Dr.Slaa sasa amtaka Kikwete ajiuzulu kuhusiana na sakata la DOWANS

Kwa hoja iliyopo hapa ... nachelea kusema sio tu kuhusu habari tumayoiona hapa ndio husika kuu..la hasha.

Mi nahisi (kwa kuunganisha na ishu ya kuzima maandamano Arusha) yawezekana raisi (Dr. wa kweli) alikuwa anataka kuzungumza mambo ya wazi na undani zaidi, lakini wakaona waanza kwa vitisho.

Kwa hoja niliyonayo, Dr anazo more evidence kuhusu hili, na inaonekana anaompango wa kumwaga radhi muda wowote, na serikali inajua hilo, so inaanza kupangua hoja kabla haijafikishwa kwa wananchi.

Subirini muone...
 
Mrema sasa tumetambuwa kuwa kusema kwake hovyo alikuwa na matatizo ya kisukari bila mwenyewe kujijuwa, baada ya kugundulika na kuanza kupata tiba, akili yake imetulia na sasa anachapa kazi ya Ubunge vizuri kabisa.

Silaa, inaonyesha ana matatizo ki-afya, wasiwasi wangu yasije kuwa ni makubwa kuliko yale ya Mrema.

Sasa hizi ni hang-over za kushindwa kwenye uchaguzi au?

Nawaomba wana Chadema mumpeleke Hospitali, isije kuwa alipoanguka kule Mwanza tatizo si mkono tu, pengine alijigonga na kichwani? Na kuna kauvimbe ka damu kanafanya mawasiliano ya kichwani yawe si sahihi.

Haya anayosema anayajuwa, mbona wakati wa kampeni hakuyatumia? Au ule mgongo wa kichwani ulimfanya ayasahau?

Namshangaa, kwanza alisema Kikwete mmiliki haijapita hata wiki anatuambia Kikwete anahusika? Mara Kikwete anajuwa, sasa ni nani aliyekuwa hajui kuwa baaday ya kushindwa Richmond mkataba wakaukwaa Dowans?

Au alikuwa na ka-pasenti kwenye kampuni fulani hivi iliokosa hiyo tenda na au tenda zingine? Au ni kuwa tu Ranchi imekufa? Na ndio inamfanya achanganyikiwe?

Nashindwa pa kumuweka! Mtu mzima hovyo!

Eti kwa maneno ya mitaani! Au kiswahili kinampiga chenda? Hajui maana ya Kizabizabina, kama hajui, ngoja tumpe somo kidogo hapa.

Kizabizabina linatokana na lugha ya kiarabu, kama ilivyo asilimia kubwa ya maneno ya kiswahili. Na ina tokana na neno "Kidhab" yaani "muongo" na neno "Kadhabin" (wa) "waongo". Kwa hiyo maana yake kamili ni "Muongo wa Waongo".

Leo haya maneno alivyoyabadili within a very short time, kutoka "mmiliki" kwenda "anahusika" inaonyesha ni kivipi huyu mtu ni kizabizabina! Anachakachuwa hata matamshi, kama si muongo ana matatizo baada ya kuanguka chooni Mwanza.
 
Chadema inao idadi ya kutosha ya kuanzisha mjadala bungeni wa kumchunguza JK juu ya kashfa ya Richmond/Dowans.......lengo is to impeach him now...........................Nina uhakika kuna wabunge wengi wa CCM wataiunga mkono hiyo hoja............................Huyu jamaa now has gone too far..............................

Atakuwa Raisi wa kwanza katika historia ya nchi yetu kushitakiwa na Bunge na hili lianze sasa na swahiba zake akina Rostam Aziz, Lowassa, karamagi na wengineo kama akina Dr. Idrissa Rashid watafuata baadaye........................
Wabunge wa CCM hawawezi wakaunga mkono, wao ni ndio mzee, wakiambiwa na kikwete sasa tunaenda kuiba fedha za wananchi utasikia yanaitikia ndio mzee.
 
mkwere hawezi jibu hoja ya dowans kwani ni mnafiki na ni mmoja ya wana genge hilo la wezi, pia ngeleja kutetea malipo hayo hasa hiyo ndio kazi yake alioutumwa na rostam azizi na mamvi kwani tunajua wao ndio walimtoa vodacom alipokua mwanasheria tena fara tu kama wengine na kumtuma akagombee sengerema then akapewa wizara hiyo nyeti ili alinde migodi na maslahi ya watu hao. Mkwere moto wake ni ule atakaoungua friaun, hudu na samud. Jahanam ya chini kabisa.
 
Mrema sasa tumetambuwa kuwa kusema kwake hovyo alikuwa na matatizo ya kisukari bila mwenyewe kujijuwa, baada ya kugundulika na kuanza kupata tiba, akili yake imetulia na sasa anachapa kazi ya Ubunge vizuri kabisa.

Silaa, inaonyesha ana matatizo ki-afya, wasiwasi wangu yasije kuwa ni makubwa kuliko yale ya Mrema.

Sasa hizi ni hang-over za kushindwa kwenye uchaguzi au?

Nawaomba wana Chadema mumpeleke Hospitali, isije kuwa alipoanguka kule Mwanza tatizo si mkono tu, pengine alijigonga na kichwani? Na kuna kauvimbe ka damu kanafanya mawasiliano ya kichwani yawe si sahihi.

Haya anayosema anayajuwa, mbona wakati wa kampeni hakuyatumia? Au ule mgongo wa kichwani ulimfanya ayasahau?

Namshangaa, kwanza alisema Kikwete mmiliki haijapita hata wiki anatuambia Kikwete anahusika? Mara Kikwete anajuwa, sasa ni nani aliyekuwa hajui kuwa baaday ya kushindwa Richmond mkataba wakaukwaa Dowans?

Au alikuwa na ka-pasenti kwenye kampuni fulani hivi iliokosa hiyo tenda na au tenda zingine? Au ni kuwa tu Ranchi imekufa? Na ndio inamfanya achanganyikiwe?

Nashindwa pa kumuweka! Mtu mzima hovyo!

Eti kwa maneno ya mitaani! Au kiswahili kinampiga chenda? Hajui maana ya Kizabizabina, kama hajui, ngoja tumpe somo kidogo hapa.

Kizabizabina linatokana na lugha ya kiarabu, kama ilivyo asilimia kubwa ya maneno ya kiswahili. Na ina tokana na neno "Kidhab" yaani "muongo" na neno "Kadhabin" (wa) "waongo". Kwa hiyo maana yake kamili ni "Muongo wa Waongo".

Leo haya maneno alivyoyabadili within a very short time, kutoka "mmiliki" kwenda "anahusika" inaonyesha ni kivipi huyu mtu ni kizabizabina! Anachakachuwa hata matamshi, kama si muongo ana matatizo baada ya kuanguka chooni Mwanza.
Ndugu yangu kweli unaona watu wachache wanaiba mali zetu still unatetea? wewe ni mtanzania kweli? unauchungu wa nchi yako kweli? Nani asijejua kikwete anahusika? MUNGU AKUSAMEHE, LAKINI SIKU MOJA UTAKULA MATUNDA YA MANENO YAKO.
 
Patamu kweli hapo katikati. Mwanzo ni chombeza time ya Dr Slaa na kisha Salva anamun'gunya makucha kama vile hataki kumbe anataka kamchezo. Kisha Slaa anabadilisha gea na kuongeza kuchoma mafuta, Salva nywiiiiiiii na Makamba kama yuko ulaya vile hasikiki na wala haoni, anajua muziki mzito kuucheza anakaa pembeni akivizia palipo padhaifu. Siku ya siku wachezaji wooote kabisa watanyenyuka ama kucheza ama kuomboleza, maana Slaa hazomoki kama Salva anavyodhania. Ai weweeee!

Ikulu sijui wamejifunza wapi kwamba mwindaji porini anamlenga paa kwa kumtania. Watanzania wa leo sio kama wa enzi ya Ng'walimu. Wamewasotea wa kusini mwa Afrika wakagundua imekula kwao, wakienda bondeni wanatoswa majini au wanauliwa eti watoto wa njaa kali. Sasa mtoto ukimzomokea hata pasipostahili unamjengea ujasiri wa kukukabili siku moja aje akuambie ukwekweli wako. Muungwana hukubali makosa. Slaa hazungumzi kwa manufaa yake binafsi, anatusemea wengi ambao hata kama ushahidi tunao tunakuwa na kigugumizi kwa sababu ya kuendeleza amani ya woga hali tunaumia.

Haiingii akilini kwamba JK hakutambua madhara ya kupanda bei ya umeme ambao haupo ili kupata pesa ya kuwapa hao wanaowajua wenyewe, wakati huohuo wakisema tukubali tu yaishe. Mwenye njaa na ambaye hana uhakika na ugali wa kesho hawezi kukubali maana hayataisha ilimradi anatakiwa kuendelea kukamuliwa kwa nguvu. Huo ni ubakaji wa kisiasa.
 
Slaa: JK atwambie kwanini tunailipa Dowans
Tuesday, 04 January 2011 21:06

Minael Msuya
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibroad Slaa amemtaka Rais Jakaya Kikwete kuwaeleza Watanzania sababu za kuwabebesha mzigo wa malipo ya fidia ya Sh185 bilioni kwa kampuni ya Dowans, hali serikali yake ikihusika na uzembe uliosababisha fidia hiyo.

Akizungumza na gazeti hili jana, Dk Slaa alisema, Dowans iliingia nchini kwa uzembe wa serikali hivyo Rais Kikwete anapaswa kueleza kwanza serikali yake inawajibikaje, kabla ya kuwataka Watanzania walipe fedha hiyo.

"Kampuni ya Dowans iliingia nchini kwa baraka za Baraza la Mawaziri wakati Kikwete akiwa mwenyekiti. Uzembe huu ulifanyika yeye akiwa anaona na kama hajui basi yeye hakuwajibika, na kama alijua basi yeye ni sehemu ya uzembe huo. Atuambie kwa nini tulipe Dowans kwa uzembe wa serikali yake?" alihoji.

Aliendelea, "Ukilitazama jambo hilo kwa undani, utagundua kuwa baada ya Lowassa kujiuzulu katika sakata la Richmond, mtu aliyetakiwa kumfuata ni Kikwete, kwani ndiye aliyebariki ujio wa kampuni hiyo nchini na baadaye Dowans."

Alisema "Kikwete anahusika na Dowans kwani mwaka 2007 ndiye aliyekutana na waandishi wa habari Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kueleza kuwa ameshawasiliana na kampuni moja kuja nchini kuzalisha umeme kwa bei nafuu. Na siku chache baadaye, mfanyabiashara mmoja maarufu nchini (jina linahifadhiwa) akaleta mitambo hiyo."

Dk Slaa alisema hayo baada ya gazeti hili kumtaka aeleze endapo ana uthibitisho wowote, anapomtuhumu Rais Kikwete kuhusika na Dowans.

Jana baadhi ya vyombo vya habari nchini, viliinukuu Kurugenzi ya Habari na Mawasiliano ya Rais Ikulu ikieleza kuwa kitendo cha Dk Slaa kumhusisha Rais Kikwete na Dowans ni uzushi na kinalenga kumpaka matope.

Lakini alipotakiwa kuzungumzia suala hilo jana, Dk Slaa alisema hawezi kujibizana na Kurugenzi hiyo inayofanya kazi chini ya rais kwa kuwa siyo saizi yake.

"Waliomjibia Kikwete siwezi kujibizana nao kwa kuwa sio saizi yangu. Nataka Kikwete mwenyewe ajitokeza ajibu kama mimi nimesema wongo," alisema Dk Slaa.

Ulipaji wa fidia hiyo unafuatia uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Biashara (ICC Court), Novemba 15, mwaka huu chini ya Mwenyekiti Gerald Aksen na wasuluhishi Swithin Munyantwali, Jonathan Parker uliamuru Tanesco iilipe Dowans kiasi hicho cha fedha.

Dowans ilifungua shauri katika ICC, ikilalamikia Serikali ya Tanzania kupitia Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kuvunja mkataba kabla ya wakati na kinyume cha makubalino kwenye mkataba husika.

Awali baada ya uamuzi huo kufikiwa, Tanesco ilionyesha nia kwamba ingechukua hatua za kukata rufaa, lakini kauli ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema kwamba haoni sababu ya kufanya hivyo inaonekana kama imeyeyusha ndoto hizo za Tanesco.
Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, William Mhando aliwahi kuwaambia wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari kuwa shirika lake lingeweza kutoa tamko kuhusu hatua za kuchukua kuhusu uamuzi wa ICC, lakini akaweka wazi kuwa walikuwa wakisubiri uamuzi huo kusajiliwa rasmi katika Mahakama Kuu nchini.

Hata hivyo, kutokana na kauli ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, sasa ni rasmi kwamba hakutakuwa na hatua zozote za kisheria dhidi ya uamuzi wa ICC na badala yake Tanesco watatakiwa kujipanga kuwalipa Dowans mabilioni hayo ya shilingi kama walivyoamriwa.

Akizungumza na Mwananchi baada ya hafla ya kuapishwa kwa Jaji Mkuu mpya, Mohamed Chande Othman Desemba 27, mwaka jana, Jaji Werema alisema ameshamaliza kuisoma hukumu hiyo na kufanya uamuzi ambao tayari ameukabidhi kwa Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja kwa ajili ya hatua nyingine baada ya kuridhika nayo.
“Mimi kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali nimeisoma hukumu hiyo kwa makini na nimeridhika nayo kuwa iko sawa,” alisema Jaji Werema.

Waziri Ngeleja juzi aliliambia Mwananchi kwamba serikali inaendelea kujipanga kutekeleza ushauri wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhusu Dowans.

Taarifa za ndani ya Tanesco, zinasema kwamba shirika hilo limeanza kuweka fedha kwa ajili ya malipo katika benki moja (jina tunalihifadhi kwa sasa) jijini Dar es Salaam.

Niliyaweka haya katika thread nyingine inayohusika na haya matamshi ya Slaa:

Mrema sasa tumetambuwa kuwa kusema kwake hovyo alikuwa na matatizo ya kisukari bila mwenyewe kujijuwa, baada ya kugundulika na kuanza kupata tiba, akili yake imetulia na sasa anachapa kazi ya Ubunge vizuri kabisa.

Silaa, inaonyesha ana matatizo ki-afya, wasiwasi wangu yasije kuwa ni makubwa kuliko yale ya Mrema.

Sasa hizi ni hang-over za kushindwa kwenye uchaguzi au?

Nawaomba wana Chadema mumpeleke Hospitali, isije kuwa alipoanguka kule Mwanza tatizo si mkono tu, pengine alijigonga na kichwani? Na kuna kauvimbe ka damu kanafanya mawasiliano ya kichwani yawe si sahihi.

Haya anayosema anayajuwa, mbona wakati wa kampeni hakuyatumia? Au ule mgongo wa kichwani ulimfanya ayasahau?

Namshangaa, kwanza alisema Kikwete mmiliki haijapita hata wiki anatuambia Kikwete anahusika? Mara Kikwete anajuwa, sasa ni nani aliyekuwa hajui kuwa baaday ya kushindwa Richmond mkataba wakaukwaa Dowans?

Au alikuwa na ka-pasenti kwenye kampuni fulani hivi iliokosa hiyo tenda na au tenda zingine? Au ni kuwa tu Ranchi imekufa? Na ndio inamfanya achanganyikiwe?

Nashindwa pa kumuweka! Mtu mzima hovyo!

Eti kwa maneno ya mitaani! Au kiswahili kinampiga chenda? Hajui maana ya Kizabizabina, kama hajui, ngoja tumpe somo kidogo hapa.

Kizabizabina linatokana na lugha ya kiarabu, kama ilivyo asilimia kubwa ya maneno ya kiswahili. Na ina tokana na neno "Kidhab" yaani "muongo" na neno "Kadhabin" (wa) "waongo". Kwa hiyo maana yake kamili ni "Muongo wa Waongo".

Leo haya maneno alivyoyabadili within a very short time, kutoka "mmiliki" kwenda "anahusika" inaonyesha ni kivipi huyu mtu ni kizabizabina! Anachakachuwa hata matamshi, kama si muongo ana matatizo baada ya kuanguka chooni Mwanza.

Hapa naona kabadili tena anasema dowans ilikubalika baraza la mawaziri. Huyu mtu kisha ona kastukiwa uzabizabina wake sasa ana haha anatafuta pakutokea hapapati.

Kwetu hunena: "mfa maji haishi kutapatapa".

Pigo la kushindwa uchaguzi lilikuwa kubwa sana kwake na nna-uhakika limemuathiri, au alipoanguka chooni ndio kumemuathiri zaidi ya hisia zake.

Pole sana Silaa, nakuonea huruma sana, kwani sasa, mtu mzima mwenzangu naona upo taabani. Naomba kapime afya yako, usisahau ma-neuro surgeons katika kupima kwako.
 
Strategy ya ushindi siku zote ni kupeleka mashambulizi kwenye goli lao kama si kufunga unaweza kusababisha penalt au wao kujifunga keep on Slaa and CDM.

Sawa sawa mkuu, my motto sikuzote ni ukitaka kuua nyoka piga kichwa! people have wasted their valuable times in mentioning other people, the key player and only striker who used his presidential opportunity is Kikwete!!

With this move you will never hear me opposing Slaa,

Go Slaa go....

Yes we can make him to stepdown, Lowassa did!
 
Mrema sasa tumetambuwa kuwa kusema kwake hovyo alikuwa na matatizo ya kisukari bila mwenyewe kujijuwa, baada ya kugundulika na kuanza kupata tiba, akili yake imetulia na sasa anachapa kazi ya Ubunge vizuri kabisa.

Silaa, inaonyesha ana matatizo ki-afya, wasiwasi wangu yasije kuwa ni makubwa kuliko yale ya Mrema.

Sasa hizi ni hang-over za kushindwa kwenye uchaguzi au?

Nawaomba wana Chadema mumpeleke Hospitali, isije kuwa alipoanguka kule Mwanza tatizo si mkono tu, pengine alijigonga na kichwani? Na kuna kauvimbe ka damu kanafanya mawasiliano ya kichwani yawe si sahihi.

Haya anayosema anayajuwa, mbona wakati wa kampeni hakuyatumia? Au ule mgongo wa kichwani ulimfanya ayasahau?

Namshangaa, kwanza alisema Kikwete mmiliki haijapita hata wiki anatuambia Kikwete anahusika? Mara Kikwete anajuwa, sasa ni nani aliyekuwa hajui kuwa baaday ya kushindwa Richmond mkataba wakaukwaa Dowans?

Au alikuwa na ka-pasenti kwenye kampuni fulani hivi iliokosa hiyo tenda na au tenda zingine? Au ni kuwa tu Ranchi imekufa? Na ndio inamfanya achanganyikiwe?

Nashindwa pa kumuweka! Mtu mzima hovyo!

Eti kwa maneno ya mitaani! Au kiswahili kinampiga chenda? Hajui maana ya Kizabizabina, kama hajui, ngoja tumpe somo kidogo hapa.

Kizabizabina linatokana na lugha ya kiarabu, kama ilivyo asilimia kubwa ya maneno ya kiswahili. Na ina tokana na neno "Kidhab" yaani "muongo" na neno "Kadhabin" (wa) "waongo". Kwa hiyo maana yake kamili ni "Muongo wa Waongo".

Leo haya maneno alivyoyabadili within a very short time, kutoka "mmiliki" kwenda "anahusika" inaonyesha ni kivipi huyu mtu ni kizabizabina! Anachakachuwa hata matamshi, kama si muongo ana matatizo baada ya kuanguka chooni Mwanza.

You are using ur domocracy....
 
Ndugu yangu kweli unaona watu wachache wanaiba mali zetu still unatetea? wewe ni mtanzania kweli? unauchungu wa nchi yako kweli? Nani asijejua kikwete anahusika? MUNGU AKUSAMEHE, LAKINI SIKU MOJA UTAKULA MATUNDA YA MANENO YAKO.

Upuuzi huo, ingekuwa si Kikwete leo mngeona vigogo wakiachia ngazi, wakiswekwa jela, wengine bado wana kesi za kujibu? Nambie kwa mamlaka aliyokuwa nayo Rais kwa katiba yetu ya sasa, na ingekuwa si straight, ungeyaona yote hayo? Msitake kuleta chuki pasipo kuwa na chuki. Kila anachofanya Kikwete, hata kiwe chema kipi, mnamzushia mabaya, ya kutowa vichwani mwenu tu.

Hayakuanzia kwa Kikwete, yalianza kwa Mwinyi, mkashindwa sasa huyu ambae anafichuwa madudu ya kina Nyerere na Mkapa ndio amekuwa mbaya?

Haya matatizo ya umeme yaliyofikia mpaka kikwete achukuwe hatua za haraka yalianzia wapi?

Wacheni hizo! Sisi tutakwenda sambamba na nyinyi na kila mpenda haki tutamuunga mkono.

Leo tuunge mkono hoja ya kutaka kujisafisha kwa uongo aliozuwa huyo Silaa? Si juzi tu, hilohilo Tanzania daima lilisema kuwa Silaa kasema Kikwete mmiliki, sasa leo vipi anabadilisha na kusema ana husika, yaani hata wewe huuoni huu uongo wa waziwazi?
 
Unalipwa bei gani?
 
Niliyaweka haya katika thread nyingine inayohusika na haya matamshi ya Slaa:

Mrema sasa tumetambuwa kuwa kusema kwake hovyo alikuwa na matatizo ya kisukari bila mwenyewe kujijuwa, baada ya kugundulika na kuanza kupata tiba, akili yake imetulia na sasa anachapa kazi ya Ubunge vizuri kabisa.

Silaa, inaonyesha ana matatizo ki-afya, wasiwasi wangu yasije kuwa ni makubwa kuliko yale ya Mrema.

Sasa hizi ni hang-over za kushindwa kwenye uchaguzi au?

Nawaomba wana Chadema mumpeleke Hospitali, isije kuwa alipoanguka kule Mwanza tatizo si mkono tu, pengine alijigonga na kichwani? Na kuna kauvimbe ka damu kanafanya mawasiliano ya kichwani yawe si sahihi.

Haya anayosema anayajuwa, mbona wakati wa kampeni hakuyatumia? Au ule mgongo wa kichwani ulimfanya ayasahau?

Namshangaa, kwanza alisema Kikwete mmiliki haijapita hata wiki anatuambia Kikwete anahusika? Mara Kikwete anajuwa, sasa ni nani aliyekuwa hajui kuwa baaday ya kushindwa Richmond mkataba wakaukwaa Dowans?

Au alikuwa na ka-pasenti kwenye kampuni fulani hivi iliokosa hiyo tenda na au tenda zingine? Au ni kuwa tu Ranchi imekufa? Na ndio inamfanya achanganyikiwe?

Nashindwa pa kumuweka! Mtu mzima hovyo!

Eti kwa maneno ya mitaani! Au kiswahili kinampiga chenda? Hajui maana ya Kizabizabina, kama hajui, ngoja tumpe somo kidogo hapa.

Kizabizabina linatokana na lugha ya kiarabu, kama ilivyo asilimia kubwa ya maneno ya kiswahili. Na ina tokana na neno "Kidhab" yaani "muongo" na neno "Kadhabin" (wa) "waongo". Kwa hiyo maana yake kamili ni "Muongo wa Waongo".

Leo haya maneno alivyoyabadili within a very short time, kutoka "mmiliki" kwenda "anahusika" inaonyesha ni kivipi huyu mtu ni kizabizabina! Anachakachuwa hata matamshi, kama si muongo ana matatizo baada ya kuanguka chooni Mwanza.

Hapa naona kabadili tena anasema dowans ilikubalika baraza la mawaziri. Huyu mtu kisha ona kastukiwa uzabizabina wake sasa ana haha anatafuta pakutokea hapapati.

Kwetu hunena: "mfa maji haishi kutapatapa".

Pigo la kushindwa uchaguzi lilikuwa kubwa sana kwake na nna-uhakika limemuathiri, au alipoanguka chooni ndio kumemuathiri zaidi ya hisia zake.

Pole sana Silaa, nakuonea huruma sana, kwani sasa, mtu mzima mwenzangu naona upo taabani. Naomba kapime afya yako, usisahau ma-neuro surgeons katika kupima kwako.

Kweli fikra zako finyu dada... maana sijui mtazamo wako unaonyesha ni ;-

1. nani aliyeathirika na matokeo baada ya uchaguzi??? (mwenzenu anajua matokeo halisi)
2.Nani aliyeathirika NA KUANGUKA ANGUKA???
 
***Asisitiza anahusika na Dowans, aahidi kutoboa siri***

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilibrod Slaa, sasa amekuja na hoja mpya ya kumtaka Rais Jakaya Kikwete ajiuzulu kutokana na kuhusika moja kwa moja na sakata la Dowans iliyorithi mikoba ya Richmond.

Dk. Slaa ametoa kauli hiyo nzito jana katika mahojiano maalumu na Tanzania Daima Jumatano, ikiwa ni siku moja baada ya Ikulu kutoa taarifa ya kejeli na vijembe vya mitaani dhidi yake kuhusu sakata hilo.

Akizungumza kwa utulivu na umakini mkubwa, Dk. Slaa alisema Rais Kikwete alipaswa kujiuzulu kabla ya aliyekuwa Waziri Mkuu na swahiba wake mkubwa, Edward Lowasa, kuchukua hatua hiyo Februari 7, mwaka 2008, mjini Dodoma.

Akitoa ufafanuzi wa taarifa ya Ikulu iliyotolewa juzi na Kurugenzi ya Mawasiliano, Dk. Slaa alisema mkuu huyo wa nchi hawezi kukwepa kuhusishwa na sakata la Dowans, kwani alilijua hata kabla mitambo yake haijaingizwa nchini.

"Nataka niwatoe Watanzania wasiwasi kwamba ingawa kurugenzi ya mawasiliano imetoa taarifa ya kumsafisha Rais Kikwete na kunikashifu mimi kwa lugha ya mtaani, nawaambia alipaswa kujiuzulu kabla na anatakiwa ajiuzulu sasa, kwani anahusika moja kwa moja na uingiaji wa mkataba wa Kampuni ya Richmond na baadaye na Dowans" alisema Dk. Slaa.

Alimtaka Rais Kikwete kutambua kuwa hawezi kukaa kimya kwa kisingizio cha kuhatarisha amani na utulivu wakati wananchi wanaibiwa mabilioni ya fedha na mafisadi wachache kupitia kampuni feki ya Dowans.

Akirejea historia ya vita dhidi ya ufisadi aliyoiasisi bungeni, Dk. Slaa aliwataka wananchi wakumbuke kuwa taifa lilipokumbwa na tatizo la umeme kabla ya mitambo ya Richmond kuingia nchini, Rais Kikwete alikwenda Marekani kwa ziara ya kikazi.

Alisema aliporejea nchini, alizungumza na waandishi wa habari kuhusu tatizo hilo na kuahidi kuwa serikali yake inalifanyia kazi na siku chache baadaye, rafiki yake wa karibu, Rostam Azizi, Mbunge wa Igunga (CCM), naye alikwenda Marekani.

"Rostam aliporejea kutoka Marekani baada ya siku chache tukaanza kusikia mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura kutoka Kampuni ya Richmond inatarajiwa kuwasili. Kweli ilitua nchini katika Uwanja wa Mwalimu Nyerere na shughuli nyingine zilifungwa uwanjani hapo kupisha ushushaji wa mitambo ya Richmond" alisema Dk. Slaa.

Huku akisisitiza kuwa ana ushahidi wa anachokisema, Dk. Slaa alisema hata baada ya Richmond kushindwa kuzalisha umeme na kusababisha mawaziri kujiuzulu, serikali ya Kikwete iliamua kuingia mkataba na Dowans iliyorithi shughuli za Richmond na hatua hiyo Rais Kikwete pia aliijua.

"Dowans nayo ikashindwa kuzalisha umeme, mwisho Bunge katika moja ya maazimio yake liliridhia uamuzi wa kuvunja mkataba huo, lakini leo Serikali inadaiwa fidia ya sh bilioni 185, je, Rais Kikwete anaweza kukwepa kwamba hana mkono wake hapo?  alihoji.

Kutokana na hayo, Dk. Slaa alimtaka Rais Kikwete amtaje mmiliki halali wa Dowans ili kuwatoa kiu Watanzania wanaohitaji kumjua.

"Sitaacha kuzungumzia masuala yanayowagusa Watanzania na mali, hasa katika kipindi hiki ambacho Watanzania wanataka kuibiwa fedha zao, wakati wa kukaa kimya umekwisha" alisema Dk. Slaa.

Alisema hashangazwi na kejeli za Ikulu na kuwataka Watanzania kukumbuka alipoanza kuwalipua mafisadi, Rais Kikwete aliwahi kutamka kwamba kelele za mlango haziwezi kumnyima mwenye nyumba usingizi na kamwe kelele za chura hazimzuii ng ombe kunywa maji.

"Lakini baada ya sisi kuamua kupambana na Richmond, Rais Kikwete alikiri linamnyima usingizi na hili la Dowans litamnyima usingizi zaidi katika kipindi hiki cha mwisho cha uongozi wake" alisema Dk. Slaa.

Ili kumaliza kelele za Dowans, Dk. Slaa alimtaka Rais Kikwete kumtaja mmiliki wake ambaye anataka kuwaibia Watanzania mabilioni ya fedha.

Katika mahojiano maalumu na gazeti la Tanzania Daima Jumapili, mwishoni mwa wiki, Dk. Slaa alikaririwa akisema chanzo cha suala la Dowans kutakiwa kulipwa fidia limetokana na uzembe wa serikali na Rais Kikwete mwenyewe anahusika kuileta Kampuni ya Richmond ambayo baada ya kuonekana ya kitapeli iliamua kurithisha kazi zake kwa Dowans.

Slaa siku zote ushindi wa mechi ni uwanjani, sio wa mezani. Sasa wewe umeshindwa kwenye uchaguzi ulio huru na wa haki, wataka JK aondoke ili wewe uchukue Urais, huo ni ushindi wa mezani ambao sie watanzania tulio wengi tuliamua kumchagua JK kwa ushindi wa kishindo na sunami. Ww jipange tu kwa 2015, acha kujitafutia umaarufu kwenye suala la dowans. Ndio maana ikulu ikakuambia kweli umechanganyikiwa, na wananchi tumeisha anza kuamini kwa hilo.
 
Hakyamungu mpaka mtachanganyikiwa safari hiii...... sisi tutabana hapohapo... najua hakukaliki huko.... yaani wewe mama, nikuambie ukweli HII NCHI MKWERE HAITAWALI TENA KWA AMANI... sisi tunae tu ..na mtatumwa sana
 
Upuuzi huo, ingekuwa si Kikwete leo mngeona vigogo wakiachia ngazi, wakiswekwa jela, wengine bado wana kesi za kujibu? Nambie kwa mamlaka aliyokuwa nayo Rais kwa katiba yetu ya sasa, na ingekuwa si straight, ungeyaona yote hayo? Msitake kuleta chuki pasipo kuwa na chuki. Kila anachofanya Kikwete, hata kiwe chema kipi, mnamzushia mabaya, ya kutowa vichwani mwenu tu.

Hayakuanzia kwa Kikwete, yalianza kwa Mwinyi, mkashindwa sasa huyu ambae anafichuwa madudu ya kina Nyerere na Mkapa ndio amekuwa mbaya?

Haya matatizo ya umeme yaliyofikia mpaka kikwete achukuwe hatua za haraka yalianzia wapi?

Wacheni hizo! Sisi tutakwenda sambamba na nyinyi na kila mpenda haki tutamuunga mkono.

Leo tuunge mkono hoja ya kutaka kujisafisha kwa uongo aliozuwa huyo Silaa? Si juzi tu, hilohilo Tanzania daima lilisema kuwa Silaa kasema Kikwete mmiliki, sasa leo vipi anabadilisha na kusema ana husika, yaani hata wewe huuoni huu uongo wa waziwazi?

Dar-Es-Salaam kuna issue that are beyond itikadi. I dont give damn a shit kuwa anayoongea Dr. Slaa yako 100% sure or what lakini kwa mtu yeyote makini lazima kwa saga zima la Dowans atajiuliza maswali yanayoazalisha maswali zaidi kuhusu ukimya wa Rais wako Kikwete. Na huu udini wako ndio unaoharibu. wapi kwenye thread hii imegusiwa Mkapa na Nyerere? Hapa ndio inaonekana kuna kitu unachotafuta behind the veil.

Najua hujali maana unazitafuna tu kirahisi na hata haya maumivu hayatakugusa maana ni miongoni mwa wateule wachache wenye guarantee ya kula za nchi hii kama vile ni za kwao peke yao

Swala la kupeleka vigogo kwangu mimi sio kipimo sahihi cha uwajibikaji na uwajibishaji wa Kikwete kwa mafisadi. Muulize Hosea atakuambia. Hili ni jambo la shinikizo hasa kwa yale ambalo anajikuta hana maslahi.

Swali ni kwa nini wanaotajwa kuwa mafisadi wakuu na ambao anaushirika nao wa karibu zaidi hakuna anaeguswa. huku yeye mwenyewe akiwasafisha kuwa watu safi?

Utaongea maana uchungu na nchi hii huna.....
 
Shame on you Dar es salaam! even if ww ni mtu wa system but sometimes lazima uwe na uchungu na nchi yako au ww ni Mu iran? coz yote anayosema Dr. ni hoja nzito jaribu kujibu hizi hoja kwa hoja kama ww ni msemaji wa serikali humu JF.
 
Upuuzi huo, ingekuwa si Kikwete leo mngeona vigogo wakiachia ngazi, wakiswekwa jela, wengine bado wana kesi za kujibu? Nambie kwa mamlaka aliyokuwa nayo Rais kwa katiba yetu ya sasa, na ingekuwa si straight, ungeyaona yote hayo? Msitake kuleta chuki pasipo kuwa na chuki. Kila anachofanya Kikwete, hata kiwe chema kipi, mnamzushia mabaya, ya kutowa vichwani mwenu tu.

Hayakuanzia kwa Kikwete, yalianza kwa Mwinyi, mkashindwa sasa huyu ambae anafichuwa madudu ya kina Nyerere na Mkapa ndio amekuwa mbaya?

Haya matatizo ya umeme yaliyofikia mpaka kikwete achukuwe hatua za haraka yalianzia wapi?

Wacheni hizo! Sisi tutakwenda sambamba na nyinyi na kila mpenda haki tutamuunga mkono.

Leo tuunge mkono hoja ya kutaka kujisafisha kwa uongo aliozuwa huyo Silaa? Si juzi tu, hilohilo Tanzania daima lilisema kuwa Silaa kasema Kikwete mmiliki, sasa leo vipi anabadilisha na kusema ana husika, yaani hata wewe huuoni huu uongo wa waziwazi?

Kweli sister wewe hamna kitu....

1.Ni kigogo GANI ALIYEACHIA NGAZI KWA SABABU YA KIKWETE??????
2.KIGOGO GANI ALIYEWEKWA LUMANDE KWA SABABU ZA KITAIFA??? (mi namjua yule waliebebeana mizigo, Amatus ishu za wivu wa mapenzi)
3.Kesi gani unayoona ipo mahakamani, inayoweza kumfanya muelewa akajua hiyo ni kesi na sio kiini macho??? Kwa hizo kesi nenda kawadanganye Bagamoyo sio hapa jamvini.
 
Tuandamane kupinga wizi huu ambao viongozi wamekuwa sehemu ya matatizo ya watanzania.

Walifoji kuingia madarakani na yote yanayofanyika hivi sasa ni usanii mtupu!
 
Strategy ya ushindi siku zote ni kupeleka mashambulizi kwenye goli lao kama si kufunga unaweza kusababisha penalt au wao kujifunga keep on Slaa and CDM.

Imeniingia vizuri sana. big up
 
Dr Slaa naona ana kinyongo na JK.

Inawezekanaje swali kama hilo amuulize Rais kabla hajapata majinabu toka kwa waziri husika? Rais anapata ushauri kutoka kwa waliokaribu zaidi na sakata, ambao ndio wanajua mchakato mzima.

Uchokozi.

Wanaohusika ni kina nani? Waliohusika mwanzoni walijiuzulu! Mpaka leo hakuna majibu yaliyotolewa! Tume imeundwa, ripoti imetolewa, kesi imefunguliwa, hela zinatakiwa kulipwa!! Bado tu Dowans hawajulikani? Wanajulikana! JK angeweza kutoa tamko kuhusu Dowans na si kwa kukaa pembeni na kusubiri waziri aseme! Mbona Obama hakuwaachia BP waseme peke yao? Ofisi za Dowans Tanzania ziko wapi?
 
Back
Top Bottom