Dr.Slaa sasa amtaka Kikwete ajiuzulu kuhusiana na sakata la DOWANS | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr.Slaa sasa amtaka Kikwete ajiuzulu kuhusiana na sakata la DOWANS

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Luteni, Jan 5, 2011.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Jan 5, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  *Asisitiza anahusika na Dowans, aahidi kutoboa siri

  KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilibrod Slaa, sasa amekuja na hoja mpya ya kumtaka Rais Jakaya Kikwete ajiuzulu kutokana na kuhusika moja kwa moja na sakata la Dowans iliyorithi mikoba ya Richmond.

  Dk. Slaa ametoa kauli hiyo nzito jana katika mahojiano maalumu na Tanzania Daima Jumatano, ikiwa ni siku moja baada ya Ikulu kutoa taarifa ya kejeli na vijembe vya mitaani dhidi yake kuhusu sakata hilo.


  Akizungumza kwa utulivu na umakini mkubwa, Dk. Slaa alisema Rais Kikwete alipaswa kujiuzulu kabla ya aliyekuwa Waziri Mkuu na swahiba wake mkubwa, Edward Lowasa, kuchukua hatua hiyo Februari 7, mwaka 2008, mjini Dodoma.


  Akitoa ufafanuzi wa taarifa ya Ikulu iliyotolewa juzi na Kurugenzi ya Mawasiliano, Dk. Slaa alisema mkuu huyo wa nchi hawezi kukwepa kuhusishwa na sakata la Dowans, kwani alilijua hata kabla mitambo yake haijaingizwa nchini.


  "Nataka niwatoe Watanzania wasiwasi kwamba ingawa kurugenzi ya mawasiliano imetoa taarifa ya kumsafisha Rais Kikwete na kunikashifu mimi kwa lugha ya mtaani, nawaambia alipaswa kujiuzulu kabla na anatakiwa ajiuzulu sasa, kwani anahusika moja kwa moja na uingiaji wa mkataba wa Kampuni ya Richmond na baadaye na Dowans" alisema Dk. Slaa.


  Alimtaka Rais Kikwete kutambua kuwa hawezi kukaa kimya kwa kisingizio cha kuhatarisha amani na utulivu wakati wananchi wanaibiwa mabilioni ya fedha na mafisadi wachache kupitia kampuni feki ya Dowans.


  Akirejea historia ya vita dhidi ya ufisadi aliyoiasisi bungeni, Dk. Slaa aliwataka wananchi wakumbuke kuwa taifa lilipokumbwa na tatizo la umeme kabla ya mitambo ya Richmond kuingia nchini, Rais Kikwete alikwenda Marekani kwa ziara ya kikazi.


  Alisema aliporejea nchini, alizungumza na waandishi wa habari kuhusu tatizo hilo na kuahidi kuwa serikali yake inalifanyia kazi na siku chache baadaye, rafiki yake wa karibu, Rostam Azizi, Mbunge wa Igunga (CCM), naye alikwenda Marekani.


  "Rostam aliporejea kutoka Marekani baada ya siku chache tukaanza kusikia mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura kutoka Kampuni ya Richmond inatarajiwa kuwasili. Kweli ilitua nchini katika Uwanja wa Mwalimu Nyerere na shughuli nyingine zilifungwa uwanjani hapo kupisha ushushaji wa mitambo ya Richmond" alisema Dk. Slaa.


  Huku akisisitiza kuwa ana ushahidi wa anachokisema, Dk. Slaa alisema hata baada ya Richmond kushindwa kuzalisha umeme na kusababisha mawaziri kujiuzulu, serikali ya Kikwete iliamua kuingia mkataba na Dowans iliyorithi shughuli za Richmond na hatua hiyo Rais Kikwete pia aliijua.


  "Dowans nayo ikashindwa kuzalisha umeme, mwisho Bunge katika moja ya maazimio yake liliridhia uamuzi wa kuvunja mkataba huo, lakini leo Serikali inadaiwa fidia ya sh bilioni 185, je, Rais Kikwete anaweza kukwepa kwamba hana mkono wake hapo?  alihoji.


  Kutokana na hayo, Dk. Slaa alimtaka Rais Kikwete amtaje mmiliki halali wa Dowans ili kuwatoa kiu Watanzania wanaohitaji kumjua.


  "Sitaacha kuzungumzia masuala yanayowagusa Watanzania na mali, hasa katika kipindi hiki ambacho Watanzania wanataka kuibiwa fedha zao, wakati wa kukaa kimya umekwisha" alisema Dk. Slaa.


