Dr Slaa usitukane wakunga na uzazi ungalipo

Licha ya hiyo beti, huu wimbo umesheheni beti nzito nzito ambazo ukizisoma utafikiri unaiona picha ya chadema inayoendelea kwa sasa:

MUHOGO WA JANG'OMBE

Date: 25 August, 2003
Kiitikio:

  • Muhogo wa Jang'ombe, sijauramba mwiko
    Usitukane wakunga, na uzazi ungaliko

  1. Kaditamati naapa, muhogo sitonunua
    Haikuwa Maimuna, aliyekwenda ung'oa
    Kapata tete kuanga, na ugonjwa wa shurua
  2. Kula dori kula dori, mshindo wa sufuria
    Guliguli guliguli, kofia ina viua
    Ndiye mimi ndiye mimi, anipataye ukoa
  3. Mungu akitaka kupa, hakuletei barua
    Hukupa usingizini, pasi mwenyewe kujua
    Kwenda mbio sikupata, bure unajisumbua
  4. Mkato wake matege, wakati anapokuja
    Naliiweka dhamiri, ya kumfulia koja
    Wallahi nimeghairi, kiumbe hana mmoja
  5. Kamfunge kamfunge, beberu wa Athumani
    Umfunge umfunge, pahala panapo jani
    Endaye tezi na omo, atarejea ngamani
  6. Sina ngoa sina ngoa, kuhadaiwa sitaki
    Ni mwerevu ni mwerevu, wala sihadaiki
    Pambanua pambanua, viwili havipendeki
  7. Ya nini kutakadamu, kwa jambo lisilokuwa
    Utahadhari na mwiko, wakati wa kupakua
    Ukitamani makoko, chungu utakitoboa
  8. Nauliza masuala, hamnambii jamani
    Watu wake wakishiba, huzidi umaluuni
    Pahala pasipo ngoma, hupandwaje na shetani
Nyimbo ya Bi Kidude
Imeletwa na Hassan O. Ali

Source: MUHOGO WA JANG'OMBE

cc Dr.W.Slaa

Ni kweli kabisa. Hebu cheki huo ubeti wa 7. Unamuhusu Slaa na mboye.
 
Nawapongeza kwa kutimiza wajibu wao ipasavyo. Mikutano ya Slaa inaligharimu jeshi la police kupambana na waandamanaji
Ni kweli mkuu acha wamsaidie mzee wetu make bado anawatoto wadogo wanamtegemea sana polisi mlindeni japo aliwatusi.
 
Ni kweli mkuu acha wamsaidie mzee wetu make bado anawatoto wadogo wanamtegemea sana polisi mlindeni japo aliwatusi.

Ni kweli mkuu, waandamanaji wanaoupinga ujio wa slaa kigoma umekuwa mkubwa tofauti na watu walivyofikiri.
 
Idadi kubwa ya polisi ni PolisiCCM, wapo wanaotenda kazi kwa weledi, japo ni wachache sana. Na wengi wao wanafanya kwasababu ya njaa, si kwasababu wanaiunga CCM mkono.
 
Wewe inaonekana bado unahitaji kurudi cdm ndio maana unaleta post kila mara cdm cdm, si madhambi yako ndio yalikufanya utimuliwe? Muongelee huyo mzee wako

Hajui kuwa kulindwa na jeshi la polisi sio hisani, wanatimiza wajibu wao.
 
Una uhakika nlitimuliwa? Nliondoka kwa hiari yangu

Ulitimuliwa, nahii ni kwa kauli yako leo ulivyokuwa unalalamika kuwa hukupewa chochote wakati ndani ya chadema kuna nguvu zako na muda wako mwingi.Au umesahau kiongozi wangu?
 
Wewe inaonekana bado unahitaji kurudi cdm ndio maana unaleta post kila mara cdm cdm, si madhambi yako ndio yalikufanya utimuliwe? Muongelee huyo mzee wako
Mkuu jitambue kwanza kwani mtu kuweka mada ya cdm lazima awe anaipenda cdm acha akili ya kushikiwa kila mtu anauhuru wa kuandika chochote ila asivunje sheria basi lakini wewe unatuletea habari na mawazo ya kibavicha.
 
Licha ya hiyo beti, huu wimbo umesheheni beti nzito nzito ambazo ukizisoma utafikiri unaiona picha ya chadema inayoendelea kwa sasa:

MUHOGO WA JANG'OMBE

Date: 25 August, 2003
Kiitikio:

  • Muhogo wa Jang'ombe, sijauramba mwiko
    Usitukane wakunga, na uzazi ungaliko

  1. Kaditamati naapa, muhogo sitonunua
    Haikuwa Maimuna, aliyekwenda ung'oa
    Kapata tete kuanga, na ugonjwa wa shurua
  2. Kula dori kula dori, mshindo wa sufuria
    Guliguli guliguli, kofia ina viua
    Ndiye mimi ndiye mimi, anipataye ukoa
  3. Mungu akitaka kupa, hakuletei barua
    Hukupa usingizini, pasi mwenyewe kujua
    Kwenda mbio sikupata, bure unajisumbua
  4. Mkato wake matege, wakati anapokuja
    Naliiweka dhamiri, ya kumfulia koja
    Wallahi nimeghairi, kiumbe hana mmoja
  5. Kamfunge kamfunge, beberu wa Athumani
    Umfunge umfunge, pahala panapo jani
    Endaye tezi na omo, atarejea ngamani
  6. Sina ngoa sina ngoa, kuhadaiwa sitaki
    Ni mwerevu ni mwerevu, wala sihadaiki
    Pambanua pambanua, viwili havipendeki
  7. Ya nini kutakadamu, kwa jambo lisilokuwa
    Utahadhari na mwiko, wakati wa kupakua
    Ukitamani makoko, chungu utakitoboa
  8. Nauliza masuala, hamnambii jamani
    Watu wake wakishiba, huzidi umaluuni
    Pahala pasipo ngoma, hupandwaje na shetani
Nyimbo ya Bi Kidude
Imeletwa na Hassan O. Ali

Source: MUHOGO WA JANG'OMBE

cc Dr.W.Slaa

Mods tafadhali tunakuomba ondoa huu uchafu kwani hsps siyo uwanja wa taarabu, wanatuaibisha wana GT.
 
Ulitimuliwa, nahii ni kwa kauli yako leo ulivyokuwa unalalamika kuwa hukupewa chochote wakati ndani ya chadema kuna nguvu zako na muda wako mwingi.Au umesahau kiongozi wangu?

Mkuu nlisema nlidemand right zangu nkafungiwa milango, sio nlitimuliwa. Tofautisha
 
Mods tafadhali tunakuomba ondoa huu uchafu kwani hsps siyo uwanja wa taarabu, wanatuaibisha wana GT.

Nauliza masuala, hamnambii jamani
Watu wake wakishiba, huzidi umaluuni
Pahala pasipo ngoma, hupandwaje na shetani
- Bi Kidude.
 
KWA MARA YA KWANZA nakupongeza sana kwa kutambua kwamba ni WAHUNI PEKEE ndiyo wanaovuruga mikutano ya cdm ( siyo ya Dr Slaa pekee , maana huyo anawakilisha chama chake ) , mwenye akili timamu na anayefahamu chezo lilivyo hawezi kupingana na MAAMUZI HALALI YA KAMATI KUU , kwa hilo angalau naweza kusema asante sana .
 
Back
Top Bottom