Dr. Slaa, wewe unanisaidiaje ktk matatizo haya yanayonipata mwanachama wako?

Eti dr slaa! Ondoa hayo mawazo mgando, foleni ya Dar haiwezi kuondolewa na mtu mmoja.
 
Ideal nzuri ila hata dr akijibu hilo swali la kufirika majibu yake nayo yatakuwa ya kufikirika mi naona asijibu tuu!

Kisimba G,
Kitu cho chote kinachotendwa lazima kwanza ianze na kufikiri hata kusema inaanza fikra ndo unaongea au unatenda. Suluhisho la tatizo lo lote lazima liwe dabated kwanza kwa njia ya fikra sahihi then utekelezaji wa jambo hilo unaanza. Kwa mantiki hiyo, tukitaka suluhisho la foleni tuanze na mjadala mzito wa fikra kwanza ndo tutekekeleze kile tunachodhani kinatekelezeka.
 
Na ifahamike kuwa nikikokotoa hasara inayotokana na muda tunaopoteza njiani sote tuanaofanya kazi ktk jiji la Dsm, Ni sawa na kujiingiza ktk umasikini usio na sababu kwa makusudi. Huku tunasherehekea miaka 50 ya uhuru kwa kutumia BIL karibu 70. Tafakari.

Halaiki inasemekana iliandaliwa na wakufunzi kutoka china.
 
Eti dr slaa! Ondoa hayo mawazo mgando, foleni ya Dar haiwezi kuondolewa na mtu mmoja.

Foleni za DSM na mikoa mingine zinasababishwa na miundombinu mibovu inayoletwa na Serikali legelege ya CCM.

MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
 
Dr Slaa anaweza kujibu au asijibu. Majibu yako na wengine ndo lengo la makala yangu. Ingewa personal kwa Dr Slaa ningempigia simu au kumtumia yeye binafsi. Mjadala unaendelea kwenye uzi huu ndio lengo lenyewe. Kufikirisha watu na kuwaamsha ili wajue kwa undani hasara ya foleni.

"Dr. Slaa, wewe unanisaidiaje ktk matatizo haya yanayonipata mwanachama wako?" HIKI SI NI KISWAHILI MKUU, AMA MIE NDIO SIELEWE? ok umeifanya personal sana kamanda, anyway premises na conclusion haviendani plus majibu yako. siyo mbaya ukijipanga Upya kwenye hiyo title yako.
 
Mkuu kwa mtazamo wangu naona Premises na conclusion ziko sahihi na zina match.Heading nayo ni sahini. Mkuu kwenye kichwa cha habari huwa tunaandika kihabari.

Tz daima ya Leo inasema ' WAZIRI MEMBE AIKOROGA CCM' Kiuandishi ambao nimeusomea kidogo kwa hiyo ni sahihi pia. Unawezaje kuikoroga ccm? CCM inakorogeka kama unga kwenye maji? Kama gazeti la Tz daima wamekosea na mimi nimekosea. Ila kwa ujumla sote mimi na Tz daima tuko sahihi.

Mkuu pompo kwa ujumla tuko pamoja kaka.
 
Good analysis... too bad that you wont get feedback from JK, his part and his team... what happen that for the past 50 years nothing has been done by them to overcome this?????. Good move that you need Dr. slaa comments has he aspire for the presidential seat....we are waiting!!!!
 
Dr SLAA hebu jitokeze ujibu hoja za Mdau. Ni muhimu kwako binafsi au kupitia katibu wa uenezi JJ Mnyika akakusaidia lakini kupitia maelekezo yako. Hii ni fursa ya kuujuza umma wa Watanganyika hasa wa DSM ungewasaidiaje kupunguza adha ya foleni?

Ndimi Bazazi!
 
Lakini tukiangalia kwa undani zaidi swali hili ilipaswa kuulizwa Kikwete na Serikali yake.

Dr. Slaa hana uwezo wa kusema neno ha[a zaidi kama tunataka atuletee Siasa tu.

MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
 
Lakini tukiangalia kwa undani zaidi swali hili ilipaswa kuulizwa Kikwete na Serikali yake.

Dr. Slaa hana uwezo wa kusema neno ha[a zaidi kama tunataka atuletee Siasa tu.

NABII MTARAJIWA!!!

MIZAMBWA
mizambwa! Ni kweli lakini aje tupime hoja zake kama kweli zingefanikiwa kupunguza kama sio kuondoa msongamano wa magari.

Unajua mizambwa kuna mambo mengi ya kufanya ili kupungua foleni.
1. Acha kuendelea kujenga maghorofa katikati ya mji.
2. Punguza ofisi za serikali zilizoko katikati ya mji
3. Anzisha miji ndani ya mji iliyokamilika. Jiulize angalau Mlimani city kumepunguza watu wangapi wa kuingia kariakoo na posta?
4. Fungua njia zingine za kutoka katikati ya mji. Mfano fungua njia ya kutokea K'ndoni makaburini toka maeneo ya mahakama ya kisutu.
5. Nk, nk, nk, nk, nk, nk, nk

Ndimi Bazazi!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu kwa mtazamo wangu naona Premises na conclusion ziko sahihi na zina match. Heading nayo ni sahini. Mkuu kwenye kichwa cha habari huwa tunaandika kihabari.
Kubali ukweli mkuu uzi huu umeelekezwa kwa mtu mmoja dr. slaa. kama vipi edit uzi ili tuchangie
 
MIZAMBWA
mizambwa! Ni kweli lakini aje tupime hoja zake kama kweli zingefanikiwa kupunguza kama sio kuondoa msongamano wa magari.

Unajua mizambwa kuna mambo mengi ya kufanya ili kupungua foleni.
1. Acha kuendelea kujenga maghorofa katikati ya mji.
2. Punguza ofisi za serikali zilizoko katikati ya mji
3. Anzisha miji ndani ya mji iliyokamilika. Jiulize angalau Mlimani city kumepunguza watu wangapi wa kuingia kariakoo na posta?
4. Fungua njia zingine za kutoka katikati ya mji. Mfano fungua njia ya kutokea K'ndoni makaburini toka maeneo ya mahakama ya kisutu.
5. Nk, nk, nk, nk, nk, nk, nk

Ndimi Bazazi!

Bazazi
Hawa CCM kutwa hawana sera wameshaishiwa hawana mpya. Hivyo wao wana-copy & paste tu.

Yaani hapa naona mnataka tumsumbue Mh. Slaa kuumiza kichwa chake ili CCM watumie michango yake na kisha mwaka 2015, mjigambe kuwa mmefanikiwa kumbe ikiwa CCM vichwa vimeingia maji tayari.

Kwa kuwa tulipewa nafasi mwaka 2010 kuchagua Rais wa kuongoza na sisi wananchi tukamchagua Kikwete; Basi tusubiri hadi mwaka 2015 tufanye maamuzi mapya.

Sioni sababu ya kumlazimisha muheshimiwa wangu aje hapa kujibu hii hoja kuhusu suala ambalo linapaswa kutekelezwa na Serikali. Je, kwani Dr. Slaa ana nafasi gani katika Serikali ya Tanzania ??

MIZAMBWA
NABII MARAJIWA!!!
 
Last edited by a moderator:
Nakubaliana na wadau wote waliotoa maoni yao, ila na mimi ninachukizwa na hili swala la kujenga magorofa kati kati ya mji bila parking,hii inatokana na sera mbovu na uongozi legelege.

1. Barabara za katikati ya mji hazipitiki kwa sababu ya watu wanapark magari yao baabarani kwa kukosa parking (Barabara ya maktaba kutoka maktaba mpaka kwenye ule mnara wa askari ni double road lakini imegeuka kuwa single road kwa sababu ya kugeuzwa parking (Na jiji na maaskari wao ambao hawafanyi kazi yao kwa maadili).

Pili, barabara ya samora kuelekea stesheni,nayo ina kashikashi hizo. Hii inatokana na watenjaji wetu kutowajibika.Hawajui majukumu yao kuyasimamia.Ningekuwa mimi,hizo barabara zote za katikati ya jiji zingebakia kuwa wazi kama barabara na sio parking.
 
MIZAMBWA
mizambwa! Ni kweli lakini aje tupime hoja zake kama kweli zingefanikiwa kupunguza kama sio kuondoa msongamano wa magari.

Unajua mizambwa kuna mambo mengi ya kufanya ili kupungua foleni.
1. Acha kuendelea kujenga maghorofa katikati ya mji.
2. Punguza ofisi za serikali zilizoko katikati ya mji
3. Anzisha miji ndani ya mji iliyokamilika. Jiulize angalau Mlimani city kumepunguza watu wangapi wa kuingia kariakoo na posta?
4. Fungua njia zingine za kutoka katikati ya mji. Mfano fungua njia ya kutokea K'ndoni makaburini toka maeneo ya mahakama ya kisutu.
5. Nk, nk, nk, nk, nk, nk, nk

Ndimi Bazazi!
Tatizo nyie ni wasahaulifu sana.

Hili tatizo la msongamamo Dar lilitabiriwa tokea dikedi 3 zilizopita ndio maana mchakato wa kuifanya Dodoma makao makuu ya serikali ukaanza. Dar kwa sasa haipangiki tena.

Suluhisho ya la kupunguza msongamano Dar ni serikali kuhamishia makao yake dodoma. Dodoma serikali imetumia pesa nyingi katika kupanga mji lakini cha ajabu serikali hiyohiyo inaendelea kujenga majengo mengine ya wizara Dar kwenye msongamano. Kama ofisi za serikali zitahamia Dodoma basi hata misheni town wataenda kule nina uhakika Dar itabaki imetosha, maji ya bomba tutapata, gharama za maisha zitapungua (mfano usafiri kutoka 17,000/- hadi 10,000/- kwa siku) hata umri wa kuishi utaongezeka!!!!

Sababu nilisozisikia lakini sina uhakika nazo juu ya serikali kutohamia Dodoma ni hizi
1. Mawaziri na maofisa wengine wa serikali watosa marupuru ya "night" hasa kipindi cha Bunge kwani bado watakuwa wapo katika vituo vyao vya kazi.
2. Dodoma hakuna Beach.
3. Bagamoyo itakuwa mbali kama wakihitaji kurichaji hirizi zao.
 
Swala la foleni linafanyiwa kazi na serikali wameanza na mradi wa mabasi tunaona ujenzi unaendelea kwa kasi ya ajabu...Slaa hawezi kukusaidia atakusaidia vipi wakati yeye mwenyewe anasema atafanya Tanzania isitawalike.
 
hakuna jipya ww
 
ntamfikishia hizi habari
Ritz wewe kama mtoto wa rais umeisaidia nini nchi yko usibishe kuwa si wewe mi nakujua vema kaka we jibu swali! Iv hata ushaur unampaga kwel
 
Swala la foleni linafanyiwa kazi na serikali wameanza na mradi wa mabasi tunaona ujenzi unaendelea kwa kasi ya ajabu...Slaa hawezi kukusaidia atakusaidia vipi wakati yeye mwenyewe anasema atafanya Tanzania isitawalike.

Kweli bnadamu tko tofaut wewe unaskia raha t kula bata eh na kutetea ujinga eh
 
Kumaliza /dawa ya foleni DSM ni kuhamisha makao makuu ya serikari yaani ikulu na ofisi zote za wizara ikiwemo hazina kuukwenda Dodoma au kwingineko watakakoona kunafaa. waalah! hutaona foleni tena DSM, lkn kuendelea kukumbatia maofisi yote makubwa hapa, Mtajenga na kupanua barabara kila mwaka bila mafanikio, Ahsanteni kwa kunisikilizaa!!!!!!
Ni mimi Jamboleo TZ.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom