Dr. Slaa: Zanzibar ni lulu.......... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Slaa: Zanzibar ni lulu..........

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Oct 26, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,785
  Trophy Points: 280
  Gazeti la Tanzania Daima limetuhabarisha leo ya kuwa Dr. Slaa katika mkutano wake wenye mafanikio makubwa kule Zanzibar aliwaahidi wazenji hao vinono kubekebe vikiwemo vya kuaachiwa kufaidi mafuta yao kama yakipatikana bila zengwe lolote la utawala wake mpya unaotarajiwa kuchukua madaraka ya dola hivi punde..

  Pia aliwaahidi kuhamasisha uwekezaji nchini humo na hivyo kupafanya pawe na vivutio vingi kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi..................Hivyo Zanzibar ni lulu haswa......
   
 2. MTWA

  MTWA JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2010
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 1,024
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Ngoja awape ya ukweli wasahau machungu ya mda mrefu!
   
 3. F

  Fanfa JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2010
  Joined: Sep 25, 2009
  Messages: 538
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Umati uliofurika hata mie sikuamini kama anaweza akapata watu zenji wengi kiasi hicho. Ukizingatia hawakusombwa na malori.

  Dr. Slaa anachana mbuga na mwaka huu ni wa ukombozi. Saa ya ukombozi ni sasa
   
 4. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2010
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Dk. Slaa: Zanzibar ni lulu
  • Kuiaga Dar kwa kishindo Mwembeyanga leo

  na Waandishi wetu
  MGOMBEA urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amesema Zanzibar ni lulu na dhahabu ya maendeleo ya kiuchumi kwa taifa.

  Akihutubia mkutano uliohudhuriwa na mamia ya wananchi katika viwanja vya Garagara, Mkoa wa Mjini Magharibi jana, Dk. Slaa alisema iwapo atashinda urais katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumapili wiki hii, atahakikisha anavirejeshea hadhi ya juu ya maendeleo visiwa vya Unguja na Pemba ambavyo ni hazina ya utajiri mkubwa wa taifa.

  Mgombea huyo wa urais alisema kihistoria tangu zama za kina Vasco da Gama Zanzibar imekuwa ni kitovu kikuu cha maendeleo ya biashara na utalii, hadhi ambayo imevurugwa na utawala wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

  Alisema iwapo atapata fursa ya kuwa rais wa Tanzania atahakikisha anairejeshea Zanzibar hadhi yake ya kuwa kitovu cha utalii na biashara ya fedha kwa kuifanya kuwa bandari huru kwa maana yake halisi na si kama ilivyo leo.

  Mbali ya hilo, Dk. Slaa ambaye alikuwa akishangiliwa kila alipokuwa akihutubia alisema ni jambo la kusikitisha kwamba pamoja na wataalamu kugundua na kuthibitisha kuwapo kwa nishati ya mafuta Zanzibar, uchimbaji wake umekwama kutokana na ubinafsi wa viongozi wa CCM.

  Alisema wataalamu bingwa wa masuala ya mafuta kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) tayari walikwisha kuwasilisha sampuli ya mafuta yanayopatikana Zanzibar bungeni na wabunge kushuhudia.

  Hata hivyo, alisema nishati hiyo inashindwa kuchimbwa na kuwanufaisha Wazanzibari kutokana na kuwepo ubinafsi huo pamoja na wananchi wa Zanzibar kuhofia mafuta hayo kunufaisha upande wa pili wa Muungano.

  Kauli ya Dk. Slaa imekuja huku Baraza la Wawakilishi Zanzibar likiwa limepitisha azimio la mafuta kuondolewa katika orodha ya mambo ya Muungano, ili yaweze kuwanufaisha wananchi wa Zanzibar.

  Akishangiliwa na wanachama wa CHADEMA pamoja na wananchi waliohudhuria mkutano huo, alisema suala la mafuta litaendelea kubakia la Wazanzibari na gesi iliyopo Tanzania Bara itanufaisha wananchi wa upande huo wa Muungano.

  “Ndugu zangu wananchi, mafuta yameshindikana kuchimbwa kwa sababu ya ubinafsi wa viongozi, mie nasema mafuta yatabakia ya Zanzibar pamoja na gesi itabakia ya Tanzania Bara,” alisema mgombea huyo wa urais.

  Aidha, alisema kamati ya kutatua kero za Muungano inayoongozwa na mgombea urais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein, imeshindwa kutatua kero za Muungano na badala yake zimezidi kuongezeka.

  Aliwaeleza wananchi kwamba kamati hiyo imekuwa ikifanya vikao vingi na kupoteza fedha, lakini kwa bahati mbaya utatuzi huo haupatikani na umebaki kwenye makaratasi.

  Alisema Zanzibar hivi sasa inachechemea kiuchumi, licha ya kuwa nchi za visiwa ni sawa na dhahabu na lulu kutokana na maumbile ya nchi kama hizo kuwa kivutio na zenye rasilimali nyingi, lakini mipango hakuna.

  Alitoa mfano wa nchi za visiwa kama Seychelles, ina viwanda vingi vya nguo wakati haizalishi pamba, lakini Zanzibar inashindwa hata kuwa na viwanda vidogo vidogo na vya kati, wakati sekta hiyo ni muhimu katika kuongeza fedha za kigeni na ajira kwa vijana.

  Mgombea huyo aliwakumbusha wananchi suala la uchaguzi kuwa wasikubali viongozi wanaotoa ahadi za kujenga barabara, reli na kununua Bajaj, wakati masuala hayo ni sawa na kuingilia majukumu ya maofisa mipango wa serikali.

  Alisema rais hapaswi kutoa ahadi kama hizo, kwa vile yeye ni msimamiaji wa mpango mkuu wa dira ya maendeleo serikalini na ahadi zinazotolewa na mgombea wa CCM, Jakaya Kikwete, ni jukumu la serikali na hakuwafanyia wananchi kama hisani.

  Mgombea huyo alisema serikali yoyote inayokusanya kodi kwa wananchi ina wajibu wa kuhakikisha wananchi wanapata huduma muhimu kama vile maji, barabara na wananchi wasione wamepewa msaada kwa vile huduma hizo zinatokana na kodi zao.

  “Tunataka kuona Zanzibar ya kipekee, yenye lulu na dhahabu ya kweli, Serikali ya Muungano itatoa mwongozo na kuweka mamlaka ya Rais wa Zanzibar ndani ya Muungano,” alisema.

  Dk. Slaa alisema sera ya CHADEMA kuhusu Muungano iko bayana, ni muungano wa serikali tatu, ambao ndio utakaoondoa manung’uniko baina ya pande mbili za muungano huo.

  Kwa upande wake, mgombea mwenza wa Dk. Slaa, Said Mzee, aliwaponda watu wanaokihusisha chama hicho na udini na kusema watu hao wamefilisika kisiasa kwa sababu hakuna ilani ya chama chochote inayosema kitaongoza kwa misingi ya udini kikipata uongozi.

  Aliwataka wananchi wa Zanzibar kuwa waangalifu na propaganda zilizotengenezwa na kusambazwa na CCM, baada ya kuona CHADEMA imeiweka CCM katika hali mbaya kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Jumapili ijayo.

  Katika hatua nyingine, mgombea mwenza huyo amevitahadharisha vyombo vya habari vya serikali kuacha kucheza ngoma wasiyoifahamu, badala yake warudi kwenye mstari kufanya kazi kwa mujibu wa taaluma yao.

  Alisema baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikifanya kazi ya kuchonganisha viongozi wa vyama na wananchi, vitendo ambavyo ni kinyume cha maadili ya uandishi wa habari.

  Hata hivyo, alionya kuwa tabia kama hiyo inaweza kulisababishia maafa makubwa taifa na waandishi wa habari kupata matatizo kama ilivyotokea mwaka 1994 nchini Rwanda.

  Suala la mafuta ya Zanzibar limetajwa sana katika mikutano ya kampeni, ingawa mgombea urais wa Zanzibar kupitia CCM, Dk. Ali Mohammed Shein, amekuwa akiligusia katika hotuba zake kwa tahadhari kubwa.

  Dk. Slaa leo anatarajiwa kuhitimisha kampeni zake mkoani Dar es Salaam kwa kishindo katika viwanja vya kihistoria vya Mwembeyanga.

  Katika mkutano huo unaotarajiwa kurushwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha TBC, Dk. Slaa anatarajiwa kuzungumzia masuala na sera nyeti zikiwamo za ulinzi na usalama, umijishaji, michezo na nyinginezo ambazo hajazijadili kwa kina katika hotuba zake za kampeni mikoani.

  Mwembeyanga ndio uwanja aliotumia Septemba 15, 2007 kutanganza hadharani majina ya watuhumiwa wa ufisadi 11, waliotafuna nchi hii na kuamsha kwa kasi hisia za upinzani nchini.

  Kabla ya mkutano huo, atahutubia mikutano ya kampeni katika maeneo ya Bagamoyo na majimbo kadhaa ya Dar es Salam

  Source: TANZANIA DAIMA
   
 5. c

  chamajani JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2010
  Joined: Sep 22, 2010
  Messages: 554
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ili awachilimue!
   
 6. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #6
  Oct 26, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Safi sana ,chanja mbuga!huu ndiyo wakati wako!!!!
   
Loading...