Dr. Slaa Sio Wa "CHADEMA" Ni Wa Watanzania wote

JIULIZE KWANZA

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
2,569
0
BAADHI yetu hatuna kawaida ya kuunga mkono wanasiasa kwa kiwango tunachoonyesha sasa kwa Dk. Wilbrod Slaa.
Wanasiasa ni vigeugeu; wengi ni wasanii na mafisadi. Watakutumia leo, watakutupa kesho.
Lakini wanapotokea wanasiasa makini wa viwango vya Dk. Slaa, hatuzungumzi tena lugha ya kutumiwa. Tunajitumia.
Hii ni zaidi ya kujitumia. Ni kuunga mkono, kuweka nguvu ya ziada katika harakati za ukombozi ambazo Watanzania wamekuwa wanalilia kwa miaka kadhaa sasa.
Maana kama tumekuwa tunasikitika kwa kuendelea kuishi chini ya ombwe la uongozi na kivuli cha ufisadi kwa miaka yote hii, hasa mitano iliyopita, tunasubiri nini kumuunga mkono mtu ambaye amekuwa mstari wa mbele kuwashika mashati bila woga mafisadi na wasanii wa kisiasa?
Katika wimbi hili jipya la mageuzi lililoikumba Tanzania baada ya Dk. Slaa kutangaza kugombea urais mwaka huu, limeondoka ombwe jingine, ambalo rafiki yangu na mchambuzi wa kisiasa, Absalom Kibanda, amenieleza kuwa lilikuwa linaukabili hata upinzani wenyewe.
Wapiganaji ni wengi, viongozi na wakosoaji katika kambi ya upinzani ni wengi; lakini wanaolingana na haiba ya Dk. Slaa ni wachache.
Nataka kuamini kwamba sasa, wapinzani wameshapata mgombea mmoja wa kumkabili Rais Kikwete. Na dhana hii ndiyo iliyonifanya niandike Jumapili iliyopita kwamba wakati sasa umefika, wapinzani wamuunge mkono Dk. Slaa.
Lakini wapo baadhi ya wasomaji makini wa safu hii ya Maswali Magumu ambao walinikosoa kwa haki kabisa, wakisema wanaopaswa kumuunga mkono Dk. Slaa si wapinzani, bali Watanzania wote.
Sababu ni kwamba Dk. Slaa anazungumza lugha ya wote. Anatetea masilahi ya wote. Na Ingawa amekuwa mbunge wa Karatu kwa muongo mmoja na nusu, wananchi ni mashahidi kwamba amekuwa mwakilishi wa Watanzania wote.
Kwa kutazama wimbi hili na mvuto alionao kwa wananchi, ni haki kabisa kusema kuwa ingawa ana wadhifa wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Slaa sasa si wa CHADEMA.
Si makosa kusema kwamba ingawa anagombea urais mwaka huu kwa tiketi ya chama hicho, Dk. Slaa si wa CHADEMA tena. Ni Slaa wa Watanzania.
Ukweli huu, ukichanganywa na historia ya utendaji wa Dk. Slaa, ndio ulimfanya mmoja wa wasomaji hao niliowataja hapo juu kuniandikia ujumbe huu:
“Nionavyo mimi, mapambano si kati ya chama na chama, bali kati ya uadilifu na ufisadi; au kati ya walalahoi na walanchi. Tujuane kwa vitendo si kwa vilemba vya sare.”
Itawauma kina Yusuph Makamba (Katibu Mkuu wa CCM) na Pius Msekwa (Makamu Mwenyekiti wa CCM- Bara); lakini Dk. Slaa anaungwa mkono hata na wana CCM wenyewe.
Na wiki hii nikiwa mikoani, nimekutana na wana CCM wengi ambao walikuwa wanaendelea na michakato ya kuwapata wabunge na madiwani wa majimbo yao, lakini kura zao za urais wameshaamua watampa Dk. Slaa.
Nimekutana na baadhi ya wana CCM ambao wamekuwa wanakerwa na mwenendo wa chama chao katika siku za hivi karibuni; kwa sababu hiyo walishaamua kutopiga kura mwaka huu. Dk. Slaa amewaamsha na kuwapa sababu ya kupiga kura.
Nimekutana na wananchi wa kawaida wanaoamini kwamba CCM ni wezi wa kura, na kwamba hata wakimpigia Dk. Slaa zitaibwa; lakini wamedhamiria wampigie ili nyoyo zao ziridhike.
Wapo pia ambao walishaona siasa, hasa za upinzani, hazina maana. Wamebadilika na kuamka upya, na sasa wako nyuma ya Dk. Slaa.
Nimekutana na wana CCM wengine ambao wangependa rais ajaye atoke CCM, lakini wanapolinganisha haiba za wagombea waliopo, nafsi zao zinawasuta. Dk. Slaa amewavuruga.
Na mmoja wa makada wa CCM mkoani Mwanza amenieleza kuwa alichokiona siku Dk. Slaa alipozuru Mwanza kuomba sahihi za wadhamini, ni ajabu ya kisiasa yenye wingi wa watu ambao aliuona mwaka 1990 Tanzania ilipotembelewa na Papa Yohane Paulo II.
Nimewasikia baadhi ya makada wakuu wa CCM na mashabiki wakuu wa Kikwete wakitamka wazi kwamba, “Dk. Slaa asipodhibitiwa anaweza kuwa kama Obama.”
CCM wana hofu ya kushindwa. Jeuri ya Ushindi wa kishindo imenyauka. Wamegundua kwamba hata kama wangetumaini kura za wanachama wao (wanajikadiria kuwa milioni nne), kama Watanzania wataamua kufanya kweli, hizo za wana CCM hazitatosha.
Lakini ukweli ni kwamba wana CCM wote hawawezi kukipigia chama chao kura; maana hata huko Karatu na kwingine ambako vyama vya upinzani vimekuwa vinashinda, ni kura za wana CCM na wapinzani.
Watanzania wanaangalia mgombea kwanza, chama baadaye. Ndiyo maana nasema kuwa unapowaweka katika ushindani wagombea wakuu wawili wa urais, Jakaya Kikwete na Dk. Slaa, unakuwa unawatega Watanzania.
Wapo ambao itikadi inawaelekeza wampigie kura mtu wa chama chao, lakini akili timamu na utashi wa nafsi zao vinawatuma kuzingatia umakini, wanafikiri na kuwaza juu ya muono mpya wa Tanzania; wanakerwa na ufisadi na wanajua kuwa CCM ni chama kilichozeeka na kuishiwa nguvu na upya unaostahili. Hawa watakaa upande wa Dk. Slaa.
Waliobaki – wanaochagua kwa kufuata fadhila, chai, pombe, khanga, kofia au fulana; au walio na udugu au ukaribu wa lazima kwa mgombea wa CCM; wanaotegemea ufisadi ili waweze kuishi, wasiokerwa na usanii wa kisiasa uliofanywa na watawala waliopo; wasio na upeo wa kuona uwezo mdogo wa Kikwete katika miaka minne iliyopita, walio sehemu ya ombwe la uongozi ambalo tumelijadili kwa miaka mitatu mfululizo, watakaa upande wake.
Kampeni hazijaanza rasmi. Lakini zitakapokuwa zimeanza, tunajua kuwa utakuwa ushindani mkali wa nguvu hizi mbili za Kikwete na Dk. Slaa. Tutahitajika kuwapima kwa vigezo halisi kutokana na kazi walizofanya, uwezo na upeo wao.
Tutasikiliza hoja zao jinsi watakavyofanya tofauti na kinachofanyika sasa; na tutapima dhamira zao na nia zao, kwa kuwatazama pia wale walio nyuma yao, wanaowasindikiza Ikulu.
Tutahitaji kutafakari vema majibu ya maswali tutakayowauliza. Tutawatazama usoni bila soni na kugundua mkweli na mwongo; fisadi na adili; kiongozi na msanii wa kisiasa; anayependwa na anayekubalika; mlanguzi wa kura na mwombaji wa kura; mwenye jipya na anayerudiarudia mambo yaliyochoka na kupauka; mwoga na rafiki wa mafisadi na mpambanaji jasiri dhidi ya ufisadi, shujaa wa Watanzania.
Hapa hakuna la CHADEMA. Ni Utanzania. Na hii ndiyo bendera ambayo baadhi yetu tunataka ipeperushwe na Dk. Slaa. Tusisite, tusione aibu kutetea kitu chema. Watanzania muungeni mkono.
 
Kadogoo

JF-Expert Member
Feb 26, 2007
2,072
1,195
Ni uchaguzi upi tena unataka tumuunge mkono? Unamaana wa mwaka 2015? Au upi? Wa 2010 tumeshamaliza yeye kajaribu na kura alizopata hazikutosha kumpeleka ikulu, hivyo kama atataka kugombea tena 2015 basi itategemea na nyota yake kama itakuwa bado inameremeta wakati huo! Ila sasa anachotakiwa kufanya ni kuendelea kukijenga zaidi chadema hasa vijijini kwenye wapiga kura wengi ambao bado hawajafikiwa na chadema pamoja na wapinzani wengine!

Na ushahidi ni uchaguzi wa mwaka huu tumeona chadema wakizoa kura nyingi mijini kuliko vijijini huko ni ccm tu!
 
QUALITY

JF-Expert Member
Sep 27, 2010
853
0
BAADHI yetu hatuna kawaida ya kuunga mkono wanasiasa kwa kiwango tunachoonyesha sasa kwa Dk. Wilbrod Slaa.
Wanasiasa ni vigeugeu; wengi ni wasanii na mafisadi. Watakutumia leo, watakutupa kesho.
Lakini wanapotokea wanasiasa makini wa viwango vya Dk. Slaa, hatuzungumzi tena lugha ya kutumiwa. Tunajitumia.
Hii ni zaidi ya kujitumia. Ni kuunga mkono, kuweka nguvu ya ziada katika harakati za ukombozi ambazo Watanzania wamekuwa wanalilia kwa miaka kadhaa sasa.
Maana kama tumekuwa tunasikitika kwa kuendelea kuishi chini ya ombwe la uongozi na kivuli cha ufisadi kwa miaka yote hii, hasa mitano iliyopita, tunasubiri nini kumuunga mkono mtu ambaye amekuwa mstari wa mbele kuwashika mashati bila woga mafisadi na wasanii wa kisiasa?
Katika wimbi hili jipya la mageuzi lililoikumba Tanzania baada ya Dk. Slaa kutangaza kugombea urais mwaka huu, limeondoka ombwe jingine, ambalo rafiki yangu na mchambuzi wa kisiasa, Absalom Kibanda, amenieleza kuwa lilikuwa linaukabili hata upinzani wenyewe.
Wapiganaji ni wengi, viongozi na wakosoaji katika kambi ya upinzani ni wengi; lakini wanaolingana na haiba ya Dk. Slaa ni wachache.
Nataka kuamini kwamba sasa, wapinzani wameshapata mgombea mmoja wa kumkabili Rais Kikwete. Na dhana hii ndiyo iliyonifanya niandike Jumapili iliyopita kwamba wakati sasa umefika, wapinzani wamuunge mkono Dk. Slaa.
Lakini wapo baadhi ya wasomaji makini wa safu hii ya Maswali Magumu ambao walinikosoa kwa haki kabisa, wakisema wanaopaswa kumuunga mkono Dk. Slaa si wapinzani, bali Watanzania wote.
Sababu ni kwamba Dk. Slaa anazungumza lugha ya wote. Anatetea masilahi ya wote. Na Ingawa amekuwa mbunge wa Karatu kwa muongo mmoja na nusu, wananchi ni mashahidi kwamba amekuwa mwakilishi wa Watanzania wote.
Kwa kutazama wimbi hili na mvuto alionao kwa wananchi, ni haki kabisa kusema kuwa ingawa ana wadhifa wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Slaa sasa si wa CHADEMA.
Si makosa kusema kwamba ingawa anagombea urais mwaka huu kwa tiketi ya chama hicho, Dk. Slaa si wa CHADEMA tena. Ni Slaa wa Watanzania.
Ukweli huu, ukichanganywa na historia ya utendaji wa Dk. Slaa, ndio ulimfanya mmoja wa wasomaji hao niliowataja hapo juu kuniandikia ujumbe huu:
"Nionavyo mimi, mapambano si kati ya chama na chama, bali kati ya uadilifu na ufisadi; au kati ya walalahoi na walanchi. Tujuane kwa vitendo si kwa vilemba vya sare."
Itawauma kina Yusuph Makamba (Katibu Mkuu wa CCM) na Pius Msekwa (Makamu Mwenyekiti wa CCM- Bara); lakini Dk. Slaa anaungwa mkono hata na wana CCM wenyewe.
Na wiki hii nikiwa mikoani, nimekutana na wana CCM wengi ambao walikuwa wanaendelea na michakato ya kuwapata wabunge na madiwani wa majimbo yao, lakini kura zao za urais wameshaamua watampa Dk. Slaa.
Nimekutana na baadhi ya wana CCM ambao wamekuwa wanakerwa na mwenendo wa chama chao katika siku za hivi karibuni; kwa sababu hiyo walishaamua kutopiga kura mwaka huu. Dk. Slaa amewaamsha na kuwapa sababu ya kupiga kura.
Nimekutana na wananchi wa kawaida wanaoamini kwamba CCM ni wezi wa kura, na kwamba hata wakimpigia Dk. Slaa zitaibwa; lakini wamedhamiria wampigie ili nyoyo zao ziridhike.
Wapo pia ambao walishaona siasa, hasa za upinzani, hazina maana. Wamebadilika na kuamka upya, na sasa wako nyuma ya Dk. Slaa.
Nimekutana na wana CCM wengine ambao wangependa rais ajaye atoke CCM, lakini wanapolinganisha haiba za wagombea waliopo, nafsi zao zinawasuta. Dk. Slaa amewavuruga.
Na mmoja wa makada wa CCM mkoani Mwanza amenieleza kuwa alichokiona siku Dk. Slaa alipozuru Mwanza kuomba sahihi za wadhamini, ni ajabu ya kisiasa yenye wingi wa watu ambao aliuona mwaka 1990 Tanzania ilipotembelewa na Papa Yohane Paulo II.
Nimewasikia baadhi ya makada wakuu wa CCM na mashabiki wakuu wa Kikwete wakitamka wazi kwamba, "Dk. Slaa asipodhibitiwa anaweza kuwa kama Obama."
CCM wana hofu ya kushindwa. Jeuri ya Ushindi wa kishindo imenyauka. Wamegundua kwamba hata kama wangetumaini kura za wanachama wao (wanajikadiria kuwa milioni nne), kama Watanzania wataamua kufanya kweli, hizo za wana CCM hazitatosha.
Lakini ukweli ni kwamba wana CCM wote hawawezi kukipigia chama chao kura; maana hata huko Karatu na kwingine ambako vyama vya upinzani vimekuwa vinashinda, ni kura za wana CCM na wapinzani.
Watanzania wanaangalia mgombea kwanza, chama baadaye. Ndiyo maana nasema kuwa unapowaweka katika ushindani wagombea wakuu wawili wa urais, Jakaya Kikwete na Dk. Slaa, unakuwa unawatega Watanzania.
Wapo ambao itikadi inawaelekeza wampigie kura mtu wa chama chao, lakini akili timamu na utashi wa nafsi zao vinawatuma kuzingatia umakini, wanafikiri na kuwaza juu ya muono mpya wa Tanzania; wanakerwa na ufisadi na wanajua kuwa CCM ni chama kilichozeeka na kuishiwa nguvu na upya unaostahili. Hawa watakaa upande wa Dk. Slaa.
Waliobaki – wanaochagua kwa kufuata fadhila, chai, pombe, khanga, kofia au fulana; au walio na udugu au ukaribu wa lazima kwa mgombea wa CCM; wanaotegemea ufisadi ili waweze kuishi, wasiokerwa na usanii wa kisiasa uliofanywa na watawala waliopo; wasio na upeo wa kuona uwezo mdogo wa Kikwete katika miaka minne iliyopita, walio sehemu ya ombwe la uongozi ambalo tumelijadili kwa miaka mitatu mfululizo, watakaa upande wake.
Kampeni hazijaanza rasmi. Lakini zitakapokuwa zimeanza, tunajua kuwa utakuwa ushindani mkali wa nguvu hizi mbili za Kikwete na Dk. Slaa. Tutahitajika kuwapima kwa vigezo halisi kutokana na kazi walizofanya, uwezo na upeo wao.
Tutasikiliza hoja zao jinsi watakavyofanya tofauti na kinachofanyika sasa; na tutapima dhamira zao na nia zao, kwa kuwatazama pia wale walio nyuma yao, wanaowasindikiza Ikulu.
Tutahitaji kutafakari vema majibu ya maswali tutakayowauliza. Tutawatazama usoni bila soni na kugundua mkweli na mwongo; fisadi na adili; kiongozi na msanii wa kisiasa; anayependwa na anayekubalika; mlanguzi wa kura na mwombaji wa kura; mwenye jipya na anayerudiarudia mambo yaliyochoka na kupauka; mwoga na rafiki wa mafisadi na mpambanaji jasiri dhidi ya ufisadi, shujaa wa Watanzania.
Hapa hakuna la CHADEMA. Ni Utanzania. Na hii ndiyo bendera ambayo baadhi yetu tunataka ipeperushwe na Dk. Slaa. Tusisite, tusione aibu kutetea kitu chema. Watanzania muungeni mkono.

Makala ni ndefu, lakini ina point. Tuendeleze uzalendo na kukataa ufisadi hapo ndipo tutaikomboa Tanzania.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom