Dr.slaa : Uteuzi wa kiongozi wa kambi ya upinzani chadema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr.slaa : Uteuzi wa kiongozi wa kambi ya upinzani chadema

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lu-ma-ga, Nov 9, 2010.

 1. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #1
  Nov 9, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Natumaini haujambo na pole udharimu wa CCM dhidi ya kura zako na wagombea ubunge wabunge wa chadema.Mimi nimesikitika sana na matukio ya kifisadi yaliyofanywa na CCM na wagombea wake naamini Mwenyezi Mungu atatuonyesha njia iliyo nyooka kuelekea ukombozi wa taifa hili.

  Hata hivyo hatuwezi kubeza hata mafanikio tuliyopata ya chama chetu hasa kwa kuweza kupata viti 22 bungeni na pia kupata Halmashauri kadhaa ambazo zitaongozwa na chadema. Na tunategemea hatutalala tutaendelea kupambana hadi kieleweke.


  Leo ninaomba kutoa ushauri wangu kuhusu uteuzi wa kiongozi wa kambi ya upinzania ambaye kwa hakika anatarajiwa kutoka chadema.Ushauri wangu kwako Dr.ni kwamba ingekuwa busara zaidi kama chama kitaacha nafasi hiyo kwa wabunge wapya lakini wenye uzoefu kazini, tunaamini kuwa kama chama kitaangalia kiongozi kwa kutoa nafasi ya kwanza kwa wabunge waliotoka mikoa ambayo kwa mara ya kwanza imetoa wabunge kupitia chadema.
  1. Mkoa wa shinyanga umeongoza kwa kutoa wabunge wengi wa upinzani kupitia chadema ni bora wananchi wangepewa motisha kwa chama kuteua kiongozi wa kambi ya upinzani kutoka huko.mapendekezo ni Prof.Kahigi ateuliwe kuongoza kwani ni msomi na mzoefu katika masuala ya kiutawala. Hii itaamsha chachu ya upinzani mkoani shinyanga
  2. Mkoa wa Mwanza umeweza kutoa wabunge watatu wa chadema kwa mara ya kwanza kama ilivyo kwa shinyanga ni changamoto kwa chadema kuhakikisha kuwa wanazingatia uteuzi kwa kuangalia the big two(shinyanga na mwanza) interms of population, ni mikoa yenye wakazi zaidi ya milioni 7.Mheshimiwa wenje ameonyesha kuwa ni mpiganaji wa kweli hasa kwa kuweza kusimama kidete na kumwangusha kigogo aliyetumia vibaya madaraka kutaka kumwangusha WENJE.
  3. mKOA WA SINGIDA UNA HISTORIA YA AINA YAKE KWANI KWAMARA YA KWANZA umeweza kutoa mbunge wa upinzani kwa tiketi ya chadema.Ni vema Tundu LISSU akapewa nafasi ya kuwa kiongozi wa kambi ya upinzani kupitia chadema
  Nimeamua kutoa mapendekezo haya ili kukifanya chama kiwe na damu changa katika uongozi bungeni Chadema wasiangalie vigogo ndani ya chadema kuwa ndiyo wagombee nafasi, ni vema wakaangalia wabunge wapya ili kuweza kupata changamoto mpya na kuweza kuibua vipaji vipya lazima chama kiwe kama ACADEMY YA KUTOA VINGOZI WAPYA KILA WAKATI KISITEGEMEE VIGOGO KILA WAKATI inabidi chadema wawaenzi wanchi waliowaletea wabunge wapya kuliko kuendelea kukumbatia wazamani
  Natumaini Dr.slaa ATAZINGATIA USHAURI HUU ILI kukiimarisha chama na pia kuepuka migogoro
   
 2. K

  Kimambo Member

  #2
  Nov 9, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 76
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  naona haina nguvu sana zaidi inejikitakwenye mambo ya hobolea, i think we have more serious issues to discuss than what you are suggesting,
   
 3. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #3
  Nov 9, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,721
  Likes Received: 1,629
  Trophy Points: 280
  kama ingewezekana kubadili mambo waliojiwekea kuhusu wabunge wa kuteuliwa basi Slaa angerudi ili aendelee kuwakabili ili ajiandae tena 2015 akiwa nje hakuna wakumsemea
   
 4. M

  Mbalinga JF-Expert Member

  #4
  Nov 9, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 1,381
  Likes Received: 407
  Trophy Points: 180
  Kwa protokali nafasi hiyo ni ya Mwenyekiti wa chama. Huwezi kumweka mbunge tu ukamwacha mwenyekiti wa chama pembeni. Tunafahamu jinsi Mbowe alivyohusika katika kukijenga chama, kumbuka operation sangara, ilivyo kijenga chama. Tusilete malumbano katika hili Mbona ndiye awe kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni. Hii ndiyo heshima ya chama.
   
