Mkondakaiye
JF-Expert Member
- Dec 5, 2011
- 838
- 174
Napenda kuchukua nafasi hii kumkumbusha Rais wetu Dr. Slaa kutimiza ahadi yako uliyoitoa wakati wa kampeni za uchanguzi ukiwa mjini njombe kuwa kama hutachaguliwa kuwa rais basi utakuwa na muda wa kupita kijiji hadi kijiji kuimarisha chama kwani utakuwa na muda mwingi wa kuimarisha chama.
Toka uchaguzi uishe kazi ya kuimarisha chama kama ulivyo ahidi bado haijafanyika. Kumbuka kuwa huku mawilayani viongozi wa wilaya wengi wao bado hawakubaliki na jamii inayowazunguka. Wale wanao kubalika wanaogopa nguvu ya ccm kuwahujumu kikazi (kama ni waajiliwa wa serikali) au kibiashara (kama ni wafanyabiashara)
Katika nchi hii kuna baadhi ya mikoa ambayo imesha amu na kujua upinzani ninini. Mikoa kama Arusha, Kilimanjaro, Mbeya (baadhi ya wilaya), Mwanza, Dar na kigoma. Lakini kuna mikoa bado nguvu ya ziada inahitajika ili kuteka kundi kubwa la watu ambao bado mawazo yao yapo kwa magamba. Mikoa kama Mtwara, Lindi, Tabora, Dodoma, Morogoro, Singida, Ruvuma na Iringa.
Kumbuka kuwa jimbo la iringa mjini wananchi walipiga kura kuwaadhibu magamba kwa kuondolewa chaguo lao. Ndo hapo CDM ikapata hicho kiti. Kwahiyo ,Tafadhali Dr slaa timiza ahadi yako ya kupita mawilayani ili kuimalisha chama. Kumbuka kuwa CDM haiwezi kuchukua nchi mwaka 2015 kwa kutegemea mikoa ya Arusha, Mbeya, Mwanza, Kilimanjaro na Dar pekeyake.
Nimefurahi kusikia kuwa kamanda lema atatembea mikoa mbalimbali kuitangaza CHADEMA. Nadhani huu utakuwa mwanzo mzuri katika kuitimiza ahadi ya Dr slaa. Nashauri kazi hiyo ianzie vijijini.