Dr. Slaa: Watanzania wanataka Maendeleo si Porojo

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,523
2,000
Kiongozi mashuhuri wa upinzani nchini ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Wilbrod Slaa amesema Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Nape Nauye ni mtu anayepiga mayowe na asiyejua ni nini watanzania wanataka na ndiyo maana sasa ameamini CCM haina agenda wala sera.

Dr Slaa anayefahamika na wengi kama Rais wa mioyo ya watu amesema kwamba anajisikia kucheka anavyoona CCM hawana agenda ya maisha ya watanzania badala yake wanadhani kumstopisha Dr Slaa ni kusema eti bado anamiliki kadi ya CCM.Amesema anachofanya Nape ni kupiga porojo huku watanzania wakitaka maendeleo.

Kiongozi huyo tishio kuu kwa CCM amesema kwamba wakati Nape akiendelea kusema Dr Slaa ana kadi ya CCM atashangaa kuikuta CHADEMA Ikulu mwaka 2015

Dr Slaa amesema CHADEMA kimeandaa mikakati thabiti kwa ajili ya maendeleo ya watanzania na wanaamini Tanzania itakuwa imara na bora zaidi chini ya CHADEMA baada ya 2015.

Source:Tanzania Daima.
 
Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
43,121
2,000
Nimepitia hii thread yote lakini sijaona wapi Dr Slaa kasema Watanzania wanataka maendeleo sio porojo.

Hichi ni kiwanda kipya cha uongo kimefunguliwa leo na Kamanda Molemo.

Thread kama hii unaweza kushangaa inakaa wiki mbili.
 
Last edited by a moderator:

Chibolo

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
4,690
2,000
Namkubali sana dr.wa ukweli,kweli magamba hawa sera wala agenda za kuwakomboa. WaTz.
 
Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
43,121
2,000
Dr Slaa kutokana na umri wako sio vema kutupiana maneno na Nape.
 
Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,523
2,000
Nimepitia hii thread yote lakini sijaona wapi Dr Slaa kasema Watanzania wanataka maendeleo sio porojo.

Hichi ni kiwanda kipya cha uongo kimefunguliwa leo na Kamanda Molemo.

Thread kama hii unaweza kushangaa inakaa wiki mbili.

Mtahangaika sana.....
 
Last edited by a moderator:

Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
43,121
2,000
Umepata thread ya Kulalia Mkuu. Vizuri mkuu upate nauli na si kurandaranda mitaa ya Lumumba Ucku huu

Kamanda naona mzimu wa Ritz, unazidi kukutafuna wewe badala ya kujadili thread unamjadili Ritz, hivi unajua kuwa ujinga wako ndio faida kwangu.
 
Last edited by a moderator:

Jakubumba

JF-Expert Member
Mar 5, 2011
1,625
1,195
Nimepitia hii thread yote lakini sijaona wapi Dr Slaa kasema Watanzania wanataka maendeleo sio porojo.

Hichi ni kiwanda kipya cha uongo kimefunguliwa leo na Kamanda Molemo.

Thread kama hii unaweza kushangaa inakaa wiki mbili.

Mkuu! Viongozi wote wa siasa ni porojo tu, kila mtu ana single yake
 
Last edited by a moderator:

S.Liondo

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
3,410
2,000
Nimepitia hii thread yote lakini sijaona wapi Dr Slaa kasema Watanzania wanataka maendeleo sio porojo.

Hichi ni kiwanda kipya cha uongo kimefunguliwa leo na Kamanda Molemo.

Thread kama hii unaweza kushangaa inakaa wiki mbili.
Yaani jinsi ulivyo-comment, kama mtu si mjanja anaweza fikiri kwamba wewe ni mtu mwenye hekima kweli.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom