Dr. Slaa umebeep, watanzania sasa wamepiga! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Slaa umebeep, watanzania sasa wamepiga!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by zumbemkuu, Oct 11, 2010.

 1. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #1
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 8,938
  Likes Received: 489
  Trophy Points: 180
  Watanzania sasa tumeendelea kidogo, tumetoka KU’DEEP mpaka KU’BEEP.

  Kwa maoni yangu, Dr. Slaa wakati anaombwa kuchukua form ya urais, nadhani alikuwa anajua kuwa hata pata urais, wala hakupima muitikio wa watanzania.

  Nionavyo mimi CHADEMA walimtumia Dr. Slaa kugombea ili kuongeza viti vya wabunge kutokana na uadilifu wake ili kuuza wagombea wa udiwani na ubunge majimboni, pia huenda lengo na madhumuni ni kukikuza chama.

  Kutokana na hali ya kisiasa kwa sasa na mwenendo wa kampeni ulivyo, na kutokana na CCM kuzidi kuweweseka, ni dhahiri kabisa kuwa mabadiliko makubwa yatatokea.

  Dr. Slaa binafsi huenda haamini kinachotokea, CHADEMA pia wanashangaa.

  Ushauri wangu kwa Dr. Slaa, KAMA ALIWA’BEEP WATANZANIA, BASI WAMEAMUA KUMPIGIA, HAWABAHATISHI, AZIDISHE KAMPENI, NA AJIANDAE KUINGIA IKULU.

  Nawakumbusha CCM na maneno ya Lula wa Ndali-Mwananzela kuwa “Mbinu ya vyombo vya dola kutumia nguvu kuzima mabadiliko zimeshaonyeshwa mara kadhaa kushindwa. Zimeshindwa Zimbambwe, zimeshindwa Ukraine, zimeshindwa Kenya, zitaendelea kushindwa kwani kila zama zina mashujaa wake na kila shujaa ana ujumbe wake”.
   
 2. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,119
  Likes Received: 117
  Trophy Points: 160
  Asante mkuu.
   
 3. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,625
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Asante
   
 4. muonamambo

  muonamambo JF-Expert Member

  #4
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 764
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  big up
   
 5. FIKRA MBADALA

  FIKRA MBADALA Senior Member

  #5
  Oct 11, 2010
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 167
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  unapoingia katika siasa hauna budi kukubaliana na hali halisi ilivyo uwanjani, ukicheza fair play na mwenzako atacheza hivyo na kinyume chake ni sahihi.
   
 6. MTWA

  MTWA JF-Expert Member

  #6
  Oct 11, 2010
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 1,013
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Kila niachangiapo kuhusu rais "Potential" na mhimu kama huyu kimsingi huwa naomba wote "tuliofunuliwa uelewa" kuwa kwa sasa tunahitaji mtu wa aina hii, basi tuombe sana maana campaign chafu zimeshafanyika tena zisizowahi tokea.

  Cheki wanafunzi wa vyuo wanavopigiliwa msumari. Hivi haki wanayosema kila wakati ni ipi hasa kama wananyimwa wasomi kwa makusudi mazima

  Tuombe watu wote wanaopiga makofi kwa ushabiki huku wakiwa na gunia la misumari ya shida kichwani waelewe kuwa RAIS wao mkombozi ndo huyu sasa kaja.

  Lakini nimezunguka koote naona bado kiza kinazunguka.

  ILA SIKU YA KURA SISI SOTE TUMPE Dr. Slaa aende pale Ikulu. hajabeep anawajibika kama mtu mwenye uwezo huo!
   
 7. FIKRA MBADALA

  FIKRA MBADALA Senior Member

  #7
  Oct 11, 2010
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 167
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kama nashindwa kukuelewa lakini kisha nakuelewa.
   
 8. FIKRA MBADALA

  FIKRA MBADALA Senior Member

  #8
  Oct 11, 2010
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 167
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama amebeep anaweza asipigiwe simu. kuna watu ukiwabeep hawapigi.
   
 9. MTWA

  MTWA JF-Expert Member

  #9
  Oct 11, 2010
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 1,013
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Hiyo ni kweli hasa wakiona kuwa hawana haja ya kupiga, au kama umeshazoea kubeep, au msaada wa tumbo lako halafu uwabeep na wao wapige! kwa nini?
   
 10. Binti Maringo

  Binti Maringo JF-Expert Member

  #10
  Oct 11, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 2,805
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mbio za sakafuni huishia ukingoni...Mtashangaa siku ya mwisho kwani ilikuwaje enzi zile za Mrema...wafuasi niwengi sana lakiniwapigakura ni wachache....CCM for 2010 read my words hakuna cha DR slaa wala cousin wake Dr Slaa.....Lets Go CCM Na tulenge JUU Thats out Motto@.

  xoxo BM
   
 11. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #11
  Oct 11, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 11,523
  Likes Received: 945
  Trophy Points: 280
  Ningesoma mistari michache tu hapo juu ningetukana mpaka kesho. Nikekufurahia ulivyomalizia, Thanx!
   
 12. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #12
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 8,938
  Likes Received: 489
  Trophy Points: 180

  MSIOJUA NA MJUE SASA, NA KAMA HAMTAKI KUJUA TUTAWALAZIMISHA KUJUA, WAPELEKEENI SALAM NA CCM NAO WAJUE KUWA CHADEMA NA DR.SLAA (PHd) WAPO JUU, HABARI NDO HIYO.
   
 13. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #13
  Oct 12, 2010
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,398
  Likes Received: 127
  Trophy Points: 160
  Baki na maringo yako, lakini ujumbe ni huo, Slaa hakuutaka Uraisi na pengine ni kweli kwamba wenzie walitaka kumtumia wapate wabunge na madiwani, lakini sasa kila ishara inaonyesha ile 'deep' sasa kweli imekuwa ni 'beep' na yeye ameichangamkia, amepiga simu na wananchi wameipokea na hakuna kum-beep tena ila wanampigia, wanamhitaji. Sasa kwa nini JK na kundi lake wanataka kuwakatia simu zao hawa wananchi wenye hamu ya kuzungumza na jamaa yao, kweli wanafanya kitu kibao mwanetu, eti hebu fikiria wewe unampigia simu mtu kwa hamu kubwa mno halafu lijamaa linakunyanganya hio simu au linapiga makelele ili usimsikie! Sio vizuri Bint Maringo, usiingilie mapenzi ya mwenzio!
   
 14. P

  PWAGU Member

  #14
  Oct 12, 2010
  Joined: Apr 23, 2010
  Messages: 30
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Uzuri wa upinzani wa bongo ni mabingwa wa kulalamika na kushindwa yaani baada ya oct 31 ccm itapokuwa imetoa kipondo, dr. Slaa atakuwa kama mrema, bingwa wa kushindwa. Kisiasa a\takuwa kaisha, hata sasa si unaona kila siku yeye na wenzake wanaongoza kwa kampeni za malalamiko na udini.
   
 15. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #15
  Oct 12, 2010
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Wabunge wengi ni Ruzuku nyingi...2015 kutakuwa hakuna kuchangishana.
   
 16. t

  titomganwa Senior Member

  #16
  Oct 12, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 126
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Dr. Slaa ni chaguo la wengi. Huhitaji kuisikia REDET au SYNOVET kujua hili, wapigie simu watu 20 kwa MTANDAO WOWOTE wasikie maoni yao. wapigie watu kumi waulize kuwa wanasikia nini watu wakisema juu ya uchaguzi huu. hata kama kura zitaibwa, haitakuwa rahisi kama mwaka 1995, kwani safari hii, wale waliokuwa na miaka nitano mwaka 1995 sasa wanamiaka 20! halafu wakesoma sekondari za kata na wakaona machungu ya uongozi wa CCEMU.:hand:
   
 17. R

  RMA JF-Expert Member

  #17
  Oct 12, 2010
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 410
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  :rain:Karibu Rais wetu Dr Slaa! :A S 465::director:


  Huyu ni mtanzania wa pili baada ya Nyerere kuchukia ufisadi kwa vitendo. Ni mtanzania wa pili kuchukia umaskini wa watanzania kwa vitendo. Ni Dr. Slaa aliyesimama na kutaja majina ya wala rushwa na mafisadi. Akataka wale wanaopinga wampeleke mahakamani. Hakuna aliyethubutu kujitokeza kumpeleka mahakamani.


  Ni Dr. Slaa aliyesimama bungeni kuomba posho za wabunge kupunguzwa kuzielekeza zaidi kwa watanzania maskini. Ni Dr Slaa aliyesimama bila woga kunyosha vidole kwa matumizi mabaya ya ofisi za umma. Ni Dr Slaa amekuwa mtanzania baada ya Nyerere kutoa hoja za nguvu zinazomlenga kumkomboa mtanzania maskini. Maisha bora kwa kila mtanzania yako wapi? Ajira milioni moja ziko wapi? Hebu mwenye mbavu za kujibu swali hili ajibu bila unafiki!:rain:


  Ni Dr Slaa anayeweza kudhibiti matumizi mabaya ya ofisi za umma. Ni Dr Slaa anayeweza kuwapa elimu ya bure watoto wetu pale mlimani. Achana na longolongo za CCM kuwatoza ushuru watoto. Waulizeni majukwaani wao Nyerere aliwatoza ada? Kama si kutaka watanzania waendelee kuwa mambumbumbu ni nini? kama si kutaka watanzania tuendelee kuwa watumwa ni nini?


  Ni Dr Slaa anayeongelea mfumko wa bei -nani hajajua dola leo hii ni sawa na tsh 1500. Uchumi unadidimia kwa kasi. Ahadi nyingine za uongo lukuki zinatolewa tena, wakati zile tulizoahidiwa mwaka 2005, hata moja haijatekelezwa. Watanzania walio wengi na hasa wa vijijini, wamelala usingizi. Wanafumbuliwa macho, lakini wamesinzia bado! Wanatabasamu, wanachekelea na kuridhika na vitisheti vya kijani na vikofia za njano. Wamekwishazoea shida kiasi kwamba wanadhani ni sehemu ya maisha yao. Ee mwenyezi Mungu, tunusuru na hili balaa..:loco:


  Ni Dr.Slaa anaweza kuzuia wizi wa matrilion ya pesa kutoka migodi yetu ya Buzwagi, Geita, Bulyankulu, Buhemba, Nyamongo, Tulawaka, Nzega na Tanzanite. CCM wameshindwa kwa sababu ni washirka wakubwa na wameruhusu wizi huo. Ni Dr Slaa anaeweza kuwalipa wafanyakazi zaidi ya shilingi 350.000 achana na longolongo za CCM ambayo imeshindwa kusimamia maliasili ambazo zingeliwapa wafanyakazi kima cha chini kinachokidhi mahitaji yao.


  Ni Dr. Slaa ambaye amepanga kubadili katiba ili Rais afuate matakwa ya walio mwajiri ambao ni wananchi. Waulize CCM hata kama mtu kaiba anapewa mda arudishe pesa. Hivi inaingia akilini kweli? Utawala wa sheria uko wapi? :director::wink2:


  CCM hawawezi hayo? Eti wanataka ushahidi. Nani kawambia rushwa tule wawili harafu tutoe vielelezo? Tunaiona rushwa kwa matokeo yake. Matengenezo ya barabara ya bilion 200, baada ya siku mbili imeharibika. Kwanini usimfukuze waziri na katibu wake wa wizara kwanza? CCM hawawezi! eti wanataka vielelezo!


  Ni Dr Slaa anayeweza kufanya hayo. Nani anabisha! Si tumeona alivyowataja mafisadi wote! hapo akiwa ni mbunge tu! Je akiwa rais si watakimbia nchi? Jamani nawambia tumpe miaka mitano tu awakurupushe muone moto utakavyowaka.. Tutapata dawa, tutapata shule za bure, tutapata madawati. Jamani hivi kweli karne ya leo watoto wanasoma wamekalia mawe? We must be serious! :alien::director: :hat:


  Nani asiye jua madaktari wetu wengi bingwa wapo botswana kwa sababu ya maisha duni Tanzania na hivi kwenda kutafuta maisha bora wakati hapa kwetu wananchi maskini wanakufa bila madawa? Nani asiyejua matatizo ya umeme, maji, makazi, maradhi, yanavyotutesa? Nani asiyejua wakulima wetu wasivyokuwa na masoko ya mazao yao? Nani asiejua asilimia 85 ya watanzania wanatumia vibatari au makoroboi kama mwanga? nani asiejua tunavyonyonywa na hawa wakoloni waliokuja kuchukua kila kitu?


  Jamani wafanyakazi, wakulima, na wanafunzi, kwa nini mnalala usingizi? Kwa nini mnapiga miayo ya njaa wakati maghala yetu yamejaa nafaka? Ni akili gani hii? Nchi yetu inazo raslimali za kututosha, lakini wanaozifaidi ni vibaka wachache. Mtalala hadi lini?:rain::spider:


  Ni Dr Slaa mzalendo wa kweli, na sio kwa ajili ya sifa, anaweza kutuvusha tulipo. Nchi hii ni maskini na umaskini wenyewe ni wa kujitakia. Tanzania ni tajiri tuna kila kitu - mito, maziwa, national parks, migodi, mazao ya misitu, na kila aina ya utajiri. Lakini kila leo rais kuwaabudu wazungu na bakuli la kuombaomba! Naona huruma na umaskini wa kifikra wa watanzania. Ee Mungu utuhurumie!


  Hivi kuna mtu hajui mapolisi wanalala kwenye vibanda vya mabati? Hivi kuna ambao hawajui mapolisi watendaji wanalipwa laki moja? Wamekosa nini hawa? Ni ajabu! pamoja na laki yao moja utakuta bado wanatumika kuwanyanyasa watetezi wao. Hata maaskari amkeni hiyo laki moja yenu haina tija hadi mrubuniwe kuwanyanyasa wapinzani ambao kimsingi wanawatetea ninyi! Hivi maaskari mnayo macho ya kuona? Jamani tuache woga inawezekana! Mbona Kenya wameweza? Mbona malawi wameweza?Mbona zimbabwe wameweza? Mbona Ghana wameweza? Kufanya mabadiliko sahihi, inawezakana na nafasi ni hii tuitumie. :wink2: :bolt:


  Tumtume Dr Slaa atukurupushie wezi wote na atuwekee katiba sawa. Huo ndio msingi wa yote. Ni Dr. Slaa asiyeogopa kuwepo na mgombea binafsi. CCM hili hawaliwezi. Wamelipinga hadi mahakamani. Wanataka wao tu ndio waendelee kututawala na kutunyonya.


  Jamani 2010 hakuna kudanganyika! enough is enough. Acheni kudanganyika. Wakati ndio huu. Watanzania msipoamua sasa, mtamlaumu nani tena? Nawatamani watu wa kule Mara -hakuna kura inaibiwa. Zote zinasimamiwa. Tukibadilika inawezekana, tena ni rahisi.


  Peleka ujumbe huu kwa marafiki, ndugu, jamaa, babu na bibi yako kule kijiji ambako wanadhani bado Nyerere ndiye rais wa nchi hii. Waambie Nyerere alikwishakufa na nchi imeishatekwa nyara na vibaka. Peleka ujumbe huu haraka kwa simu kama ipo, au kwa njia ya posta, mradi tu wale jamaa waliochoka kuishi wasiikwapue barua wakidhani ni hela..:bolt::loco:




  [FONT=Book Antiqua, serif]Kila la heri: mak.ralph@yahoo.com[/FONT]​
   
 18. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #18
  Oct 12, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,070
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Jina Lako ni dhahiri una ya Yule mgombea bingwa wa kucheza viduku
   
 19. DICTATOR

  DICTATOR JF-Expert Member

  #19
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wewe pwagu, kuna tofauti kubwa kati ya Dr Slaa (PhD) na Mrema L.A (Form Four Leaver anyway ngoja nimpe BA sijui ya nini). Kama mtu umeingia darasani sidhani kama unaweza kama mrema alivyo sasa.
   
 20. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #20
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 8,938
  Likes Received: 489
  Trophy Points: 180

  usimuamshe, ataamka mwenyewe baada ya october 31.
   
Loading...