyingine sio kweli. Ni mtaanzania aliyekuwa na frutration zake sasa anaamua kuzimalizia nyuma ya Key bord ya komputer ndio maana huwa yupo online more than 16 hours kwa siku. Kama kweli ni jamaa wa mwaka 1953 basi mwanakijiji inawezekana hana familia au basi kama anayo ni iresposible father kwa sababu kwa hali ya kawaida tuu huyo mwanakijiji hana muda wa kukaa hata na familia yeke kama kweli anayo.
 

Mnhenwa Ndege

JF-Expert Member
Dec 5, 2007
243
195
ndio maana huwa yupo online more than 16 hours kwa siku. Kama kweli ni jamaa wa mwaka 1953 basi mwanakijiji inawezekana hana familia au basi kama anayo ni iresposible father kwa sababu kwa hali ya kawaida tuu huyo mwanakijiji hana muda wa kukaa hata na familia yeke kama kweli anayo.

From the way you put it kuwa the guy is 24, 7 behind a computer then huyu si mtu mmoja bali ni ofisi yenye watu kadhaa ama a group of individuals representing a certain common idea and they are committed to their task.
 

Makanyaga

JF-Expert Member
Sep 28, 2007
5,296
2,000
Nampongeza Mzee Mwanakijiji kwa CV nzuri, kichwa chenye fikra lazima kiwe hivyo, Mzuri darasani na anapokuwa nje ana hoja pia. Tatizo letu sisi wengi wetu tunakuwa na A's za kwenye mitihani halafu tukiwa nje zinakuwa E's. Hapo ndipo tunapoanza kuahangaika na watu wenye hoja. Tuwe na hoja kwenye karatasi ndani ya vyumba vya mitihani na pia nje ya vyumba vya mitihani. Tukishindwe kuwa hivyo basi tusiwachukie wale ambavyo wamejaliwa kuwa navyo vyote hivyo viwili. MZEE MWANAKIJIJI BIG UP AND LONG LIVE, HATISHWI MTU HAPA!
 

Gembe

JF-Expert Member
Sep 25, 2007
2,505
1,225
Siataki kutoka Comments Mpaka Mzee Mwanakijiji ajibu mwenyewe,Sasas kwanini Dr. WHo ajamtaja Mwanakijiji kwa jana kwamba yeye ndio Yuda>:
 

Wambandwa

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
2,253
1,500
Dr.Who

Tofauti na ulivyoainisha hapo juu, mimi naona ni wewe unayetaka kutuchanganya kwa kuto wasifu usiokuwa sahihi (potofu) wa MKJJ!

Ni kipi hasa ambacho kafanya huyu bwana ambocho si cha kujenga nchi na kutetea walal hoi?

Ni makala ngapi wewe Dr.Who umeandika ama kuchangia kwenye magazetim ya bongo??

AU UNATAKA KUPANDA CHATI KWA HIYO POSTING YAKO YA KUMKANDIA MKJJ BILA SABABU YOYOTE?

Naona unatafuta cheap populality by trying to tarnish MKJJ's name..

Jirudi Dr.Who
 

Kasana

JF-Expert Member
Apr 3, 2007
417
195
Nafikiri tulivyojichanganya kuhusu hii mada kuamini au kutokuamini.
Je ni vipi kwa wananchi wa kawaida wasio na uwezo wa kuchanganua pumba na mchele? (hapo kidhungudhungu).

Sisi tuendelee kukata issue kwa manufaa ya taifa.
 

Nzokanhyilu

JF-Expert Member
Feb 19, 2007
1,086
0
Kuna swali hili liliulizwa, mpaka leo halijajibiwa.

Jamboforums is a great place indeed. Lakini I have questions that have been passed onto me. And for sometime I havent really bothered to ask, but rather to observe. I picked this up myself, but it didnt really bother me.

Mfano, it seems one can not REGISTER ANONYMOUSLY.By this, it doesnt mean you create a fake email and fake name. By this I mean, unless jamboforums knows your consistency with an IP Adress, your account will not be activated. There is a particular individual who tried to register at least more than 12 times. The account was never activated, if it was, they got the wrong password. This person knows their IT stuff pretty well.

A few months ago, different people tried to register from different IP adresses...but their accounts were never activated. What happened next, I complained on behalf of them, and voila, their accounts started working. But they were skeptical.

So their question is, is Jamboforums a smart way of someone powerfull (either the government or the opposition), to monitor what people say? I.e a 'SPY's PARADISE'. While people think they are actually anonymous, but they arent. I wonder why Mbowe asked people to use their real names.

Some may not like what I have asked, but it had to be asked, cos its been bugging me for a while. I dont mind my identity being known, but there are others who actually believe they are anonymous, but they possibly arent. If there is a database of IP adresses, then its possible, through time, to know who is who through the forwarded emails etc etc.

Someone says this website is beign ran by a couple of individuals on their expenses. How can people (who think they are anonymous), be assured that the 'Moderators' have the best of intentions. I guess there is a price for everything. I have heard of instances whereby, data (txt messages etc) from mobile companies in Tanzania has been leaked by unscrupulous workers to individuals without the concerned person knowing of the misuse of their data.

INVISIBLE PLEASE DONT DELETE MY POST. I AM HERE, SITOKI NA TUTABANANA HAPA KWA HAPA. ILI NIZIDI KUTANGAZA JF, NAOMBA MAJIBU.
 

Mzeeba

Senior Member
Sep 25, 2007
144
0
Hapa kweli naona tunajichanganya. Kwani kikubwa nachokipata toka kwa DRwho ambaye na yeye yuko nyuma ya mwavuli ni namna/njia (means). To me it does not matter who MKJJ is or anyother who is behind names. wengi wanasababu za kuwa nyuma ya hivyo vivuli. Lakini natumaini kubwa hapa JF ni kuisaidia Tanzania yetu kukua na kuimarika kiuchumi, kijamii na pia katika siasa. mwisho wa siku kila mtanzania anufaike na utajiri huu tuliopewa na Mungu.

sasa kama MKJJ anafanya hivyo kwa kuwa shushushu, au whatever you can call it tatizo liko wapi? lamaana ni kwamba je hao wanaomtuma wanabadilika baada ya kupata maoni na uchambuzi wa watanzania? maana kama wanabadilika na kuijenga TZ then sioni shida. (wakati mwingine the end might justify the means).

Nadhani nafurahi kumsoma MKJJ au Drwho au SteveD na wengine bila kuwajua ni kinanani kwa undani zaidi ya ujumbe wao. wengi hapa tungejuana kwa undani nadhani kuna baadhi ya threads zisingesomwa kabisa, kwa sababu tu ya kumjua fulani.

Jamani letu si moja? Tanzania yenye mafanikio kwa watanzania wote? tena by watanzania wenyewe? kama hatukabiliani katika hili nadhani na hiki kijiji hakina mpango.
 

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,812
1,250
Kabla sijaingia undani wa mada, naomba kautoa angalizo moja:

Hao wanaoitwa USALAMA WA TAIFA nadhani kwa hali ya sasa sioni kama wanatisha. Jambo la msingi hapa ni kwamba kama mtu unajiamini hakuna sababu ya kuogopa. Mfano watu wote wana akili timamu na wale wanaofanya kazi makini ni MAKINI pia zaidi ya hao USALAMA WA TAIFA, na pia KAMA USALAMA WA TAIFA UNAFANYA KAZI KWA MASLAHI YA TAIFA KWA MAANA YA KULINDA KWA DHATI USALAMA WA TAIFA NA SI USALAMA WA WACHACHE, basi wan JF hawana sababu ya kuogopa yeyote na kwa maana hiyo, kama ni MAJUNGU yaliyochanganywa ukweli na uongo ama kama ni kweli kuhusu Mwanakijiji, hakuna sababu ya kuogopa na badala yake ni moja ya sababu ya KUJIVUNIA kwamba JF nako tuna watu wa kila fani... HONGERA JF KWA KUKUA
 

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,110
2,000
Kuna swali hili liliulizwa, mpaka leo halijajibiwa.
Nzokanhyilu,

Si kila swali huwa najibu mkuu. Huwa nanyamaza ili kuona kama kuna members wanaweza kusaidia kujibu. Well, wacha nijibu hoja zako moja baada ya nyingine

Jamboforums is a great place indeed. Lakini I have questions that have been passed onto me. And for sometime I havent really bothered to ask, but rather to observe. I picked this up myself, but it didnt really bother me.
Enhe....
Mfano, it seems one can not REGISTER ANONYMOUSLY.By this, it doesnt mean you create a fake email and fake name. By this I mean, unless jamboforums knows your consistency with an IP Adress, your account will not be activated.
Wrong! How many clients have fake names? How many clients have fake emails? How many clients are not activated? Who said this? None is not activated. Unless nimekusoma vibaya lakini kila member mwanachama anayejisajili hupewa ruksa ya kuweza kuwa mchangiaji. Waliojisajili sasa hv wanaweza kukuthibitisha hilo. Haijalishi am not on my pc then natumia mobile kuhakikisha kila anayejisajili anakuwa huru kutoa mawazo yake.

There is a particular individual who tried to register at least more than 12 times. The account was never activated, if it was, they got the wrong password. This person knows their IT stuff pretty well.
Then the guy is not a compute geek! He/she should have done it easily! I repeat, none is not activated. Am pretty sure of what am writing here. Hakuna kitu sipendi kama uonevu wa ku-ban, kutoruhusu mtu kuandika pindi amejisajili na ku-censor maneno ya mwanachama flani. Sipendi na ikifikia nikachukua maamuzi haya huwa nasema wazi kuwa si kwa mapenzi yangu. Unapoandika kuwa "The account was never activated" unakuwa unanishtaki mimi kwakuwa ndiye ninaye-approve registrations za members hapa, none else.
A few months ago, different people tried to register from different IP adresses...but their accounts were never activated. What happened next, I complained on behalf of them, and voila, their accounts started working. But they were skeptical.
Ghosh! Same things buddy, did you complain? Ooops, then these computer geeks are not good in remembering their passwords. I assure you, (and this' normally what I do) whenever someone sends me an email regarding their lost passwords (maybe forgotten) I do reset em ASAP. Am kinda good in forgetting, can't blame em either.
So their question is, is Jamboforums a smart way of someone powerfull (either the government or the opposition), to monitor what people say? I.e a 'SPY's PARADISE'. While people think they are actually anonymous, but they arent. I wonder why Mbowe asked people to use their real names.
This might be why I didn't want to be involved in this buddy. The intention of this post might be on blue inked sentence. Nzokanhyilu, you have a website, can you tell someone who the hell is he/she via his/her IP address? How many clients from Tanzania are hitting ur site? Have u ever know their real names, real locations, real IDs I mean!? Man u know the truth of this.
Some may not like what I have asked, but it had to be asked, cos its been bugging me for a while. I dont mind my identity being known, but there are others who actually believe they are anonymous, but they possibly arent. If there is a database of IP adresses, then its possible, through time, to know who is who through the forwarded emails etc etc.
Ooops! Well, as I said, u have a web man,,, do u normally trace IP addresses of your clients? Do you normally send em spam mails? Do u use their email addresses to fetch their passwords? At JF things are different. We respect clients, we have no restriction on using FAKE mails and you've all options for changing your email to kikulacho@jamboforums.com or the like. None needs your real email address.
Someone says this website is beign ran by a couple of individuals on their expenses. How can people (who think they are anonymous), be assured that the 'Moderators' have the best of intentions. I guess there is a price for everything. I have heard of instances whereby, data (txt messages etc) from mobile companies in Tanzania has been leaked by unscrupulous workers to individuals without the concerned person knowing of the misuse of their data.
Shabaaash! Kwa hiyo unataka tuanze kuwatoza gharama watu wanaotembelea JF ili wajue kuwa hakuna cha bure? Au tufanyeje ndugu yangu? YES, hakuna cha bure! Hilo ni sahihi kabisa, tunachofanya hapa kwenu wasomaji na wachangiaji SI BURE. Ni kwa manufaa ya vizazi vijavyo. Kama ni suala la gharama kukubali kuzibeba kwa sasa si tatizo, muda niupotezao hapa na Mods na wachangiaji si bure! Ni kwa manufaa ya umma wa watanzania na walimwengu wote. Kutoa ni moyo mkuu. Kaka narejea niliyoongea awali... Wasi wasi mwingi hauna nafasi JF! Kama member hajiamini anatakiwa kufanya yafuatayo:

1. Badili email address yako weka iwe @jamboforums.com
2. Sema tukusaidie kubadili jina lako ulilojisajili nalo (kama ni la kweli) na wewe mwenyewe badili location uliyoandika upo
3. Achana na nickname unayotumia kwa sasa na sajili nyingine na isipokubaliwa registration andika barua pepe kwenda kwa webmasterATjamboforumsDOTcom au invisibleATjamboforumsDOTcom na nitahakikisha narekebisha lolote linalowezekana.

