Elections 2015 Dr. W. Slaa ni fisadi kuliko Lowassa

FaizaFoxy

Platinum Member
Apr 13, 2011
92,748
108,948
Hilo wala si uongo.

Slaa alikuwa anatuaminisha kuwa Lowassa ni fisadi.

Lakini leo nnaona Slaa kazimwa na Mwenyekiti Mbowe, hasikiki wala haonekani.

Nnauhakika kazimwa kwa ajili ya ufisadi wake na alikuwa anadanganya kuwahadaa Watanzania kuwa Lowassa ni fisadi.

Mimi nnaamini Lowassa ni mtu safi kabisa, hana ufisadi hata chembe, kama anavyoamini Mbowe na wana UKAWA wote na ndiyo maana alivyoingia tu chadema, siku hiyo hiyo kakaribishwa kwa kupewa kadi ya uanachama na siku hiyo hiyo kapewa nafasi ya kugombania Urais wa Tanzania.

Hakuna sababu nyingine yeyote zaidi ya kuwa Lowassa ni msafi, na ana uwezo kuliko mwana chadema yoyote katika uongozi ndiyo maana akapishwa haraka haraka kuchukuwa nafasi ya kugombea urais Tanzania.

Kwa upande mwingine, nnaamini kabisa kabisa kuwa Daktari wa Kanoni Slaa siyo mwadilifu na ni zaidi ya fisadi na ndiyo maana kapigwa chini na chadema na UKAWA kwa ufisdi wake hafai kugombea urais wala hafai kuwa Katibu Mkuu wa Chadema

Hali kadhalika kwa muasisi na aliyetowa wazo la UKAWA na aliyeongoza watu kutoka BMK, Professor Harun Lipumba. na yeye ni fisadi na kahongwa ndiyo maana kaachia Uenyekiti wa CUF.

Kumbe mafisadi tulikuwa nao tena mmoja ni Katibu Mkuu na mmoja ni Mwenyekiti wa vyama vyetu mahiri vya upinzani CUF na CHADEMA, hatukuwastukia mpaka hizi dakika za mwisho.

Ahsante Lowassa kwa kutujulisha kuwa hao ndiyo waliokuwa mafataani waliokuwa wanatukosesha ushindi miaka yote.

Tujadili.
 
Slaa kasema mumuache MACCM Bado mnamchokoza tu,kisa untaka aongee tu,na hawezi kukurupuka cha zaidi atakuumbua humu humu jf,
 
Ili uyaelewe maudhui ya hili bandiko lazima utumie gia ya reverse. Au uproove kuwa Slaa<Ufisadi
 
Mimi nnaamini Lowassa ni mtu safi kabisa, hana ufisadi hata chembe, kama anavyoamini Mbowe na wana UKAWA wote na ndiyo maana leo hii Mbowe alivyoingia tu chadema, siku hiyo hiyo kakaribishwa kwa kupewa kadi ya uanachama na siku hiyo hiyo kapewa nafasi ya kugombania Urais wa Tanzania.

Bibie FaizaFoxy, ukiwa unatunga uongo wako ujue siku zote mwisho wa siku utaumbuka tu! Haya huyo Mbowe unayesema siku aliyojiunga Chadema ndio siku aliyopewa nafasi ya kugombea urais ni Mbowe yupi? Huyuhuyu Freeman au kuna mwingine?
 
slaa kasema mumuache MACCM Bado mnamchokoza tu,kisa untaka aongee tu,na hawezi kukurupuka cha zaidi atakuumbua humu humu jf,

Ataniumbua mimi wakati nnaushahidi wa yeye kumuita Lowassa fisadi? Au nikuwekee umsikie?
 
Kuna kaukweli hapo kwa ushahidi mdogo ule wa kukopa hela za ruzuku ya chama kwa matumizi binafsi
 
Hana wema huyo Faiza Foxy -

Ana wema gani huyo ? Ni sawa sawa na wale waliokuwa wanamwambia Mbowe asimpokee Lowasa

Anataka lake jambo.

Hupati kitu hapa.
 
Nimeamini kimya kingi kina mshindo! Pamoja na kupiga zake kimya mzee wa watu Dr. Slaa bado kuna watu wanapata usingizi wa mang'amung'amu.

Heri ya mchawi kuliko mchonganishi...
 
Hilo wala si uongo.

Slaa alikuwa anatuaminisha kuwa Lowassa ni fisadi.

Lakini leo nnaona Slaa kazimwa na Mwenyekiti Mbowe, hasikiki wala haonekani.

Nnauhakika kazimwa kwa ajili ya ufisadi wake na alikuwa anadanganya kuwahadaa Watanzania kuwa Lowassa ni fisadi.

Mimi nnaamini Lowassa ni mtu safi kabisa, hana ufisadi hata chembe, kama anavyoamini Mbowe na wana UKAWA wote na ndiyo maana leo hii Mbowe alivyoingia tu chadema, siku hiyo hiyo kakaribishwa kwa kupewa kadi ya uanachama na siku hiyo hiyo kapewa nafasi ya kugombania Urais wa Tanzania.

Hakuna sababu nyingine yeyote zaidi ya kuwa Lowassa ni msafi, na ana uwezo kuliko mwana chadema yoyote katika uongozi ndiyo maana akapishwa haraka haraka kuchukuwa nafasi ya kugombea urais Tanzania.

Kwa upande mwingine, nnaamini kabisa kabisa kuwa Daktari wa Kanoni Slaa siyo mwadilifu na ni zaidi ya fisadi na ndiyo maana kapigwa chini na chadema na UKAWA kwa ufisdi wake hafai kugombea urais wala hafai kuwa Katibu Mkuu wa Chadema

Hali kadhalika kwa muasisi na aliyetowa wazo la UKAWA na aliyeongoza watu kutoka BMK, Professor Harun Lipumba. na yeye ni fisadi na kahongwa ndiyo maana kaachia Uenyekiti wa CUF.

Kumbe mafisadi tulikuwa nao tena mmoja ni Katibu Mkuu na mmoja ni Mwenyekiti wa vyama vyetu mahiri vya upinzani CUF na CHADEMA, hatukuwastukia mpaka hizi dakika za mwisho.

Ahsante Lowassa kwa kutujulisha kuwa hao ndiyo waliokuwa mafataani waliokuwa wanatukosesha ushindi miaka yote.

Tujadili.
wewe ile sheria ya mitandao inakuhusu
 
Back
Top Bottom