Dr. Slaa: Tukishika Dola tutaruhusu utengenezaji wa pombe ya gongo kisheria

ifweero

JF-Expert Member
Jun 12, 2013
7,957
1,327
Saturday, 14 December 2013 ·

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetoa mpya baada ya kueleza kuwa kitakapofanikiwa kushika dola kitaruhu Shirika la Viwanda Vidogo Vidogo (SIDO) kutengeneza mitambo ya kutengenezea pombe aina ya gongo. Katibu Mkuu wa Chadema, Dk.Willbroad Slaa, akizungumza na wananchi wa Jimbo la Kasulu Vijijini alisema kama gongo itatengenezwa kwa mitambo maalum itaondoa mianya ya rushwa kwa polisi ambao wamekuwa wakiwakamata wanaotengeneza kwa kificho na kuwafanya vitega uchumi vyao.

"Gongo sasa hivi ni haramu sababu inatengenezwa kwa kificho katika mazingira machafu, tukishika dola tutataka SIDO itengeneze mitambo ya kutengeneza gongo ili iwe katika hali ya usafi," alisema.

Mitambo hiyo itakayotengenezwa na SIDO itakapouzwa itaiingizia mapato serikali pia wauzaji wa gongo watafanya biashara hiyo kwa amani tofauti na sasa ambapo wanaifanya kwa kificho na wakikamatwa fedha zote wananufaika polisi.

Dk. Slaa alisema hata suala la kukamata watu wanaotengeneza silaha linapaswa kuangaliwa upya kwani wanaokamatwa wakifanya kazi hiyo wangekuwa wanashikiliwa kwa muda na baadaye wanapelekwa katika kiwanda cha serikali cha kutengenezea silaha ili watuhumiwa hao wapeleke ujuzi huo huko badala ya kuwafunga jela.

Dk. Slaa alisema matatizo yote yanatokana na wasomi kutofikiri namna ya kuisogea nchi mbele kimaendeleo.

"Nchi hii imelala, imechoka sababu waliopewa madaraka wamelala, wamejisahau hawatambui kuwa wamepewa nafasi hizo ili kuwatumikia wananchi," alisema.

MTAMBO WA KUPIKIA GONGO KATIKA PICHA.
attachment.php

CHANZO: NIPASHE
 
Nchi ya Tanzania Mapato yake asilimia kubwa ni yanatokana na POMBE na TUMBAKU!

Tafakari!
 
Haya kazi kwenu Great Thinkers!Inawezekana kweli hiyo au just political gimick?
 
Hahahahaha hii kali.

Yaani kukamatwa na silaha kiwe kigezo cha mtu kupewa ajira!!! Kijana akikosa ajira anajikamatisha na silaha haramu halafu anapewa ajira!

Tuliwaambieni kuwa Slaa ni mwanasiasa mlaghai, sasa mnaona? Kapokewa na kikundi cha wauza gongo anaona awalaghai kwa kuitetea gongo!
 
Hata kama ni Bangi ikitungiwa Sera na Ikachambuliwa Vizuri itakua ni vema kuliko kukataza wakati kuna namna ya Kuitengeneza.
Hongera Chadema kwa Uchambuzi Mzuri.
 
Hahahahaha hii kali.

Yaani kukamatwa na silaha kiwe kigezo cha mtu kupewa ajira!!! Kijana akikosa ajira anajikamatisha na silaha haramu halafu anapewa ajira!

Tuliwaambieni kuwa Slaa ni mwanasiasa mlaghai, sasa mnaona? Kapokewa na kikundi cha wauza gongo anaona awalaghai kwa kuitetea gongo!
Mkuu, ndio mana inaitwa siasa. Unacheza tu na akili za watu
 
Hata kama ni Bangi ikitungiwa Sera na Ikachambuliwa Vizuri itakua ni vema kuliko kukataza wakati kuna namna ya Kuitengeneza.
Hongera Chadema kwa Uchambuzi Mzuri.
Pole sana mkuu. Hivi binadamu ana miguu mingapi, sita ee?
 
Gongo=viroba, kwani viroba vinauzwa mafichoni? Msimuonee wivu dr kwa ubunifu wa ajira
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom