Elections 2010 Dr. W. Slaa: Shujaa wa Karne YA 21

Sabi Sanda

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
409
31
Kutokana na hali ya matokeo mpaka sasa ya UBUNGE nadiriki kutamka kuwa Dr. Slaa anastahili kuitwa SHUJAA wa KARNE HII YA 21.

Amechangia sana kwa ushindi wa majimbo ya ubunge ambayo CHADEMA wamepata mpaka sasa.

Ni matumaini yangu kuwa Yeye ndiye Rais Wetu Ajae.
 
Tuko pamoja mkuu hata asipopata Urais bado ni rais wa wengi mioyoni. Wabunge ametupa kazi kwetu kuwatumia.
 
Uzuri kila mtu kwa sasa anamjua sasa wakiiba sasa tungoje 2015 uraisi lazima
 
Dr wa ukweli ni shujaa amewatia wazimu ccm hata sasa wanahaha wote kuchakachua matokeo.........
Mabadiliko makuuu yatatokea nyie subiri tu.....
 
Kama kuna mashujaa wa karne ya 21 slaa ni nambari one. Kwa yote yaliyotokea tanzania hii kwa mwaka huu 2010 uchaguzi slaa umebadilisha uipepo wa kiasiasa tanzania hii haijawahi kutokea. Hatujui ilikuwaje lakini watu walikuwa na ari ya kutisha kwenye chaguzi hii. Hatutakusahau kamwe wilbroad peter slaa umetulisha kitu ambacho hatujawahi kulishwa kwenye chaguzi zote zilizofanyika tanzania hii na ccm wanalijua hili kama ingekuwa katiba hii inarusu kupewa shafu serikalini you deserve it. Utaendelea kuwepo mioyoni mwa watanzania na tutakuwa nawe daima mpk mwaka 2015.tunaomba mungu atupe uhai sote tuione hiyo 2015.
Ninachosisitiza ni kuwa kilichobaki ni kuimarisha chama na kuhakikisha hakuna migogoro ya kipumbavu kutokea wakati huu maana tumeshuhudia vyama vingi vinapoteza matumaini baada ya uchaguzi ila kwa chadema hatutaki hili litokee kama wakati wa nccr mageuzi. Mapambano yanaendelea hata nje ya uchaguzi.
Mungu ibariki tanzania
mungu ibariki afrika
 
Sure hadi sasa matunda ya mabadiliko yanaonekana. What is going on now will change our country for the benefit of the poor and marginalized
 
Nadhani sio busara kuzungumzia mambo ya mwaka 2015 kabla ya kusikia matokeo yote. Ni nani ajuaye kuwa Rais wetu ni Dr. Slaa
 
Nashindwa kuelewa kama wabunge na madiwani wamechaguliwa wa chadema iweje wapiga kura haohao wasimchague raisi wao?
 
Tunakata tamaa na mazingira haya ya kuhesabu na kutangazwa matokeo wanavyofanya ndio maana tunakubali tu slaa kashindwa.hatujui kinachotangazwa na makame cha kweli ama la.na wameahirisha mpk kesho usiku huu nkinafanyika nini na nani analinda wa chadema?huu utata mtupu ndio maana tunajikatia tamaa kwamba president wetu atakuwa slaa ama fisadi anarudi tena.
Inauma sana nchi maskini kukosa demokrasia, majimbo yaliyobaki kutangazwa ni magumu kwao na hatujui usiku huu watafanya nini.
 
Dr. Slaa mapinduzi unayoyasikia kutoka pande zote za nchi ni kwa sababu yako. Wananchi tupo nyuma yako usikate tamaa kwani ukombozi upo mlangoni unabisha hodi. Mungu atatuwezesha.
 
Najisikia Faraja sana vile tumefika mbali. Namuombea Dr. Slaa Mungu ampe nguvu zaidi katika siasa. Ametufungua sana macho na Mioyo yetu. MUNGU AKULINDE WAKATI WOTE. YOU'RE THE HERO!
Hawataweza kutuibia Malaika wakuu kutoka mbingu wanatusimamia katika hili. Amen!
 
Kama kuna mashujaa wa karne ya 21 slaa ni nambari one. Kwa yote yaliyotokea tanzania hii kwa mwaka huu 2010 uchaguzi slaa umebadilisha uipepo wa kiasiasa tanzania hii haijawahi kutokea. Hatujui ilikuwaje lakini watu walikuwa na ari ya kutisha kwenye chaguzi hii. Hatutakusahau kamwe wilbroad peter slaa umetulisha kitu ambacho hatujawahi kulishwa kwenye chaguzi zote zilizofanyika tanzania hii na ccm wanalijua hili kama ingekuwa katiba hii inarusu kupewa shafu serikalini you deserve it. Utaendelea kuwepo mioyoni mwa watanzania na tutakuwa nawe daima mpk mwaka 2015.tunaomba mungu atupe uhai sote tuione hiyo 2015.
Ninachosisitiza ni kuwa kilichobaki ni kuimarisha chama na kuhakikisha hakuna migogoro ya kipumbavu kutokea wakati huu maana tumeshuhudia vyama vingi vinapoteza matumaini baada ya uchaguzi ila kwa chadema hatutaki hili litokee kama wakati wa nccr mageuzi. Mapambano yanaendelea hata nje ya uchaguzi.
Mungu ibariki tanzania
mungu ibariki afrika

Inatia moyo kuona kuwa safari ya kuelekea 2015 nayo imeanza.
 
Duuh Kumbe posti ya mwaka jana lakini ukweli umebaki palepale amengia kwenye record ya mashujaa wa nchi hii Mungu amzidishie nguvu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom