Dr. Sulle "Mafanikio ya Simba ni sababu ya maneno ya Haji Manara, sio Yanga walikuwa hawana timu''

LIKUD

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
15,106
27,085
Mhadhiri na mhutubu maarufu Dr Sulle amedai kuwa maneno ya aliyekuwa Msemaji wa Klabu ya @simbasctanzania Haji Manara yalikuwa na mchango mkubwa kwenye mafanikio ya timu hiyo na wala sio kuwa watani wao wa jadi Yanga walikuwa hawana timu lahasha.

Dr Sulle anaamini #simbasc msimu ujao haitakuwa na mafanikio makubwa ukilinganisha na miaka hiyo minne ambayo Manara alikuwa akiitumikia kwakuwa anaamini 'Propaganda' za Marana zilikuwa na nguvu na kuwaogopesha wapinzani.

''Vurugu zote mlizoziona miaka minne za Simba ni mineno ya Manara basi, sio kwamba Yanga walikuwa hawana timu lakini ule mdomo wa Manara ulikuwa unawatisha, mkitaka kubisha subirini baada ya kutoka kwake mtaona kama itafanya vizuri mwakani Propaganda ni kitu kikubwa kuliko mnavyofikiria.''- Dr Sulle

MANARA.jpg
 
Kama kweli huyu ni mhadhiri basi anaowahadhiri nawapa pole sana.

Manara amebebwa na uwekezaji uliofanywa miaka hiyo unayosema.

Wakati Simba anaingia fainali za CAF huyo Haji alikuwepo?

Masuala mengine angewaachia mashabiki wasio na elimu maana msomi hawezi kuja na conclusion ya kizembe namna hii
 
Mhadhiri na mhutubu maarufu Dr Sulle amedai kuwa maneno ya aliyekuwa Msemaji wa Klabu ya @simbasctanzania Haji Manara yalikuwa na mchango mkubwa kwenye mafanikio ya timu hiyo na wala sio kuwa watani wao wa jadi Yanga walikuwa hawana timu lahasha...
Sasa Yanga wamchukue basi Manara, halafu tuone kuanzia msimu ujao kama Yanga itaweza kufanya iliyoyafanya Simba misimu minne mfululizo.

Tusisahau na achievement ya Simba Champions league ndani ya hiyo miaka.
 
Hivi ni mimi tu siajamuelewa huyo Dr. Sule. Kwa mfano Manara akienda kuwa msemaji wa Mbeya City au Kagera Sugar kwa misimu minne je watapata mafanikio kwa misimu minne ijayo kama ilivyokuwa Simba.

Kuhusu kuwa kuanzia sasa Simba haitapata mafanikio eti kwa sababu Manara kaondoka sio kweli kabisa. Kitakachotishia ufalme wa mafanikio ya Simba kuanzia msimu ujao ni vitu vitatu vikubwa navyo ni.

1. Udhamini wa AZAM media wa mamilioni ambao utasaidia sana hata vilabu vidogo kuwa na uwezo wa kusajili wachezaji wazuri, kuweka kambi na posho kwa wachezaji wao, n.k. Kwa hiyo timu kubwa hazitapata ushindi kirahisi dhidi ya timu ndogo kwenye ligi msimu ujao.

2. Yanga walianza kujenga timu yao misimu miwili iliyopita na imeanza kukaa vizuri na kocha waliye naye sasa hivi ni kocha mzuri. Kwa mwaka huu katika usajili wa Yanga watakuwa wanamalizia sehemu chache sana zenye mapungufu kwa hiyo timu yao itakuwa ipo tayari kupambana na Simba kikamilifu.

3. Usajili waliofanya AZAM mwaka huu nao ni mzuri sana na wameonyesha ni jinsi gani watakuwa tayari kupabana kutafuta makombe mwaka huu. Iwapo Simba na Yanga hawatajipanga vizuri basi wajue tu kuwa AZAM mwaka huu timu ya wanaume siyo ya wavulana tena.
 
Mhadhiri na mhutubu maarufu Dr Sulle amedai kuwa maneno ya aliyekuwa Msemaji wa Klabu ya @simbasctanzania Haji Manara yalikuwa na mchango mkubwa kwenye mafanikio ya timu hiyo na wala sio kuwa watani wao wa jadi Yanga walikuwa hawana timu lahasha.

Dr Sulle anaamini #simbasc msimu ujao haitakuwa na mafanikio makubwa ukilinganisha na miaka hiyo minne ambayo Manara alikuwa akiitumikia kwakuwa anaamini 'Propaganda' za Marana zilikuwa na nguvu na kuwaogopesha wapinzani.

''Vurugu zote mlizoziona miaka minne za Simba ni mineno ya Manara basi, sio kwamba Yanga walikuwa hawana timu lakini ule mdomo wa Manara ulikuwa unawatisha, mkitaka kubisha subirini baada ya kutoka kwake mtaona kama itafanya vizuri mwakani Propaganda ni kitu kikubwa kuliko mnavyofikiria.''- Dr Sulle

View attachment 1878989
Aende Al Ahaly..wamechukua ubingwa wa Africa bila kua na mtu kama Haji manara,tuache ujinga wakati mwingine
 
Back
Top Bottom