Dr Slaa, tafadhali toeni tamko kuhusu ufisadi wa kupindukia unaofanywa na NEC | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr Slaa, tafadhali toeni tamko kuhusu ufisadi wa kupindukia unaofanywa na NEC

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mwafrika, Nov 1, 2010.

 1. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #1
  Nov 1, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Dr Slaa,

  Kwanza kabisa, Asante sana kwa kazi nzuri uliyotufanyia watanzania mwaka huu. Mafanikio ya vyama vya upinzani katika ngazi za udiwani na ubunge yamechangiwa kwa kiasi kikubwa sana na ushiriki wako kwenye kampeni za uraisi.

  Hata hivyo, hii speed ya kutangaza majimbo 14 kwa siku inayofanywa na tume ya uchaguzi, na hili la kuchagua tu baadhi ya majimbo ambayo "wamefanya vizuri" kwa mtizamo wao, ni jambo ambalo linahitaji tamko kubwa sana toka kwako na viongozi wa chadema.

  Jana wakati tukifuatilia matangazo ya uchaguzi toka kwenye TV mbali mbali Tanzania, watangazaji wote walikuwa wanakwepa kutaja matokeo ya ngazi ya uraisi. Ilifikia hatua Masako wa ITV anamkataza mmoja wa watangazaji kutangaza matokeo ya uraisi kutoka katika vituo mbalimbali.

  CCM waligundua kitu kimoja, watanzania walikuwa wanajumlisha matokeo ya kura yaliyokuwa yanatangazwa toka katika kila kituo. Na kama ukifuatilia uchaguzi wa kenya wa mwaka 2007, hii ndiyo ilisababisha ugumu sana kwa tume ya uchaguzi kubadilisha matokeo maana wananchi walikuwa wanajua tayari hesabu yao (kutokana na kura za kituo kimoja kimoja).

  CCM wamecheza mchezo wa kuficha kura za uraisi toka kituo kimoja kimoja na wanazitoa kwa mafungu. Huu ni wakati wa nyie kutoa tamko ili kuwahakikishia wafuasi wenu (nikiwemo mimi) kuwa matokeo yanayotolewa sasa hivi na tume ya uchaguzi yanalingana na yale ambayo wasimamizi wenu wa kila kituo cha uchaguzi wameyathibitisha.

  Again, asante sana kwa kazi nzuri unayolifanyia taifa la watanzania.

  No matter what jeshi la wananchi watanzania litaamua kufanya, You are my president Dr Slaaa.

  Asante
   
 2. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #2
  Nov 1, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Angalizo na swali muhimu, ni nani mwenye mamlaka ya kupinga kinachoendelea sasa hivi? Kama nijuavyo mimi, matokeo yakishatangazwa ndio imetoka hivyo... je strategy ni ipi?
   
 3. mtuwatu

  mtuwatu Member

  #3
  Nov 1, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 95
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi kwanini wananchi tusigome tukawasusia nchi hao CCM tuone watamtawala nani?
   
 4. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #4
  Nov 1, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  ccm wana msemo kuwa mkisusa wao wala (watakula tu). CUF waliwahi kususia enzi za komandoo na haikusaidia
   
 5. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #5
  Nov 1, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,377
  Likes Received: 3,140
  Trophy Points: 280
  gud straegy
   
 6. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #6
  Nov 1, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  tubanane nao tu mkuu mpaka kieleweke
   
 7. i

  ilboru1995 JF-Expert Member

  #7
  Nov 1, 2010
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,331
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  Makame na kiravu must die....wanacheza na future yetu watanzania.
   
 8. Wakuletwa

  Wakuletwa Senior Member

  #8
  Nov 1, 2010
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tena muda si mrefu mwenyekiti wa tume katoka kusema eti inaweza kufika hadi ijumaa.
  chanzo by bbc
   
 9. nzitunga

  nzitunga Senior Member

  #9
  Nov 1, 2010
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hii inasikitisha sana. Ambako upinzani wameshinda, --recount--, ambako CCM wameshinda --straight anouncement--. Hii peke yake si sawa. Kwenye kambi za CCM, matokeo harakaharaka. Kwenye Kambi za Upinzani hasa CHADEMA, matokeo mpaka wananchi watishie kulala barabarani. Hii ni sawa jamani? Unapominya haki unachangia umwagaji damu, maana amani ni huzaliwa na haki.
  Hivi hatutakubali kabisa, hata mabomu watupige, ni heri kufa unapigania uhuru wa nchi yako, uliyopewa na Mungu kuliko huu udhalimu.
  Lakini hata hivyo, kuna raha gani kutawala pasipo kushinda, huu ni ufisadi wa kisiasa. Dr. wa ukweli toa tamko tafadhali.
   
 10. gillard

  gillard JF-Expert Member

  #10
  Nov 1, 2010
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 227
  Likes Received: 149
  Trophy Points: 60
  kwa kweli hili linabidi kuangaliwa hawa ccm wanatuandaa kisaikologia kwa kutangaza majimbo ambayo wameshinda ili hata hapo watakapochakachua na kuja na takwimu zao wenyewe tusishtuke wanatafuta ushindi wa lazima kwanini jamani wasikubali kushindwa jamani wahusika wanaoweza kulizungumzia hioli hebu chukueni hatua tunaibiwa.
   
 11. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #11
  Nov 1, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  slow down buddy ... we are not ( ) to determine that
   
 12. Emma Lukosi

  Emma Lukosi Verified User

  #12
  Nov 1, 2010
  Joined: Jul 22, 2009
  Messages: 932
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Jino kwa jino hasusi mtu, Na wakitulazimisha Hatutawaliki ng'ooo!....
   
 13. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #13
  Nov 1, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  na jamaa kila wanakofanya recount, wanashinda....

  chadema acheni kucheza nice na ccm, mnapoteza kura hivi hivi.
   
 14. nzitunga

  nzitunga Senior Member

  #14
  Nov 1, 2010
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mwafrika, kilichobaki ni wananchi kuchukua madaraka tu. Sheria inayotumika ni mbovu, na hii ndo huwakatisha tamaa watanzania kupiga kura, sababu ni usanii mtupu. Only people's power can work.
   
 15. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #15
  Nov 1, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  itakuwa kazi kwa wananchi kuchukua madaraka mkuu, ni vigumu sana. Cha muhimu ni kwa chadema kuhakikisha wanatoa tamko sasa hivi ili kuweka mwelekeo wa nini kifanyike kwa muda huu
   
 16. P

  PapoKwaPapo JF-Expert Member

  #16
  Nov 1, 2010
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 380
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  mamii usijali chadema wanafanya mkutano kesho Arusha......nadhani watatumia nafasi hiyo kulizungumzia hili..hope umenisoma
   
 17. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #17
  Nov 1, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  they betcha
   
 18. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #18
  Nov 1, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  CHADEMA tambueni hili
  Wakati wa kura kuhesabiwa na mawakala vituoni idadi inaandikwa na kwenye fomu wanasaini. Ila mchezo hutokea inbetween kituo to wilayani. hapo kati kama gari halisindikizwi na wakala basi masanduku mapya yanapakizwa kwenye gari ili wakifika mwisho wa safari msimamizi analazimisha recount.
  Lazima mtoe tamko ili dunia ielewe kinachoendelea.
  TUMEZILINDA KURA, SASA NI KAZI YENU KUYALINDA MATOKEO
   
 19. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #19
  Nov 1, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Hiki ni kitu ambacho ingebidi wakifanye over and over hadi makamba na yule pirate Kinana waogope
   
 20. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #20
  Nov 1, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  kufikia ijumaa watakuwa wamempa Kikwete asilimia 95 ya kura
   
Loading...