Dr. Slaa rusha vipindi vya Televisheni kila siku hadi tarehe ya uchaguzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Slaa rusha vipindi vya Televisheni kila siku hadi tarehe ya uchaguzi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Watanzania, Oct 26, 2010.

 1. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Katika hatua za kumalizia ushindi, namshauri Rais mtarajiwa na kampeni meneja wake, warushe vipindi vya televisheni kila siku kuanzia leo hadi tarehe ya uchaguzi. Hii itasaidia watu ambao hawajapata nafasi ya kusikia sera za Dr. Slaa za elimu bure, vifaa vya ujenzi rahisi na mengine mengi waweze kumsikiliza na kuongeza ushindi. Chadema pia walengeshe vipindi vyao vingongane na mikutano au vipindi vya televisheni vya JK. Watu siku hizi hawataki kuwasikiliza CCM.
   
 2. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  ni wazo zuri tatizo suna uhakika kama wana pesa za kutosha kwa mda huu mkuu,nadhani wanatamani pia lakini nahisi gharama za kurusha matangazo kwenye television ni kubwa sana
   
 3. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Speaker, siyo lazima walipe cash, Chadema ni Chama kinachopendwa na watanzania wengi, tutawachangia kulipa madeni hata baada ya uchaguzi. Sisi wananchi tumeamua. Mwenye mawasiliano na Chadema na Dr. Slaa afanye haraka iwezekanavyo leo hii. Hili ni suala la kufa na kupona, hakuna mchezo. Sisi watanzania tunamwamuru Rais mtarajiwa Dr. Slaa na Chadema watekeleze ombi hili, tutalipa gharama kwa kutoa michango, hata baada ya uchaguzi, ni kwa ajili ya ukombozi wetu kutoka kwenye minyororo ya CCM.
   
 4. K

  KIURE Member

  #4
  Oct 26, 2010
  Joined: May 8, 2009
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  TV itawaongezea CHADEMA kura. Aliyekataa mdahalo kajitia kitanzi mwenyewe! Uliona wapi mtu anataka kuoa lakini hataki kujitokeza mbele ya wakwe? Ati anataka kwenda ukweni kwa kunyata! Hiki kituko cha mwaka!
  Mzee hapa tulipofikia ni sawa na Haiti ilivyokwa wakati wa PAPA DOC! Kikundi cha mafioso kilihodhi nchi hadi pale wananchi walipowatoa nduki! Tanzania inahitaji kuwatoa nduki wahujumu nchi sasa! bahati mbaya hawaruhusu sisi tulio nje kupiga kura, yangu ingeenda kwa SLAA. Siku ya kupiga kura walinde kura zao, wtu wasitoke vituoni hadi kurazihesabiwe.
  Mungu ibariki Tanzania.
   
 5. Safina

  Safina JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2010
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 498
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kitu kinachonishangaza, huku ukipita kila mahali watu wengi wanaonekana kumchoka mkwere na chama chake, na yeye mwenyewe ameshasisitiza kuwa, tumchague, tusimchague, ushindi kwa CCM ni lazima, hivi huyu jamaa anajiamini nini lakini, halafu hata watu waliomo humo ndani inaonekana wameshachoshwa na mambo ya humo lakini kwa nini mwisho wa siku wataibuka washindi!!!!!!!!!!
   
Loading...