Dr Ulimboka atoa tamko, amtaja Ramadhani Ighondu

Status
Not open for further replies.
amechelewa sana, angeongea mapema heshima yake ingekuwa juu kinoma

Wakati mwingine tuwe wakweli jamani watanzania tumezoea kukaa kwenye keyboard na kushangaa tuuuuuu......haya huyo Ulimboka angetoa hiyo ripoti mapema nani angefanya nini??? Zaidi sana tungekuja humu ndani na kubaki na Aaaah..........Eeeeeeeeeeh ...............Kumbe!!!!!!.........mwanahalisi walitoa na wakafungiwa wewe Nazjaz umewasaidia nini mpaka sasa hivi??...............tuache unafiki labda wataacha kucheza na akili zetu!
 
Last edited by a moderator:
Habari zilizopendwa. Kwa sasa ni RPC (RIP) B & uchomaji wa makanisa. Tunaomba atusaidie kurudisha gazeti letu la Mwanahali. Angetoa taarifa hii mapema lisinge fungiwa.
 
Shahidi namba moja wa kusaidia Jamhuri, kuhusu kutekwa, kusukumizwa kwenye gari, kupigwa, kufungwa mikono na Miguu, kunyofolewa kucha na kutolewa meno na hatimaye kutupwa katika Misitu ya Mabwepande, Dr. Ulimboka Stephen Mwenyewe amesema kuwa aliyemtesa yeye ni Ramadhani Abeid Mohamed Ighondo. Hakumtaja Mkenya Joshua Mlundi. Aliyeteswa anamjua aliyemtesa. Polisi walikuwa wanatuhadaa katika tukio hili kama walivyotuhadaa katika Tukio la Mwangosi...... tutaendelea kweli kuona mafuta ya walipa kodi yanampeleka Joshua Mlundi Mahakamani wakati Ulimboka hajamtaja katika taarifa yake aliyofunguka leo? Aibu kwa serikali yetu kuwa ya kijinga kiasi hiki.


Mkuu mbona kwenye thread nyingine wamesema aliyempigia simu ndiyo Ramadhan Ighondu,sasa hii ya kusema aliyempiga ndiyo huyohuyo mbona inatuchanganya sasa?
 
Serikali haiwezi kuunda tume huru itakayowachoma kisu cha mgongo. Jambo la msingi ni kwamba watanzania tumefahamu kwa uhakika aliyemteka na kumtesa, kazi iliyopo sasa ni watanzania kumlinda kwani serikali hii kwa aibu inayoipata na itakayoipata haichelewi kuandaa part II.
 
Alikuwa wapi leo ya Shehe Mponda na Farid yanazuka ndio anaingia nae Ulimboka hakuna atakaekuamini hata umtaje aliekungoa kucha.
 
Hiyo movie scriptwriter ni LIWALO NA LIWE. Kama utategemea Ramadhani Ighondu akamatwe basi subiri mpaka ujio wa kristo.
 
Jamani, huyu Dr. Alikuwa bado anamonitor afya yake, na alikuwa anatafuta the njia sahihi ya kuaddress hii issue kwenye public.Mimi nadhani ameona kuwa muda muafaka umefika wa kuongea na ameamua hii issee aipeleke kisheria zaidi.Maana what they did to him ulikuwa ni unyama.Ukizingatia hii kesi yake iko mahakamani,wasinge mruhusu yeye kuiongelea.Nadhani amepata advise nzuri kwa hii approach aliyoamua kuitumia.It is a step forward,kama tuliweza kuwa naye kipindi chote alichokuwa anaumwa mpaka akapona,mimi naona ni busara tumuache atatuambia ni nini actually kilitokea as hizi information alizoreveal leo ni muhimu sana na changamoto kwa jeshi la polisi.Amesema kuna watu hawataki yeye aongelee hii issue but he will do so kwa kupitia wanasheria wake.
 
Tanzania ni nchi ya magenius wameshasoma mchezo kitambo wakaona hakuna kitu hvy hata akitoka akaongea watu wataona porojo sababu amesubiri hamu imeisha ndio anataka kuwalisha wakati wameshazoea na njaa yenyewe

KAMA WEWE NI MTAFUTA HAKI,HUWEZI KUISHIWA HAMU YA KUTAFUTA UKWELI NA KUUPIGANIA VINGINEVYO WEWE UNAFAA KUWA KATIKA KUNDI LILE LA WACHA UPEPO UPITE...

.NA UNAJIHALALISHA KUWA WATZ WA AINA YAKO NI WATU WA MATUKIO TU NA HAMUWEZI KUFUATILIA LOLOTE SABABU NIA YAKO NI KUANGALIA MATUKIO KAMA BURUDANI NA SI KUCHUKUA HATUA. ...na watu tumejaaliwa hatua tofauti...hatua yako moja inaweza iwe tofauti na mwingine..yako inaweza kuwa fupi zaidi au ya kurudi nyuma badala ya kwenda mbele...kila unalolifanya angalia lina faida gani kwa wanaoukuzunguka
 
Do, Mimi naisikitikia tu Serikali hii. Kweli sasa naamini wafanyakazi wake wengi shule hakuna. Sasa Verse ya kwanza aliflow Kova sasa ya pili ndo hiyo sasa, let us wait verse ya tatu, hope mzee wa kaya atashika mike.
 
amefanya bad timing. Sasa hivi tuna sakata la kidini, barlow na kadhalika. Tuombe tu ishu yake ifunike haya mengine
Hakuna cha timing,tumieni akili,kuna procedures,aliyetajwa ni mtu wa usalama wa Taifa.Nyie na vivuli vyenu humu ni heri muufiche ujinga wenu.Mashabiki tu.

Na wengine kusema eti sijui muvi mara eti sijui mnafiki!Wanafiki ni nyie mnaotumia majina bandia na kutukana watu humu huku mkijidai eti mna msimamo na hamwogopi.

Unafiki ni asili ya watz wengi.Akili za kitoto sana humu,tope kabisa,eti timing sijui mara kuhusu makanisa kuchomwa,akili kama za kuazima,sijui ni utoto ama ni kitu gani.

Hata kama this is the home of great thinkers,uwezo wa kununuwa simu na kuingia humu JF hauhitaji great thinking,ndo maana kuna ***** humu kila uchao.

Badala ya kushurutisha hatua zichukuliwe kwa waliotajwa,badala ya kuibana serikali,eti mafala wanakuja kusema eti timing!Upuuzi mwingine bana!No wonder JK alisema ni upepo tu utapita,maana anafahamu sana akili za mibongo zilivyokuwa hovyo.
 
itakuwa wamemrusha hela za ahadi,na leo nimeona watoto wanaandamana kudai chao serikal haina ela baba mwanaasha kasafri na ufunguo wa store ya mahela

This is exactly what happened!!! Mahela waliyomwahidi hakupewa na sasa anapoteza muda kueleza kitu ambacho mjadala wake ulishafungwa.

Wakati kuna tetesi kuwa amepewa hela mbona hakukanusha kama ilikuwa uongo? Inakuwaje anajidai sasa kusema sema mbofu!!!!! Malipo ya kununuliwa ndiyo hayo!!!
 
Wadau tuandamane ili serikali ifungulie gazeti letu la Mwanahalisi.
 
amenifanya nilikumbuke Mwanahalisi,manake ni kama amedesa tu.!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom