Dr.Ulimboka ni nani mgomo wa madaktari? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr.Ulimboka ni nani mgomo wa madaktari?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Independent Voter, Jul 3, 2012.

 1. I

  Independent Voter JF-Expert Member

  #1
  Jul 3, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 279
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kuna taarifa za serikali zinasema kwamba Dr.Ulimboka sio mtumishi wa serikali,swali langu je ni kweli kwamba jamaa sio mtumishi wa serikali?na je kama sio muajiriwa wa serikali alikua anashiriki kwenye mazungumzo kati ya serikali na ma dokta ambao ni waajiriwa wa serikali kama nani?

  Msaada tutani kwa wanaoufahamu undani wa ushiriki wake kwenye harakati za migomo
   
 2. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #2
  Jul 3, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,127
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Inaelekea ulimwelewa Kikwete Katika lile alilotaka ulielewe.Ukweli ni kwamba madaktari kama wanataaluma wanamadai na Dr Ulimboka Kama mwanataaluma mwenzao alichaguliwa kuwakilisha madai hayo..ni jambo la kawaida kwa wanataaluma.
   
 3. M

  Makalla23 New Member

  #3
  Jul 3, 2012
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dr Ulimoka ni Mtanzania mwenye uraia wea Tanzania ili atetetee Watanzania katika kuhakikisha watanzania wanapata huduma bora hasa wale wa vijijini, maskini na wale wasioweza kwenda ulaya kupata matibabu.

  Dr Ulimboka sio mbinafsi na ndio maana anawatetea waajiriwa wa serikali maana Watanzania wote kama hujatibiwa hospitali ya serikali maishani mwako basi ulipelekwa huko wakati mama yako ni mjamzito ama ndugu/ jamaa / rafiki ashawahi kutibiwa huko.

  Dr Ulimboka, ni mtu wa Watanzania wote ndio maana anatetetea hospitali zetu ziwe bora hasa kwenye upande wa vitendea kazi, madawa n.k.

  pata mfano huu, serikal;i inasema huduma kwa watoto chini ya miaka 5 ni bure.

  swali: je, kuna practical katika hili? bora waseme,..."MATIBABU NJE YA NCHI,NYUMBA,POSHO, LANDCRUSER VX8 NI BURE KWA KILA KIONGOZI WA SERIKALI".

  pia wanasema "HUDUMA KWA WAJAWAZITO NI BURE"
  SWALI: JE, NI KWELI? ULISHAWAHI KWENDA MWANANYAMALA, AMANA AU TEMEKE UKAONA HOSPITALI ZINAVYOJAA NA WAJAWAZITO WANALALA CHINI? UMEONA WANAVYOKOSA DAWA? je, ushawahi kuona mke wa kiongozi anakwenda huko kujifungua?

  Dr Ulimboka, anawatetea wote hao, watoto na wajawazito.

  huyo ndiye dr Ulimboka....kama bado una swali...uliza
   
 4. m

  majebere JF-Expert Member

  #4
  Jul 3, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,520
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280
  Uli alikua ni kibaraka wa chadema, alivyo shindwa kazi magwanga wakaamua kuua
   
 5. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #5
  Jul 3, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,127
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Inaelekea ulimwelewa Kikwete Katika lile alilotaka ulielewe.Ukweli ni kwamba madaktari kama wanataaluma wanamadai na Dr Ulimboka Kama mwanataaluma mwenzao alichaguliwa kuwakilisha madai hayo..ni jambo la kawaida kwa wanataaluma.
   
 6. h

  hukumundo JF-Expert Member

  #6
  Jul 3, 2012
  Joined: Oct 8, 2011
  Messages: 764
  Likes Received: 267
  Trophy Points: 80
  Dr. Ulimboka ni kiongozi wa jumuiya ya madaktari. Nitoe analojia labda. Endapo kiongozi wa chama cha wafanyakazi nchini ataungana na walimu wa shule za serikali kudai maslahi yao na mashule yao, je atakuwa amefanya kosa? Hali kadhalika, basi, ninaona ni halali kabisa na wala sioni utata wowote kwa Dr. Ulimboka kuongoza harakati za madaktari wa serikali ilhali yeye si mfanyakazi wa serikali.
  Tuache kushabikia serikali. Huu si mchezo kama mpira. Maisha ya watu yamo hatarini, maisha ya vizazi vijavyo yamo hatarini kama mambo hayarekebishwi. Kila mmoja wetu anajua kwamba serikali inafanya vibaya sana na kila mara inapotosha ukweli wa mambo. Wakati umefika wa kuiwajibisha serikali. Lazima tubadili uelekeo.
   
 7. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #7
  Jul 3, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,127
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  It a sin to implicate someone in a political move without evidence. You are a devil advocate and hell is where you belong
   
 8. KOMBESANA

  KOMBESANA JF-Expert Member

  #8
  Jul 3, 2012
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 862
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  kuna Majebere moja ilisoma hapa mkoa wa pwani f v na vii miaka ya 1990s na alipenda sigara fulani vile ambayo hawauzi dukani.isijekuwa bado unaendelea kuivuta mkuu wangu.Yaani sasa hata mvua zisiponyesha watakuwa ni Chadema na magwanda yao?
   
 9. Wachovu

  Wachovu JF-Expert Member

  #9
  Jul 3, 2012
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 1,197
  Likes Received: 388
  Trophy Points: 180
  Kwani Mr Mgaya yule mzee aliyesutwa na Rais alikuwa ni mfanyakazi wa serikali , kuwa kiongozi sio lazima uwe mwajiriwa wa serikali
  Shida kubwa humu kuna vilaza wengi
   
 10. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #10
  Jul 3, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Unaweza kunisaidia namba ya usajili ya chama hicho kinachodaiwa kuongozwa bwana Ulimboka.Kitu kingine tusisahau kwamba ulimboka ni muajiriwa huko mtaani ambako kuna watu wanasubiri huduma yake na wengine kupoteza maisha yao kwa kumsubiri yeye ambae muda mwingi amekua akiutumia kushughulika na migomo ambayo ingeweza kushughulikiwa na inaowahusu,hivi ina maana yeye ulimboka analipwa vizuri sana na muajiri wake huko mtaani?kama hapana mbona hatujasikia akimgomea muajiri wake huyo,anaogopa nini kufanya hivyo?
   
Loading...