Dr W. P. Slaa asafishiwa njia Kyela | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr W. P. Slaa asafishiwa njia Kyela

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by amba.nkya, Aug 19, 2012.

 1. amba.nkya

  amba.nkya JF-Expert Member

  #1
  Aug 19, 2012
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 431
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Wana JF, Habari za sikuu ya Eid el Fitri?
  VYAMA mbalimbali vya siasa hapa nchini vimekuwa katika harakati tofauti za kujiimarisha kisiasa na kikubwa kila kimoja kikiwa na lengo la kutaka kushika dola
  Moja kati ya vyama hivyo ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)ambacho kimeanzisha oparesheni nyingi ambazo zinalenga kukiimarisha chama hicho na kufikisha ujumbe kwa jamii juu ya malengo ya chama hicho ya kutaka kushika dola katika Nchi hii
  Oparesheni zilizoanzishwa ni pamoja oparesheni Sangara,Twanga kotekote iliyofanyika wilayani Chunya ikiwa ni pamoja na nyingine nyingi ambazo zimefanyika maeneo mbalimbali hapa nchini na kupelekea jamii kuijua kiundani CHADEMA na madhumuni yake na kuweza kuvua wanachama wengi ikiwa ni pamoja na wengine kuhama kwenye vyama vyao kikiwamo na chama tawala CCM
  Wilaya ya Kyela ni moja kati ya eneo ambalo watu wake wana utashi mkubwa wa kisiasa huku Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt Wilibrod Slaa anatarajia kuzuru wilayani Kyela kwa mujibu wa Ratiba yake kwenye Mkoa wa Mbeya wakati wa Operesheni Sangara ikihuishwa na M4C inayoendelea nchi nzima. Kyela ni moja kati ya wilaya zilizojipanga kuhakikisha kuwa wanatengeneza mazingira yatakayopelekea oparesheni hiyo kuzaa matunda zaidi ya matarajio
  Mlezi wa CHADEMA wilayani Kyela Bw Abraham Mwanyamaki ambaye pia ni Kiongozi wa CHADEMA (Kimara, DSM), Mwanaharakati na mzaliwa wa Kyela hivi karibuni alifanya ziara wilayani Kyela ikiwa ni mwendelezo wa majukumu yake ya kukijenga Chama wilayani Kyela, aliweza kutembelea karibia kata zote za wilaya ya Kyela na kufanya kazi mbalimbali za kukiimarisha Chama hicho kiasi kwamba inaonyesha ni jinsi gani Dkt Slaa alivyosafishiwa njia wilayani Kyela kabla hajaanza Ratiba ya Operesheni Sangara wilayani humo
  Nasema kusafishiwa njia kutokana na mafanikio makubwa aliyoyapata Bw Abraham Mwanyamaki katika ziara yake ya siku 11 wilayani Kyela ambayo imeacha gumzo kubwa kwa jamii ya Kyela ikitafakari juu ya yaliyotokea kutokana na wananchi wengi kukubali mabadiliko ikiwa ni pamoja na makada wa CCM kutimukia CHADEMA na kupatikana kwa wanachama wengi wapya, ikizingatiwa kuwa wananchi hao walivyokuwa wamekishiba Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani humo
  Baadhi ya mambo aliyoyafanya Bw Abraham Mwanyamaki ni kufanya mikutano ya hadhara na harambee kwenye maeneo mbalimbali, kugawa kadi zaidi ya 2,000, mipira, bendera, katiba na mabaraza, kukutana na kuzungumza na wazee wengi. Aidha, ameshiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo ya kijamii kama kuanzisha vikundi vya ujasiliamali vya vijana, kutoa msaada wa kisheria, kuhudhuria mialiko kwenye makanisa mbalimbali, kufanya shughuli za usafi maeneo ya masokoni, mahospitalini na maeneo mengine ambayo yalikuwa na mvuto mkubwa kwa watu kujitokeza kushiriki shughuli hizo ikiwa ni pamoja na wengi kuamua kujiunga na chama hicho
  Bw Abraham Mwanyamaki akizungumza kwenye maeneo mbalimbali aliyotembelea kama vileKata za Ipinda, Matema, Busale, Ikolo, Kyela mjini na mpakani mwa Tanzania na Malawi Kasumulu alisema kuwa wananchi wapo tayari wakihamasishwa kujiletea maendeleo lakini kinachotakiwa ni kuwepo kwa mgawanyo mzuri wa keki ya taifa ambayo hivi sasa inaliwa na wachache
  Alidai kuwa Tanzania haina sababu ya kuwa masikini na kutegemea zaidi misaada bali wananchi sasa wanahitaji kuwa na serikali makini ambayo itaweza kusimamia ipasavyo rasilimali za Wananchi wake kwa kuhakikisha kuwa wananchi wote wanapata mgao sawa wa rasilimali zao ambazo ni haki yao
  ‘’Watanzania tuna fursa nyingi za kujiletea maendeleo kutokana na hazina kubwa ya rasilimali zilizopo; tumekosa tu usimamizi madhubuti na kuwapo kwa watu wenye tamaa za kutaka kujilimbikizia mali na kilichobaki sasa ni kuipata serikali makini yenye watu makini ambao wataweza kusimamia maslahi ya Watanzania na kuwapo watu wenye uzalendo’’
  Katika ziara hiyo ya Mlezi huyo Bw Mwanyamaki ambayo ilianza rasmi Julai 18 na kuhitimisha Julai 28 2012 kwenye viwanja vya siasa mjini Kyela licha ya kuzoa wanachama wengi, kugawa kadi, mipira , katiba na bendera za chama katika maeneo mbalimbali ya wilaya Kyela pia ameweza kufungua Matawi 5 na kukusanya fedha zaidi ya sh. Milioni 7 za harambee toka kwa wanachama na wadau mbalimbali siku ya kilele cha ziara yake.
  Mwenyekiti wa CHADEMA wilayani Kyela Bw Erick Satta baada ya kazi hiyo alisema kuwa CHADEMA moja kati ya vikwazo inayokumbana navyo ni ukata wa fedha na harambee waliyoianzisha katika kila kata italeta mafanikio makubwa za kuendesha shughuli za chama wilayani humo
  Bw Satta alimshukuru sana Mlezi wa Chama kwa kujitolea kwa hali na mali kulea chama wilayani humo na kusisitiza kuwa chama ni cha wanachama hivyo wanachama wenyewe ndiyo wenye dhamana ya kukiendesha chama na ndiyo maana wameona kuwa ni bora sasa wakapita kwa wanachama wao na kufanya harambee ya kukichangia chama ili kisonge mbele
  Alidai kuwa zamani vyama vya upinzani vilionekana kuwa ni vyama vya msimu na hilo CHADEMA hawalitaki na ili kuweza kuifuta dhana hiyo ni lazima kuwepo kwa fedha na wenye uwezo wa kuliwezesha hilo kufanikiwa ni wanachama wenyewe kuchangia chama chao
  ‘’Chama ni cha wanachama hivyo ni vema wenyewe wakazijua gharama za uendeshaji na kujitoa ili kila mmoja aweze kuhoji na kuona kuwa yeye anawajibika moja kwa moja katika kukiendeleza chama na kufikia maendeleo halisi ambayo kila mmoja anayategemea’’
  Katika kuona kuwa Dkt,Slaa anasafishiwa njia ya kuendesha oparesheni Sangara kwa mara ya pili katika mikoa ya nyanda za juu kusini unaweza kuona ni jinsi gani viongozi wa CHADEMA wa mikoa hiyo walivyojipanga katika kuhakikisha kuwa oparesheni hiyo inazaa matunda mara dufu ya yale yaliyopatikanika
  Katibu wa CHADEMA wilayani Kyela Bw Mwiteni Mohammed alipozungumza na majira mara baada ya kuhitimisha ziara yao alisema kuwa kati ya vipindi ambavyo CHADEMA itafanya oparesheni zake kwa urahisi na kuzoa wanachama wangi ni sasa na hii ni kutokana na jinsi ambavyo wao kama viongozi mikoani na katika ngazi zote walivyojizatiti na kuamua kujitoa katika kukitumikia chama ipasavyo
  Bw Mohammed amesema kuwa mapema mwakani mkoa wa Mbeya unatarajia kupokea viongozi wa kitaifa kufuatia oparesheni Sangara na kuwa ifikapo mwakani ni lazima kwanza wao kama viongozi kuhakikisha kuwa chama chao kimejengeka ipasavyo na wakati huo ukifika iwe ni hitimisho la maandalizi ya kushika dola kwa chama hicho
  Kyela ni moja kati ya wilaya ambazo wananchi wengi hawakubaliani na baadhi ya mambo yanayofanywa na serikali kiasi sasa cha kuiona CHADEMA kana kwamba ndiyo mkombozi na hivyo CHADEMA kwa upande wake nayo imejipanga kuhakikisha inafikia matarajio ya wananchi.
  Kuweza kupima mafanikio ya CHADEMA kwa mkoa Mbeya ni jinsi ambavyo wazee walivyoweza kujiunga kwa wingi na kuondoa dhana iliyokuwa imejengeka siku za huko nyuma ambapo vyama vya upinzani vilionekana ni kama vigenge vya wahuni baada ya Wazee kutokuwamo ndani ya vyama vingi vya siasa vya upinzani
  Kyela ni moja kati ya mifano iliyojidhihirisha kwa Wazee kuweza kujitokeza kwa wingi na kujiunga na CHADEMA waziwazi na kueleza mikakati yao namna ya chama hicho kuweza kushika dola na wao kuwa tayari kuhakikisha kuwa wanakilinda chama hicho kuweza kuepukana na migogoro isiyo kuwa na msingi
  Kitendo cha Wazee kumtaka Mlezi wa CHADEMA wilayani Kyela Bw Abraham Mwanyamaki kwenda kuwaeleza viongozi wa juu wa chama hicho kuwa sasa wao hawataki migogoro ndani ya chama, ni moja kati ya mambo yanayotia faraja ndani ya chama hicho kuwa sasa dhamira ya wananchi ni kutaka sasa chama cha upinzani kinaongoza nchi
  Tanzania imeingia katika mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 na kushiriki uchaguzi wa kwanza mwaka 1995 tuliingia kwenye uchaguzi mkuu uliowezesha kupata Wabunge na Madiwani wa kutoka katika vyama vya upinzani, na hali hiyo imeendelea na kuwezesha kupata viti vingi vya ubunge na uwakilishi bungeni na matunda yao imekuwa ni sehemu ya kivutio cha wengi kutaka sasa vyama vya upinzani vichukue dola
  NB: Picha zimeambataniswa zenye baadhi ya matukio ya ziara ya Mlezi CHADEMA Kyela.
  Source: Shuhuda kutoka Kyela
   

  Attached Files:

 2. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #2
  Aug 19, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,640
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Mnamuuzi kikwete, ngoja awapeleke fasta Malawi.
   
 3. M

  Molemo JF-Expert Member

  #3
  Aug 19, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Jamani mbona rahaaaaaaaaaaaa......
   
 4. M

  Makupa JF-Expert Member

  #4
  Aug 19, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  loh, hizi picha ni za wakati wa uchaguzi mkuu 2010 acheni kuwwhadaa watanzania
   
 5. mjombo's

  mjombo's JF-Expert Member

  #5
  Aug 19, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 495
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  jaribu kusumarize next tym its too long
   
 6. tz1

  tz1 JF-Expert Member

  #6
  Aug 19, 2012
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 2,118
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Karibu kukaja
   
 7. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #7
  Aug 19, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hii kasi magamba wanayopelekwa ndiyo unaowafanya wacheze rafu na vikao visivyoisha.mpk kufika 2015 hakuna rangi mtaacha ona
   
 8. Mtanzania1

  Mtanzania1 JF-Expert Member

  #8
  Aug 19, 2012
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 1,169
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  ......he! ikija kuwa sehemu ya malawi???......
   
 9. amba.nkya

  amba.nkya JF-Expert Member

  #9
  Aug 19, 2012
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 431
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Mkuu Makupa, usiwe Tomaso, waache makamanda wafanye kazi, picha hizo are mostly recent, you have to believe
   
 10. S

  STIDE JF-Expert Member

  #10
  Aug 19, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 999
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mh!! Hivi Kyera inapakana na Arusha au Moshi!!? Na huyu Mohammed na Abraham wamebatizwa na nani!!?

  Ccm mnalo mwaka huu!!!
   
 11. amba.nkya

  amba.nkya JF-Expert Member

  #11
  Aug 19, 2012
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 431
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Pamoja mkuu; Mohammed (Mwislamu) na Abraham (MKristu, KKKT) na Kyela ipo kusini, Arusha na Moshi huko Kaskazini, CCM kwa sasa ni kifo cha mfa maji...!
   
 12. tanira1

  tanira1 JF-Expert Member

  #12
  Aug 19, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 938
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  we bwana usitusababishie ban kwani habari ukuilewa? kama za 2010 so what? kwa hiyo 2010 inakuwasha kwa kuwa unajua uliiba?
   
 13. M

  Makupa JF-Expert Member

  #13
  Aug 19, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  mkuu embu ondoa herufi n kwenye jina lako uweke herufi h itakuwa safi sana
   
 14. k

  kipuri Senior Member

  #14
  Aug 19, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 157
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ulieandika huu ***** huijui vizuri Kyela, pale kuna kichwa kinaitwa Harrison Mwakyebe... 2010 viongozi wako walilazimika kumpigia kampeni walipoenda kule baada ya kuambiwa kuwa hawahitaji mbunge mwingine zaidi yake
   
 15. amba.nkya

  amba.nkya JF-Expert Member

  #15
  Aug 19, 2012
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 431
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Pamoja Tanira1, mwambie huyo pengine atageuka
   
 16. amba.nkya

  amba.nkya JF-Expert Member

  #16
  Aug 19, 2012
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 431
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  kipuri, kweli hizi ID zinaficha uhalisia wa mtu, hivi unajua maana ya kipuri au umejipachika tu hiyo ID waulize waliosoma seco miaka ya `80-90 wakuambie maana ya kipuri, waingereza wanasema "No Research No right to Speak", Kyela ya 2010 kwa huyo unayemfagalia sio sasa na alipewa support na CDM kwa wakati huo lakini kwasasa hana chake, fanya utafiti halafu urudi tena na upu....wako. Subiri 2012 uone.
   
 17. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #17
  Aug 19, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  hiyo ipo wazi zaidi Mbeya ni kambi ya upinzani maana ilibaki Kyela tu
   
 18. k

  kipuri Senior Member

  #18
  Aug 19, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 157
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu, Kipuri ni neno la kiswahili sanifu..
  Mi naandika kutoka 'site' najua kinachoendelea sasa kyela, by the way mwaka 2012 si ndio huu au....
   
 19. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #19
  Aug 19, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  halafu hili jimbo alisema hatagombea tena ni kama lipo wazi vile
  na hawa watu walimpa kura Dr
   
 20. amba.nkya

  amba.nkya JF-Expert Member

  #20
  Aug 19, 2012
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 431
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  I mean, from now 2012 to 2015, hiyo site ipi hasa? yaelekea haupo Kyela kwasasa, afterall, huyo Dr alishatamka hagombei tena au ni kigeugeu?, jitahidi kufanya utafiti mkuu
   
Loading...