  Alisema hashangazwi na kejeli za Ikulu na kuwataka Watanzania kukumbuka alipoanza kuwalipua mafisadi, Rais Kikwete aliwahi kutamka kwamba kelele za mlango haziwezi kumnyima mwenye nyumba usingizi na kamwe kelele za chura hazimzuii ng ombe kunywa maji.


  "Lakini baada ya sisi kuamua kupambana na Richmond, Rais Kikwete alikiri linamnyima usingizi na hili la Dowans litamnyima usingizi zaidi katika kipindi hiki cha mwisho cha uongozi wake" alisema Dk. Slaa.


  Ili kumaliza kelele za Dowans, Dk. Slaa alimtaka Rais Kikwete kumtaja mmiliki wake ambaye anataka kuwaibia Watanzania mabilioni ya fedha.


  Katika mahojiano maalumu na gazeti la Tanzania Daima Jumapili, mwishoni mwa wiki, Dk. Slaa alikaririwa akisema chanzo cha suala la Dowans kutakiwa kulipwa fidia limetokana na uzembe wa serikali na Rais Kikwete mwenyewe anahusika kuileta Kampuni ya Richmond ambayo baada ya kuonekana ya kitapeli iliamua kurithisha kazi zake kwa Dowans.
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Jan 5, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  President Kikwete Can Steal from Tanzanians at Get Away with it Most-of-The-Time But Not All-of-The-Time; ON THIS 'DOWANS SCANDLE' RESIGN NOW!!

  President Kikwete MUST resign immediately with regard to the Dowans Tanzania Limited Scandal.

  This would be the most honourable thing that Dr Jakaya Mrisho Kikwete can do for this great and most loving nation as a sure measure to SAVE HIMSELF A FACE from further embarassment as a once respected deplomat of international repute. Anything sort of this the leader has a lot to loose with every single day that go-by.

  There is no way he can purport to be leading this poor third world economy to any level of prosperity whereas on another he himself DARE SET SCHEMES TO LOOT the same taxpayers, that he is intent to lead, of the never-enough common fund from the public cofers.

  With the 2010 stolen elections in favour of his very badly resented CCM party following their new-found friendship championing the wishes of MEGA-CORRUPTION (MAFISADI) HEROS in the country, deviding the once united nation along religious lines and MUZZLING OPPOSING VOICES QUIETLY IN THE DARKNESS, Hon Kikwete has got no business stay in the country' state-house any longer.

  There is no way a person who has dubiously BETRAYED PUBLIC TRUST bestowed on him by Tanzanian voters in 2005 by ripping them off a hobbling Tanzania shillings in billions, resulting into frigtening deaths of infants in hospitals because of lack of quality medication, dwindling fortunes in employment and questionable drive in barricading the very TENETS OF GOOD GOVERNANCE can still supperimpose himself on the shoulders of his victims as a leader of any mean repute.

  Please, honourably resign from office now before the public of Tanzania could be informed of even WORST-DAMAGING SIDE deliberately kept away to afford you a HONOURABLE EXIT than waiting until people push you out the GBAGBO way in Ivory Coast.

  We want to start afresh as Tanzanians deserve nothing but ther best of RELIABLE and most TRUSTWORTHY personalities to lead them. Huwezi ukatuibia kodi zetu kiujanja ujanja tena ukatuibie uchaguzi kiujanja ujanza na rasilmali za taifa hivo hivo na bado ukafiki tutaendelea kuchekeana kila siku. Enough is enough!!

  Remember the internatinal community can be watching you any better today that ever before after catching a glimpse of your darkest you.
   
 3. Jay One

  Jay One JF-Expert Member

  #3
  Jan 5, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 11,083
  Likes Received: 4,667
  Trophy Points: 280
  as i know Mwiraqw Dr. W. P. Slaa ndio ameanza mechi, Kikwete atakwenda na maji amuulize Iddi Simba etc, alilia, Ndio kaanza GO Dr Slaa, leta
  vya ndani hiden issues, weka hadharani, JK anatufanya hivi:caked::caked::caked:na sisi tunacheka
   
 4. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #4
  Jan 5, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Strategy ya ushindi siku zote ni kupeleka mashambulizi kwenye goli lao kama si kufunga unaweza kusababisha penalt au wao kujifunga keep on Slaa and CDM.
   
 5. Tekelinalokujia

  Tekelinalokujia JF-Expert Member

  #5
  Jan 5, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 353
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hivi mbona inakua rahisi kwao kusema lazima Dowans walipwe ila kuhusu nani ni akina Dowans inakua kama kutaka kushika upepo ambao unajua upo ila haushikiki? Siku zote ukweli unauma na ndio maana Ikulu walivyorudi na majibu ya hasira na vijembe bila kuadress hoja kwa majibu thabiti inatufanya tupate hisia kuwa kuna uhusika wa wakubwa kwenye habari hii. Kama walivyotoa vijembe mwanzo na hili tuwasikilizie.
   
 6. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #6
  Jan 5, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,516
  Likes Received: 19,940
  Trophy Points: 280
  Inabidi wananchi tufumbuke macho naona mechi waliyoianzisha watu wa ikulu sasa inaelekea kuwameza DR.Slaa still the strongest man here in Tanzania(lost land)
   
 7. malipula

  malipula JF-Expert Member

  #7
  Jan 5, 2011
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 318
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  kazi ipo!!
   
 8. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #8
  Jan 5, 2011
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Ngoja tumsubiri Mzee wa vijembe na mipasho (Salva Rweyemamu) kutoka pale magogoni aje alete mipasho zaidi!!! Salva tunakusubiri ukanushe tena au mpeleke Dr. Slaa mahakamani kwa kumdhalilisha Rais halafu mje msikie Muziki wake!!!!

  Please kanusha tena and believe me or not I like your mipasho in the name of state house press release!!!!

  Tiba
   
 9. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #9
  Jan 5, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0

  PRESIDENT KIKWETE & THE COHORT 'MAFISADI' MUST NOT WAIT TO BE KICKED OUT OF OFFICE:

  This government forced down our throats never feel ashamed of anything under the sun. They CHEAT ON US EVERY OTHER DAY and ever further the vice to our very face, THEY KEEP CHEATING ON THE DONOR COMMUNITY all in our name yet no meaningful development seems to come a full circle in our citizenry in spite of our country being THE EVER PEACIFUL COUNTRY IN AFRICA since independence 47 years ago.

  With this kind of a most disturbing scenario even THE DULLEST MIND in the world would seek to UNCOVER A POSSIBLE HIDDEN MUCK that has since perenially prevent our country from registering GLITTERING LEVELS OF ECONOMIC PROSPERITY with all the unique resources that God has endowed us with.

  Indeed anybody out there would be most deservingly be excused in wondering what the mess that is tha has since sought to wither off the (i) DIAMOND-STRONG FOUNDATIONS ON SELF-SUSTAINING PEACE, (ii) ROCK-SOLID SENSE OF NATIONHOOD AND (iii) A RIVER-JORDAN FREELY FLOWING GENUINE LOVE FOR ONE ANOTHER that Tanzania has most authentically been identified with nationally and internationally!!!

  President Kikwete and YOUR COHORTS MUST RESIGN immediately to save yourselves the impending worst damages from the now WORTS-DISSAPPOINTED Tanzanian populace. Tanzania badly need a FRESH RE-INVENTION for greater citizenry-focused economic growth and sustainance.
   
 10. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #10
  Jan 5, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Bravo Dr.Silaa!! hao wezi watajichanganya na watakuja kwenye mtego tuu, Tumsubiri na kibaraka Makamba na familia yake waropoke!
  Nachopenda kila wakiropoka humohumo hujikuta wanautoa ukweli.
   
 11. a

  awtu Member

  #11
  Jan 5, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Thanks for this advance news! Dr Slaa is the unsung hero of Tanzania. One day we will owe it to him when we get out of the woods whether he is around or not. Remember that Tanzanians still remember what the Iraqw people showed to the rest of Tanganyikans when they rejected TWICE TANU's choice of Amri Dodo for the Mbulu constituency, the only place where TANU lost an election. They dealt TANU an indelible mark and so has the (real) Dr!
   
 12. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #12
  Jan 5, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Salva anataraji kushirikishwa kwenye ALBUM MPYA ITAKAYOZINDULIWA NA JAHAZ MODERN TAARABU,WIMBO UTAITWA KIZABIZABINA.
   
 13. m

  mgalisha Member

  #13
  Jan 5, 2011
  Joined: Oct 16, 2010
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mwisho wa siku itafahamika tu,
   
 14. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #14
  Jan 5, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kwa uchambuzi alioutoa Mwana jf Ndg FAREED, sasa naanza kuamini kwamba si Alhaj Karamagi tu ndiye aliyekua na tabia ya KUTEMBEA NA MUHURI WA SERIKALI MFUKONI MWAKE popote aendako enzi zake akiwa waziri wetu.

  Kwa upande mwingine kumbe hata na mwandishi wa habari mwandamizi kama Dr Salva Rweyemamu naye pia keshaidaikia hiyo tabia mbaya ya kutembe na muhuri wa ikulu kwenye kaptula yake na kuweza kuomba wahudumu kwenye baa ya Mango Garden pale getini kwake, akiwa kwenye vikao vya hiari saa tana usiku, ki-karatasi na kuandika chochote wakati akijua vizuri kwamba bia unapoyamimina tumboni hayageuki kuwa maji ya Uhai ya Bahkresa tena. Tanzanians had never known Dr Rweyemamu to be anything closer to A FLASHY GUY CALLING ATTENTION TO HIMSELF this much!!

  Nani angetegemea kama tungefika mahala tukaona muhuri wa ikulu ikitumika vibaya hivi kupitisha maneno yasio na staha!!! Hebu kumbuka taarifa kwa vyombo vya habari isiyowekwa kwenye letterhead ya ikulu, ikaandikwa saa tano usiku na saa 12 alfajiri gazeti limebeba habari yake yenye lugha ya 'Rusha Roho', mijigambo, kiburi, kejeli na vitisho vya kilevi juu kwenda mitaani??

  Je, ni maafisaa wangapi wa serikali yetu ambao nao wanatembelea vitendeakazi vyao kwapani hapa nchini na ni kwa malengo gani hasa?
   
 15. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #15
  Jan 5, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Go Dr, JK should be ousted of office now and real president to be in office
   
 16. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #16
  Jan 5, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,234
  Trophy Points: 280
  Chadema inao idadi ya kutosha ya kuanzisha mjadala bungeni wa kumchunguza JK juu ya kashfa ya Richmond/Dowans.......lengo is to impeach him now...........................Nina uhakika kuna wabunge wengi wa CCM wataiunga mkono hiyo hoja............................Huyu jamaa now has gone too far..............................

  Atakuwa Raisi wa kwanza katika historia ya nchi yetu kushitakiwa na Bunge na hili lianze sasa na swahiba zake akina Rostam Aziz, Lowassa, karamagi na wengineo kama akina Dr. Idrissa Rashid watafuata baadaye........................
   
 17. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #17
  Jan 5, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,234
  Trophy Points: 280
  Impeach kikwete to end this nonsense.......................
   
 18. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #18
  Jan 5, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,234
  Trophy Points: 280
  Slaa: JK atwambie kwanini tunailipa Dowans
  Tuesday, 04 January 2011 21:06

  Minael Msuya
  KATIBU Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibroad Slaa amemtaka Rais Jakaya Kikwete kuwaeleza Watanzania sababu za kuwabebesha mzigo wa malipo ya fidia ya Sh185 bilioni kwa kampuni ya Dowans, hali serikali yake ikihusika na uzembe uliosababisha fidia hiyo.

  Akizungumza na gazeti hili jana, Dk Slaa alisema, Dowans iliingia nchini kwa uzembe wa serikali hivyo Rais Kikwete anapaswa kueleza kwanza serikali yake inawajibikaje, kabla ya kuwataka Watanzania walipe fedha hiyo.

  "Kampuni ya Dowans iliingia nchini kwa baraka za Baraza la Mawaziri wakati Kikwete akiwa mwenyekiti. Uzembe huu ulifanyika yeye akiwa anaona na kama hajui basi yeye hakuwajibika, na kama alijua basi yeye ni sehemu ya uzembe huo. Atuambie kwa nini tulipe Dowans kwa uzembe wa serikali yake?" alihoji.

  Aliendelea, "Ukilitazama jambo hilo kwa undani, utagundua kuwa baada ya Lowassa kujiuzulu katika sakata la Richmond, mtu aliyetakiwa kumfuata ni Kikwete, kwani ndiye aliyebariki ujio wa kampuni hiyo nchini na baadaye Dowans."

  Alisema "Kikwete anahusika na Dowans kwani mwaka 2007 ndiye aliyekutana na waandishi wa habari Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kueleza kuwa ameshawasiliana na kampuni moja kuja nchini kuzalisha umeme kwa bei nafuu. Na siku chache baadaye, mfanyabiashara mmoja maarufu nchini (jina linahifadhiwa) akaleta mitambo hiyo."

  Dk Slaa alisema hayo baada ya gazeti hili kumtaka aeleze endapo ana uthibitisho wowote, anapomtuhumu Rais Kikwete kuhusika na Dowans.

  Jana baadhi ya vyombo vya habari nchini, viliinukuu Kurugenzi ya Habari na Mawasiliano ya Rais Ikulu ikieleza kuwa kitendo cha Dk Slaa kumhusisha Rais Kikwete na Dowans ni uzushi na kinalenga kumpaka matope.

  Lakini alipotakiwa kuzungumzia suala hilo jana, Dk Slaa alisema hawezi kujibizana na Kurugenzi hiyo inayofanya kazi chini ya rais kwa kuwa siyo saizi yake.

  "Waliomjibia Kikwete siwezi kujibizana nao kwa kuwa sio saizi yangu. Nataka Kikwete mwenyewe ajitokeza ajibu kama mimi nimesema wongo," alisema Dk Slaa.

  Ulipaji wa fidia hiyo unafuatia uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Biashara (ICC Court), Novemba 15, mwaka huu chini ya Mwenyekiti Gerald Aksen na wasuluhishi Swithin Munyantwali, Jonathan Parker uliamuru Tanesco iilipe Dowans kiasi hicho cha fedha.

  Dowans ilifungua shauri katika ICC, ikilalamikia Serikali ya Tanzania kupitia Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kuvunja mkataba kabla ya wakati na kinyume cha makubalino kwenye mkataba husika.

  Awali baada ya uamuzi huo kufikiwa, Tanesco ilionyesha nia kwamba ingechukua hatua za kukata rufaa, lakini kauli ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema kwamba haoni sababu ya kufanya hivyo inaonekana kama imeyeyusha ndoto hizo za Tanesco.
  Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, William Mhando aliwahi kuwaambia wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari kuwa shirika lake lingeweza kutoa tamko kuhusu hatua za kuchukua kuhusu uamuzi wa ICC, lakini akaweka wazi kuwa walikuwa wakisubiri uamuzi huo kusajiliwa rasmi katika Mahakama Kuu nchini.

  Hata hivyo, kutokana na kauli ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, sasa ni rasmi kwamba hakutakuwa na hatua zozote za kisheria dhidi ya uamuzi wa ICC na badala yake Tanesco watatakiwa kujipanga kuwalipa Dowans mabilioni hayo ya shilingi kama walivyoamriwa.

  Akizungumza na Mwananchi baada ya hafla ya kuapishwa kwa Jaji Mkuu mpya, Mohamed Chande Othman Desemba 27, mwaka jana, Jaji Werema alisema ameshamaliza kuisoma hukumu hiyo na kufanya uamuzi ambao tayari ameukabidhi kwa Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja kwa ajili ya hatua nyingine baada ya kuridhika nayo.
  “Mimi kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali nimeisoma hukumu hiyo kwa makini na nimeridhika nayo kuwa iko sawa,” alisema Jaji Werema.

  Waziri Ngeleja juzi aliliambia Mwananchi kwamba serikali inaendelea kujipanga kutekeleza ushauri wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhusu Dowans.

  Taarifa za ndani ya Tanesco, zinasema kwamba shirika hilo limeanza kuweka fedha kwa ajili ya malipo katika benki moja (jina tunalihifadhi kwa sasa) jijini Dar es Salaam.
   
 19. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #19
  Jan 5, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,234
  Trophy Points: 280
  Jibu jepesi ni kuwa wabunge wa Chadema wamfungulie JK mashitaka ya ufisadi Bungeni na nguvu ya wananchi itahahakikisha ya kuwa wabunge wa CCM na unafiki wao wanaiunga mkono...tutafanya maandamano nchi nzima kuunga mkono JK kuchunguzwa na Bunge na wabunge wa CCM watanywea.....na baada ya JK kufukuzwa kazi na Bunge hapo mchakato wa katiba mpya uendelee chini ya usimamizi wa Bunge na kwa kuundiwa sheria .........................

  Hatuwezi kukubali mafisadi wachache waiteke nyara nchi yetu...................na kutuachia taifa lote maumivu.................
   
 20. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #20
  Jan 5, 2011
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Dr Slaa naona ana kinyongo na JK.

  Inawezekanaje swali kama hilo amuulize Rais kabla hajapata majinabu toka kwa waziri husika? Rais anapata ushauri kutoka kwa waliokaribu zaidi na sakata, ambao ndio wanajua mchakato mzima.

  Uchokozi.
   
Loading...