Ukiwa JF jisikie huru; watu mna deal kubwa sana kiasi hamjiamini eh? Duh!
INVISIBLE PLEASE DONT DELETE MY POST. I AM HERE, SITOKI NA TUTABANANA HAPA KWA HAPA. ILI NIZIDI KUTANGAZA JF, NAOMBA MAJIBU.
Angalia red inked sentense! Yaani haihitaji kufikiria sanaaaa....! Yani kila kitu mnaamini watu wataubana ukweli? No, not to me. Nafuta matusi na name calling kwenye forums hizi. Naheshimu sana mawazo ya mtu na anayeuliza ANATAKA JIBU! Kiu ya jibu hukatwa na jibu.

Angalia blue inked words, nazo yawezekana ndizo zilisababisha nikachelea kujibu hoja hii. Am sorry kwa kuchelewa kujibu lakini NASHUKURU kwa maoni yako. Nayaheshimu SANA na nakuomba usisite kunifahamisha mimi ama mod yeyote awaye online juu ya tatizo lolote. Tunaheshimu usalama wa mtu awapo mtandaoni na tunapenda kuwapa uhuru kamili. Yani wewe na keyboard yako na ukimaliza YOU'RE DONE. Ukitukana ama kusababisha matatizo kwa members wengine na wakakulalamikia tutakushughulikia kiungwana.

Ukweli unatuweka huru daima...

Invisible

MEMBERS:
Am sorry for this OFF TOPIC post but I had to respond accordingly. Even the previous post was post was an off topic one that's probably why I did not respond to it on time.

Thanks
 

Nzokanhyilu

JF-Expert Member
Feb 19, 2007
1,086
0
Kabla sijaingia undani wa mada, naomba kautoa angalizo moja:

Hao wanaoitwa USALAMA WA TAIFA nadhani kwa hali ya sasa sioni kama wanatisha. Jambo la msingi hapa ni kwamba kama mtu unajiamini hakuna sababu ya kuogopa. Mfano watu wote wana akili timamu na wale wanaofanya kazi makini ni MAKINI pia zaidi ya hao USALAMA WA TAIFA, na pia KAMA USALAMA WA TAIFA UNAFANYA KAZI KWA MASLAHI YA TAIFA KWA MAANA YA KULINDA KWA DHATI USALAMA WA TAIFA NA SI USALAMA WA WACHACHE, basi wan JF hawana sababu ya kuogopa yeyote na kwa maana hiyo, kama ni MAJUNGU yaliyochanganywa ukweli na uongo ama kama ni kweli kuhusu Mwanakijiji, hakuna sababu ya kuogopa na badala yake ni moja ya sababu ya KUJIVUNIA kwamba JF nako tuna watu wa kila fani... HONGERA JF KWA KUKUA

Ishu sio shushushu wanafanya nini wala kujua nini, ishu ni je wanapataje hizo data zao? Legally? Misleading?
Kuna watu wanataka kuchangia lakini wanashindwa kwasababu JF wao wanaona ni front nzuri sana ya kipelelezi.

Whether DrWho is right or wrong..........., huwezi jua labda mashushu wenyewe wameanza kuanikana......maana kawaida yao lol.
 

Game Theory

JF-Expert Member
Sep 5, 2006
8,557
0
Nilitaka kuwaambia kuwa mimi jina nililokuwa nalitumia mwanzo ni hilo la DR WHO lakini looks like kuna mwingine huko Bongo celebrity

Hivyo ningependa kuwafahamisha kuwa sina uhusiano wowote na huyo mwandishi lakini hiyo haiondoi ukweli kuwa huwa ninatofauti zangu nyingi na MKJJ na huwa ninamwabia straight lakini vile vile bado tuko OK

mimi sina muda wa kuanza na hizi personality attacks zisizo na kichwa wala miguu na sihitaji kuwa na platform ya pili ili nim criticise MKJJ kwani nishamwambia humu humu

Hata flow ya hiyo post mtaona iko tofauti kabisa na flow zangu. Hopefully nitakuwa niwaoanda doubts za kunishanganya na na huyo ambaye probably milifikiri ni clone wangu
 

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,110
2,000
Hata flow ya hiyo post mtaona iko tofauti kabisa na flow zangu. Hopefully nitakuwa niwaoanda doubts za kunishanganya na na huyo ambaye probably milifikiri ni clone wangu

Mwanzo nilidhani NI WEWE, lakini flow kama ulivyosema hapo juu nikagundua SI WEWE. Ni vigumu kumtetea mtu na kumhukumu kabla ya yeye kusema. Heri umesema. That cleaned out the air. Hapo members mkiwa mnajadili kumbuka Dr. WHO mwandishi wa hii kitu si GAME THEORY! That's it
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom