Dr. Slaa usitunyang'anye tonge mdomoni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Slaa usitunyang'anye tonge mdomoni

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Remmy, Aug 30, 2010.

 1. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #1
  Aug 30, 2010
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Silaa tafadhali kutaka kwako kura kusikufanye ukatunyang"anya tonge wafanyakazi mdomoni. Tunazitaka sana hiyo nyongeza ya mshahara no matter imetangazwa wapi? we mbona umeahidi mengi? hizo ahadi si rushwa na si kinyume na maadili ya kampeni? kabla ya kuzinduliwa kwa kampeni ulizitaka kura zetu na ukaahidi kuongeza mshahara hiyo si rushwa? Nilikupenda sana niliapa kutopiga kura mwaka huu lakini ulipokuja wewe nikahamasika lakini kwa hili unaniboa na kinirudisha kulekule. Wafanyakazi hatudanganyiki na nyongeza ya mshahara hata akiongeza kama hatukumtaka tusimgempa na hata kama asipoongeza kama tulimtaka tungempa. NImegundua kuwa wagombea wote wapo kwaajili ya kura tu na wala si maslahi ya wananchi, kama kweli unamaslahi nasi ungeacha wafanyakazi mwezi huu wa nane japo tufikie hiyo 175,000/= tupambane na maisha. Khaa bee!!!!
   
 2. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #2
  Aug 30, 2010
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mmeshaanza enh? Si ndio mkakati wa intelijensia na CCM kama tulivyohabarishwa humu JF? Kwa taarifa yenu Watanzania safari hii HAWADANGANYIKI!
   
 3. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #3
  Aug 30, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  na hatudanganyiki kabisaaaaaa
   
 4. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #4
  Aug 30, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Maentelijensia wameishasema kwamba mtakuja na habari hizo

  Dada/kaka REmmy Hujasoma nyakati tulia kwanza
   
 5. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #5
  Aug 30, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Ndo maana mtaendelea kuumia kwa short sightedness yenu. ijisenti vidogo hivyo ndo mnahongwa kirahisi? Kweli nimeamini kama kila mfanyakazi yuko kama wewe basi MIFANYAKAZI MLIVYO!
   
 6. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #6
  Aug 30, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Heeee.....
  Hivi yale mambo ya idara ya inteligencia na CCM ndo hivyo eeeh! Acha njaa hiyo mkuu wangu. FUta hawa jamaa uwe na amani ya muda mrefu, acha kudanganyika na mafuta ya mgongo wa chupa!!
   
 7. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #7
  Aug 30, 2010
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Nimethibitishiwa na rafiki yangu aliyepo INTELIJENSI ( lakini yeye ni Mzalendo mwenzetu) kwamba huo ndio mkakati ulioandaliwa katika kujaribu kupunguza nguvu kubwa ya Dr Slaa. Nadhani pamoja na mambo mengine tuwaelimishe wenzetu wa Intelijensi kwamba sio wajibu wao kuupotosha umma kuhusu vyama vinavyotaka kuing'oa CCM madarakani baada ya kushindwa ku-deliver. Hawa ni intelijensia kweli au Pumbavunsia?
   
 8. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #8
  Aug 30, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,182
  Trophy Points: 280
  Tatizo wafanyakazi hawaelewi kwamba quality of life haiongezwi na nyongeza za mishahara, inaongezwa na uzalishaji zaidi tu.

  Ukiongeza mishahara, bei za vitu zitaongezeka maradufu na kufanya hali iwe mbaya zaidi, wafanyakazi watalilia nyongeza nyingine ya mishahara ambayo kama itakubaliwa itaongeza mfumuko wa bei, duara hili lisilo mwisho litaendelea hivyo.
   
 9. SILENT WHISPER

  SILENT WHISPER JF-Expert Member

  #9
  Aug 30, 2010
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 2,231
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  nadhani ni uwezo mdogo wa remmy kuelewa...! sijui wewe ni mfanyakazi wa level gani..?

  anyway.......omba ueleweshwe kwanza slaa anaongea nn ..? hujamuelewa kabisaaaaa...!

  nilitaka nikusaidie lakini upo mbaaaali saana...ni sawa na prof kuanza kumfundisha mwanafunzi wa darasa la 4.
   
 10. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #10
  Aug 30, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Remmy, rudi ofisini umesahau bahasha yako juu ya meza.
   
 11. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #11
  Aug 30, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mshahara tutaramba Kura kwa Slaa
   
 12. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #12
  Aug 30, 2010
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Remmy; Usiache Mbachao kwa Mshahara Upitao!

  Simple!

  Anachopigania Dr. Slaa ni zaidi ya unachoahidiwa.

  October 31st si mbali. Vumilia kidogo!
   
 13. Kagemro

  Kagemro JF-Expert Member

  #13
  Aug 30, 2010
  Joined: Jan 11, 2010
  Messages: 465
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45

  watu wengine bwana hata huwa hamsikilizi hoja na kuzifatilia mnabwabwaja tu,kumbuka Dk Slaa alianza kudai wafanyakazi muongezewe mshahara jana aliliongelea hilo miaka mitatu iliyopita.msikurupuke na kuropoka
   
 14. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #14
  Aug 30, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Pamoja na hoja zako Kiranga whether mshahara unapanda au haupandi bado mfumko wa bei umepanda tu. Wewe unajua pamoja na kutopandisha mshahara wa kima cha chini kwa muda mrefu lakini mfumuko wa bei umekwenda karibu 100%.

  Sasa unadhani mfanyakazi ambaye mshahara wake ni wa kutumia wiki moja kwa kulipia pango na nauli ya kwenda kazini na kurudi nyumbani kwa wiki moja sasa afanyeje? Bila shaka atakachofanya ni kudai apate pesa za kumsaidia kumaliza shida zake. Mambo mengine jamani ebu tufikilie kidogo. Unadhani mtu anayepata mshahara wa 2,000,000 ana kilio cha upungufu katika mshahara wake kama huyu anayepata 100,000 kwa mwezi? Alafu unapomwambia habari za uzalishaji wakati yeye huja kazini na kushida akifanya kazi kwa nguvu zake zote, na mwisho wa mwezi apate that amount utamshawishi vipi kwamba aongeze uzalishaji?

  Kama mimi na wewe twafanya kazi ofisi moja na wote tunafanya kwa bidii faithfully na wewe unapata 2,000,000 na mimi napata 100,000 kweli uta justify vipi kwamba hatuzalishi vizuri ndio sababu napata kidogo na wewe unapata kikubwa?

  Ndio sababu mara nyingi nimedhani if that is the case, then, tuanzishe malipo kwa kila saa anayofanya mtu katika kulipa mishahara. La sivyo Kiranga hizi ni story tu za kutudanganya wakina mchukia fisadi.
   
 15. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #15
  Aug 30, 2010
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145

  Dada,

  Tatizo ni kwamba wewe hukutazama - kwa umakini - hotuba ya Dk. Slaa alipozindua kampeni pale Jangwani, Jumamosi, au hukutazama kabisa.

  Unacholalama kinatokana na DISINFORMATION CAMPAIGN inayoendeshwa na vyombo vya habari vilivyonunuliwa na CCM, kupotosha kila kilichosemwa na Dk. Slaa. Naomba nikufahamishe:

  1. Slaa amesema kwamba CHADEMA haitoi ahadi ya kupandisha mishahara, kufikia Shs 350,000/- kama HONGO kwa wafanyakazi, amesema kwamba ni HAKI ya wafanyakazi kupata kiwango hicho cha mshahara.

  2. Slaa ametamka wazi kwamba suala la maslahi ya wafanyakazi, hata kiwango hicho cha chini, ni suala ambalo lina muda mrefu, kwa sasa ni miaka nne, si suala geni.

  Kwa hiyo dada, tafakari kwanza kabla ya kubwata (umebwata bila kuwa na uhakika wa unachokisema). Kumbuka, wako watu wengi sana wanaosoma kurasa hizi pepe... zaidi ya wanachama milioni 4... wengi wao wenye uwezo wa kutoa maamuzi mazuri na mabaya kwetu sote. Hata Mkuu wa Nchi naye ni mwanachama humu ndani, na anasoma tunachoandika, anakifanyia kazi.

  JK alisema Serikali yake HAIWEZI - nilisikiliza hotuba yake siku hiyo - kupandisha mishahara, hata kama wafanyakazi wakigoma miaka nane, na alisema "kama ni kukosa kura, niko tayari kuzikosa..." Hana haja na kura za wafanyakazi.

  Sasa bora mumpe tu Slaa, ambaye amesema anahitaji kura zenu, na kwamba CHADEMA itakuwa na uwezo wa kupandisha mishahara pamoja na kuweka mazingira bora zaidi ya kazi.

  Una cha zaidi cha kukusumbua, tukutoe dukuduku lako?

  -----> Mwana wa Haki

  Njia nyeupe mbele kwa mbele hadi Ikulu. Uchafuzi wa CCM ni mtaji wa CHADEMA. Wakichafua, wananchi wanachukia, wanaipa kura CHADEMA!

  People's Power! Hatudanganyiki!
   
 16. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #16
  Aug 30, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Kagemulo. Achana na pandikizi hili. Halina hoja mbali na kutumwa.

  Hana hoja maana hata hoja anazolalamikia Dr Slaa hazijui. Yupo kuandika pumba akidhani tutamshangilia kumbe tumemgeuza sawa na karatasi ya kupangusa uchafu choon.
   
 17. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #17
  Aug 30, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  kiranga umenena nipe mkakati wako wa kutusaidia kuelimisha wafanyakazi na kisha wakulima, hata kama sio hapa ni lazima baada ya oktoba 2010 tuingie msituni kwa maana ya kuyafuata makundi yenye idiadi kubwa ya watanzania yaani wafanyakzi na wakulima huko walipo tuwaelimisha kwa miaka mitano ndio 2015 tu claim ushindi wa kishindo. Big up sana
   
 18. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #18
  Aug 31, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  JAMANI MBONA MMEMZONGA REMMY KIASI HICHO, PENGINE HAELEWI AU NDIO KESHADANGANYWA. NILIFIKIRI MAMBO YA HUMU TANAYAFANYIA KAZI, LAKINI KAMA NI KUTUHUMIANA WENYEWE JF KWA WENYEWE NA NDIO MWISHO WAKE HAMNa TIJA.

  REMMY kauli yako ya mwisho in red imenifanya niamini kuwa uko very genuine hasa maneno mawili ya mwisho. Ila usichofahamu ni kuwa Serikali ya JK kutokea iingie madarakani 2005 imewahi kuongeza mishahara na marupurupu kwa viongozi wa Serikali waandamizi wakiwemo Wabunge, Mawaziri, Makatibu Wakuu, Majaji, wakuu wa vyombo vya usalama n.k. na kuwaacha watumishi wa ngazi za chuini wakitaabika kwa ukosefu wa ujira wa kuweza kumudu gharama za maisha

  Katika nyongeza hizo Serikali ya Jk ililipa pia malimbikizo ya mishahara kutokea tarehe madai ya viogogo hao yalipowasilishwa Serikalini hadi tarehe yalipolipwa.

  Hivyo kama ilivyokuwa kwa viongozi waandamizi wa Serikali, watumishi wa Serikali nao walikuwa na haki ya kulipwa malimbikizo ya mishahara baada ya Serikali kukubali kuwa wana haki ya nyongeza za mishahara. na ndio anachopigania Dr Slaa, kuongeza kimya kimya ni kutaka kuwapunja wafanyakazi, kwa kuwa haiwezekani kupeleka suala hili katika mahakam za Kazi pasipo mwajiri kutoa maandishi ya kuongeza mshahara kutokea tarehe ipi.

  Kwa kuwa TUCTA iliwasilisha madai ya nyongeza za mishahara za kima cha chini kwa watumishi wa umma mwaka 2006. Mara tu mwajiri wao yaani Serikali ilipokubali kuwa madai hayio yalikuwa ya haki na kuyatekeleza, wafanyakzi hao walistahili kulipwa malimbikizo ya nyongeza ya mishahara kutokea tarehe madai yalkipowasilishwa hadi tarehe ya utekelezaji wa amdai hayo.

  Malimbikizo hayo ni kama ifuatavyo, kima cha zamani Shs 104,000/=. Kima kipya kilichofikiwa baada ya TUCTA na CHADEMA kushikamana katika madai hayo katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 2010, Shs 235,000/=.

  Hivyo basi ongezeko hilo ni Shs 235,000 -104,000= Shs 131,000/= kwa mwezi; zidisha kwa miezi 48 kutokea Juni 2006 TUCTA ilipowasilisha madai Serikalini hadi hadi Juni 2010, hatimaye Serikali ilipokuja kukubali kutoa nyongeza hiyo. Shs 131,000/= X miezi 48= Shs 6,288,000/=.

  Hivyo wafanyakazi wa kima cha chini wa sekta ya umma walistahili kupokea malimbikizo ya mishahara kwa Shs 6,288,000/= pamoja na mshahar mpya wa Julai 2010 kama walivyofanyiwa viongozi waandamizi wa Serikali

  Kitendo cha kuwalipa watumishi whawa mishahara mipya ya mwezi Juklai 2010 tu, kuendeleza dhuluma dhidi ya wanyonge.

  Kama wafanyakzi wa Tanzania wangekuwa wanatendewa haki namna hii na viongozi wanaowachagua kwa kishindo, pangekuwa na mfanyakzi anayeshindwa kununua kiwanja cha kujenga nyumba bora; kumlipia mtoto ada ya sekondari, kupata matibabu bora, kujijengea nyumba bora; kununua bati n.k.

  Ni kutokana na viongozi tunaowachagua kwa kishindo kujikumbuka wenyewe ndio maana ni wao tu ndio wanamiliki magari mazuri, watoto wao wanasoma shule nzuri na hata nje ya nchi, wanajenga nyumba kama mahekaru n.k.

  Wakati umefika wa kuamka na kuacha kudanganyika, acha kusikiliza blah blah kuwa wafanyakazi tunakumbukwa na wale tunaowapeleka Dodoma kutoka kambi moja tu.

  Haki hizi za wafanyakazi zinzaweza kudaiwa na wabunge wa uopinzani tuu, hivyo tuwapeleke kwa wingi huko Dodoma 2010.
   
 19. M

  Malyamungu JF-Expert Member

  #19
  Aug 31, 2010
  Joined: Jul 5, 2009
  Messages: 363
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Here comes phylososphy of misunderstanding between Slaa and salary increase. Slaa anachokisema ni huwa maendeleo ya wananchi yanawekwa rehani mpaka siku za uchaguzi ,mfano; maji, umeme, barabara, waalimu, madarasa, (sijui kompyuta mashuleni-hizi komputer ajue asije akasemasema ovyo kwani itakuja kuwa EPA nyingine hiyo sidhani kama anajua kompyuta moja gharama zake ni shs ngapi) vivuko, mishahara; nchi kama Australia mishahara kupanda siyo mambo ya kisiasa ni lazima upande kama sarafu imeshuaka thamani and not othewrise yaani ya JK yanakuwa kisiasa zaidi kuliko huduma. A tax payer money zinakuwa rehani kama vile CCM wazaliwa nazo wamesahau kuwa ni za walipa kodi na siyo otherwise. JK alikuwa awaeleze wananchi amefanya nini na siyo atafanya nini na kulingana na hizo sheria za uchaguzi kama zimepitishwa bais ni makosa makubwa mno kutoa ahadi kwani anavunja sheria.
   
 20. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #20
  Aug 31, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Usiwe na wasiwasi, hizo zimekwishatangazwa hazitaondolewa zitabaki hivyo hivyo, kwa hiyo utazipata tu; ila aliyezitangaza ndiye atakiona cha moto.
   
Loading...