 5. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #5
  Nov 9, 2010
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  ningeomba uteuzi/uchaguzi ufuate sifa, sheria na taratibu zilizopo. tusifuate umaarufu, uwepo wa muda mrefu, umkoa, mara ya kwanza kutoa mbunge, wala kabila
   
 6. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #6
  Nov 9, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Kwanini umeelekeza ushauri wako kwa Dr. Slaa? Chama kina uongozi wake na taratibu za kufanya maamuzi, Dr. Slaa kuwa mgombea uraisi haina maana yeye ni kila kitu. Ni vizuri mawezo yakaelekezwa kwa uongozi bila kutaja jina la kiongozi
   
 7. m

  mzalendo2 Senior Member

  #7
  Nov 9, 2010
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  anguko la chadema liko njiani anakufa kabla hajazaliwa

  akiwa tumboni
   
 8. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #8
  Nov 9, 2010
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  CHADEMA saivi ndio watakuwa tested by the maxim of" Power corrupts and Even a lilttle (not absolute..lol) POWER corrupts " Free hafai kuwa kiongozi wa upinzani. Mpeni Lissu tuone mambo kweli. CHADEMA wakubali Mwenyekiti wao sio kichwa wala nini na kinachohitajika ni mtu wakuwapelekesha CCM adi wa float... Lissu for Leader of the Opposition.
   
 9. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #9
  Nov 9, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Dr.Slaa ni katibu mkuu wa chama!kaa kimya sio lazima uchangie kama humpendi slaa
   
 10. mchillo

  mchillo JF-Expert Member

  #10
  Nov 9, 2010
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 433
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Acheni propaganda za uchochezi. Kiprotokali nafasi ya kiongozi wa kambi ya upinzani ni ya Mwenyekiti wa chama na inapotokea yeye si mbunge nafasi hiyo hupewa kiongozi au mbunge mwingine kwa baraka za uongozi wa chama. Usemi wa Mwenyekiti wa CHADEMA si kichwa ni wa upotoshaji usio na ukweli wowote kama si uchochezi wa waziwazi wenye lengo la kukivuruga chama. Naona ile kazi ya CCM kukivuruga CHADEMA imeshaanza na kinaNaamini Kinyambis wanatumiwa kwa malengo ya kuinufaisha CCM, kwani kwetu tunaoifahamu CHADEMA Freeman Mbowe ni kichwa kwelikweli na mchango wake CHADEMA si wa kubezwa kamwe. Kwanza ombwe la kukosekana Dr. Slaa Bungeni litazibwa na Mbowe ambaye kabla hajagombea urais mchango wake Bungeni ulikuwa makini na wa kusisimua sana. Mbowe na Dr. Slaa ndiyo source ya inspiration kwa kazi nzuri iliyofanywa na wabunge wa CHADEMA katika Bunge lililopita. Ni utovu wa shukrani kutotambua mchango wa mwanamapinduzi na mpiganaji huyu. Natoa wito kwa wana CHADEMA kugundua njama zote za kijasusi za kukihujumu chama na kuziweka hadharani ili 2015 tuuangamize mfumo huu wa kimafia.
   
 11. DCONSCIOUS

  DCONSCIOUS JF-Expert Member

  #11
  Nov 9, 2010
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 1,272
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Bora yoyote lakin sio zitto kabwe coz huyu jamaa ana umimi na mpenda sifa .
   
 12. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #12
  Nov 9, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,508
  Trophy Points: 280
  Huu ndiyo ukweli huwezi ukawakabidhi watu cheo kutokana na upigaji kura hata uzalendo wao na utashi wao ndani ya Chama haujapimwa na ukapimika..................
   
 13. T

  Thesi JF-Expert Member

  #13
  Nov 9, 2010
  Joined: Aug 8, 2010
  Messages: 998
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Umesema kweli ukweli mtupu.
   
 14. afroPianist

  afroPianist Member

  #14
  Nov 9, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani suala la "protokali" ni la msingi, lakini la maana zaidi ni kuchagua mtu ambaye ana ukomavu wa kifikra na kisiasa, mzalendo wa kweli na atakayeleta umoja zaidi na mafanikio kwa kambi ya upinzani na taifa (kama mlivyo mteua Dr.Slaa kugombea urais wakati M/kiti Mbowe akigombea ubunge).

  Kwahiyo anaweza akawa Mbowe, Lissu, Zitto ila ni lazima mjiridhishe kuwa uteuzi wake utaleta tija.
   
 15. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #15
  Nov 10, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Mambo ya chama yatajadiliwa kichama
   
 16. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #16
  Nov 10, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,656
  Likes Received: 21,872
  Trophy Points: 280
  Wewe ndio sio kichwa kama umeshindwa kuona kuwa Mbowe ameipandisha kiasi gani CHADEMA kiasi cha kuwa chama chenye kuweza kushika dola. Jee unasemaje kuhusu mwenyekiti wenu? CCM ikoje toka aichukue kutoka kwenye uongozi wa Mkapa? jibu utapata kuwa yeye ndio sio kichwa. Kuwa mkweli katika nafsi yako,jee bila ya wizi na ghiliba katika uchaguzi huu hali ingekuwaje kwa CCM?
   
 17. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #17
  Nov 10, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Test Number 1 ya "maturity" ya CHADEMA as chama ndiyo hii:

  Kupitia Idhaa ya Kiswahili ya BBC jana niliwasikia Mh. Zitto na Mh. Mbowe wakiohojiwa kuhusu hili:-

  Zitto. ameshatanganza nia, Mbowe anasema hawezi kulizungumzia nje ya CHAMA!

  Zitto alitoa mfano wa mwaka 95 kuwa Mrema alishinda Temeke na alikuwa Mwenyekiti wa Chama chenye wabunge wengi Bungeni na angetakiwa kuwa Kiongozi wa upinzani bungeni, lakini alimwachia Mh. Ndorobo. Hii inaonyesha kuwa Zitto is in for it, lakini alitoa remarks kuwa anasubiri MAAMUZI ya chama! Looks like kuna "fight-for-power" inaendelea ndani ya CHADEMA between Zitto and Mbowe!
   
 18. E

  Endaku's JF-Expert Member

  #18
  Nov 10, 2010
  Joined: May 25, 2007
  Messages: 322
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Who is we ?????? Are speaking for everybody here ?
   
 19. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #19
  Nov 10, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Sijasema simpendi ila michango yote hapa JF inayohusu CHADEMA inaelekezwa kwa DR. Slaa kama vile chama ni mali yake binafsi. Hofu yangu hoja za humu JF zinamweka Dr.Slaa juu ya mwenyekiti wake kitu ambacho kinaweza kuwagombanisha, sikuwa na maana nyingine wala simchukii mtetezi wa wanyonge Tanzania
   
 20. Kagemro

  Kagemro JF-Expert Member

  #20
  Nov 10, 2010
  Joined: Jan 11, 2010
  Messages: 465
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45

  ushahuri wako ni mzuri sana,hata mimi ningetamani iwe hivyo,lakini kumbuka katika uongozi mamlaka hueshimiwa na si tu kama unavyofikiri,yapo mambo magumu yanayotakika maamuzi magumu na siyo swala lautawala tu bali uzoefu wa uendeshwaji wa bunge na mambo mengine kama hayo.

  Lakini pia kumbuka Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mboyo yupo Bungeni katika utawala wowote nafasi ya mtu huheshimiwa,yeye ndiye anayestahili kuwa Kiongozi na sivinginevyo ili abaki na heshima yake kama Mwenyekiti wa Chama na wengine wataongoza nafasi nyingine kwani zipo nyingi.Litakuwa jambo la ajabu kwa watu ambao hawajawahi kuingia Bungeni wakapewa kiti hicho Bunge linakanuni zake siyo chombo tu kinachoendeshwa kiaina,hivyo anaitajika mtu makini atakaye kuwa tayari kuuliza na kushahurika.

  Nafikiri tuwashahuri na tuwaachie wafanye maamuzi maana wao wanawajua vema wabunge wao.
   
Loading...