Watanzania
JF-Expert Member
- Jul 7, 2009
- 727
- 42
Ni jambo la wazi kuwa Watanzania wengi waliokupigia kura mwaka huu 2010 wanahamu kubwa kusikia kutoka kwako juu ya shughuli zako za kila siku za kutuongoza watanzania katika kuiendeleza nchi yetu. Dr. Slaa umebeba morali ya watanzania kiasi kwamba uongozi wako kwa watanzania unahitajika kila siku. Hivyo hata kama utakuwa umebanwa sana na shughuli tunaomba uandae utaratibu wa kiofisi ili kila siku tufahamu shughuli za kisiasa unazofanya katika kusaidiana na watanzania kuleta mabadiliko ya uongozi katika nchi yetu kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa taifa letu. Mungu ibariki Tanzania.