Dr. Slaa umesahau mambo uliyopigania kwa miaka 20?

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,898
Mzee wangu Dk Slaa kwanza hongera kwa uteuzi wako wa Ubalozi wa nchi isiyojulikana na pia pole kwa masahibu yote yaliyokupata huko Ughaibuni, kunawakati tukasikia umekuwa supermarketkeeper kitu ambacho kilitushtua na kutuumiza sana hasa Wanachadema wenzako kwani sisi hatukukufukuza na wewe unajua tulikulipa vizuri sana zaidi ya mshahara Wa mkuu Wa mkoa/waziri kwa mwezi pamoja na marupurupu lukuki yaliyofanya karibu jumla ya fedha za Kitanzania mil 10. Pale tuliposikia huna kazi ilituuma sana kama Watanzani wengine.

Pili nimpongeze sana aliyekuteu na niseme amechelewa sana kukulipa fadhila yako kwa namna ulivyomsaidia kwa propaganda zako wakati Wa uchaguzi mkuu Wa mwaka 2015 baada ya kuamua kuwasaliti watoto Wa masikini kwa vipande vya fedha kitu ambacho naamini kimegeuka laana nyingine kwako na najua matokeo umeanza kuyaona kwa macho yako hapahapa Duniani

Mzee wangu Dk Slaa ile dhambi kubwa uliyoifanya kwa mara ya kwanza ya kulisaliti kanisa la Mungu kamwe haitafutika kwako na itakuandama tu popote uwapo. Nikweli kuwa dhambi hii ilikufuata CHADEMA na najua itakufuata popote utakapokuwa either hai au umekufa.
Hebu kumbuka Uliapa kufia useja/kutokuoa bila hofu ukasaliti ukaoa, uliapa kufia CCM ukasaliti ukahamia CHADEMA,Uliapa kufia CHADEMA ukasaliti tena ukahama leo tena uko CCM ,Dk Slaa hii sio bure ni laana ya uasi kwa Mungu.

Mzee wangu Dk Slaa huna historia ya kuwa mwaminifu tangu kuzaliwa kwako historia haidanganyi,
Umemdanganya Mama Rose Kamili ukasaliti ndoa ukamwacha,Leo uko na Josephine sijui kesho utakuwa na nani ni Mungu Wa mbinguni anajua,Hakika sasa nimesadiki Kweli cheza na vyote ila kamwe usicheze na "KIAPO" kiapo ni agano kiapo ni nadhili ,kiapo ni maombi, ogopa sana kiapo Mzee wangu Dk Slaa.

Juzi tena nimekusikia unaendeleza laana zako kwa kutudanganya na kutaka kutuhaadaa Watanzania ukidhani sisi sote tunalaana kama ulivyo Wewe,
Mzee wangu Dk Slaa umesikika Ikulu ya magogoni ukisema kuwa "YALE YOTE TULIYOYAPIGANIA KWA ZAIDI YA MIAKA 20 YANATEKELEZWA NA RAIS MAGUFULI" kimoyomoyo nikauambia moyo wangu "Moyo wangu tulia usaliti ni dhambi mbaya sana chini ya jua"

Pengine kwakuwa haukuwepo nchini kwa muda mrefu wamekudanyanya , Sikia Mzee wangu Dk Slaa Tanzania kwa sasa hali ni mbaya zaidi ya wakati wowote tangu tupate Uhuru mwaka 1961 katika kila sekta.

Mzee wangu Dk Slaa Labda nikukumbushe kama kweli umesahau mambo ambayo mimi na Wewe tuliyapigania kwa zaidi ya miaka 20 ambayo naamini umedanganywa kwamba yanafanyika

1. *Kwa zaidi ya miaka 20 tumepigania uwepo Wa Katiba mpya/Katiba ya wananchi* najua walikudanganya kuwa tayari imeshapatikana Ila ukweli nikwamba "katiba mpya bado" ulipashwa kujiridhisha kabla ya kuropoka hadharani,Kama katiba mpya bado Wewe ulimaanisha ipi? Au ile Katiba ya CCM

2. *Kwa zaidi ya miaka 20 Tumepigania kuondoa ufisadi na mafisadi nchini,* Najua aliyekuteua amekwambia kuwa anapambana na ufisadi jibu ni hapana kwani mpaka sasa hakuna hata fisadi mmoja aliyetiwa hatiani tunawaona wanatanua mitaani na kupewa vyeo umemuuliza wale mafisadi Wa ESCROW,RICHMOND, MEREMETA,DEEP GREEN, RADA,NDEGE YA RAIS Walishakimbia nchi?

3. *Kwa zaidi ya miaka 20 tumepigania Ajira kwa vijana wetu*, Ukweli ni kwamba zaidi ya vijana 100,000 wahitimu Wa kada mbalimbali hawana ajira mpaka sasa, Wewe wamekwambia vijana wetu wale waliokupenda na kukuona mkombozi wao Wa ajira wameajira lini/wapi ?Mzee wangu Dk Slaa unaposema yote yametekelezwa unamaana gani au ndio laana za uasi.

4. *Kwa zaidi ya miaka 20 tumepigania Kuimarisha uchumi utakaowagusa watu Wa chini* Hapa ndio hovyo kabisa kwani pamekuwa na mdororo Wa uchumi ambao haujawahi kushuhudiwa tangu kumalizika kwa vita vya Kagera mwaka 1979, Uchumi huu haujawihi kukua kwa zaidi ya mwongo mmoja sasa tena sasa ni mwendo Wa kushuka tu toka ule wastani 7% mpaka 6.8 , Mzee wangu Dk Slaa ,Je wamekwambia ukuaji umefikia kiwango gani? Au ndio laana ya usaliti kuropoka ropoka.

5. *Kwa zaidi ya miaka 20 tumepigania Utawala bora (the rule of law)* Najua wamekudanga kuwa mihimili ya nchi inajiendesha kwa Uhuru na kujitegemea ila ukweli ni kwamba kila kitu anafanya huyo aliyekuteua ambaye Wewe umesema unampenda tangu zamani ndio huyohuyo ameshindwa hata kumpata aliyempiga risasi 38 rafiki yako Lissu amegoma hata kumuhudumia tu katika matibabu yake. He tumekuwa tukipigania Tanzania ya kupigana risasi au ulimaanisha lipi.

6. *Kwa zaidi miaka 20 Tumepigania Mishahara minono pamoja na stahiki nyinginezo kwa watumishi Wa umma* Najua wamekwambia wameongeza mishahara ila ukweli ni kwamba wameongeza Tsh 10,000 Je ni kweli kwa miaka 20 tumekuwa tukipigania ongezeko la elfu kumi au uliropoka tu.

7. *Kwa zaidi ya miaka 20 Tumepigania elimu bora na ya uhakika (Quality & credible education)* angalia matokeo ya Kidato cha nne Kati ya shule 10 bora hakuna hata moja ya Serikali, Je watoto wao wanasoma shule zipi? Dk Slaa miaka 20 tulipigania madaraja/classes haya ya watu wenye Mali na wasizonazo

Mzee wangu Dk Slaa ukweli ni kwamba hakuna hata moja kati ya yale tuliyoyapigania mimi na Wewe kwa nguvu nyingi kwa zaidi ya miaka 20 yamefanyika kwa ukamilifu wake Ila niseme hongerakwako kwani Wewe na familia yako mmefanikiwa ila si- sisi watoto Wa masikini tunaopigwa risasi na kupotezwa kama nguruwe pori.Pole sana mzee hukuwa na njia tofauti zaidi ya kumsifia mteuzi kwani hakika umeshiba na sasa umewasahau kabisa wana Wa nchi uliolia nao kwa zaidi ya miaka 20.
 
Pole mkuu mbowe alimsaliti slaa kwa vipande vya pesa vya lowassa,katiba mpya walioipigania wakina slaa alioipinga kwa nguvu na ushawishi wake lowassa chadema walimchukua,fisadi namba moja chadema walimchukua,hoja ya ufisadi chadema haipo tena na wala si kipaumbele chao.je slaa amechukua kadi ya ccm!
 
Mimi ndio maana nimeachana na mambo ya Madokta, yaani wengi wao wanakua na matatizo flani flani hivi
 
Pole mkuu mbowe alimsaliti slaa kwa vipande vya pesa vya lowassa,katiba mpya walioipigania wakina slaa alioipinga kwa nguvu na ushawishi wake lowassa chadema walimchukua,fisadi namba moja chadema walimchukua,hoja ya ufisadi chadema haipo tena na wala si kipaumbele chao.je slaa amechukua kadi ya ccm!
weka fact
 
Ahsante kwa ushauri lakini ndege iko angani sasa haiwezi kutua tena! Jijenge kwanza kabla ya kujenga wengine
 
Dr slaa ameshawaambia siasa ni sayansi, ina misingi yake!
Haitaki uwongo uwongo na ulaghai, mambo ya kusema mamvi fisadi badae unageuka unasema tena mamvi mkombozi ni uzwazwa.
Pambaneni na hali yenu kamanda.
Hahaha ...komaa kamanda
 
KWa wale wanaomuona Dr. Slaa hajitambui, nawapa pole zao sana kwani Dr. Slaa na Dr. Pombe ni kati ya watanzania wachache sana wanaojitambua kwa zaidi ya 98%. Sisi akina kajamba nani na pangu pakavu tia mchuzi ndo hatujitambui tukiongozwa na mwanahabari huru kwa siku ya leo. Ni vyema tuka mweka mwanahabari huru kwenye maombi na duaaa ili mnyaazi mungu amjalie maarifa, hekima na busara na zaidi sana akili ya utambuzi wa mambo kwani IQ yake ya kujitambua bado iko chini sana 12%.
 
Kati ya chedema na Dr slaa nani alisahau mambo aliyoyapigania kwa miaka mingi
Kuna uhusiano gani kati ya slaa kuondoka chadema na hoja ya mtoa mada kuhusu Dr slaa kumuunga mkono magufuli??

Tukiachana na yote hakuwa na sababu ya kusema tuliopigania miaka 20 yametekelezwa ilihali kuna mambo upinzani wanalilia mpaka leo ikiwemo katiba mpya haijapatikana

Hapo alikosea sana Dr slaa
 
KWa wale wanaomuona Dr. Slaa hajitambui, nawapa pole zao sana kwani Dr. Slaa na Dr. Pombe ni kati ya watanzania wachache sana wanaojitambua kwa zaidi ya 98%. Sisi akina kajamba nani na pangu pakavu tia mchuzi ndo hatujitambui tukiongozwa na mwanahabari huru kwa siku ya leo. Ni vyema tuka mweka mwanahabari huru kwenye maombi na duaaa ili mnyaazi mungu amjalie maarifa, hekima na busara na zaidi sana akili ya utambuzi wa mambo kwani IQ yake ya kujitambua bado iko chini sana 12%.
Kwahiyo ni kweli tuliopigania upinzani kwa miaka 20 yamtekelezwa na magufuli??
 
Dr slaa ameshawaambia siasa ni sayansi, ina misingi yake!
Haitaki uwongo uwongo na ulaghai, mambo ya kusema mamvi fisadi badae unageuka unasema tena mamvi mkombozi ni uzwazwa.
Pambaneni na hali yenu kamanda.
Kma ina misingi kwanni yye kasaliti hyo misingi??? Alituaminisha katiba mpya ndio suluhu ila haijapatikana mpaka leo alafu anasema rais katekeleza

Hivi slaa si alitaka list of shame wawekwe jela na wataifishwe sasa mbona hawajakamatwa hilo nalo limetekelezwa??? Slaa hakupaswa kujikomba kiasi kile tunamheshimu sana ila kwa hili kakengeuka
 
Kwahiyo ni kweli tuliopigania upinzani kwa miaka 20 yamtekelezwa na magufuli??
YANATEKELEZWAAA...KAMA HAMTAKI YATEKELEZWE MTUJULISHE KWANI NDO TUNACHOKIONA KUTOKA KWENU. MPAKA SASA HATUJUI MNAPINGA NINI NA MNAUNGA MKONO NINI?
 
Kuna uhusiano gani kati ya slaa kuondoka chadema na hoja ya mtoa mada kuhusu Dr slaa kumuunga mkono magufuli??

Tukiachana na yote hakuwa na sababu ya kusema tuliopigania miaka 20 yametekelezwa ilihali kuna mambo upinzani wanalilia mpaka leo ikiwemo katiba mpya haijapatikana

Hapo alikosea sana Dr slaa
Moja ya ajenda kuu ya chadema ni ufisadi na Dr slaa aliishikia bango kwa zaidi ya miaka ishiri
nahisi majibu unayo tayari
 
YANATEKELEZWAAA...KAMA HAMTAKI YATEKELEZWE MTUJULISHE KWANI NDO TUNACHOKIONA KUTOKA KWENU. MPAKA SASA HATUJUI MNAPINGA NINI NA MNAUNGA MKONO NINI?
Katiba mpya ikwapi ambayo tokea NCCR inaanzishwa ndio kilio cha upinzani hata Dr slaa kampeni za 2010 kipaumbele ilikuwa katiba mpya ssa kma magufuli kaipuuza hoja ya kusema anatekeleza inatoka wapi
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom