Kwani chama ni nini? Chama siyo physical object bali sura ya chama hutambulika kwa mwonekano wa viongozi wake yaani misimamo yao na kile wanachoamini, malengo yao, miongozi na zaidi jinsi wanavyoishi kile wanchokitamka.
Wapiga kura wengi walio makini humchagua mtu na wala siyo chama, hiyo ni kwa mataifa yote. Hata chaguzi za mataifa yaliyoendelea kama Marekani, leo hii wanavyoendesha tafiti zao, wanalinganisha wagombea wanavyoungwa mkono, wala siyo vyama vyao jinsi vinavyoungwa mkono.
Si kitu cha ajabu kusikia na kutokea kuwa watu ambao watawachagua wagombea wa CHADEMA, wengi wao watafanya hivyo kwa kuangalia ni nani aliyesimamishwa. Hata mimi nitafanya hivyo maana sera za chama au manifesto havina maana yeyote kama huna imani na msimamizi mkuu, ambaye ni Rais. Kama CHADEMA wasipomsimamisha ambaye dhamira yangu inaamini ana uwezo wa kusimamia mabadiliko, sitamchagua mgombea wa CHADEMA lakini pia sitamchagua mgombea wa CCM.JApo amutegemeae mwanadamu amelaaniwa but Tuko kuangalia nani zaidi anaposema anamaanisha. KAma Dr.Slaa asipoteuliwa kugombea kwa mizengwe ya kinafiki watu wengi hawatapiga kura kabisa. Mwaka 2010 Dr.Slaa alifanya kazi kubwa na hata CDM ikapata wabunge wengi tu kwa mgongo wake.