Dr. Slaa sikuelewi, Badilika! La sivyo wewe na CHADEMA... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Slaa sikuelewi, Badilika! La sivyo wewe na CHADEMA...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by wakuziba, Jul 14, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. w

  wakuziba Senior Member

  #1
  Jul 14, 2012
  Joined: Jun 24, 2012
  Messages: 123
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  nianze kwa kusema kuwa nakukubali dr slaa kwa kazi nzuri ulioifanya bungeni kipindi cha 2005 - 2010 kabla hujagombea urais. nilikuelewa kama mtu alie makini, mzalendo aso yumbishwa na porojo za kisiasa! siyo siri hicho kipindi ulilitumikia taifa kama mzalendo halisi. hongera kwa hili! lakini baada ya kugombea urais dr umekua ukibadilikabadilika kimsimamo na umekua hueleweki na wafuasi wako. Elewa kuwa ktk uchaguzi wa 2010, uliungwa mkono na watanzania wakikutaka wewe kuwa rais wao. hawakujali itikadi za vyama vyao. walikuona kama mkombozi wao. mambo yafuatayo, nionavyo mimi, yanakutoa kwenye msitari uliyokujengea umaarufu.


  KAULI ZAKO TATA
  wewe ni dokta. una phd (hata kama ni ya mambo ya kidini lkn ni phd). upeo wako wa kuchambua mambo lazima uwe wa hadhi ya phd. kauli hizi zinanitia wasiwasi kuhusu uwezo wako wa kiuchambuzi na kifalsafa!
  "Leo asubuhi Ofisa wa Makao Makuu ya Polisi amenipigia simu kuomba appointment ya kukutanana na polisi kwa mahojiano. nasema sina muda. sisi hatuendi polisi kwa sababu walishatudanganya mara nyingi tu. kama wanataka waje watukamate lkn sisi hatuendi polisi". la kushangaza, jana majira ya saa 4 na dkk 45 asubuhi, dr slaa na lema walikwenda wenyewe makao makuu ya jeshi la polisi kwa mahojiano! walihojiwa kwa saa 2 kisha wakaruhusiwa kuondoka. alipohojiwa na waandishi wa habari nje ya makao makuu ya polisi, slaa alisema "tumehojiwa lkn hatukukubali maelezo yaandikwe. hakuna sehemu ambayo tumetia sahihi maelelezo ya mahojiano".

  namuuliza dr yafuatayo;
  1- ulisema piga, ua, garagaza hutokwenda polisi labda waje kukukamata. la kushangaza ulikwenda mwenyewe!
  2- mahojiano siyo lazima yaandkwe. mahojiano ya kuandikwa kwa teknolojia ya leo hayana mashiko sana. mahojiano mazuri ni yale ya sauti inayosikika. una uhakika hujarekodiwa!?

  Hivi majigambo, ubeberu na ukaidi kwa jeshi la polisi uliouonesha jumatatu ulipoongea na waandishi wa habari vimeishia wapi? hukupima na kuelewa kuwa jeshi la polisi lina nguvu sana!? hukuelewa kuwa wafuasi wako watakushangaa wakiona unakwenda polisi mwenyewe? dr wangu pima kauli zako. nina mifano mingi ya kauli zako tata lkn nazihifadhi hadi siku nyingine.


  Kadhia ya rose kamili na josephine mshumbusi (sp)
  suala hili limekukalia vibaya dr. kwanza ulimpendelea rose ubunge ili akae kimya lkn inaelekea hajaridhika na ofa ya ubunge! ulitaka ufunge ndoa mwezi huu na josephine. umewekewa pingamizi. nakushauri ujitahidi kumalizana na mam rose nje ya mahakama. la sivyo suala hili litakugharimu sana na hadhi yako itaendelea kushuka sana. ss hivi jua kwamba ww siyo slaa aliegombea urais 2010. kosa ulofanya kuzaa ukiwa padri. kosa ulofanya kumtorosha na kujimilikisha mke wa mtu mama josephine, hayatokuacha salama! umeteleza kijamii na kisiasa lkn jitahidi kumalizana na mama rose. mpe hizo 50 m ili mambo yaishe. tunamtaka slaa mwenye uono wa kimantiki kama ule wa 2005-2010 bungeni.


  USHAURI WA BURE KWA CHADEMA
  chadema ya akina slaa na zitto bungeni ya 2005 - 2010 ilikua chdm yenye mikakakati maridhawa. walikua wachache lkn walitegemea kitu kimoja. KUJENGA HOJA. hiyo ndiyo silaha ilioipa chdm umaarufu. chdm ya 2010 hadi sasa bungeni imekua chdm ya "fungeni milango tupigane" "mwongozo wa spika", "mh spika taarifa", "pigeni wanaonunua viwanja kawe hata kuwaua sawa. nitajibu kama mbunge wenu", "nchemba ulishiriki ktk EPA", "majaji ni wazee na hawana elimu. wanabebwatu" "Rais ni dhaifu" nk........... chdm yenye constructive points and ideologies iko wapi? ccm wamekupandisheni hasira ili kukuyumbisheni kwenye mijadala ya bunge na nyinyi mkaingia mkenge! bado fursa ya kubadilika ipo

  Dr slaa wewe ni jembe. nimeandika haya ili kukushauri kama shabiki wako wa 2005- 2010. sasa hivi nimesimamisha ushabiki kwako hadi nione umebadilika! ni hayo tu!


  Wakatabahu: wakuziba (mzee wa maneno yanayochoma nyoyo!)
   
 2. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #2
  Jul 14, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 760
  Trophy Points: 280
  Unahamu ya matusi wikendi hii?
   
 3. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #3
  Jul 14, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Slaa ni flipflopper
   
 4. Scofied

  Scofied JF-Expert Member

  #4
  Jul 14, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,017
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  nachelea kucomment hapa,nataka weekend yangu iende vizuri...lakini wew ni likaza...over
   
 5. Aleyn

  Aleyn JF-Expert Member

  #5
  Jul 14, 2012
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 10,228
  Likes Received: 13,678
  Trophy Points: 280
  Umeeleweka vzr sana.
   
 6. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #6
  Jul 14, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Hivi hizi personal attack mlizozianzisha hamziachi? Mods wapi?
   
 7. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #7
  Jul 14, 2012
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,541
  Likes Received: 2,239
  Trophy Points: 280
  Yani hii ni Person attack yani hata maswala unyumba unaleta humu yani unaona wivu wewe wakuziba??sasa kati ya hao wewe ulitaka uwe wa tatu??Tuma application kwa chadema kuna kandidate wengi wanaweza kukusaidia kukutolea hicho kinachokuwasha badala ya kumfaata Dr Slaa...kwani yeye tayari ana mke...!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. Pendael laizer

  Pendael laizer JF-Expert Member

  #8
  Jul 14, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 961
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Sisi wananchi tunampendea hayo yote uliyoyaandika wewe magamba wauaji wakubwa, nasi tutalipiza one day haya yote mnayotufanyia.
   
 9. w

  wakuziba Senior Member

  #9
  Jul 14, 2012
  Joined: Jun 24, 2012
  Messages: 123
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  nimeamini jina langu la wakuziba lina uzito wake. kwanza nikishaziba, kuzibua hoja zangu ni shughuli nzito sana. pili lakabu yangu ya "mzee wa maneno yanayochoma nyoyo" ni mujarab na maridhawa kabisa! wengi wanaosoma makala zangu, huumizwa sana na ukweli wa maneno yangu. huwa uwezo wao hauwaruhusu kuzijibu kwa hoja. huishia ama kutukana au kukosa la kuandika! ASANTE MUNGU KWA KUNIPA UWEZO WA KIUCHAMBUZI NA KIMAONO!

  Wakatabahu: wakuziba (mzee wa maneno yanayochoma nyoyo)
   
 10. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #10
  Jul 14, 2012
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Wewe si wakuziba bali unazibwa wewe na akili zako fupi.Soma au elewa kwamba waliitwa kwa simu wakakataa na ndipo wakawaandikia barua .Sasa penye barua ni ushahidi zaidi kuliko mwito wa simu na mtu staarabu akiitwa basi anaitikia wito they did it ubaya uko wapi wewe unaye zibwa ?
   
 11. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #11
  Jul 14, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,905
  Likes Received: 2,334
  Trophy Points: 280
  Kwani mtoa sredi kakosea?
  Ugoni unaisumbua CHADEMA nzima, achilia mbali Dr Slaa mwenyewe.
  Na ndio maana nasema jamaa akitinga Ikulu 2015, masekretari wote hapo wakae chonjo, maana watakuwa na likizo za uzazi kila baada ya miezi tisa.
  Wawe wameolewa au la!
  Aikwa Padiri tu alitikisa nyavu, itakuwa huko Ikulu!!!!!!
   
 12. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #12
  Jul 14, 2012
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,541
  Likes Received: 2,239
  Trophy Points: 280
  Lijali....na wewe ukikaa sawa tegemea hilo!
   
 13. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #13
  Jul 14, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,905
  Likes Received: 2,334
  Trophy Points: 280
  Kama ulivyokalishwa sawa au vipi?
   
 14. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #14
  Jul 14, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  sijaona kosa la mtoa sred,pamoja na personal atack lakini kuna ka ukweli flani.
  dr angesimamia msimamo wake wa awali mpaka akamatwe,au atuambie alikuwa anafikisha ujumbe kwa polisi kuwa hana imani nao ili kwa hili wawe makini na kushughulikia shutuma?
   
 15. Havizya

  Havizya JF-Expert Member

  #15
  Jul 14, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,573
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Nakwambia wenzako,tunampenda na tunamkubali dr wetu Slaa, kuliko tulivyokuwa tunampenda 2005 na 2010, wewe na wajinga wenzako wanaofanana na wewe kwa ujinga unaokaribia kuwa upumbavu Slaa hawahitaji na hawapendi kabisa. Nasi wanachadema tumewakataa kabisa.
   
 16. Kasimba G

  Kasimba G JF-Expert Member

  #16
  Jul 14, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,568
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  Ndugu, unazifahamu hesabu za ku inntergrate na kudifferentiate? Kwani Dr.Uli hajambo? Huwezi kujificha? You are you!
   
 17. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #17
  Jul 14, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  nilijua hautakosekan kwenye hii mada
   
 18. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #18
  Jul 14, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 760
  Trophy Points: 280
  Unadhani ukweli ndio kinga, hapa ukienda kinyume na CDM jiandae mitusi.
   
 19. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #19
  Jul 14, 2012
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  CDM itake isitake lazima waanze kumfikiria mtu nwingine. Huyu mzee kachafuka vibaya sana. CCM wakifanikiwa ku-form alliance na kanisa huo ndio utakuwa mwisho wa CDM!
   
 20. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #20
  Jul 14, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  majibu mazuri, lakini nawashangaa waliokuwa wanachochea ghasia jana eti kisa slaa na lema wako polisi. kwani polisi jehanamu?
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...